Tuesday, December 31, 2013

CUF ITAENDELEA KUSIMAMIA MISINGI YA HAKI NA USAWA (MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA LAZIMA ITOWEE NCHI YETU YA ZANZIBAR)

Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Mzee Hassan Nassor Moyo, akihutubia katika mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika Kinyasini, jimbo la Chaani
Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Mzee Hassan Nassor Moyo,(MTU MZIMA DAWA) akihutubia katika mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika Kinyasini, jimbo la Chaani

Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,Makamo wa Raisi wa nchi ya Zanzibar akihutubia katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika viwanja vya Kinyasini, jimbo la Chaani Unguja
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama chake kitaendelea kusimamia misingi ya haki na usawa, ili kuhakikisha kuwa kila Mzanzibari anapata haki yake inayostahiki.
Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameeleza hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara ya chama hicho uliofanyika viwanja vya Kinyasini, jimbo la Chaani.
Amesema Chama hicho kitaendelea kuwa mstari wa mbele kudai mamlaka kamili ya Zanzibar kwa lengo la kuhakikisha kuwa Zanzibar inaongozwa kwa misingi ya haki na usawa, ili  wazanzibari waweze kuamua mambo yao wenyewe bila ya kuingiwa na mamlaka nyengine.
Amesifu umakini wa kamati ya Maridhiano yenye wajumbe sita wakiwemo watatu kutoka Chama Cha Mapinduzi na watatu kutoka Chama Cha CUF, na kwamba wajumbe wa kamati hiyo wameonesha uzalendo wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya maridhiano Mzee Hassan Nassor Moyo, amebainisha kuwa mambo yanayodaiwa kutolewa katika orodha ya Muungano sio mageni, kwani yalikuwemo kwenye mamlaka ya Zanzibar kabla ya kuungana na Tanganyika mwaka 1964.
Ameyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na sarafu, mambo ya nje, pamoja na rasilimali ya mafuta na gesi asilia.
Mzee Moyo amewanasihi  Wazanzibari kuepuka chuki, fitna na ubaguzi, na badala yake waungane kupigania maslahi ya nchi yao.
Amepongeza hatua iliyochukuliwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume na mwenzake Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad ya kufikia maridhiano ambayo yamewaunganisha Wazanzibari.
Nae Mjumbe wa Kamati hiyo ya maridhiano Mansoor Yussuf Himid (CCM), amesema Zanzibar ni ya Wazanzibari wote, na kwamba kila mzanzibari anastahili kupata haki sawa na mwengine.
Amesema ataendelea kuungana na Wazanzibari kupigania haki ya Zanzibar ndani ya Muungano, ili iweze kuendesha mambo yake yenyewe, na kuwashajiisha vijana kutorudi nyuma katika kupigania haki hiyo.
Akizungumzia kuhusu rasimu ya pili ya katiba inayotarajiwa kuwasilishwa kesho (leo) tarehe 30/12/2013 katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam, Mansoor amesema ikiwa rasimu hiyo haitokidhi angalau wastani wa matakwa ya Wazanzibari hawatoikubali, na wataikataa kabisa.
“Watu wa mjini huwa tuna wimbo tunasema ‘supu tayari…’ lakini tunasema ikiwa supu hii ya Jaji Warioba itapungua chumvi au pilipili manga tutaiongeza, lakini kama mbaya hailiki tutamuachia mwenyewe supu yake” alidokeza Mansoor.
Wajumbe wengine wanaounda kamati hiyo ambao wote walikuwepo mkutanoni na kuzungumza ni Abubakar Khamis Bakar (CUF), Ismail Jussa Ladhu (CUF), Eddy Riyami (CCM) na Salim Bimani (CUF).
Katika Mkutano huo Mhe. Maalim Seif alikabidhi kadi 459 kwa wanachama wapya walioamua kujiunga cha chama hicho, sambamba na kuweka mawe ya msingi katika matawi matatu mapya ya CUF ndani ya jimbo la Chaani, pamoja na kufungua barza ya vijana, iliyoyopewa jina la barza ya Maalim Seif Sharif Hamad katika kijiji cha Bandamaji Chaani.
Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Mansoor Yussuf Himid akizungumza katika mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika Kinyasini jimbo la Chaani
Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Mansoor Yussuf Himid(KIBOKO YA WANAFIKI NA WAHAFIDHINA) akizungumza katika mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika Kinyasini jimbo la Chaani
Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano maarufu Eddy Riyami akizungumza katika mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika Kinyasini jimbo la Chaani
Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano maarufu Eddy Riyami(MR DELETE FUTA KABISA) akizungumza katika mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika Kinyasini jimbo la Chaani
Mfuasi wa CUF akifurahia hotuba iliyotolewa na mmoja kati ya wajumbe wa kamati ya Maridhiano kwenye mkutano huo
MAA MAMA WA NCHI YA ZANZIBAR NA CUF akifurahia hotuba iliyotolewa na mmoja kati ya wajumbe wa kamati ya Maridhiano kwenye mkutano huo
Baadhi ya wafuasi wa CUF na vyombo vya habari, wakifuatilia kwa umakini mkutano huo Picha: Salmin Said
WATU WALIOFURIKA KATIKA MKUTANO wa CUF na vyombo vya habari, wakifuatilia kwa umakini mkutano huo
Picha: Salmin Said

TUTA FIKE TU WANA WA MAMLAKA KAMILI


WAKOMBOZI NA WAASISI WA MARIDHIANO YA NCHI YETU YA ZANZIBAR NDIO HAWA MAALIM SEIF NA KARUME

Kwanza niaze kutoa pongezi zangu kwa wazanzibar wote wenye kutaka mamlaka kamili ,Kitendo cha Warioba kutangaza tu hadharani kwamba asilimia 60 ya Wazanzibari walitaka Muungano wa Mkataba peke yake ni ushindi mkubwa kwa kila mzanzibar mwenye kuipenda nchi yake.
Niseme wazi kwamba wazanzibar sasa tumepiga hatua moja kubwa mbele leo hii,lakini pia kinachotakiwa hatutakiwi kuonesha hisia kama sasa tumefanikiwa safari ndio kwanza inaanza,kinachotakiwa hivi sasa ni kuendelea na harakati ambazo zifanyike kwa njia ya amani na kidemokrasia kukamilisha mambo yaliobakia.
Lakini pia wale wote wanaosema tumekosa hiki au kile kwa hatua hii warudi kwenye historia ya Mkataba wa Hudaibiya ambapo mengi yalikosekana lakini hatimaye kupitia Mkataba huo ambao awali baadhi ya Maswahaba walimbeza Mtume (s,a,w)kwa kukubali kwake mkataba huo kwani ulionekana kama wenye sura ya kuwakandamiza Waislamu lakini mwisho wake ukapatikana ukombozi wa Makka kwakutokana na makafiri kushindwa kutimiza makubaliano ya mkataba huo wa hudaibiya.
Kutokana na kisa hichi ni wazi kabisa wazanzibar tunatakiwa kujifunza,kuwa na subra na uvumilivu wa hali ya juu huku tukiendeleza harakati zetu kwa njia ya amani kuhakikisha tunayashika yale yote yaliobakia kutoka katika orodha ya muungano huu feki unao ila nchi yetu ya Zanzibar.
Ikiwa tutaendelea kushikamana na kuwa wamoja bila ya kubaguana basi ukombozi wa Zanzibar unakuja karibuni Inshallah.

VIDEO-POROJO LA MASULTANI WEUSI WATANGANYIKA RASIMU YA 2


Friday, December 27, 2013

UPANGA WA DHAHABU NI MUHIMU ZAIDI YA MAISHA YA MWANANCHI WA ZANZIBAR


JESHI LA POLISI NCHINI ZANZIBAR LIFANYIWE MABADILIKO ZAIDI-WAWAKILISHI WA AMKA SASA.

