Wednesday, January 30, 2013

WANAUME WA MTWARA MWEZI MOJA TU SEREKALI YA TANGANYIKA IMEKUBALI MAOMBI YAO NA GESI HAIKUTOKA MTWARA.WANAUME WAZENJI TUMEBAKI KUCHEZA MDUWARA,LELE MAMA,KIBAO KATA,TAARAB,SUMSUMIA,KANGA MOKO KILA KUKICHA NCHI INAFANYWA KIJIJI CHA TANGANYIKA TUSUBIRI MAFUTA YATACHIMBWA NA PAIPU ZITAPELEKWA DAR WAZENJI TUNAKULA UROJO.


WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amefanikiwa kutuliza jazba za wakazi wa Mkoa wa Mtwara baada ya kueleza jinsi watakavyonufaika na gesi itakayozalishwa mkoani humo kabla ya kusafirishwa kwa bomba hadi Dar es Salaam.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia amewaomba radhi wananchi wa mkoa huo kutokana na kauli Desemba 21, mwaka jana akiwakebehi baada ya kumwomba apokee maandamano yao ya kupinga mpango wa kusafirisha gesi hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa majumuisho uliofanyika jana baada ya kusikiliza madai ya wananchi hao kwa siku mbili mfululizo, Pinda alisema hakuna tone la gesi ghafi itakayosafirisha kwa njia ya bomba na kusema kiwanda cha kusindika gesi ghafi kitajengwa katika Kijiji cha Madimba, mkoani humo ili mabaki yatokanayo na gesi hiyo yatumike kuvutia uwekezaji wa viwanda.

“Wataalamu wanasema gesi haiwezi kwa namna yoyote ile kusafirishwa kama ilivyo, lazima ibadilishwe kuwa hewa au barafu… kiwanda cha kusafisha gesi kitajengwa Madimba. Gesi yote itakayotoka Mnazi Bay itasafishwa hapo na masalia yote yatabaki huku ili kuvutia viwanda vya mbolea na vingine vinavyotumia malighafi hizo,” alisema Pinda na kuongeza:

“Kama tungekuwa tunasafirisha gesi ghafi basi hata kiwanda cha Dangote kisingejengwa hapa… gesi itakayopelekwa Dar es Salaam ni ile iliyosafishwa kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme… tusaidieni wenzetu kuliokoa Taifa na tatizo la umeme.”

“Gesi lazima isindikwe Mtwara, haitoki hadi viwanda vije… nadhani hili ni jambo jema lazima tuliwekee utaratibu. Nikawauliza wataalamu wangu kwani kiwanda cha kusafisha gesi kinajengwa wapi, wakanijibu Madimba… nikasema kumbe tatizo kubwa ni kutowaeleza vya kutosha wananchi suala la gesi.” alisema Waziri Mkuu huku akipigiwa makofi... “Nafikiri tatizo ni sisi Serikali hatukuwa na mpango mzuri wa kuwaelimisha wananchi.”

Awali, madai ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara yalikuwa ku pinga usafirishaji wa gesi ghafi kwenda Dar es Salaam wakieleza kuwa mpango huo utafukuza uwekezaji wa viwanda mkoani humo ambao ungechochewa na upatikanaji wa malighafi baada ya kusafishwa kwa gesi.

Pia wananchi walipinga ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme Kinyerezi, Dar es Salaam wakiitaka Serikali kujenga mitambo hiyo mkoani Mtwara.

Alitoa wito kwa wabunge wa Mkoa wa Mtwara kufuta tofauti zao za kisiasa ili waweze kuharakisha maendeleo ya mkoa huo... “Purukushani hizi ndani ya chama hazina tija, tuseme basi… wabunge hawaelewani, sasa bungeni wanakwendaje... kila mtu na lake … hebu tuseme watu kwanza mimi badaaye,” alisema Pinda huku akishangiliwa.

Katika siku hizo mbili mkoani Mtwara, Waziri Mkuu alikutana na viongozi wa vyama vya siasa, dini, wafanyabiashara, madiwani na wenyeviti wa mitaa na wanaharakati mbalimbali.
RC aomba radhi
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa, Simbakalia aliwaomba radhi wakazi wa Mkoa wa Mtwara akisema alipotoka kuwaita wananchi hao wapuuzi na baadaye wahaini kauli ambazo ziliwaudhi wengi

“Kupitia hadhara hii nawaomba radhi kwa kuwakwaza, nimesikitishwa kwa kauli yangu ambayo imepokewa kwa hisia kwamba niliwadharau,” alisema Simbakalia.

Baadaye Waziri Mkuu aliwasihi wananchi wa Mtwara kumsamehe Mkuu wao wa Mkoa wa Mtwara kwa kauli hiyo aliyoitoa 21 Desemba, mwaka jana katika kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa, (RCC), pale alipoombwa kuyapokea maandamano ya wakazi wa mkoa huo Desemba, 27, mwaka jana
“Binadamu kukosea lazima, lakini kubwa zaidi ni kuomba msamaha… amefanya hivyo, sasa tusahau yaliyopita tugange yajayo,” alisema Pinda.
Mawaziri wazungumza
Akizungumzia hali ya usalama mkoani huo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi alisema wizara yake imejipanga vyema kukabiliana na vurugu zozote zitakazojitokeza kuanza sasa.. “Hali ni shwari, tumejipanga vya kutosha kwa watu na vifaa.”

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa alisema wizara yake imeamua kuifanya Veta Mtwara kuwa kituo cha umahiri ili wahitimu wake waweze kuajiriwa katika sekta ya gesi huku Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka akisema wizara yake imekamilisha mipango miji kwa Mji wa Mtwara uendane na mabadiliko ya kiuchumi.

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alisema Bandari ya Mtwara haijauzwa na kwamba inapanuliwa ili iweze kukidhi mahitaji ya baadaye huku akiahidi kufika Mtwara kila baada ya miezi mitatu ili kutoa taarifa ya maendeleo ya bandari na uwanja wa ndege kwa wananchi.

“Tulikuwa na eneo la hekta 70 tu za Bandari ya Mtwara, sasa tumepanua na tunazo hekta 2,994. Tumetenga hekta 110 ili tuweze kuwa na bandari huru itakayowezesha kuongezeka kwa matumizi,” alisema Dk. Mwakyembe.

Wenyeji waridhika
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vyama tisa vya siasa mkoani Mtwara, Uledi Abdallah alisema madai ya wananchi yalikuwa mitambo ya kusafisha gesi ghafi ijengwe Mtwara na kwamba iwapo Serikali imeamua kufanya hivyo madai yao yatakuwa yamekwisha.


“Kama gesi itakayosafirishwa kwenda Dar es Salaam ni ile iliyosafishwa, sisi hatuna tatizo,” alisema Abdallah
Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji alimpongeza Waziri Mkuu kwa hatua yake ya kuwasikiliza wananchi na kwamba mzozo huo uliodumu kwa takriban mwezi mmoja sasa umefikia tamati.


Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Mtwara Mjini, Saidi Kulaga alimpongeza Waziri Mkuu kwa hatua aliyoichukua na kumwomba awaachie huru wale waliokamatwa kutokana na vurugu zilizotokea Mtwara na Masasi ili kujenga mwanzo mpya wa uhusiano baina ya Serikali na wananchi, ombi ambalo Pinda alilipokea na kuahidi kulifanyia kazi ndani ya wiki mbili.

