Friday, February 8, 2013

KILA MZANZIBARI AMBAE HANA KITAMBULISHO CHA KITANGANYIKA HAPIGI KURA YA 2015 ZANZIBAR.VITIABULISHO VYA KIZANZIBARI VYA FUKIWA NA VITAMBULISHO VYA KITANGANYIKA.


MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA AZIDI KUIBURAZA ZANZIBAR KATIKA SHIMO NA KUJIMARISHA KATIKA UCHANGUZI WA 2015 MAZIKO YA WAZANZIBAR YAJA


Haya mambo mengine mapya hayo!!!!!
Jana Rais Jakaya Kikwete ameitaka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kufanya haraka haraka sana kukamilisha kazi ya utoaji w avitambulisho hivyo kwa sababu ndivyo vitakavyotumika wakati wa uchaguzi Mkuu wa 2015.Haya ameyasema mwenyewe Bob Kikwete jana wakati anazindua vitambulisho vya taifa — NIDA. vya KITANGANYIKA NDIVYO NINAVYO VITA MIMI MAANA SISI NI WAZANZIBARI SIO WATANGANYIKA.
Haya baadhi yetu tuliyajua mapema, kuwa Zanzibar itafunikwa tu na vitambulisho vya NIDA VYA KITANGANYIKA.
Lakini tujiulize NIDA imetoa vitambulisho vingapi kwa Wazanzibari..? Jawabu: ni vichache sana, na mpaka sasa wafanyakazi wa taasisi za umma pekee ndio waliohakikishiwa, na then, watapewa vitambulisho hivyo. Sisi tuliokuwa sio waajiriwa wa umma, itakuaje..? au hatuna haki...?
- Je, vile vitambulisho vya Uzanzibari vya nchi yetu tunayo ipenda zanzibar, itakuaje: vitatumika…..au ndio hivi vya NIDA vya Mfalme wa watwana wa kitanganyika mweusi ndio vitatumika?
- Je, ambao hawatabahatika kupata vitambulisho vya NIDA vya mkoloni mweusi, ndio hawatapiga kura..? ni yale yale yale yakuwa walete vitambulisho vya mkoloni mweusi kisha uchanguzi wa 2015 wazanzibari musipige kura wanyika waliojaa zanzibar watapiga kura kisha mutambiwa CCM imeshinda na sasa tunaeleke katika serekali moja au sio hivi….?
Inachekesha kidogo kuona kama kuwa Wazanzibari wameshindwa kupata ZAN-ID, lakini watapewa TANGANYIKA-ID..? Which is which; and which nation is superior than other..? Ipi halali, na ipi ni haramu...?
KUMBUKA: Kuanzishwa kwa NIDA (TZ-ID) hii haijaridhiwa na Baraza la Wawakilishi (BLW);na inashangaza kuona makosa haya kwa haya yanarudiwa kila siku (just… they take Zanzibar for a ride) wakitaka, wasitake watafanya tu. Huyo ndiye Kikwete, huyo ndiye Shein na timu yake (Maalim Seif VP1, na Balozi Seif Ali Iddi, VP2).
Mimi ninafahamu vizuri kuwa moja ya mkakati wa CCM kushinda uchaguzi kwa ‘nguvu’ au kwa ‘kishindo’ ni kutumia vitambulisho ili kupata ushindi, tabaan na BUNDUKI, mtutu wa BUNDUKI.
Hivi sasa, kwa upande wa Zanzibar, tayari wanatumia mfumo wa photocopy, kuiba ZAN-ID za watu tofauti ili kuzighushi na kutekeleza mradi wao huu wa wizi wa kura 2015. Hili liko wazi, na sio tena siri unless wabuni nyengine jipya.
Tujue kuwa hizi TZ-ID au NIDA-IDs, wamepewa kila mtu, mpaka wa-Congo, Wa-Burundi n.k (tokea lini ikawa na takwimu sahihi za watu na hususan wageni). Ni nchi isiyokuwa na mipaka wala makisio — ni nobody’s land. Mpaka wale wakimbizi wa Burundi pia wamepewa au watapewa hizo IDs. Na wote hawa kwa vile ni “Watanzania” pia watapiga kura hata Zanzibar.
Inasikitisha sana kuona pia Zanzibar inafanywa isiwe na mipaka. Mimi ninavyojua, nchi zote za visiwa ambazo ni jirani au ni sehemu ya bara (mainland county) kama Hong Kong-China (Mchina si rahisi tu kuingia huko na kutaka kuishi); au hata England (UK) na vikataa vyake kama wales, n.k — ipo control fulani. Leo Zanzibar kila atakaye AJE na apige KURA. Tunamalizwa na tunajimaliza.
Tunamalizwa kwa Katiba MPYA, ID mpya, Sera Mpya za CCM, viongozi wapya wa CCM akina Kinana na wenzake — hii ndio hali ngumu inayoikabil Zanzibar.
Wengine hamuamini, lakini ukitaka usitake hiyo ndio hali halisi ya Zanzibar. Tanganyika hawakubali kuitoa au kuiwacha Zanzibar hata siku moja. Tanganyika hata kama wapate mafuta, gesi, dhahabu, na ile ardhi yao igeuzwe kuwa almasi, lulu, na Zanzibar iwe vumbi tupu hawatoitoa na kuiwacha huru, na sisi hatutofaidika hata siku na chochote chao, lakini wao watafaidika na hilo vumbi – pia kwao ni tija WAZANZIBARI AMKENI AU ENDELEANI KULA BATATA ZA UROJO TU.

No comments:

Post a Comment