Wajumbe wa baraza la wawakilishi wametaka jeshi la polisi nchini Zanzibar lifanyiwe mabadiliko ya uongozi kutokana na kushindwa kuwakamata wahalifu wa vitendo vya mauwaji, tindikali na kuibiwa upanga wa dhahabu ndani ya jeshi hilo.(DUUUH SASA NDIO MNAJUWA KAMA ASKARI WENYEWE NI WEZI..?)
Mwakilishi wa jimbo la Chaani Ussi Jecha amesema jeshi la polisi nchini Zanzibar limeshindwa kukabiliana na vitendo hivyo na kuitia doa nchi ya Zanzibar kwa kuibiwa upanga wa dhahabu unaotumika kwenye mikutano ya nchi wanachama wa SAPCO.
Amesema kutokana kushindwa kuwakamata wahalifu hao na kuibiwa upanga huo iko haja ya kulifanyia mabadiliko jeshi hilo badala ya kufanyiwa mabadiliko ya kamishna pekee.
Nae waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais mnafiki Aboud amesema kumetokea vitendo vingi vya uhalifu, lakini jeshi hilo limeshindwa kuwakamata wahalifu.
Amesema hali hiyo bado inaonesha jeshi hilo lina matatizo na kuunga mkono ushauri uliotolewa na mwakilishi huyo wa kutaka jeshi lifanyiwe mabadiliko ya uongozi…
Kuhusu wizi wa upanga wa dhahabu uliotokea mikononi mwa jeshi la polisi nchini Zanzibar Aboud amesema uchunguzi wake unaendelea na nchi ya Bostwana itakayokuwa mwenyekiti wa mkutano wa SAPCO imejitolea kutoa upanga mwengine bila ya kulipisha.

ALIKUWA NAHODHA SASA NI MPIGA DEBEE (HANA JIPYA ANABWABWAJA TU KAMA MLEVI WA GONGO PALE ALABAMA)


Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa nchini Tanganyika ambaye atii ni Mzanzibari, Shamsi Vuai Nahodha amesema licha ya kuvuliwa uwaziri ataendelea kuwa kiongozi wa kisiasa na kukitumikia chama chake na wananchi bila ya kuvunjika moyo.(wachawee)
Nahodha, ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa ametoa kauli hiyo siku chache baada ya kutimuliwa kwenye Baraza la Mawaziri na Rais Jakaya Kikwete wa nchi ya Tanganyika kutokana na uzembe kuto kuufahamu kazi yake katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
Akihutubia wanachama wa CCM na Wahafidhina wenzake na kumsikiliza kwenye Ofisi ya chama hicho Mkoa wa Mjini Magharibi, hapa nchini Zanzibar, Nahodha alisema yaliyomtokea ni mambo ya kawaida katika medani za utumishi wa umma.(bora nichekea kwanza hahahahahaha hukujuwa wakati ule unamrisha majeshi yawauwe wapemba...?? kwamba iko siku kiti utakiwacha ulipo kikuta..?)
“Pamoja na hayo yaliyotokea, nitaendelea kulitumikia taifa,(tunakuliza taifa lipi..?? maana la Tanganyika lishakutimuwa, kama ni la Zanzibar omba mungu shein andele kuwa raisi wa kisonge au hata hapa Zanzibar pia tutakutimuwa maana huna faidi hata moja) chama changu na wananchi kwa uaminifu, juhudi na uwezo wangu wote,” alisema Nahodha, ambaye pia ni Mwakilishi wa Mwanakerekwe.
Alisema amewajibika serikalini kutokana na matakwa ya wajibu katika utendaji wa pamoja na kusema kitendo hicho ni mfano wa ajali inayoweza kumkuta mtu yeyote katika safari ya maisha.(hata bado hii dunia tu baba bado akhera sasa)
“Sina kinyongo wala muhali, yaliyotokea ni mambo ya kawaida katika medani za uongozi, wajibu na dhati yangu ni kuwa mtii kwa Serikali zote. Pia kuitumikia CCM na kushirikiana na wananchi wenzangu. Binadamu hawezi kujiepusha na mitihani, ”alisema Nahodha. Alisema alikabidhiwa dhamana na viongozi wake ili kulitumikia taifa na kutimiza wajibu ipasavyo katika nyadhifa mbalimbali na yaliyomtokea ameyapokea kwa mikono miwili na hana kinyongo.(ata ukiwa na kinyongo kitampata nani unafikiri..?)
Mauwaji ya Wazanzibari (Mapinduzi)
Akizungumzia mauwaji ya Wazanzibari (Mapinduzi) ya Zanzibar, Nahodha alisema ni ufunguo uliofungua milango ya fursa kwa wananchi wanyonge waliokandamizwa na ukoloni (haya makandamizo ya mkoloni mweusi Tanganyika huyaoni maana unakula nao sahani moja ila iko siku utayaona pale ukibaki na kijumba chako tu bila ya madaraka yoyote.) huku akisifu uongozi kwa miaka minane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, hayati Mzee Abeid Amani Karume.
Alisema kiongozi huyo licha ya kuongoza Mapinduzi ya Januari 12, 1964,(wacha kusema uwong mzee karume hakuongoza mapinduzi wala hakuwepo kabisa hapa Zanzibar na hata alikuwa hajuwi kama kuna mauwaji ya wazanzibari yanakuja kutokea alikuwa huko Tanganyika ulikotimuliwa) aliifanyia mema Zanzibar na watu wake katika kuwaletea maendeleo na kwamba atakumbukwa na vizazi vyote hadi mwisho wa dunia.(Nahodha wewe ni mema yapi uliyo wafanyia Wazanzibari au maendeleo gani uliyowaletea watu wa jimbo lako tu wachana na Zanzibar kwa ujumla jimbo lako tu ni maendeleo gani uliyowaletea...??)
“Kufanya Mapinduzi haikuwa kazi nyepesi. Waliofanya walikuwa ni majasiri na wazalendo. Juhudi zao ni matunda haya leo baada ya miaka 50 kupita nchi ikiwa katika utulivu na amani,” (ni nani aliyekudanganya Nahodha kuwa kabla ya mauwaji ya Wazanzibari(mapindizi) hapa Zanzibar palikuwa hapana utulivu na amani..?)  alisema Nahodha, ambaye alikuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar kuanzia mwaka 2000 hadi 2010. na hana moja alilolifanya la faidi kwa Wazanzibari.
“Uongozi wa Mzee Karume ni mfano wa aina yake, mwaka 1964 hadi 1972 aliiletea mabadiliko makubwa Zanzibar. Alijenga viwanda, makazi bora, elimu bila malipo, barabara na kuimarisha huduma za jamii,” alisema Nahodha.(mzee karume kafanya yote hayo kwa 1964 mpaka 1972 wewe Nahodha umefanya nini kuanzia mwaka 2000 hadi 2014..?)
“Nasikia kuna watu hawataki kulisikia neno Mapinduzi, hao ni wapuuzi na wapuuzeni. Mapinduzi na Muungano ni uti wetu wa mgongo, Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Karume waliona mbali, tusibeze mitazamo yao kwa tamaa za madaraka,” alisema.(yupi hapa mwenye tama ya madaraka wewe au sisi muwakilishi,mbunge,cheo walicho kuvuwa Watanganyika,hukutosheka ulekuwa unataka kuwa raisi wa Tanganyika ndio maana wamekutimuwa sasa ni nani mroho wa madaraka Nahodha..?)
Kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Nahodha alisema angependa ubaki katika mfumo na Serikali mbili na kusema pamoja na uzuri wake, zipo changamoto na kasoro zinazohitaji kurekebishwa na kuwa na muungano wenye nguvu za kiuchumi.(yagujuu mbona hukuyasema hayo ulipokuwa na vyeo vya Kitanganyika..?)
Alisema kazi ya kurekebisha makosa ni nyepesi lakini wazo la kuvunja Muungano lina gharama kubwa kuliko inavyofikiriwa na baadhi ya watu wanaotaka uvunjike.(wewe hamia huko Tanganyika Wazanzibari hatuti viraka sisi hatuna asili ya viraka.)
“Sina uwezo wa kuwachagulia watu kitu wanachokipenda na kukitamani. Imani yangu ni kwamba nje ya Muungano hatutabaki salama kama ilivyo sasa.(in shaa allah shari unayotutakiaya itakurudia mwenye na sisi tutajitenga na kuwa na nchi yetu ya Zanzibar kwa amani) Muungano wetu umekuwa kinga na nguzo kwa nchi zetu mbili na usalama na wake,” alisema Nahodha.
Aliitolea mfano Sudan Kusini ambayo ilitaka ipewe mamlaka yake kamili akisema hivi sasa imejikuta ikiwa katika machafuko na vita ya wenyewe kwa wenyewe pamoja na kuibuka kwa mgawanyiko wa kijamii unaotishia mustakabali wa Taifa hilo.(usitulete vitisho vya sudan wala kwengine ulimwenguni wao wanakili zao na sisi tuna akili zetu sisi sio kama wewe unategemeya akili za nyerere ambaye ashakufa ndio maana huweze hata kufikiri maana akili zako zishakufa nyerere kenda nazo.)
“Itazameni Sudan Kusini, tusipokuwa waangalifu na makini yanaweza kutukuta. Angalia vita ya Somalia inaitesa Kenya na kutukosesha amani, tusikubali kugawanywa na viongozi ambao wanawaza madaraka.”moja wapo ni wewe unayetaka kuwagawa wazanzibari waendele kuwa chini ya MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA NA SIO KUWA HURU.

