Sunday, February 10, 2013

JUSSA ACHAA KUMUAMBIA MAALIM USICHUKUWA KITAMBULISHO CHA KITANGANYIKA AENDA NUNGWI KUWAMBIA WAZANZIBARI NI WASTARABU EEBOOO!!!!!!!!!Mhe Ismaili Jussa Ladhu aliufahamisha umma kupitia mkutano wa hadhara uliofanya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja kwamba katu wazanzibari hawatawaachia watanganyika waendelee kuitawala Zanzibar kwa kuwa hawana historia ya kukubali kutawaliwa. Mhe Jussa aliwaambia watu wa Nungwi kuwa mataifa makongwe zaidi duniani na yaliyostaarabika mapema mno katika historia hayana historia ya kutawaliwa au kukubali kutawaliwa.
Hivyo ndivyo lilivyo Taifa la Zanzibar ambalo ni kongwe kwa zaidi ya miaka 1500 na lililostaarabika tokea miaka hiyo. Hivyo basi kama wazanzibari walipinga makoloni kadhaa huko nyuma kuwatawala katu hawatashindwa kuutia mwisho ukoloni wa Tanganyika, nchi ambayo historia yake na ustaarabu wake ni kiasi cha miaka 80 tu nyuma tokea kujulikana kwake ikilinganishwa na taifa kongwe mno la Zanzibar.

No comments:

Post a Comment