Wataalamu wa gesi
Awali, kutokana na vurugu hizo, zaidi ya wataalamu 50 waliokuwa mkoani Mtwara kwa ajili ya kusimamia mradi wa ujenzi wa bomba la gesi waliondolewa mkoani humo,FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI tumebaini.
Taarifa zilizotufikia jana zilieleza kuwa watalaamu hao wapo Dar es Salaam tangu Jumamosi iliyopita na wamefikia katika Hoteli ya JB Belmont kupisha vurugu za wananchi waliokuwa wakipinga ujenzi wa bomba hilo kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam.


Mmoja wa viongozi wa hoteli hiyo, ambaye alikataa kutaja jina lake kwa maelezo kuwa si msemaji alikiri kuwapo kwa watalaamu hao katika hoteli hiyo… “Wapo ila walisema kuwa hawataki kuzungumza na vyombo vya habari.”

Bunge laingilia kati
Spika wa Bunge, Anna Makinda ameunda kamati itakayokwenda Mtwara kuzungumza na kada mbalimbali kuhusu vurugu na mustakabali mzima wa gesi.


Makinda alisema hayo jana muda mfupi kabla ya kuahirisha kikao cha kwanza katika Mkutano wa 10 wa Bunge… “Bunge ni chombo cha amani, tutawatuma wabunge kwenda kuzungumza nao…suala hili linahitaji busara sana.”

JE WAZANZIBARI MAFUTA YETU MBONA MPAKA LEO HAYAJAONDOLEWA KATIKA MUUNGANO..? WALIO SHIKWA KWA MUDA WIKI MBILI WATACHIWA WOTE MBONA MPAKA LEO MASHEIKH WAMEGANDA KINUWA MIGUU NA HAWANA HATIA YOYOTE..? MBONA MPAKA LEO TANGANYIKA HAITAKA KUTOWA KARATASI YA MAKUBALIANO YA MUUNGANO..? MZANZIBARI ZINDUKA HATUNA NCHI TUNATAWALIWA NA WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA KINASHEIN NA MAALIM SEIF NA WENGINE WAMEWEKWA HAPO GERASHA TU TUONE TUNA NCHI LAKINI HATUNA NCHI.

Sunday, January 27, 2013

WATU WA MTWARA WAWAFUNDISHA WAZANZIBARI JINSI YA KUDAI HAKI YAKO KUTOKA KWA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.


Moja ya ikiteketea wakati wa vurugu mkoani Mtwara ambapo magari katha, pikipiki  viliteketezwa kwa moto  vyote vikiwa ni mali za halmashauri ya Masasi na baadhi ni vya watumishi wa halmashauri hiyo iliyo zowea kuwakandamiza watu wa mtwara na kuifaidisha mitumbo ya viongozi wa serekali ya kitanganyika isiyokuwa na imana na rai wake.

magari yakiendelea kuteketea kwa moto.

Hili ndio jengo la Mahakama ya madhalim walio zowea kuthulumu watu wa mtwara lililochomwa moto.
 
Nyumba inayosemekani ni nyumba ya waziri ikiwa nayo pia imeshughulikiwa vizuri sana maana wao mawaziri wamewekwa kutumikia watu lakini wangalie wao wanavyo ishi na familia zao na watu wanavyo lala na njaa kila siku na wao hata hawajali wanasubiri siku za changuzi tu ndio utawaona basi hii ndio hali muache nayeye aone utamu wa kuharibikiwa safi sana mtwara.
 
Nyumba inayosemekana ni ya Mwenyekiti wa CCM baada ya kushughulikiwa pia vizuri na watu wa mtwara huyu ni mwenyekiti tu wa CCM angalia nyumba yake huku watu chumba kimoja wanalala familia nzima baba na mke na watutu wanafika sita au kumi wote chumba kimoja tena cha kumpangisha lakini mwenyekiti wa CCM anaikulu yake mwenyewe.

makaburu weusi wakiendele kuwashika rai wema wanaotetea gesi yao ya mtwara isisafirishwe kwenda dar kushibisha matumba ya viongozi waroho wasio shiba juju wa majuju.

hapo hapo watu wa mtwara mpaka kieleweke

hakuna cha hivi wala vile gesi ni ya mtwara kila kitu kifanywe mtwara washazowe kunyonya rai kisha wanasinzia dodoma katijumba lao la ufisadi

IKIWA MTWARA WAKO TAYARI KUANZISHA VITA ILI GESI YAO ISITOKE MTWARA BASI WAZANZIBAR NI HALALI ZAIDI KWA MAANA WAO NI NCHI HASWAAAAWahenga walisema ‘adhabu ya kaburi aijuae ni maiti’. Dunia imewahi kuishuhudia Tanganyika ikipambana vikali na Uganda katika mwaka 1979 kwa madai ya kuvamiwa na sehemu ya nchi yake katika Mkoa wa Kagera kukaliwa kwa mabavu na Iddi Amin. Halkadhalika dunia imewahi kushuhudia mara kadhaa Tanganyika ikikwaruzana na jirani yake mwengine, Malawi, kwa madai kwamba eneo lake la ziwa Nyasa limevamiwa na nchi hiyo. Halkadhalika tumewahi kushuhudia jamii mbali mbali za watanganyika wakiuwana na kuchinjana wenyewe kwa wenyewe kwa kugombania raslimali kadhaa, kila mmoja akidai kudhulumiwa. Hili limejitokeza wazi katika mapambano kadhaa ya kugomania raslimali ya ardhi, raslimali za madini na udini pia nk. Hivi sasa mapambano yamepambamoto katika raslimali ya gesi iliyoko katika Mkoa wa Mtwara na lazima tukumbuke kuwa mtwara imo ndani ya nchi ya Tanganyika.

Somo lililopo katika utangulizi hapo juu ni kwamba kumbe kila mmoja anathamini kitu chake na anakioniye uchungu na hataki kichezewe kabisa na kukiona ni bora kuliko cha mwenzake, na bila shaka yuko tayari kwa lolote lakini kitu chake hicho kisimtoke mikononi mwake. Hii ndio maana Tanganyika iliingia vitani na Uganda kuipigania Kagera na kutuchukuwa sisi wazanzibari kwenda kutulisha katika vita visivyo tuhusu, hii ndio maana Tanganyika imekua ikitishia mara kadhaa ikilazimika itaingia vitani na Malawi kulinusuru ziwa Nyasa. Halkadhalika hii ndio maana watanganyika wa jamii mbali mbali wamekua wakipigana wenyewe kwa wenyewe kama vile jamii za wafugaji dhidi ya wakulima. Wamekua wakipigana na wawekezaji katika maeneo yao kama vile mapambano ya wanavijiji dhidi wamiliki wa migodi. Hakadhalika wananchi wamekua wakipambana na serikali yao ya Kitanganyika kukataa maamuzi ambayo kwa mtazamo wa wananchi wa Tanganyika wanaona maeneo hayo ni kuibiwa raslimali zao na badala yake ni kwenda kuwanufaisha wengine. Mfano wa haya ndio kama yanayojiri hivi sasa katika Mkoa wa Mtwara. Wananchi wa Mtwara wanaendelea kupambana na serikali huku watu kadhaa wakipoteza roho zao alimradi tu wanahakikisha raslimali yao ya gesi haitoki ndani ya Mtwara na badala yake inabaki Mtwara na  inatumika kwa ajili ya maslahi na maendeleo ya watu wa Mtwara shabashiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.