ASKOFU DAMIANI DALLU ACHANGANYA DINI NA SIASA (AKEMEA UTANGANYIKA AHOFIA MUUNGANO)


MUBAKI NA TANGANYIKA YENU MUENDELEZE ULANISI WENU HUKO HUKO TANG

ASKOFU wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Geita, Damiani Dallu amekemea vuguvugu la watu wanaotaka kuirejesha NCHI YA TANGANYIKA katika siasa za Muungano.
Akizungumza kwenye Ibada ya Sikukuu ya Krismas Geita jana, Askofu Dallu alisema Tanganyika iliishi kwa muda mfupi mpaka mwaka 1964 na baada ya hapo kwa miaka 50, imekuwepo Tanzania:
“Hao wanaoitaka Tanganyika nawashangaa…kama wanataka kutoka  watoke…sisi tutatangulia mbele tukiwa Watanzania,” alisema Dallu.
Alisema katika Afrika si kitu cha ajabu kwa nchi kubadilisha jina baada ya kupata uhuru na kuhoji: “Ni nani ambaye jina analoitwa leo alizaliwa nalo?,” aliongeza:
“Nchi nyingi za Afrika zimebadilisha majina yake ya zamani…hii haiwafanyi eti wasisherehekee uhuru siku waliyoupata…Tuache upuuzi tujenge nchi yetu Tanzania hata kama wenzetu katika Muungano walibaki na jina lao,” alisema Dallu.
Alizitaja nchi za Malawi, Msumbiji, Ghana, Zimbabwe na Zambia ambazo majina yake ya awali hayakuwa hayo, lakini bado zinasherehekea uhuru wao kwa muda waliyoupata.
Alisema ni kawaida katika jamii kuwa na watu watakaojitokeza kupinga mambo na watu hao huwa chachu ya kufanya mageuzi ya kweli.
Askofu Dallu, pia alitaka Watanzania kumuomba Mungu, ili kupata Katiba ambayo itaendeleza furaha ya kweli, iliyodumu kwa miaka 52 sasa.
Naye, Askofu Mkuu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaa, Mhashamu Titus Mdoe alitaka Watanzania wenye nyadhifa za uongozi kuwa na hofu mbele ya Mungu, na kuacha vitendo vya kinyama na udhalilishaji dhidi ya binadamu wenzao.
Askofu Mdoe alisema hayo kwenye mkesha wa Krismas katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, na kuongeza kuwa umefika wakati kwa viongozi hao kujitoa kwa ajili ya maisha ya watu na si yao binafsi.
Alisema wapo baadhi ya watu wenye nyadhifa (viongozi) wanaojiona ndiyo kila kitu kwa wenzao na kujiona kuwa ndiyo wenye haki ya kuwafanyia wengine kila ubaya, bila kujali kuwa nao ni binadamu wanaostahili haki kama wao..
FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA TUNAKUAMBIA DALLU TANGANYIKA NDIO BABA YENU NA MAMA YENU, WASWAHILI WANASEMA MKATA KWAO MTUMWA , SIO WATANGANYIKA TU HATA SISI WAZANZIBARI HATUTAKI TENA KUWA NA NYINYI WATANGANYIKA MSHATUUWA SANA SIKU ZA CHAGUZI,MSHATUIBIA SANA MPAKA MEETUTIA UFUKARA KILICHOBAKI SASA NI KUWA WAZANZIBARI TUNATAKA WENYEWE KILE KIBWAGIZO CHETU NA NYINYI MUCHUKUWE CHENU CHA TAN-TANGANYIKA , NA SIS TUCHUKUWE CHETU CHA ZAN-ZANZIBAR TUNATAKA ZAN YETU TIMECHOSHWA NA NYINYI MITANGANYIKA.
KIKWETE JE UTAFUNGA JELA ASKOFU DALLU KWA KUCHANGANYA DINI NA SIASA KAMA ULIVYO MFUNGA SHEIKH MPONDA NA MASHEIKH WETU WA UAMSHO HUKU ZANZIBAR AU UTAMUACHIA ASEME ANAVYO TAKA MAANA NDIO WAO WALIOKUWEKA HAPO KATIKA KITI CHA URAISI WA TANGANYIKA...????

Thursday, December 26, 2013

HAKUNA ANAYEKATAA USHIRIKIANO, PIA HAKUNA ATAKAYEKUBALI UKOLONI


Na, Ismail Jussa.
Ni ndefu kidogo lakini utapata kujifunza zaidi kuh. Madai yetu yaliyo wazi.
Katika dunia ya leo hakuna anayeweza kukataa USHIRIKIANO ila pia hakuna atakayekubali UKOLONI.
Haya yanayofanywa dhidi ya Zanzibar ni akhasi ya ukoloni. Hata huyo Mngereza hakuifisidi Zanzibar namna ambavyo inafisidiwa na mfumo uliopo wa Muungano. Mngereza alikuwa akifidia nakisi ya bajeti ya makoloni yake.
Huyu wa leo anakamua mpaka maziwa hayatoki tena. Ulikuwa uongezee nukta nyengine kwamba katika PAYE, kuna watumishi wa Muungano waliopo Zanzibar ambao huduma zao zote zinatolewa na SMZ kupitia bajeti yake lakini PAYE wanazolipa kama shilingi bilioni 10 kwa mwaka zinachukuliwa kwenda Tanganyika.
Isitoshe kuna mashirika na taasisi yanayoitwa ya Muungano na humo Zanzibar siyo tu haina mamlaka yoyote katika uendeshaji wake bali hata mapato yake yote yakijumuisha huduma zinazotolewa na matumizi ya eneo la Zanzibar kama anga yake hakuna senti nyekundu inayovuka maji kuja Zanzibar. Mashirika hayo ni pamoja na TTCL, TPC, TPDC, TCAA, na TCRA.
Tunadanganywa kuwa tunapewa asilimia 4.5 ya mapato ya Muungano wakati ukweli ni kwamba tunapewa asilimia 4.5 ya fedha zinazotolewa na nchi wahisani au washirika wa maendeleo kama misaada ya moja kwa moja ya bajeti (General Budget Support-GBS).
Kwa upande mwengine, Tanganyika ikiendelea kujivika joho la Muungano kwa mambo yasiyo ya Muungano imekuwa ikikusanya matrilioni ya shilingi kama misaada ya kisekta (sectoral development programs) ambayo senti moja haivuki maji kuja huku.
Zanzibar imetoa asilimia 11.02 ya hisa iloanzisha Benki Kuu (BOT) lakini haikupata gawio lolote la faida (dividend) kwa miaka 28 tokea 1966 – 1994. Na baada ya hapo imekuwa ikipewa gawio la asilimia 4.5 badala ya asilimia 11.02 ya kima cha hisa katika mtaji uloanzisha BOT.
Zanzibar imelazimishwa kuingia katika kile kilichoitwa usawazishaji wa kodi (harmonisation of tariffs) ili kuua uchumi wake huku ikijulikana hakuna usawazishaji wowote maana bado bandari za Tanga na za mipakani Namanga na Horohoro hutoza viwango vya chini ya vile vilivyowekewa Zanzibar. Hatua hizo zimechukuliwa bila ya kufanywa au kutekelezwa mpango wowote wa kuifidia Zanzibar hasara ya usawazishaji huo ambao kama ingekuwa na mamlaka yake ingeweza kusarifu sera zake za uchumi
vile ipendavyo kwa maslahi yake.
Zanzibar ilifika mahala ikaamua kuanzisha sera ya Off-Shore Banking na Off-Shore Companies na kufikia kuandaa miswada ya sheria kwa madhumuni hayo lakini Waziri wa Tanganyika mwenye mamlaka Kighoma Malima (wakati huo) akamzuia Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Amina Salim Ali, asiiwasilishe Barazani kwa sababu Mtawala hajataka.
Tunaambiwa Mambo ya Nje ni mambo ya Muungano lakini Zanzibar haifaidiki na fursa zozote na ilipotaka kujiunga na OIC ikaamriwa ijitoe. Leo hata makao makuu ya Wizara zote, Idara zote, Mashirika yote, Vikosi vyote vya Muungano yapo Tanganyika na hiyo
maana yake ni fursa ya ajira, uwekezaji, mzunguko wa fedha kibishara katika matumizi, ongezeko la mchango katika GDP na fursa nyengine nyingi na zote hizo ziko Tanganyika. Haya ni
machache zaidi ya yale makubwa uliyokwisha yaeleza kwa ufasaha
mkubwa Abu Muhammad.
Basi labda haya ndiyo hiyo SPECIAL STATUS tunayoambiwa tunaipata. Kama alivyosema Kaplan (ambaye kwa hakika anakariri tu maneno au dira ambayo imeshaelezwa kinaga ubaga hapa hapa), hakuna wa kuizuia Zanzibar kuwa mlango mkuu wa biashara baina ya Afrika ya Mashariki, Kati na Kusini na Bahari ya Hindi. Nafasi ya Zanzibar ni kama zilivyo bandari za Bombay, Dubai, Hong Kong na Singapore. Tatizo ni kukandamizwa kiuchumi, kisiasa na kijamii na kukoseshwa mamlaka ya kujiamulia sera zake huru katika kuyafikia malengo yake ya maendeleo.
Lengo ni kuizuia isijitutumue lakini kwa sasa wahafidhina wamekwama. Umma wa Zanzibar haudanganyiki tena na propaganda za kitoto za Uhizbu na kumrudisha Sultani. Kizazi kipya Zanzibar kinataka mamlaka kamili ya nchi yao kitaifa na kimataifa ili
kujipangia na kujiamualia mustakbali wao utakaopelekea ujenzi wa uchumi imara utakaotoa ajira na kipato cha maana kwa watu wake. Wanaoumizwa na hili watafute pain killers mapema.
— with Ismail Jussa.

