Saturday, February 2, 2013

DR KUMBI SHEIN ASEMA YEYE HATI YA MUUNGANO ANAYO IKO KWENYE MEZA IKULU NA U.N. NEW YORK COPY YAKE DUUUUUUUH


Juzi wengi wetu tulibahatika kuhudhuria na kusikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi wa sherehe za kutimiza miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM. Dr. Kumbi Shein, rais feki aliyewekwa na watanganyika nchini Zanzibar na pia Makamo Mwenyekiti wa CCM – Zanzibar ndiye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo. Nilikwenda hapo kama ‘observer’.
Hotuba yake ilijaa vijembe kama mwanamke shangingi lililo kubuhu umalaya,kejeli na dharau kwa wale anaowahisi yeye kuwa hawautaki Muungano wa sasa (serikali mbili –kama tulivyo).
Jambo kubwa sana alilolisema Dr.Kumbi Shein ni kuwa ‘HATI YA MUUNGANO IPO ZANZIBAR’;DUUUUUUUUUUUH. KWA KUMNUKUU ALISEMA HIVI: “Hati ya Muungano tunayo” — Dr.Kumbi Shein
Alisema Dr.Kumbi Shein kuwa anashangaa sana kuona baadhi ya watu wanataka kujua ilipo hati ya Muungano lakini alisema hawajafanya juhudi za kuitafuta kwani serikali inayo na nakala yake ipo makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York.sisi wazanzibari tunamshanga yeye anaejita mumini wa kweli na kuswali sala za jumaa na kusema uwongo mbele ya umaa wa watu tunamshanga sana.akiendelea kusema“Hati ya Muungano ipo pale IKULU Zanzibar kuna chumba na meza inayotumika kuwekea saini anetaka kuiona aende Umoja wa Matifa wanayo kopi hakuna haja ya kuhangaika”, alisema Dr.Shein akinukuliwa na gazeti la kila siku la Zanzibar Leo, gazeti la serikali ya mapinduzi ya Zanzibar la tarehe 1 februari 2013
Alisema kuwa Muungano wa serikali mbili unatosha kwa Zanzibar kwani ndio pekee unaoweza kuwaletea manufaa wananchi.swali manufaa hayo yako wapi maji hayatoke umeme umezidi mgao au manufaa ya maneno kila siku na kudanganya wananchi basi hawadanganyiki tena umechelewa.
Alisema Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana hazikufanya hivyo kwa kubahatisha kwani zilitambua umuhimu wa kuwa na muungano wa pande zote mbili
Alisema kuwa Zanzibar katika muungano huo imekuwa inafaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na wengi wa Wazanzibari wanaishi eneo kubwa la Tanzania bara kuliko watu wa bara wanaoishi Zanzibar.hii ni fitina anatia.swali tunamuliza wazanzibari wanao ishi oman,dubai,u.k,holland,germany,belgeim,france,canada,u.s.a,astaralia je nchi hizi pia tumeugana nazo...? na kuna wazanzibari kibao wanaishi.
“Nilipokuwa Makamu wa Rais nilitembelea mikoa mbali mbali ya Tanzania na kila nilipoenda nilikutana na Wazanzibari, tuutuzeni Muungano wetu kuona unabakia imara na lazima tutafakari ndani ya miaka hii 39″, alisema Dr.Kumbi Shein akinukuliwa na gazeti hilo la serikali.
Shabash ! sasa maoni yangu:
1. Kama hati hii ya Muungano ipo pale Ikulu zanzibar, kwa nini sasa tukaitafute New York..?
2. Kwa nini UN New York waturuhusu kuiona, Ikulu — home sweet home washindwe kutuonyesha — kwa kuzingatia kuwa hii hati ni public/umma unayo haki ya kujua...?
3. Pale akina Amani Karume,jumbe,maalim seif,adirisi abduwakili,salmin amour komando wa udongo na marais wote waliotangulia Zanzibar, walikuwa hawajui hilo, na hawaijui meza hiyo iliyopo Ikulu yenye Hati Hiyo au meza hiyo umeweka wewe na kikwete....?
(Hapa nitamlaumu sana Amani Karume, kwa nini alisema yale, kudai aonyeshwe hati ilhali yeye juzi tu alikuwa pale Ikulu ikiwa ni kweli hayo asemayo Dr Kumbi Shein la kama ni unafiki wake tu basi)
4. Inanishangaza sana kuona Rais Mstaafu anasema kuwa ‘aonyeshwe hati hati ya muungano ilhali successor wake Dr.Kumbi Shein anasema ipo vereje mambo haya...?
5. Sasa – niwalaumu wote Dr.Kumbi Shein na Amani Karume na waliotangulia –kwa nini msitueleze bayana juu ya suala hili. Sasa, tumuamini nani:Kumbi Shein au Karume na wenzake: kuwa hati haipo...? hati ipo..? wengine wanasema Karume Sr, hakutia saini (kitu ambacho siwezi kuamini) au ninaweza kuamini..? which is which..? Kwa nini mnatuweka roho juu wananchi..?
6.maalim seif pia sasa yuko hapo ikulu kweli ajuwo mambo haya anyamaze kimyaaaaa...? basi maalim pia ashabatizwa na machogo ikiwa ndio hivyo.
7. Kwa ufupi, Rais feki wa Zanzibar, Dr.Kumbi Shein naona anazidi kuturudisha nyuma kwa msimamo wake huu wa serikali mbili. Kwa historia yetu na uongozi ulivyo na kauli zao akina Kumbi Shein, Kikwete, Warioba wa Tume ya kubadilisha katiba feki ya kitanganyika naona kama muungano utabaki kama ulivyo. Kikwete anaamini kuwa ‘serikali haiwezi kusikiliza wachache” (suala la Mtwara); kadhalika kumbi Shein — hizi ndio rhetoric zao/zetu za utawala.
Sifikiri kama maoni ya wananchi hasa wa Zanzibar kama yatasikilizwa.
Lakini nimuulize Dr.Kumbi Shein, kwa nini haiwi tatizo mtanganyika kudai serikali tatu, au kudai Tanganyika yao, hao wan-CCM Tanganyika, ila inakuwa kosa kwa mwana-CCM zanzibar au Mzanzibari kudai serikali tatu, au Mkataba au n.k..?
Tuizungumze CCM: wote ni CCM hao — lakini naona mmoja anayo haki; na mwengine hana haki. WHY..?
Baadhi ya kauli za Dr.Kumbi Shein — zina nia ya kufitinisha pande mbili hizi kwa mfano aliposema kuwa ‘wazanzibari wanaishi eneo kubwa zaidi huko Tanganyika lakini Wabara ….sio wengi Zanzibar”. Huu ni ubaguzi na nia ni kufitinisha.

MUUNGANO OYEEEE MUUNGANO OYEEEE MUUNGANO OYEEEEE MUUNGANO OYEE

No comments:

Post a Comment