Maelezo yote hapo juu yanaonyesha jinsi watanganyika walivyokua wamechachapaa kwa ushujaa kupambana na mataifa jirani ili kulinda maeneo ya nchi yasivamiwe. Pia maelezo hayo yanaonyesha jinsi watanganyika wenyewe kwa wenyewe (jamii moja na nyengine) wanavyopambana kwa ushujaa ili kulinda maslahi ya sehemu zao, ardhi zao au raslimali za jamii zao husika zisichukuliwe na wengine. Sasa basi iweje narudia tena iwe ni jambo dogo linaloonekana halina maana kwa wazanzibari kusimama kidete, kujanza munkari, mori na hamasa kupigania nchi yao iliyomezwa na kupokonywa mamlaka yake yote ya kiuchumi, kisiasa, kijamii,kiutamaduni na kiutawala....? Hivi ni mtu gani mwenye akili yake asiyefahamu kama gesi haina thamani mbele ya nchi nzima.......? Mbele ya utamaduni wa taifa zima..........? Mbele ya thamani ya watu wa taifa zima......?

Alipopambana Mzee Aboud Jumbe wakati ule wa Nyerere yaliitwa ni machafuko tu ya hali ya hewa Zanzibar ina bidi nicheke kwanza hahahahaha yaliyolengwa kuuhatarisha Muungano feki, machafuko ambayo yalihitaji kudhibitiwa kwa kufukuzwa Mzee Jumbe katika kiti cha urais wa Zanzibar. Alipopambana Maalim Seif na wenzake wakati ule wa Nyerere ulionekana ni uchochezi uliolengwa kuigawa CCM na kuuhatarisha Muungano feki, uchochezi ambao ulihitaji kudhibitiwa kwa kufukuzwa Maalim Seif na wenzake katika chama na katika nyadhifa za serikali pamoja na kufungwa jela.

Wana CUF walipoandamana mwaka 2001, pale Unguja na Pemba enzi ya Benjamin Mkapa kida la manyani kudai pamoja na mambo mengine mabadiliko ya katiba feki ya Tanganyika ili kutoa fursa ya muungano huu feki kuwa wa haki na usawa baina ya Tanganyika na Zanzibar walifanywa kama wahalifu tu na hivyo kuvamiwa na vikosi vyote vya ulinzi na usalama na kumiminiwa risasi za moto na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 50, walemavu, wajane, mayatima na maelfu ya wakimbizi. Halkadhalika wazanzibari walipopambana na vyombo vya dola mara kadhaa katika mwaka wa 2011 chini ya harakati za taasisi za kiislamu kudai Muungano feki kuwa wa haki, hadhi na heshma ya Zanzibar kurejeshwa waliitwa wahuni, magaidi, Alshababb,buku haramu, Alqaida nk. Walivamiwa na polisi kupigwa, kuumizwa, kuwekwa vizuizini na kufunguliwa kesi wao na viongozi wao wa harakati hizo.
Hapa ndipo pale penye lengo la makala yangu hii. Lengo ni kuwauliza watawala,wakoloni weusi,makaburu weusi,madikteta,wauwaji,makatili,wanyonyaji,masultani wa kitanganyika na vitumwa vyao  vilivyo kuweko kule Zanzibar, kama wazanzibari wanaopigania nchi yao nzima iliyotekwa na watu tuliyodhani ni majirani  zetu wa kitanganyika na kutuita ni wahuni, magaidi, Alshabab na Alqaida,kwa kuwa tunataka nchi yetu ya Zanzibar. jee hawa wanaopigania gesi tu isichukuliwe tena na serikali yanu wenyewe mutawaite vipi...? Kati ya hawa wazanzibari waliopigana kujibu na kupinga maonevu ya vyombo vya dola dhidi ya harakati zao, na wale waliojipanga wenyewe kuanzisha harakati za mapambano ya kupinga gesi yao isitoke nje ya Mtwara ni nani gaidi zaidi.....? alkaida zaid...i? Muhuni zaidi...? Au alshabab zaidi..?

Wazanzibari tunasema kama ambavyo wana Mtwara wanayo sababu ya kupambana kulinda gesi yao isichukuliwe kwenda kuimarisha Dar es Salaam, Dodoma na Arusha basi wazanzibari wanazo zaidi sababu za kupigania nchi yao iliyohodhiwa na watanganyika na hatimae kuirejesha katika mikono yao hata kama wataendelea kuitwa magaidi, alshabab, alqaida, wahuni nk. Halkadhalika wataendelea na mapambano ya kuimezua nchi yao hata kama makombora yote makubwa ya Tanganyika yataelekezwa Zanzibar. Kama wana Mtwara wanayosababu ya kuipigania gesi yao ambayo bado imo katika matayarisho ya kuchukuliwa Dar es Salaam basi wazanzibari wanazo zaidi sababu za kupigania nchi yao iliyomezwa miaka 49 iliyopita na raslimali zake kadhaa kuibiwa na watu wake kuachwa maskini tokea miaka hiyo hadi leo wahoi bin tabani.

Wanaoijuwa athari ya gesi ya Mtwara kwenda Dar es Salaam na kuwaacha watu wa Mtwara wakiendelea kuwa masiki ni watu wa Mtwara. Halkadhalika, waijuwao athari ya Zanzibar kumezwa na Tanganyika huku wazanzibari wakibakia wanyonge hawana maamuzi, hawana heshma ya nchi yao, hawana mamlaka ya nchi yao na uchumi wao ukizidi kufa ni wazanzibari. Adhabu ya kaburi aijuae ni maiti. Wazanzibari wamechoka kunyanyasika na wataendelea kupambana kuliko walivyowahi kupambana mpaka watakapoyatia mikononi mwao mamlaka kamili ya nchi yao. Jamhuri ya watu wa Zanzibar Kwanza!!!!!