Wednesday, December 25, 2013

TUTAENDELEA KUDANGANYWA NA MAENDELEO YA MANENO AMANI NA UTULIVU MPAKA LINI..??

WAZANZIBARI AMKENI AMKENI ZANZIBAR KWANZA ZANZIBAR KWANZA ZANZIBAR TUNAWEZA HATUNAHAJA YA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA WALA WAHAFIDHINA

DARASA LA SABA (7) LA MKOLONI NI BORA KULIKO DARASA LA (12) LA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA HAPA NCHINI ZANZIBAR

A4253
A4127 (1)
HAYA NDIO MACHOGO YALIYO LETWA PEMBA KUENDELEZA SHEREHE ZA MAUWAJI YA WAZANZIBARI KIWANJA CHEUPE SHEIN NA MACHOGO WAKE ALIYO WALETA BASI
Wete – Pemba
Rais wa Maskani ya Kisonge, Ali Mohammed Shein,  amesema miaka 50 ya Mauwaji ya Wazanzibari nchi ya (Mapinduzi),  Zanzibar imeshuhudia mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu.(bora ni cheke kwanza hahahaahha)
Rais wa Maskani ya Kisonge Shein amesema wakati huu Zanzibar ikiadhimisha miaka 50 ya Mauwaji ya Wazanzibari   (Mapinduzi), wananchi hawana budi kujivunia maendeleo makubwa yaliyopatikana  katika sekta hiyo ya elimu.(bora nicheke tena hahahahahaha)
Aliyasema hayo katika sherehe za ufunguzi wa Skuli za Sekondari za Chasasa na  Skuli ya Sekondari ya Wanawake ya Utaani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini  Pemba.
Hiyo ilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mauwaji ya Wazanzibari  (Mapinduzi) ya mwaka  1964, zinazofikia kilele chake Januari 12, mwaka ujao.
Alisema vikwazo vya elimu kabla ya Mapinduzi haikuwa ada ya skuli pekee,  lakini hata fursa zenyewe hazikuwapo kwa watoto wa familia maskini kwani mtu  angeweza kupata ada lakini akashindwa kupata nafasi kwa kuwa anatoka familia ya  kinyonge. (swali tunakuliza wewe shein ulikuwa katika familia ya kinyonge au yakitajiri...?)
Alisema madhila ya aina hiyo waliyokuwa wakifanyiwa wananchi maskini wa  Zanzibar, ndiyo yaliyokifanya Chama cha Afro Shirazi kusimama kidete kutetea  haki za wanyonge.  ( mbona paka leo basi bado wazanzibari tunaishi katika madhila makubwa kuliko huko tulikotoka na wanao nufaika ni nyinyi viongozi,wake zenu,watoto wenu basi tulio baki tunasaga mawe miaka 50 na sultani wakitanganyika katukalia kooni hata hatupumuwi sasa huwo ukombozi wa Afro Shirazi uko wapi....?)
Alisema azma ya Serikali ya Mauwaji ya Wazanzibari  (Mapinduzi) ya Zanzibar tangu wakati huo ni  kuwapatia elimu watoto wote hadi kikomo cha uwezo wao na ndiyo maana kila wakati  imekuwa ikiongeza fursa za elimu nchini.
Je wewe ulikuwa unaishi katika familia ya kitajiri kabla ya mapinduzi haram Shein...??:..Acha kudangaya vipofu sisi wenyemacho katu hatukubaliani na hayo wazee wetu kila kukicha wanasema darasa la (7) saba la mkoloni nibora kuliko darasa la kumi na mbili(12),La mkoloni mweusi Tanganyika skuli zenyewe za kujivunia mapinduzi ni zipi....?au za pale kwenu Kengeja.....??? miaka 50 sasa ni skuli ngapi zimejengwa na serekali ya mauwaji....?? hospitali ngapi...? barabara ngapi...? maji na umeme mpaka leo hamjayaweza mpaka leo kula ni yatabu watu wanafuturu ugali siku za ramadhani amakweli maendeleo.
ELIMU A A ELIMU BILA MALIPO ELIMU AA ELIMU BILA MALIPO

HII NI HOSPITALI YA PEMBA JE SHEIN MKEO AU MWANAO AKIUMWA UTAMLETA KATIKA HOSPITALI HII...???
MIAKA 50 YA MAUWAJI YA WAZANZIBARI YANAENDELEA KUWAUWA KILA KUKICHA HIZI NDIO FAIDA ZA MIAKA 50

Saturday, December 21, 2013

HALI HALISI YA SKULI YA KENGEJA-PEMBA NCHINI ZANZIBAR HAYA NDIO MAENDELEO YA MIAKA 50 MAPINDUZI YA ZANZIBAR AMAKWELI TUME ENDELEA

kengeja
Huyu ni moja katika wanao ijuwa skuli hii ana haya ya kusema. Mimi ni Skuli ya Kengeja Secondary nimezaliwa mnamo mwaka 1922 nimetoa elimu kwa watu wengi sana wa Kengeja na maeneo jirani kama vile Mwambe,Kiwani,Kangani kwa kipindi cha nyuma wakati wa kuanzishwa kwangu.
Kwa sasa naendelea kutoa elimu bado ingawa nimechoka sana kutokana na uchakavu wa majengo yangu,naomba msaada kwa Serikali na wasamaria wema kunifanyia alau ukarabati tu na ikiwezekana kujengwa upya.

WANNE WATIMULIWA KATIKA BUNGE LA NCHI YA TANGANYIKA. EMMANUEL NCHIMBI ALIYEWAITA WAZANZIBARI MAGAIDI..SHAMSI VUAI NAHODHA DAMU YA MAUWAJI YA WATU WA PEMBA.



