Monday, February 18, 2013

EMMANUEL NCHIMBI AINGIA NCHINI ZANZIBAR KAMA CHOONI NA KUMWAGA CHUKI


NCHIMBI YAKITOKEA NCHINI KWENU TANGANYIKA SIO UGAIDI YAKITOKEA ZANZIBAR NDIO UGAIDI..?

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt, Emmanuel Nchimbi amesema serikali itahakikisha inafanya juhudi kuhakikisha inawakamata watu waliomuua Padre Evarist Mushi wa kanisa katoliki nchini Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Makao makuu ya Polisi Zanzibar Dkt, Nchimbi amesema serikali ya Tanganyika imesikitishwa na tukio hilo alilolieleza kuwa ni la kigaidi huku akishtumu kuwa wana lengo la kuingiza nchi katika machafuko nchi ngani..? Tanganyika au Zanzibar..?
Amesema kuwa tukio hilo si tukio la ujambazi bali tukio la kigaidi kwani limelenga zaidi katika kuwashambulia viongozi wa kidini.
Amesema kuwa tukio hili limefanana na tukio lililotokea mwishoni mwa mwaka jana la kushambuliwa kwa risasi Padre Ambrose Mkenda wa Kanisa katoliki parokia ya Mpendae. mbona hutaji lakutekwa sheikh FARID HADI AHMED au kwakuwa yeye ni muislamu..?
Aidha ameeleza kuwa katika kukabiliana na matukio ya kihalifu hapa nchini nchi ngani..? taja jina Tanganyika au Zanzibar..? Wizara imeomba kibali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa (Tanzania)Tanganyika kushiriknia na mashirika ya kimataifa ya upelelezi ili kuwakamata wahalifu hao.
Dkt, Nchimbi amewataka (Watanzania) wapi Tanganyika au Zanzibar kuwa wavumilivu na kujiepusha katika mtego wa kuchukia na kwa misingi ya kidini katika kipindi hichi ambacho Jeshila Polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo.
wewe mwenyewe umeleta tayari chuki maana umesema magaidi na neno hilo linajulikana duniani kuwa ni waislamu wanao uwa watu sasa kama hukuja kupandikiza chuki mbona umelitaja neno hilo...? - Tumeona mauwaji ya Geita ya waislamu – serikali yako  ya Tanganyika  Nchimbi imeruhusu wakiristo kuchinja wanyama (mbuzi, ngombe, kondoo, kuku n.k) kwa ajili ya matumizi ya binadamu, na kuuzwa public, kitendo ambacho hakuna nchi hata moja iliyoruhusu hivyo. Kenya mpaka leo wanaochinja wanyama for general public ni Waislamu, Uganda kadhalika, Ethiopia kadhalika, n.k kwengineko.
- Wakati wa ukoloni, Mngereza, Ujerumani – Tanganyika, pia waliokuwa wanaruhusiwa kuchinja wanyama kwa ajili ya kula – ni Waislamui. Nyie pangu pakavu wakoloni weusi mnakataa ukweli huo, na mmesababisha mauwaji kwa waislmu bila sababu kwa kitu ovyo kabisa. Kikwete anacheka, Mwinyi anacheka, na Said Mwema anakeneua — hamna uongozi, hamna maamuzi — its’ nonsense. Hebu mjiulize kama kweli mna akili — imeanza lini, imeanza vipi, nini motive...? Tanganyika Mkoani Geita mauwaji yalio tokea huko na watu kadhaa kujeruhiwa kutokana na vurugu za kidini na haikusikika kauli ya waziri Nchimbi akiyaita mauwaji hayo na vurugu hizo kuwa ni ugaidi unaofanywa Nchi  ya Tanganyika  badala yake kistaarabu kabisa waziri Mkuu amekwenda Geita na kujaribu kutuliza hali hiyo.. “Kwa nini kauli za ugaidi ni kwa Zanzibar tu..?

No comments:

Post a Comment