Friday, January 25, 2013

HILI NDIO BARAZA LETU LA WAWAKILISHI KAZI KUCHEZA MDUWARA,SUMSUMIA NA KANGA MOKO SIO KUTETEA WANANCHI NA NCHI YA ZA,BAR LAAAWazanzibari tujiulize kwa pamoja kitu gani ambacho baraza la wawakilishi  wanashindwe kuchukua maamuzi magumu katika kulinda, kusimamia, mustakbali na maslahi ya nchi na wananchi  wa Zanzibar....?Hatuoni kwmba baraza  hili limekosa ridhaa na uaminifu kwa wananchi..? Jee baraza hili kwanini linashindwa kulinda mali za nchi..?Sababu kuu za 
kuanza kujiuliza haya masuala (3)
Baraza limesikia kilio cha wananchi wa visiwa vya unguja na pemba kwamba Muungano huu hawautaki wa kikatiba wa miaka 49 wamechoka nao ni nusu karne na hakuna moja lililo nufaisha Wazanzibari.Wanataka muungano wa mkataba wenye kuheshimiana, wenye maslahi kwa pande zote mbili zilizoungana, Wanataka kila taifa liendeshe shughuli zake za ndani na kimataifa yani nje bila kuingiliana katika uendeshaji wa kazi za serikali hizi mbili.
Wanataka kila taifa liwe huru katika kujiamulia mambo yake wenyewe, isiwe tukitaka kwenda kununuwa omo kenya lazima tukaulize dodoma je tukanunuwe omo ....? laaa tunaka kununuwa tunanuwa tu. haya ndio maoni yaliokushanywa na chombo cha kisheria kilichopitishwa na bunge la Jamhuri ya Tanganyika na pia kuungwa na kupata baraka za baraza la wawakilishi(tume ya jaji Warioba) Jee kwanini baraza la wawakilishi haliitishi kura ya maoni kumalizia pale ambapo wananchi walishapaanza..? au nyote humu ndani ni majibwa koko....?
Tujiulize tena nini baraza hili wanasubiri..? hakuna haja ya kusubiri na kuendelea na huu mchakato wa katiba ikiwa mshiriki mmoja wa muungano amesema kwa asilimia 67 % kwamba anataka muungano wa mkataba Inaonekana baraza hili la wawakilishi halina mamlaka yoyote ya kusimamia haki na maamuzi ya wananchi wa Zanzibar limekuwa ni kama banda la kucheza karata na bao la kete. Baraza linaendeshwa kwa nguvu za DODOMA  ambacho chama kinanguvu kuliko chombo kilichochaguliwa ama kihalali au kwa mizengwe.
Tunaliambia baraza la wawakilishi liitishe kura ya maoni au waitishe kikao cha dharura kujadili maoni ya wananchi kuhusiana na katiba mpya sio kusubiri mpaka wakoloni tanganyika waje na msaada wa kupinga kikao chochote kile cha kujadili matokeo ya maoni ya wananchi kuhusiana na hii katiba mpya naikiwa bara latishindwa kufanya hivyo basi Wazanzibari tusisubiri tena maana misra mubaraka hakuondolewa na baraza kaondolewa na vijana barabrani niwakati wa kujitolea na kujuwa ima ya mussa au ya firauni tu sasa masheikh walio kuwa wakisema kweli washawafunga jela na sisi ndio tu kae tu kama mayatima mpaka lini au ndio tuishi hivi hivi mpaka miaka mingine 49 imelizike....?
Hii ni wake up call kwa baraza linalojulikana baraza la kuwatetea Wazanzibari katika hali yoyote, tunataka kuona hii mitumbo iliyo jazana humu kufanya kazi zake sio kusinzia tu,na kupiga kelele kwamba Tangnyika wanatunyonya wakati uwezo wa kuondoa unyonyaji munao lakini hamufanyi.Tunakuambiyeni wajumbe mitumbo mikubwa na vicha vya samaki tumieni nguvu zenu za kikatiba kuitisha kura ya maoni kuhusiana na huu muungano feki. Kama baraza hili lina nguvu kisheria na haliingiliwi katika maamuzi yake na chombo chochote kile basi wakati umefika kwa kusikia kauli za wajumbe hawa ikiwa ccm au cuf, wakati umefika laaa kama nyote humu ndani ni vipusa kazi kutia hina na piko na kujiremba na maskara huku mukiweka viluwa na asimini katika kitanda ili bwana wenu tanganyika akija afurahi na kuwa kuna kuna nyinyi basi sawa nyamazeni maana ndio bwana wenu sio.
Tumemsikia Mh. Amani Abeid Karume anasema kwamba yuko teyari kusimamia Serikali katika kipindi cha kuandaa Muungano wa mkataba ikiwa dr kumbi shein aliye wekwa na dodoma madarakani atakuwa hajiamini na hana uwezo wa kusimamia Serikali kwa kipindi hicho cha mpito. Jee kwanini hamuchukui maamuzi magumu kumalizia pale ambapo wananchi na viongozi wengine wamekufikishieni...? Waswahili husema kwenye miti hakuna wajenzi, usemi huu unakubalika hakuna mwenye hoja ya msingi kuupinga Wawakilishi tunakuambiyeni muchukue maamuzi magumu kama mupo katika hicho chombo kwa ajili ya maslahi ya nchi na wananchi wa visiwa hivi vya unguja na pemba au nchi hii ya Zanzibar.” La leo lifanyike leo, Wananchi wanakufa na njaa, maradhi, ukosefu wa elimu, miundombinu, uhusiano wa kimataifa, uchumi na sarafu” Marehemu Mzee Karume alisema koti likikubana…..livuwe mambo 11 yaliokubaliwa katika muungno sasa ni mambo48 na toka tungane nao sasa ni miaka 49 inamanisha kila mwaka wameongeza moja na kulifanyia kazi vizuri ili watuangamize wajube bado tu hamja amkaa..?
Huku koti likizidi kupanuliwa na Watanganyika, kwenu linabana kwao wanalipanua na yao yanawaendea vizuri sisi tumo tu muungano weeee katiba weee muungano weee katiba weee. Nakuambiyeni wachangiaji muwaulize wajumbe hawa wa baraza la wawakilishi wanasubiri nini, au hawana uwezo, wanaogopa tanganyika asije akawaekea vikwazo vya kiuchumi....? ikiwambia kuanzia sasa hatuwaletei tena BATATA NA MAHARAGE NA VITUNGU HAHAHAHAHAHA

WAZANZIBARI HATUNA HAJA YA UMEME WA TANESCO JUWA TU.

WAZANZIBARI KAMA HUYU DIKTETA HATUJA MTOWA KATIKA NCHI YETU HAYA YOTE YATAKUWA NI NDOTO JUWA JUWA SI DISSELI WA PETROLI JUWA JUWA TU SISI TUTAKUWA NA UMEME WAKUTUMIA NA WAKUWAUZI KENYA,UGANDA NA TANGANYIKA PIA NA MAJI YATAKUWA BURE LAKINI WAPI JINAMIZI LIMETUKA JUU YA KICHA HATUFURUKUTI KILA KUKICHA WANANCHI DUMISHENI AMANI NA UTULIVU NDIO MAENDELEO YATAKUJA YAWAPI MIAKA 50 NI NUSU KARNE SASA.
A large power network with very low electricity losses allows clean electricity to be generated from renewable sources at the most advantageous locations. The type of technology used on site depends on local circumstances, as well as on the wishes of the country concerned and the investors.

In desert regions near the coast, solar-thermal power plants can be combined with seawater desalination so that they not only produce electricity, but also drinking water. Air-cooled solar-thermal power plants combined with water-saving cleaning robots are particularly useful in desert locations inland. Many coastal areas are excellent locations for inexpensive wind power plants. Photovoltaic systems are useful for covering peak mid-day demand, for example from air conditioning systems. Solar-thermal power plants, as well as biomass, geothermal, hydroelectric and pumped storage plants, provide valuable, controllable electricity. This means they can be used to balance out the fluctuations of wind and photovoltaic power, so that more of these variable energy sources can be used in the future electricity mix.High-Voltage Direct Current (HVDC) transmission
HVDC transmission is a way of carrying clean electricity over long distances to the places in the world which consume large amounts of energy. Around 90% of the human population live less than 3000 kilometers from deserts and could be efficiently supplied with clean desert electricity. The line losses are very low – only around three percent per 1000 kilometers – and the extra cost is only one or two cents per kilowatt hour. This is more than compensated because solar power plants located in deserts are much more efficient due to the longer and more intensive solar irradiation and less winter months. The same is with wind power plants that benefit from stronger and more constant winds at optimum sites. An extended grid and connected backup power plants compensate for fluctuations in renewable energies and downtime in power plants and transmission lines.