Dar es Salaam / Dodoma nchini Tanganyika. Ripoti ya Kamati ya Maliasili, Ardhi na Mazingira iliyowasilishwa jana asubuhi bungeni mjini Dodoma, imewang’oa madarakani mawaziri wanne ambao wizara zao zilishindwa kusimamia vizuri utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
Kung’oka kwa mawaziri hao kulitangazwa bungeni jana usiku na Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyeeleza kuwa Rais Jakaya Kikwete ametengua uteuzi wao baada ya kuwasiliana naye kwa mashauriano akiwa nchini Marekani kwa matibabu.
Mawaziri waliong’olewa kutokana na ripoti ya kamati hiyo iliyoongezewa shinikizo na michango ya wabunge wengi ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alyewaita Wazanzibari kuwa ni MAGAIDI, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha anaye jipendekeza kwa Watanganyika na kushirikiana nao katika kutaka kupote Taifa la Zanzibar na kuigeuza kuwa ni KIJIJI CHA PWANI ya nchi ya Tanganyika na sio nchi ya Zanzibar na Waziri wa  Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo.
Waziri wa  kwanza kutangaza kujiuzulu alikuwa ni Kagasheki huku uamuzi wa mawaziri watatu kujiuzulu ukitangazwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Kagasheki alitangaza kujivua wadhifa huo sa 2:09 usiku alipokuwa akichangia majumuisho ya ripoti ya kamati hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo James Lembeli ambaye ni Mbunge wa Kahama (CCM).
Katika maelezo yake Kagasheki alisema: “…Mimi ni mtu mzima nimesikia hisia nzito sana kwa waliyoyasema wabunge.  Rais Kikwete aliponiteua ilikuwa ni kwa furaha yake na operesheni hii, yaliyotokea yametokea hali ya wanyama huko si nzuri;
Mimi mwenyewe nimewasikia na nachukua fursa hii kuteremka ngazi hii ya uwaziri na nitachukua taratibu za kawaida kuijulisha sehemu inayohusika(Rais).
Baada ya Kagasheki kutangaza hatua hiyo, Spika aliwaita mawaziri Dk Nchimbi na Nahodha kuchangia hoja hiyo, hata hivyo hawakuwepo ndipo alipoitwa Dk Mathayo na kutoa maelezo yake.
Katika maelezo yake Dk Mathayo alisema kuwa ripoti hiyo haikumtendea haki kwani kamati ya Lembeli haikumwita kumhoji na kwamba hata ripoti nzima haikueleza kuhusika na kashfa hiyo. Hata hivyo akihitimisha hoja hiyo Lembeli alisema Dk Mathayo ameshindwa kusimamia mapendekezo tisa, yakiwemo matatizo    ya wafugaji aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete Januari 18, 2006 alipoteuliwa kushika nafasi hiyo.
Akitoa maelezo ya kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri hao, Waziri Mkuu Pinda alisema: “Niliona nimtafute mkuu wa nchi (Rais Jakaya Kikwete), nilimpa picha yote ya kinachoendelea, alikubali ushauri wa Bunge; ..amekubali kuchukua uamuzi wa kutengua uteuzi wao(mawaziri).”
Akihitimisha mjadala huo wa ripoti ya kamati yake, Lembeli alisema: “...Katibu Mkuu na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii nao wawajibishwe kutokana na kuhusika kwao na unyama uliotokea kwenye mpango wa Operesheni Tokomeza Ujangili. Rushwa iliyopo ndani ya wizara hiyo ni kubwa inakusanywa kwa kutumia simu, hivyo Serikali izichunguze simu zao kuanzia leo.”
Awali hali ya hewa ndani ya kumbi wa Bunge jana ilichafuka baada ya wabunge kuchangia kwa hisia kali, wakitaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kujiuzulu sambamba na mawaziri wengine watatu.
Mawaziri wanaotakiwa kujiuzulu ni wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.
Mbunge wa Longido, Lekule Laizer (CCM), alienda mbali zaidi na kutaka Bunge livunjwe endapo Waziri Mkuu na mawaziri hao watatu watakataa kujiuzulu kwa lengo la kung’ang’ania madaraka.
Michango ya wabunge hao ilitokana na ripoti ya kamati ndogo ya uchunguzi ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira chini ya Mwenyekiti wake, James Lembele iliyowasilishwa bungeni jana.
Ripoti hiyo inayohusu Operesheni Tokomeza Ujangili (OTU), ilibainisha kuwapo mauaji ya watu 13 na askari sita, utesaji wa kutisha wa watuhumiwa, ubakaji, rushwa na uporaji wa mali za wananchi.
Hata hivyo pamoja na kamati ya Lembeli kumtaka Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David apime kama bado anastahili kuongoza wizara hiyo, wabunge walimsafisha.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), alisema hakuna jinsi ya kuonyesha namna wabunge walivyokasirishwa na vitendo hivyo zaidi ya Serikali nzima kwa maana ya Pinda kujiuzulu.
“Naomba Waziri Mkuu uchukue ‘political responsibility’ (uwajibikaji wa kisiasa) na siyo kwamba kwa kufanya hivyo anahusika la hasha… Kama hachukui hatua Bunge libebe dhamana hiyo,” alisema.
Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia alisema ripoti hiyo ya Lembeli imetaja kuwapo baadhi ya wabunge wanaotuhumiwa kwa ujangili na kuhujumu OUT akitaka kamati iwataje ndani ya Bunge.
“Bungeni kazi yetu, sisi Wabunge ni kuisimamia Serikali kwa hiyo wale wabunge waliotajwa kwenye ripoti watajwe ili nao wawajibike ili Bunge letu liwe na nia thabiti ya kuisimamia Serikali,” alisema Mbatia.
Wabunge waliochafua zaidi hali ya hewa kutokana na michango yao ya hisia kali dhidi ya Pinda ni Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), na Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.
Lugola alisema makosa ya operesheni hiyo yalianza mapema wakati operesheni ya kijeshi ilipopelekwa kwa raia na kusema; “Hainiingii akilini kwamba aliyekuwa ana command (kutoa amri) ni mwanajeshi.”  “Wakati operesheni hii ikitokea wanawake wanabakwa na watu wawili…Watu wameteswa, mwanaume mwenzetu amelazimishwa kufanya mapenzi na mti Waziri Mkuu ulikuwa wapi haya yakitokea..?” alihoji.
Lugola aliongeza; ”Kwa utaratibu wa nchi yetu tumekupa kila aina ya usafiri kuanzia helikopta, ving’ora kila wakati vinalia ulikuwa wapi Waziri Mkuu wakati mambo haya machafu yanatokea..?” alihoji tena.
Alisema Vuai hawezi kupona katika suala hilo kwa kuwa wanajeshi ndiyo waliobaka, kuua na kujeruhi na ndiyo walioua mifugo kwa risasi na kwamba atapona katika Bunge hilo mbele ya haki hatapona. Vivyo hivyo alisema Dk Nchimbi hawezi kupona katika kashfa hiyo kwa vile askari polisi ndiyo walioua, kubaka, kuwapa watu vile na kuua mifugo akisema; ”Utaponea wapi Dk Nchimbi..?”
Lugola alisema pamoja na ripoti ya kamati kumnukuu Kagasheki akidai alinyang’anywa mamlaka yote katika utekelezaji wa OTU, akihoji ni waziri wa namna gani aendelee kukalia kiti cha uwaziri.
“Nimeisoma ripoti hii hakuna mahali Dk Mathayo alipohusika anataka kutolewa kafara… Mifugo yake imeuliwa hahusiki na sera yeye anahusika na wafugaji waliouawa pamoja na mifugo,” alisema Lugola.
Hata hivyo Lugola alisema Dk Mathayo anahusika na uzembe kwa kuwa wafugaji imeuawa, mifugo imeuawa na kuhoji waziri huyo alikuwa wapi wakati hayo yakitokea ndani ya Tanganyika au Zanzibar (Tanzania).
“Naendelea kumshauri Rais kama tunaitakia mema nchi hii na kama tunataka CCM kiendelee kuaminiwa na Watanganyika na Wazanzibari, Rais amfukuze Waziri Mkuu mara moja,” alisisitiza mbunge huyo.
Aliongeza kusema; “vv       Mawaziri wake hao hawawezi kukwepa hili, watu wanachukua ‘political responsibility’ kwani Maige (Ezekiel) alichukua Twiga porini..?” alihoji na kuongeza kusema;
“Kama tunataka tuwe na Bunge lenye viwango, Bunge lisilokuwa na ‘double standard’ (upendeleo) na nyinyi watu wameua watu na nyinyi lazima muondoke ndiyo tutajenga heshima ya nchi hii,” alisema.
Lugola alenda mbali na kusema endapo Rais atashindwa kumfukuza Pinda katika wadhifa wake huo, yeye atakuwa wa kwanza kupeleka hoja bungeni ili wabunge wapige kura ya kumng’oa Waziri Mkuu.
Kwa upande wake, Msigwa alisema wabunge wanapopendekeza Waziri Mkuu aachie ngazi hawana chuki naye, lakini kwa madudu yaliyotokea chini ya usimamizi wake ni lazima awajibike.
“Na kama mnatuheshimu, mheshimiwa Waziri Mkuu ungekuwa unatayarisha makaratasi saa hizi unaandika barua za kujiuzulu, tukufanyie sherehe ya kukuaga na nyie wa chini yake mfuate,” alisema. Msigwa alienda mbali zaidi na kumnyooshea kidole Vuai kwamba ana rekodi mbaya kuanzia huko kwao nchini Zanzibar na kwamba dhambi ya damu ya mauaji ya raia huko Pemba inamlilia na kumfuata hadi kwetu Tanganyika.
“Hata sisi tunasema hamkuhusika ‘direct’ (moja kwa moja) lakini hapa tunazungumzia uhai wa watu na watu waliokufa siyo wanachama wa CCM wala wa vyama vya upinzani…Tutangulize utaifa,” alisema.
Mbunge huyo alisema siku zote cheo ni dhamana na kwamba wasingependa Chadema itakapochukua nchi iwapeleke mawaziri hao Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, iliyopo The Heague nchini Uholanzi, kwa kuwa hawatapona.
Lekule ndiye aliyepigilia msumari wa mwisho aliposema endapo Bunge litamaliza mkutano wake huo bila kuwapo mawaziri watakaowajibika, basi Rais alivunje Bunge ili ufanyike uchaguzi mwingine

ALHAMDULILAHI OMAR MUSA MAKAME ACHIWA KWA DHAMANA BADO MASHEIKH WETU WA UAMSHO SASA

Mtuhumiwa wa Mauwaji ya  Padri Evaristus Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar Omar Musa Makame akitoka nje ya mahakama kuu ya Zanzibar baada ya kupewa dhamana.
MTUHUMIWA aliye singiziwa MAUWAJI YA PADRI EVARISTUS MUSHI WA KANISA KATOLIKI nchini ZANZIBAR OMAR MUSA MAKAME AKITOKA NJE YA MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR BAADA YA KUPEWA DHAMANA.
Mtuhumiwa aliyesingiziwa Mauwaji ya  Padri Evaristus Mushi wa Kanisa Katoliki nchini Zanzibar Omar Musa Makame amepewa dhamana  katika mahakama kuu ya nchi ya Zanzibar kutokana na kutokamilika kwa ushahidi wa kesi hiyo aliyo singiziwa.
Akitoa dhamana hiyo Jaji Mkuu Omar Othman Makungu amesema mtuhumiwa huyo amepewa masharti mawili; moja kuwa atalazimka kupata wadhamini wawili watakoandika bondi ya laki tano  kila mmoja wakiwa na vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi (ZAN ID).
Na sharti la pili ni kuwa na barua ya sheha na kuripoti katika Mahakama mbele ya Mrajis Mkuu kila siku ya Jumatatu.
Mapema mwendesha mashitaka wa serikali, Abdalla Issa Mgongo alidai mahkamani hapo kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo kesi hiyo ipangiwe siku nyengine kwa kutajwa.
Nae kwa  upande wake Wakili anayesimamia kesi hiyo, Abdalla Juma aliomba Mahakama hiyo kuwa muda  umeshakuwa ni mwingi na  ushahidi bado haujakamilika hivyo ni vyema kesi hiyo kufutwa ikiwa haikuwezekana basi mtuhumiwa apatiwe dhana.
Kwa kuwa muda umeshakuwa mwingi na ushahidi hadi hii leo haujapatikana basi kesi ifutwe au Mtuhumiwa apewe dhama”alisema Wakili huyo Mahakamani hapo.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali Issa Mgongo alipingana na ombi hilo la kutaka kesi ifutwe na kusema ombi hilo hakubaliani lililotolewa na Wakili wa upande wa Mtuhumiwa.
Alisema ombi la pili lifanyiwe kazi likizingatiwa  masharti yatakayokubaliwa na mahakama.
Mtuhumiwa Omar Musa Makame  amesingiziwa kumpiga risasi na kumuua Padre Mushi Februari 17 mwaka huu.Omar Musa Makame Alitiwa mbaroni na Polisi Machi 17 mwaka huu ili kutiwa adamu kwa yale aliyo yasema katika mdahalo hii ilikuwa ni adabu tu.

TANGAZO MUHIMU SANA TUNASIKITIKA KUWA SHIRAZI ABEID JUMA AMEFARIKI DUNIA AFRIKA YA KUSINI YOYOTE ANAYEJUWA FAMILIA YAKE AIGHARIFU TAFADHALI

picha jumaa abeid
  • Jamaa au mtu anaemfahamu marehemu tafadhali wasiliana na Abdallah Hussein +27 71 216 8505
  • unnamed (62)
  • Watanganyika na Wazanzibari waishio Johannesburg wanawatafuta ndugu, rafiki au jamaa wa Shiraz Abeid Juma (pichani), ambaye sasa ni marehemu. Shiraz alifariki wiki hii na kuzikwa siku ya Jumanne huko Johannesburg, Afrika ya Kusini.
    Marehemu alifika Afrika Kusini akitokea eneo la Mpendae nchini Zanzibar kama nyaraka alizoacha zinavyoonyesha. Namba za simu zilizokuwa kwenye vitabu vya marehemu hazipatikani. Kwa yoyote mwenye kumfahamu marehemu, tafadhali wasiliana na Abdallah Hussein +27 71 216 8505

Friday, December 20, 2013

DULA HUSSENI NI MZANZIBARI KWELI AU NI CHOGO LILILO TUMWA KUJA KUHARIBU MDAHALO WA KUMBUKUMBU YA UHURU WA ZANZIBAR!!!


WATU WANASEMA KUWA WAO SIO WAZANZIBARI JAPOKUWA WAMEZALIWA ZANZIBAR LAKINI SIO WAZANZIBARI SAWA TUMEFAHAMIYANA VIZURI SAANAAAA