There are dozens of lines up to 1700 km long (Inga-Shaba, Democratic Republic of Congo) with capacities of up to 5 gigawatts (Yunnan-Guangdong, China) already in operation around the world. HVDC lines are also used in Europe: Sardinia is connected to the mainland by undersea HVDC cable and there is a whole network of HVDC connections between central Europe and Scandinavia. HVDC lines take up less space than conventional AC power lines and can be laid over long distances underground. This increases public acceptance and means the network can be extended faster. A study by the DLR confirms the positive eco-balance of the transmission lines used for DESERTEC. Wikipedia contains a list of existing and planned lines around the world.

Concentrating Solar-thermal Power (CSP) plants
CSP plants are key to the DESERTEC Concept because they are ideal for utilizing the solar potential of the world’s deserts and supplying electricity on demand. A reflector area of just 20 square meters in a solar-thermal power plant is enough to supply all the electricity one person needs (including electromobility) day and night with no carbon emissions.

Solar-thermal power plants use mirrors to concentrate solar energy in order to heat water and produce steam. This creates pressure, which is used to drive a conventional steam turbine and generate electricity. Solar-thermal power plants can produce clean electricity from solar energy day and night, because heat, unlike electricity, can be stored in large quantities. Heat storage tanks supply energy to the steam cycle at night and especially during times of peak demand. This means that these power plants, when combined with other renewable energy sources, can compensate for the inherent fluctuations of photovoltaic and wind power and thus help stabilize the grid.
At sites near the coast, solar-thermal power plants can use sea water to cool the steam cycle. This way, a collector array designed for a 250 megawatt steam turbine can produce 200 megawatts of electricity and 4 million liters of drinking water every hour through thermal seawater desalination. This method is already used on a large scale at the fossil-fired plant at Jebel Ali in Dubai. At inland sites, air cooling is most suitable – which means that the ideal locations for solar energy can be used, regardless of whether there is a water source. Water-saving brush robots are already successfully used for cleaning the collectors.

Thursday, January 24, 2013

SHEHIA YA KENGEJA PEMBA WALIA NA SKULI YAO.HIZI NDIO TIJA ALIZOZITAJA BILALI NA FAIDA ZA MUUNGANO HUU


TIJA NA FAIDA ZA MUUNGANO HUU FEKI ANAO USIFU BILALI KUWA UNAMANUFA

Wananchi wa Shehia ya  Kengeja Mkoa wa kusini Pemba walia na ujenzi wa skuli yao nikizungumzia kengeja nadhani miongoni mwenu  wengi mnaweza kupafahamu au kutokupafahamu.
Kijiji cha kengeja kipo mkoa wa kusini Pemba na nimiongoni mwa kijiji maarufu hapo zamani kwa upikaji wa Tosi pia kuwa na wakaazi wengi sana wa kihindi ndani ya kengeja kuna Skuli iliojengwa mnano mwaka 1945 mpaka leo hii ndio inayotumika kwa ajili ya kutowa elimu kwa wananfunzi mbali mbali.
Hapo mwanzo kabla ya Kuja kwa mapinduzi ilitoa elimu kwa wakaazi wengi wa maeneo jirani kama Vile Mwambe,Mtambile,Kiwani na maeneo mengien ya karibu licha ya kuwa katika maeneo mengi sana ya Unguja na  Pemba kwa sasa kumekuwa kukijengwa skuli mpya siku hadi siku lakini cha kushangaza na cha ajabu kwa skuli hii hadi leo hii  imebaki kuwa na majengo yale yale ya zamani ya 1945 na wanafunzi ndio wanayosomea ingawa hayafai hata kidogo kwa sasa kulinganisha na hadhi yake.
Kitu ambacho ukweli kimnifanya nishindwe kuvumilia sasa kwa vile mimi pia ni miongoni mwa wazaliwa wa kijiji hichi na nimewahi kusoma katika skulii hii ni kwamba wananchi wenyewe wa kengeja wamekuwa akihangaika sana kuhusu suala lakutafuta msaada wa hali na mali ili waweze kujenga skuli yao lakini jitihada hizo ni sawa na kugonga ukuta  kutokana na  kutokuzaa mafanikio yoyote kwao.
Ingawa kuna msemo usemao abebwae hujikaza ndio maana wananchi wenyewe kwa nguvu zao huku wakijawa na imani kuwa baada ya jitihada zao wangeweza kusaidiwa na ndio maana hadi hivi sasa wameweza kuchangia kiasi cha shilingi takribani milioni nane wakisubiri kupatiwa msaada zaidi ili wafanikishe lengo lao la kuwa na skuli mpya na wao kwa faida ya watoto wao au hata kufanyiwa ukarabati lakini hali mpaka sasa bado imebaki kuwa giza sijui ni kwamba hakuna tena wafadhili ambao husaidia ujenzi wa skuli mbali mbali hapa Zanzibar kama zilivoweza kusaidiwe nyengine nyingi za kisiwani Pemba.
Ni suali la kujiuliza hivi hawa wanaotowa misaada ya ujenzi wa mashule wanavigenzo gani ambavyo huzingatia ili waweze kutoa msaada wao pengine sisi hatuna  na tusiweze kusaidiwa hadi leo hii,ukweli inauma sana kuwona takribani skuli nyingi za unguja na pemba kwa sasa zikiwa na mazingira mazur ya kusomea lakini kwa skuli hii hali nikinyume na skuli nyengine ambazo zinaendelea kukarabatiwa pia kujengwa mpya siku hadi siku.
Ni ukweli usiofichika kuona wananchi wakijitahidi kuchaguwa viongozi huku wakiwa na matumaini kuwa watawasaidia katika kuhakikisha kuwa wanapiga hatuwa kimaendeleo ndani ya sehemu zao  lakini wapi sijawahi kusikia kuwa kuna mtu alieweza kufika na kusaidia alau msaada ambao utaisidia katika suala zima la ujengwaji wa skuli hio.
Siwezi kuondoa shukrani zangu kwa mwakilishi wa jimbo la Mtambile ambae pia ni mkaazi wa Kengeja yeye ukweli amejitahidi ni hivi karibuni tu aliweza kutoa msaada wa Set ya Computer na printer yake kwa ajili ya matumizi ua ofisi ndani ya skuli hio licha kuwa muonekano wa majengo ya skuli hio yamechakaa na hayaendani na matumizi ya Computer badala yake palihitajika pajengwe mwanzo.
Nazidi kujiuliza maswali mengi sana kwa upande wa Mbunge wa jimbo hili hivi hii hali ya skuli hii haioni au hajui kama wananchi waliomchagua watoto wao wanasoma ndani ya skuli hii tena kwenye  mazingra magumu ya tafutaji wa elimu,haoni kwamba anapaswa kutoa msaada wake tena wa hali ya juu,amesahau kuwa amepelekwa bungeni kuwatetea wananchi wake nilini amesimama bungeni na kuelezea hali halisi ya skuli hii angalau pengine angeweza kuwapa moyo wananchi wake kuwa anawatetea lakini wahusika ndio hawataki lakini hafanyi hivo.
Ushauri wangu kama ni mzaliwa wa kengeja waiteni viongozi wenu muwape matatizo ya skuli yetu wayapeleke kunako husika tusikae tukatupia lawama Serikali tu wakati hao wahusika wakuuu wakuyafikisha matatizo yetu hawajayafikisha kunakotakiwa nadhani tukifanya hili huwenda tukafanikiwa inshallah.pia NAPENDA KUMULIZA BILALI ALIPOTOWA MAONI YAKE NA KUSEMA MUUNGANO UNATIJA JE HII NI MOJA KATIKA HIZO TIJA ALIZOZITAJA.....?

BILALI ASEMA MUUNGANO UNA TIJA.(KWA WAKE ZAKE,WATOTO WAKE,FAMILIA YAKE,UKIBADILISHWA ATAKOSA ULUWA BORA UBAKI HIVI HIVI MPAKA AWE RAISI WA ZANZIBAR HAHAHAHA)Makamu wa Rais wa Tanganyika Dkt. Mohammed Gharib Bilal amekutana na ujumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba feki Mpya iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Agostino Ramadhan. Mheshimiwa Makamu wa Rais amepata fursa ya kukutana na Tume hiyo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika muktadha huo, Jaji Warioba sambamba na kumpa fursa ya kuchangia maoni yake mengine anayopenda alimtaka Mheshimiwa Makamu wa Rais kujikita zaidi katika suala la Muungano kufuatia yeye kuwa na uzoefu wa kiuongozi katika serikali zote mbili yaani ya Tanganyika sambamba na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Akizungumzia suala la Muungano Makamu wa Rais wa Tanaganyika Dkt. Bilal ameieleza Tume kuwa yeye ni muumini wa Muungano wa serikali mbili na kwamba haoni sababu ya kubadili mfumo uliopo kwa kuwa umeipatia tija nchi yetu na kuipambanua kama nchi yenye muungano wa mfano katika dunia.hahahahahahahahaha.(tija sio kwa nchi yetu bali tija kwako wewe na familia yako ila umechelewa utanguka kama alivyo anguka gaddaf libya ngoja tu.)
Pia alifafanua kuwa mfumo wa serikali mbili  umesaidia kujenga na kudumisha udugu, amani na utulivu baina ya wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani kwa kipindi cha miaka 49 sasa.
Tanzania imechangia kitu kikubwa katika historia, kudumisha Muungano wa mfumo wa serikali mbili kati ya nchi mbili, kubwa na ndogo, jambo ambalo kwa nchi nyingine za Afrika wameshindwa. Kumekuwepo na nchi nyingi ambazo ziliungana na kushindwa kudumu kama tulivyo sisi. Hatuna haja ya kujifunza mfumo mpya wakati tulionao umeweza kudumu, « alisema.(kikwete kamdanganya kuwa atakuwa raisi wa zanzibar ndio maana anabibinyekea hahahahhahahaha masikini zezeta ni zezeta tu.)

Wednesday, January 23, 2013

KARUME JR AOMBA KUPATIWA HATI HALISI YA MUUNGANO WA ZANZIBAR NA TANGANYIKA.JE IPO AU NDIO IMEFUKIWA GININGI..?Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume, ameomba kupatiwa hati halisi (Original) ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo imetiwa saini na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume.
Ombi hilo la Karume limekuja kufuatia utoaji wake wa maoni mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Joseph Warioba, makamo Mwenyekiti Assa Rashid na wajumbe wengine aliyokutana nayo juzi nyumbani kwake Mjini Unguja.
Karume alisema yeye hana hati ya Muungano na hajawahi kuiona na iwapo Tume hiyo inayo hati hiyo basi angeomba kupatiwa kwani ni wazanzibari wengi wanahitaji kuiona hati hiyo ambayo ni mkataba kati ya nchi mbili zenye mamlaka kamili kila moja na zilizoungana mnamo mwaka 1964 kila nchi ikiwa huru.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya tume hiyo, kimesema Karume mbali ya kutaka kupatiwa hati ya Muungano lakini pia alisema anaunga mkono kuwepo kwa Muungano wa Mkataba ambao kila nchi itakuwa na mamlaka yake kamili na kisha kufuatia huo mkataba ambapo alisema Zanzibar kwa takriban miaka 50 sasa imekuwemo katika Muungano lakini imekuwa hainufaiki kiuchumi ndani ya Muungano huo.
Aidha Karume alisema yeye yupo tayari iwapo kutakuwepo na kipindi cha mpito kutoka Muungano huu uliopo na kuingia wa Makataba pale alipoulizwa na Mjumbe wa Tume hiyo, Salim Ahmed Salim ambaye alionesha khofu yake na uzoefu wa chaguzi zinazofanyika nchini kwamba zinakuwa na machafuko.
Karume alisema hakuna machafuko yoyote yatakayoweza kutokezea katika kipindi hicho cha mpito na iwapo Rais aliyekuwepo madarakani hataweza kusimamia na hatajiamini kwa hilo basi yeye anaweza kuchukua nafasi hiyo ili aweze kusimamia hilo na akaahidi kwamba hali itakuwa shuwari na kuivusha Zanzibar katika machafuko kama alivyoweza kusimamia Maridhiano kati ya vyama vikuu vya CCM na CUF mwanzo hadi mwisho wake.
Karume ambaye amekuwa rais kwa miaka 10 Zanzibar amesema amepata uzeofu mkubwa sana katika kipindi cha uongozi wake akiwa madarakani ambapo ameishuhudia Zanzibar ikidhoofika kiuchumi wakati upande wa pili wa Muungano ukinufaika zaidi.
Alisema ni wakati mwafaka kupitia katiba mpya watu kuwa wawazi na kusema ukweli kwa kubainisha kero na matatizo yote ya Muungano ili hatua za lazima zichukuliwe katika kuwaletea wananchi katiba iliyo nzuri na yenye usawa wa nchi mbili zilizoungana na zenye hadhi sawa.
Karume alisema waziwazi kwamba kwa kipindi cha miaka 10 ameshuhudia mengi sana katika suala zima la maslahi ya Zanzibar, lakini pia alisema sasa ni zama mpya za ukweli na uwazi na kwa hali iliyofikia sasa hakuna njia nyengine zaidi ya kila nchi – Zanzibar na Tanganyika – kurejesha mamlaka yake (sovereignty) kitaifa na kimataifa na kisha nchi hizo mbili kushirikiana kupitia Muungano wa Mkataba kati yao, hivyo ndivyo alivyosema Mheshimiwa Karume.
Hata hivyo Karume aliwaambia wajumbe wa tume hiyo kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliotiwa saini na Mwalimu Nyerere na Mzee Karume ulikuwa na heshima hapo zamani na ukiheshimiwa sana lakini kumekuwepo na dharau fulani ambazo zimekuwa zikifanywa na viongozi na baadhi ya watendaji jambo ambalo linadhoofisha Muungano huo na kusababisha malalamiko makubwa miongoni mwa pande mbili hizo.