IWEJE BASI HAWA WAWE WAZANZIBARI..??NA WENGI WAO HAWA HAWAKUZALIWA HASWA HAPA ZANZIBAR WALIKUJA MIGONGONI MWA MAMA ZAO WAKITOKEA NYASA NA TANGANYIKA AU WALILETWA TU KUJA KUTAWALA KWA NGUVU ZA MASULTANI WAKITANGANYIKA WAKOLONI WEUSI NI VIPI WAO WAWE WAZANZIBARI NA WALIO ZALIWA HAPA WASIWE WAZANZIBARI....?
DULA HUSSENI NI MZANZIBARI KWELI AU NI CHOGO LILILO TUMWA KUJA KUHARIBU MDAHALO WA KUMBUKUMBU YA UHURU WA ZANZIBAR!!!
Siku ya tarehe 14 Disemba, kule Forest Gate jijini London Uingereza, kulifanyika mdahalo wa kihistoria kuhusu kumbukumbu ya Uhuru wa Zanzibar wa Disemba 10 mwaka 1963. Mdahalo huu uliandaliwa kwa hisani kubwa ya jumuiya ya MUWAZA ikishirikiana na Wazanzibari walio wengi wanaoishi hapa Uingereza, hasa hasa Wazanzibari wanaoishi London.
Mdahalo huu ni miongoni mwa harakati chache za Wazanzibari wenye uchungu na nchi yao kutaka kudumisha na kuilinda historia ya nchi yao ambayo inaelekea kufifia katika siku za hivi karibuni. Itambulike kwamba, Zanzibar ilikuwa chini ya Utawala wa Waarabu wa Oman kuanzia miaka ya 1840 pia ikiwa himaya ya Uingereza hadi Disemba 10 mwaka 1963 nchi hiyo ilipopata Uhuru. Uhuru ambao si wengi kati ya wananchi na vizazi vipya kuutambuwa ipasavyo.
Kuna sababu lukuki zinazofanya tukio la uhuru wa Zanzibar liwe halitambulikani kama inavyotegemewa. Katika nchi zote zilizotawaliwa, siku ya uhuru ndio sikukuu pekee inayowaunganisha wananchi wa aila zote na imani zote bila kuwagawa. Kama hili ni kweli, Zanzibar haimo katika nchi za aina hii kwa sababu ni nchi pekee ambayo haisherehekei uhuru wake na badala yake, inasherehekea Mapinduzi ya mwaka 1964 siku ambayo ilitakiwa kuwa siku ya majuzi maana wazanzibari wengi waliuliwa na machogo.
Uhuru na Mauwaji ya Wazanzibari (mapinduzi) kwa Zanzibar zimekuwa ni dhana mbili kuu ambazo zinaichanganya historia, akili na hata fikira za watu mbali mbali hapa nyumbani na nje ya nchi. Kuna wanaoamini kuwa Zanzibar ilipata uhuru mwaka 1963 – hawa ndio akina MUWAZA na wengineo wenye imani na msimamo kama huu. Kuna wanaoamini kuwa Zanzibar haikuwahi kupata Uhuru na kama ilipata ulikuwa uhuru JINA au uhuru wa Bandia na sio hata wa Bendera. Kundi hili ndio lile akina Dula Husseni,Borafya,Shein,Ali Vuai N.K. – Kijana ambaye alitoa maoni makali na yenye kutafautiana na karibu wote waliohudhuria mdahalo pale Forest Gate siku ile. Hali ambayo ilimfanya aonekane mtu wa ajabu ijapokuwa maoni yake yalipasa kusikilizwa na kuthaminiwa kwa upande mwengine. Vyoyote iwavyo, dhana hizi mbili- Uhuru na Mauwaji ya Wazanzibari (Mapinduzi) ndio mpaka hapa zinaunda kambi mbili ambazo kiutafiti na kiuhalisia ndio hasa zinazowakilisha jamii ya watu wa Zanzibar walio nje na ndani ya nchi yao. Ukweli ni kwamba, ndani ya Zanzibar wako akina MUWAZA wengi na wako akina Dula Hussein idadi chekea.
Nimelazimika kumtaja Dula Husseni katika hafla ile nzima kwa sababu alikuwa mtu wa aina yake. Mtu wa kipekee yaani ‘Unique’ katika mdahalo ule pale Forest Gate siku ile. Upekee wa Dula Hussein umekuja kwa sababu ya misimamo yake iliyotafautiana na wajumbe wengine wote waliokuwepo pale. Misimamo ambayo haikuwa matarajio ya Wazanzibari wengi kumsikia Mzanzibar mwenzao halisi akiweza kuitowa mitazamo yake ile hadharani kiasi kile.
Msimamo wa MUWAZA ulikuwa ni wa kuutambuwa na kuuenzi uhuru wa Zanzibar wa Disemba 10 mwaka 1963. Msimamo huu hautowi nafasi ya Mauwaji ya Wazanzibari (Mapinduzi) ya Zamzibar ya mwaka 1964 kuwa ndio jiwe la msingi la kuianzia historia ya Zanzibar huru kwani kimsingi, MUWAZA inaamini kwamba, Mapinduzi hayafanyiki kwenye nchi isiyokuwa huru. Huu ndio mtazamo na hoja ya wale wasioamini mapinduzi kuwa ndio tukio muhimu la Uhuru wa Zanzibar. Kwa mtazamo kama huu, tunafahamu kwamba hakuna Mapinduzi bila ya Uhuru. Na hapa ndio MUWAZA iliposimamia hoja zake na Wazanzibari wengi kwa Ujumla.
Tukigeuza upande wa pili wa shilingi, tunaona sura ya Dula Husseni na kaumu yake. Yaani wafuasi wake wenye msimamo na mitazamo kama yake. Kwa maoni ya Dula Husseni, Wazanzibari waafrika kwa fikra zake – yaani watu weusi wenyeji wa Zanzibar hawapaswi kujivunia Uhuru wa mwaka 1963 kwani haukuwa uhuru kweli. Haukuwa Uhuru uliomkomboa mtu mweusi kwa thana zao.Ndio wakaja na Mkulima na mkwezi. Dula anaendelea kwa kusema kwamba utasemaje Zanzibar imepata uhuru wakati bado kuna Sultani juu ya kiti..?? Tena Sultani wenyewe wa Omani ingawa amezaliwa Zanzibar yeye na baba yake. Uzawa huo haumfanyi yeye awe Mzanzibari. Kwa maana hiyo, Uhuru wa mwaka 1963 haukuwa uhuru bali ulikuwa changa la macho tu kwa Wazanzibari kwani hatamu ya utawala bado ilikuwa kwa Muarabu. Kwa maana hiyo, Dula Husseni anadai kwamba wanaoshangiria na kuutukuza Uhuru wa Zanzibar wa mwaka 1963, ni vibaraka wa Ukoloni wa Kiarabu wasiomtakia mema Mzanzibari ambaye ni mkulima na mkwezi. Kwa mantiki hii, Dula Hussein anayatmbuwa rasmi mapinduzi ya mwaka 1964 kuwa ndiyo hasa yaliyomkombowa Mzanzibari mweusi, dhidi ya makucha ya mkoloni Mzungu na Muarabu. Kwa mantiki hii hakuna Uhuru wa Zanzibar hoja ambayo inaleta dhana nyengine ya kuyafanya mapinduzi ya Zanzibar kuwa ndio Uhuru wenyewe pia. Kwa lugha nyepesi hapa Mapinduzi ni Uhuru na dhana hizo zinaweza kutenganishwa iwapo hali isiyohusiana na hii ya Zanzibar inahusika. Kinyume na hapo, dhana hizi mbili haziwezi kutenganishika.
Naam! Baada ya kutowa hoja hizi zilizochafuwa hali ya hewa katika ukumbi ule uliojaa wafuasi wa MUWAZA wenye kuamini Uhuru wa mwaka 1963, Dula Husseni aliamsha hisia kali na maoni yenye kuagawika pale ukumbini. Kikubwa kilichojitokeza pale ni kumuona Dula kama ni mtu aliyepotoka na kupotosha ukweli lakini ukweli unabaki kuwa aliyoyasema yana Ukweli mkubwa ndani yake, na kwa upande mwengine, wanayodai MUWAZA yana ukweli pia. Tushike lipi..?? Kwa mimi nitaanza hapo paa Mzee Karume yeye hakuzaliwa Zanzibar kabisa dula unatuambiyaje hapo..? John Okello aliyeyaongoza mapinduzi ya kuwauwa Wazanzibari ni mganda dula unatuambiyaje..? ikiwa dula anasema kuwa uhuru wa 1963 ni wa bandiya na wa 1964 ni wa haki kwakuwa aliyekalia kiti alikuwa ni mfalme ok je ni kwa nini ASP ilishiriki katika mkutano wa kudai uhuru wa 1963 kule london..? je ni kwa nini wasipinduwe wakati bado Mgereza alikuwa akitawala..? je ni kwa nini baada ya mapinduzi tu ya zanzibar hao walio itwa ndio wazanzibari walio pinduwa walianza kuuwana wenywe kwa wenyewe..? dula je zanzibar sasa wewe unaona iko huru chini ya mkoloni mweusi Tanganyika..? Dula tunakuliza kusema kwamba Zanzibar imepata uhuru1964 wakati bado kuna Sultani wa kitanganyika juu ya kiti na amri zote zinatoka Dodoma..?? Je baba yake Mzee karume na Mzee karume waamezaliwa Zanzibar...?? babu yake Ali hassan Mwinyi na baba yake Ali Hassan Mwinyi wamezaliwa Zanzibar...?? Pima, fikiria na amuwa! Tumia haki yako ya kujieleza na kutowa maoni bila Kumnyooshea kidole mwengine.

Maasalaam!