JE UNAJUWA KAMA MUUNGANO IKIVUNJIKA TANGANYIKA ITAKUWA HAINA KITI U.N...?Tumesikia maoni ya kutaka kufanya katiba mpya  ya Tanganyika. Tumewasikia viongozi wastahiki wa Zanzibar waliotoa maoni yao katika kuifanya hiyo katiba mpya (kama itakua!), tumeona msimamo mzuri wa viongozi wetu: Karume Jr, Maalim Seif, Moyo, Salim Rashid, n.k ni wengi – wote wameitetea haki ya Zanzibar.
Sijui kama wengi mnajua kuwa Tanganyika haikuwa na kiti pale UN, na walipokuwa nacho, kiliwekwa rehani (walafukuzwa na U.N) baada ya Nyerere kuiunga mkono serikali ya Nigeria kuhusu jimbo la Biafra (successionist). Hapa UN iliwapa red card Tanganyika 1967 nakuwatimuwa kabisa na hawajarudishiwa kiti kile mpaka leo nini kilitokea baada ya Tanganyika kufukuzwa katika U.N...?
Walichokifanya Tanganyika wakati ule ni kukikalia kiti cha Zanzibar kilichopo U.N nakuva koti la Utanzania na kukifanya kiti kile kama ndio chao. Yule Rashid Salim Adi, anayeshughulikia sana suala hili analijua vizuri suala hili, na kama anasoma mada naomba pia achangie au asaidie fikra kwa umankini na umahiri zaidi ili umma wa Zanzibar upate kujua zaidi na zaidi. Haya ni mambo yamefichwa sana chini ya carpet. Vijana wengi wa Zanzibar na Tanganyika wamefundishwa sana ohooo ‘amani na utulivu tuuuuuu,huku viongozi yao yakiwaendea na rai mukiendelea kula joto ya jiwe   na pia kudanganywa kuwa Tanganyika na Zanzibar ni Tanzania ni nchi mojamawe —vijana wengi hawajui kuwa Zanzibar ilikuwa na hadhi kubwa kuliko Tanganyika (hili mpaka leo).
Naomba hapo mtupie jicho. In short, Kiti kile pale UN cha Zanzibar (au walichokikalia (Tanzania) Tanganyika) na akina Membe wanakwenda kujinasibu — ni kiti chetu, halali yetu, damu yetu na flus za walipa kodi wa Zanzibar.
Ukijumlisha hilo, na utoaji wa maoni ya kuunda katiba mpya: tuseme Warioba na CCM wenzake wakate kuifanya katiba mpya,hii nikuonyesha kuwa wao walikuwa na mpango mwengine ila wameona hautafanikiwa ndio wataivirigiza mpaka isiwe. pia nataka kuwakumbusha kuwa Zanzibar ina KATIBA yake hilo moja na nchi nyengine kabisa sasa vipi sisi tuwasaidie wao kutafuta katiba yao maana wao hawana katiba na hiyo waliokuwa nayo ya viraka ndio ati wamejifanya kuwa ni katiba ya muungano na hayo sio moja katika makubaliano ya muungano kama kweli hawa watwana wana kheri basi walikuwa wasema ok Tanganyika irudi kwanza huko dodoma waliko ifukia wakaifukuwe.
kisha waseme ok Tanganyika iwe na katiba yake mpya na mambo yake kisha sisi na wazanzibari tukae chini meza moja na kutunga katiba ya muungano hapo kweli lakini laaaa lilelile katiba lao lenyeviraka tele ndio hilo hilo wanalolita la muungano na ndio hilohilo wanalotaka sasa kuligeuza geuza kisha watuambiye hakuna haja ya katiba ya zanzibar madamu sasa tunakatiba ya  muungano na nakuhakikisheni wakiliambiya lile buju pale ikulu basi litakubali maana ashasema atafanya jambo ambalo wazanzibari hawatamsahau naam asha anza kufanya maana mpaka leo masheikh wamo ndani bila ya hatiya yoyote.ila naona kashachelewa kwa sababu wazanzibari wote hatutaki muungano kwa sababu wazanzibari takriban wote hatutaki Muungano huu uliopo sasa — Je, Zanzibar tufanye nini? Strategy…………..1
Tunaweza kufanya tena na tena petition U.N kwa kutumia maoni hayo hayo ya 66% na ushei plus+plu+ plus, na kusukuma ajenda ya madi yetu U.N na haina shaka kwa mujibu wa taratibu zao, kama wananchi/raia walio wengi kwa kupiga kura au opinions zinakataa jambo fulani — basi wananchi hao watakuwa na mandate ya kudai haki yao kimsingi.
Kwa hivyo kama akina warioba na Salim Ahmeid Salim (watoto wa Nyerere wataikataa maoni ya katiba mpya feki) basi wanashindwa hata  kuifanya ‘oral constitution’ — yaani a sort of fatwa.
Mawazo yangu: mimi binafsi nitaona ajabu sana, sana kama mtu kama warioba ataweza kufanya HAKI, wallah laadhimu. Nitaona ajabu sana, na nitaiweka katika world book of record; hana utamaduni huo, wala value system yake haimruhusu kufanya hivyo. Sijui wallah allah yaalam.
Ninasema hivi sio kwa kukata tamaa ila ni historia na mwenendo wa nchi: ni lini (TZ)TANG au Zanzibar ikakubali au kutekeleza maoni ya ya wananchi au kufuata mapendekezo ya report za uchunguzi. LINI, LINI, LINI – kuanzia report za wizi hadi zile za M.V Spice au Skagit — ipi iliyowahi kufuatwa. Hii ni challenge tu ninatoa, haihusiani na mada ya hapo juu.
Tuendelee kudai haki yetu mpaka tuipate Zanzibar. Hata CCM wanataka Zanzibar yetu kama nchi, basi wewe Warioba hujashtuka tu.

Tuesday, January 22, 2013

MTWARA NI TANGANYIKA NA WAMEGOMA GASI YAO ISIPELEKWE DAR SISI NCHI NCHI NCHI TUNAIWACHA NAKUFANYWA DAGUURO KWELI WAZANZIBAR BATATA ZA UROJO ZIMETULEMAZASAKATA la kupinga ujenzi wa bomba la gesi inayovunwa katika Kijiji cha Msimbati mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam, limechukua sura mpya baada ya maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara kujiandikisha katika fomu maalumu kupinga mradi huo.
Tayari majina hayo yamekabidhiwa kwa Katibu wa Wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya kwa ajili ya kuyawasilisha bungeni kama kielelezo halali cha wananchi hao kupinga mradi huo, ambapo utaratibu wa wananchi hao kujiorodhesha uliandaliwa na chama hicho.
Taarifa zinaeleza kuwa zaidi ya wakazi 30,000 wa Mtwara wamejiorodhesha kupinga mradi huo wa gesi.
Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka wilaya zote tano ya mkoa huo, ambao hawakujali mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
Watu wa kada mbalimbali waliliambia Mwananchi Jumapili kwamba haijawahi kutokea umati mkubwa wa watu kuhudhuria mkutano wa hadhara mkoani humo kama ilivyokuwa kwa mkutano wa jana.
Walisema kuwa idadi hiyo ya watu ni zaidi ya waliojitokeza katika maandamano ya kupinga mradi huo, yaliyofanyika Desemba 27 mwaka jana.
Majina hayo yalikabidhiwa na makatibu wa CUF wa wilaya za mkoani huo  huku mwakilishi wao Saidi Kulaga, akisema kuwa zaidi ya watu 30,000 wamejiandikisha kupinga mradi huo.
Alisema wananchi hao wanataka Serikali kujenga mitambo ya kufua umeme  mkoani humo, ili kuinua uchumi wa mikoa ya kusini.
“Kwa niaba ya wananchi hawa na mbele yao,  nakukabidhi majina na  sahihi zao, wakipinga mradi wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam. Wazee wetu waliwaondoa wanyonyaji weupe, sasa ni zamu ya vijana kuwaondoa wanyonyaji weusi,”  alisema Kulaga huku akishangiliwa na umati wa watu.
Akipokea fomu hizo, Sakaya alisema kuwa wabunge wa CUF, wamesikia kilio cha wananchi wa Mtwara na kwamba watahakikisha wanawasilisha katika Bunge lijalo.
Katika mkutano huo mabango kadhaa yalibebwa na baadhi yakisomeka: “Shemejiii gesi haitoki…: Kikwete tuachie gesi yetu.”
Kabla ya mkutano kuanza umeme ulikatika eneo hilo hali  iliyosababisha kundi la vijana kuivamia Ofisi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), mkoani humo wakiishinikiza urudishwe, kitendo kilichowalazimu polisi kuingilia kati na kufyatua mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi hao.
Wananchi waliondoka eneo la ofisi hizo na kurudi uwanja wa mkutano, ambapo baadaye na mkutano huo uliendelea kwa  amani na utulivu, huku polisi wakiwa katika tahadhari kubwa.