Wednesday, December 18, 2013

NCHINI TANGANYIKA WATOTO WA MITAA(MACHANGU DUWA) WAZIDI WENGI WAO WALAWITIWA ILI WAPEWE CHAKULA NA PAHALA PA KULALA


Watoto kulawitiwa ili wapate hifadhi ya kulala au kupewa chakula kizuri ni sehemu ya maisha ya baadhi ya watoto waishio nchini Tanganyika mitaani mjini Sumbawanga mkoani Rukwa nchini Tanganyika.
Hii ni siri kubwa ambayo imejificha miongoni mwao, ili uweze kupata siri hii inakulazimu lazima ujenge uhusiano wa karibu na wa muda mrefu na watoto hao.
Watuhumiwa wakubwa wa kuwaingilia kinyume na maumbile watoto hao ni baadhi ya walinzi wanaolinda katika maduka ya biashara na vijana waliowazidi umri; vitendo hivyo vinaonekana  kushika kasi.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na Mwandishi wa makala haya kwa miezi kadhaa, umebaini kuwa vitendo vichafu vimesababisha baadhi yao kuathirika kisaikolojia hivyo kujikuta wakiona jambo hilo ni la kawaida na hulifurahia.
Watoto hao hufanyiwa vitendo hivyo hasa kipindi cha masika ambapo mvua huwa zinanyesha, maeneo ambayo hupendelea kulala nyakati hizo kwenye majumba ambayo ujenzi wake haujamalizika (Mapagala) huwa yanavuja maji ya mvua hivyo hulazimika kuzikimbia kujisalimisha popote.
Baadhi ya watoto wa mitaani waliozungumza na mwandishi walikiri kwamba ni kweli kuna tabia hiyo lakini ni kwa usiri mkubwa kwani iwapo itabainika mtu anamlawiti mtoto mwenzao huwa wanapambana naye.
“Unajua sisi tunawasaidia walinzi katika malindo yao nyakati za usiku, tulishakubaliana kama kuna mwenzetu analawitiwa na anakubali tutamtenga.
Wapo watoto wawili tayari tumewatenga katika kundi letu kwa tabia ya kupenda kulawitiwa, sasa kama wapo wengine tukiwafahamu nao tunawatenga hata wakipata matatizo hatuwezi kuwasaidia” mtoto mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jose (jina kapuni).
Naye mtoto aitwaye paul anasema kuwa kinachowaponza watoto wengine ni tamaa na sio hifadhi ya kulala pekee kwani wapo watoto ambao wamezitoroka familia zao kwa kisingizio cha ugumu wa maisha na kukimbilia mitaani kufanya kazi ya kuombaomba ambapo wamekuwa wakidanganyika kwa vyakula kama Chips na pombe katika baa za usiku.
“Sisi wengine tupo huku mitaani kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kipato duni cha familia zetu, malezi mabaya kama vile kulelewa na kina mama wa kambo ambao ni chanzo matatizo kwa sehemu kubwa lakini sio sababu ya kukubali kulawitiwa.
Ila wapo wale wanaopenda pombe na chips ndio wanajikuta wakishawishiwa na sio tu na walinzi lakini pia hata baadhi ya watu ambao hutumia kisingizio cha ulevi wa pombe ili kufanya vitendo hivyo,” anasema mtoto Maiko (jina kapuni). 
Baadhi ya walinzi  walihojiwa kwa nyakati tofauti na mwandishi wa makala haya walikiri kwamba wapo wenzao wamekuwa na tabia ya kuwaingilia kinyume cha maumbile watoto hao.
“Ni kweli wapo wenzetu wana tabia hii hasa mtaaa wa Nyerere road (barabara ya kuelekea mkoani) na kuna tukio la mauaji liliwahi kutokea ambapo kuna mtu alikuwa mlinzi anamlawiti mtoto usiku wa manane akamshushia kipigo hadi kumsabishia kifo” anasema mlinzi mmoja anayelinda mtaa wa Kiwelu ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.
Hata hivyo, mlinzi aliyejitambulisha kwa jina moja la Peter alisema kwamba yeye binafsi hajawahi kusikia kama kuna baadhi ya walinzi wanafanya vitendo hivyo na watoto ila anachofahamu ni walinzi kuwahifadhi watoto hao kwa kuwapa eneo la kulala kwenye vibaraza vya maduka wanayolinda hali ambayo huwasaidia pia kiulinzi.
Afisa maendeleo ya Jamii Manispaa ya Sumbawanga, James Biseko anasema hivi sasa manispaa hiyo ina watoto wa mitaani 6872 ambapo kati ya hao 3268 ni wavulana na wasichana ni 3604 takwimu zilizopatikana baada ya utafiti uliofanywa kati ya uongozi Manispaa hiyo na Shirika la Pact - Tanganyika.
Shirika hilo lilishirikiana na Manispaa hiyo kutafuta takwimu hizo wakati wakianza kutekeleza mradi wa pamoja tuwalee unaolenga kumtaka mwana jamii  kutunza na kusaidia watoto hao.
Aidha, uchunguzi wa kina uliofanywa na mwandishi mjini Sumbawanga, umebaini kuwa ongezeko la watoto wa mitaani ni kubwa na linasababishwa na hali ya umasikini wa kipato unaozikabili familia nyingi.
 Hali hiyo inawalazimu wazazi kuzikimbia familia zao hivyo watoto kulelewa na kina bibi wasio na uwezo kiuchumi na kuwatumia watoto hao kama sehemu ya kujipatia kipato cha siku kwa kupita  mitaani kuomba fedha.
Anaeleza kuwa baada ya watoto hao kuzoea maisha ya kuomba mitaani hulazimika kutorudi kwa walezi wao (bibi) zao, hivyo hubaki mijini wakiendelea na maisha ya kuomba omba.
Anaeleza kwamba sababu nyingine ni migogoro ya kifamilia na malezi ya wazazi wa kambo.Pia  tamaa ya baadhi ya watoto kupenda kukimbilia mjini wakifikiri maisha ni rahisi.
Kwa upande wake, Deo Mlwafi ambaye ni mratibu wa mradi wa pamoja - unaotekelezwa na Pact - Tanganyika kwa kushirikiana na Shideph+  Mkoa wa Rukwa anasema kuwa wao jukumu ni kuijengea uwezo jamii kupitia kamati za mitaa ili kamati hizo ziweze kuwasaidia watoto hao.  Kuhusu Maambukizi ya ukimwi.
Makamu mwenyekiti wa Shidepha+ taifa, Godfrey Mwikala anaeleza kuwa watoto hao wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya Ukimwi kwa kuwa wamekuwa wakishiriki ngono isiyo salama.
 “Si watoto wa kike wala wa kiume wote wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kuwa wanashiriki ngono zembe, hawana elimu yoyote.
Nafikiri ipo haja ya kuwepo kwa mradi mwingine ya kuwafikia moja kwa moja watoto hawa kuwahifadhi katika vituo maalumu, kuelimisha kuhusu athari ngono zembe, kuwapima afya ili kuona namna ya kuwasaidia maana mradi wa Pact - Tanganyika unalenga kuwaisaidia lakini kupitia ngazi ya jamii tu” anasema
Serikali ya Tanganyika kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto imekuwa na mipango na mikakati ya kuhakikisha kwamba watoto  wote wanastawi na kuwa na maisha bora kutokana na kupatikana kwa haki zao za msingi ambazo ni kuishi, kuendelezwa, kulindwa na kushiriki katika mambo yanayowahusu bila ubaguzi wa hali yoyote.
Hiyo ni sehemu ya mipango na mikakati ya Serikali ya Tanganyika ambayo ipo kwenye maandishi, pasipo utekelezaji wa aina yoyote ile ndio maana ongezeko la watoto wa mitaani ni kubwa, na hakuna wenye kuchukua hatua si Serikali kuu ya Tanganyika,si za mikoa wala wilaya huku taasisi  zisizo za kiserikali zilizoanzishwa kwa ajili ya kusaidia kupunguza tatizo hilo zimekuwa zikiishia kujinufaisha zenyewe na kujitajirisha.
Baadhi ya wananchi wanashauri Serikali ya Tanganyika kushirikiana na familia ili kuhakikisha wanakuwa na maisha bora, tofauti na ilivyo sasa, kwani kuna idadi kubwa ya watoto wa mitaani.
Mkazi wa Sumbawanga, Julian Francis anasema wakati umefika kwa Serikali kuwa na mkakati thabiti katika kutokomeza vitendo hivyo vichafu; polisi wanatakiwa kufuatilia hilo.