MZEE MOYO NA SALUM RASHID WATOWA MAONI YAO BILA YA KUTAFUNA MANENO-WASEMA KUVUNJIKA KWA MUUNGANO SIO JAMBO GENI.TUME ya mabadiliko ya Katiba mpya nchini Tanganyika, imeelezwa kuwa Baraza la Mapinduzi halikushauriwa wala kushirikishwa katika Muungano feki wa Tanganyika na Zanzibar, uliyoundwa Aprili 26, 1964.
Wanasiasa wakongwe waliyokuwa katika Serikali ya Mapinduzi, wakati wa kuundwa kwa Muungano huo, Bw Salum Rashid na Bw Hassan Nassor Moyo waliiyambia Tume hiyo, walipokuwa wakitoa maoni yao Maisara, mjini Zanzibar.
Katika maoni yao walisema: Tangu awali ya kuundwa Muungano huo, kulikosekana uhaliali wake, licha ya kuwa umedumu kwa miaka hamsini huku kukiwa na malalamiko kadhaa ya wananchi.
Wakizungumza kwa pamoja, Wanasiasa hao waliunga mkono kuwepo kwa Muungano, lakini walishauri mfumo mpya wa Muungano wa Mkataba, ili kila nchi kuwa na mamlaka yake kamili:
“Kwa hali ilivyo miaka 50 ya Muungano kushindwa kutatua mambo mbali mbali, mfumo pekee unaofaa kwa sasa na kwa kizazi hiki ni Muungano wa Mkataba. Utaratibu wake utajulikana baadae,” walisema Wanasiasa hao.
Bw Moyo alisema Serikali ya Muungano, isiogope maoni ya wananchi kwani kwa takriban miaka 50 matatizo ya Muungano yameshindwa kutatuliwa na njia pekee kwa sasa ni kukubali kubadilisha mfumo wa Muungano huo:
“Tukiwa na mfumo mpya wa Muungano, utakwenda sambamba na wakati huu ambao idadi kubwa ya wananchi wameamka na kuona kuna matatizo katika Muungano wetu,” alisema Bw Moyo.
Bw Moyo ni Waziri wa kwanza wa Sheria wa Serikali ya Muungano, na Bw Salum Rashid alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi.
Kwa pamoja walishauri kuwepo kwa Muungano lakini walisisitiza, ili kuimarisha Muungano kwa nchi zote mbili, ni kusikilizwa kwa maoni ya wananchi ambao wanataka aina mpya ya Muungano wa Mkataba:
“Sisi ndiyo tulikuwa na dhamana wakati ule na tulitakiwa tuunganishe Serikali kwa kuimarisha udugu na kuimarisha uchumi wetu, bahati mbaya sasa kuna kero,mimi siziiti kero naita ni matatizo, ni wakati wake kuondoshwa” alisema na kubainisha:
“Msimamo wangu ni Serikali ya Mkataba na ndiyo ninavyoamini na naamini kwamba huu muungano tuliyonao ni Muungano wa Mkataba, hili siyo jambo jipya, Mwalimu Nyerere na Mzee Karume walitia saini ya Mkataba,” hili sio jambo jipya,” alisisitiza Mzee Moyo.
Bw Moyo alitaka kurudishwa kwa utaratibu wa zamani, ili Rais wa Zanzibar aendelee kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, akimaanisha Muungano huo ni wa Tanganyika na Zanzibar.
Naye, Katibu Mkuu wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi, Bw Salum Rashid ambaye alikuwa Dar es Saalm na Mzee Karume siku ya kusainiwa Mkataba wa Muungano, alisisitiza kuwepo kwa Muungano wenye maslahi kwa wananchi wa nchi zote mbili:
“Serikali ya Muungano isiwe na woga wa kuvunjika kwa Muungano. Hilo sio jambo kubwa na wala siyo jambo geni, baadhi ya nchi za Afrika ziliwahi kuungana, na Muungano ukavunjika,” alisema na kufafanua zaidi:
“Sioni jambo zito kuvunjika kwa Muungano, mbona Muungano wa Senegal na Gambia ulivunjika na wote walikuwa ni wanachama wa Umoja wa Afrika na hakuna jambo lolote lililotokea,” alisema Bw Salum Rashid.
Alisema wananchi wanaotaka Muungano wa Mkataba, hawamaanishi kuvunja Muungano, bali wanataka mfumo mpya wa Muungano ili kuirudishia Zanzibar, mamlaka na madaraka yake kamili.
Alisema ifahamike kwamba, kuwa nje ya Serikali siyo sababu ya kuwa ni fursa ya kuzungumza hayo, lakini wakati ule likizungumzwa suala la Muungano, ilikuwa inaonekana ni uhaini:na hukumu ya haini kwa wakati ule ni kunyongwa sasa  sisi wakati ule tutazungumza nini alihoji.
Alisema kwa sasa haiwezekani tena kuburuzwa na hasa vijana. Hivyo matumaini yake kwa tume hiyo ni makubwa: “Naamini watafanya kazi zao kwa uadilifu mkubwa na maoni ya wananchi ambayo wameyatoa kwa Tume, yatatekelezwa,” alisema Bw Salum Rashid.
Alisema Muungano wa Mkataba ndiyo sahihi kwa sasa na hakuna sababa ya viongozi kuogopa hilo, Wazanzibari na hasa vijana wanataka nchi yao kuwa na mamlaka kamili.
Bw Moyo na Bw Rashid wote wawili kwa pamoja wamewatoa hofu Wazanzibari kuhusu utendaji wa Tume hiyo, na walisema wanaiamini kwamba itafanyakazi yake kwa uadilifu, bila upotoshaji.
Tume hiyo inayongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba na Katibu wa Tume, Assa Rashid tayari imeshachukuwa maoni ya baadhi ya viongozi wakuu, pamoja na Marais wastaafu wa Seriakli ya Zanzibar.
Viongozi waliyokwisha toa maoni yao ni pamoja na Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Rais Mstaafu Dk Salmin Amour, Dk Amani Abeid Karume na baadhi viongozi wengine wa Serikali ya Zanzibar..