Wednesday, March 27, 2013

KATI YA CHADEMA NA CUF NANI NI CCM B..????

Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, kuelekea uchaguzi wa 2010 kilikuja na mkakati wa kupambana na vyama wenzake vya upinzani hususan CUF kwa lengo la kushikilia nafasi ya chama cha kwanza chenye nguvu cha upinzani. Kilitekeleza na kinaendelea kutekeleza mkakati huu kwa kutumia mbinu mbali mbali kama vile kukituhumu chama cha CUF na kukihusisha na Uislamu na Kukibandika jina la CCM-B. Pumbazo hilo lilisimamiwa vyema na CHADEMA na watanganyika wakapumbazika na kudhani CHADEMA ndio chama mbadala cha kuwatetea wanyonge na makabwela wa Tanganyika.
Sababu kuu iliyotolewa na CHADEMA juu ya u-CCM B wa CUF ni hatua ya kuundwa kwa serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar baina vyama vya CUF na CCM baada ya uchaguzi mkuu wa 2010. Chadema waliipa CUF tuhuma hii ya u-CCM B wakifahamu kwamba serikali hiyo ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar imeundwa ili kuzima chuki, ubaguzi, migogoro, hasama na mpasuko mkubwa wa kisiasa uliodumu Zanzibar kwa miaka mingi, na hivyo kuwa njia pekee ya suluhisho la wazanzibari kuishi kwa amani na utulivu. CHADEMA haikufurahia hayo na inafahamu kwamba hakuna chama kilichoungana na mwenzake kati ya vinavyounda serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar. Kila kimoja kati ya hivyo kina ajenda zake, mitazamo yake, misimamo yake na sera zake. Kila chama kati ya hivyo kinazisimamia itikadi na imani zake kwa nguvu zote. Jambo hili liko wazi kabisa kwani ukiachilia hali ya amani na utulivu iliyopatikana nchini Zanzibar tofauti za mitazamo na mapambano ya hoja na mijadala mikali baina ya CUF na CCM Zanzibar juu ya agenda mbali mbali za kisiasa zipo pale pale. Halkadhalika CHADEMA wanafanya hivi wakifahamu kuwa serikali za pamoja, serikali za mseto na serikali jumuishi ndio mifumo ya kisasa ya kiserikali duniani huku na wao wakiwa ni chama rafiki na vyama kadhaa vinavyounda serikali za aina hii duniani.
Uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu uliyofanyika nchini Zanzibar mwezi wa Septemba 2011 ndani mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa umeonyesha wazi kwamba hakuna vyama vilivyoungana kwani CUF ilipambana kama kawaida yake kudhibiti wizi wa kura unaofanywa na CCM miaka yote huku na CCM nao wakitumia ubabe na hata kufikia kutumia risasi za moto ili kushinda uchaguzi huo kwa hila. Hata hivyo wakati CHADEMA wakiita CUF ni CCM B, chama hicho kimekuwa kikitumia wanasheria wake na makada wake kuwatetea watuhumiwa wakuu wa ufisadi mahakamani. Chama hicho pia kimekuwa kikishuhudiwa kuwa na utamaduni wa kubadilishana wanachama baina yake na CCM. Utamaduni uliozoeleka wa mwanachama wa CHADEMA anapoamua kukihama chama hicho huhamia CCM badala ya kuhamia vyama vyengine vya upinzani ni suala linoloashiria usiri mkubwa juu ya kuwepo mahusiano maalum baina ya vyama hivi viwili.
 
 

hii ni siku ya uchanguzi wa bububu uliosababisha polisi kuwafatulia risasi wafuwasi wa cuf na kusababisha kifo cha mtoto mwenye umri wa miaka 14
 
Makada na matajiri wa CCM wazi wazi wamekuwa wakikifadhili chama cha CHADEMA kwa mamilioni huku CCM ikikaa kimya wakati Bahresa aliwahi kutuhumiwa tu kuifadhili CUF na kupelekea CCM kuharibu mali zake za mamilioni ya pesa. Baada ya kubainika suala hilo ni uzushi, Bakhresa alishinda kesi mahakamani na kulipwa fidia. Mbona Mustafa Sabodo hapokei bugudha yoyote katika biashara zake au kufukuzwa uwanachama wa CCM kwa tabia yake ya kuifadhili CHADEMA mamilioni ya pesa? Viongozi wa CUF walikuwa wakikamatwa ovyo na kufikia hadi kufungwa miaka kadhaa jela bila ya kuwa na hatia. Viongozi wa CHADEMA wanaonekana wazi wakihamasisha na wakifanya vitendo kadhaa vya kuvunja amani ya nchi huku CCM na dola ikiwatazama na ikiwaogopa na wao wanaendele kupeta tu
Jeshi la polisi likiandamana na kuwalinda CHADEMA katika barabara
 
Wanachama wa CUF walipoamua kudai haki zao dhidi ya unyanyasaji wa dola walikiona cha moto kwa kuvamiwa vijiji vyao, kuvunjiwa nyumba zao, kuibiwa mali zao na kuharibiwa mali zao, kubakwa, kupigwa risasi, kutiwa ulemavu na kuuliwa. Wakati hayo yamekuwa yakifanywa na CCM dhidi ya CUF inaonekana hali ni tofauti kwa CHADEMA, kwani ama huachiwa wafanye watakavyo au kwa ustaarabu polisi hupambana na CHADEMA bila ya kufanya unyama wa mauwaji ya kutisha kama wanavyofanyiwa CUF, ubakaji na uharibifu wa mali kama inavyofanywa kwa CUF na wana CUF kulazimika kuhama majumba yao na miji yao kwa miezi kadhaa huku familia zao zikiteseka. Hali hufikia mbali zaidi kwani viongozi wa dola huchukua hatua ya kuwaita viongozi wa CHADEMA na kuzungumza nao na kuweka makubaliano ili kuepusha shari jambo ambalo halikuwahi kufanywa kwa CUF. Ipi ni CCM B kati ya CHADEMA na CUF dungu msomaji tupe jibu..???
Kada wa CCM, Mustafa Sabodo akimkabidhi Mbowe burugu la mamilioni kama msaada wake kwa chama hicho cha CHADEMA.
 
Kama hilo halitoshi kiashiria kipya kimepatikana kinachowapa watanganyika ushahidi wa wazi kwamaba CHADEMA ni CCM iliyovaa nguo nyengine na kamwe haina nia wala shabaha ya kupigania maslahi yao. Kile kinachozungumzwa na Viongozi wa CUF kwamba Tanganyika ((Tanzania)) hakuna chama kinachoonyesha nia safi ya kupigania maslahi ya watu zaidi ya CUF kimebainika. Katika sura ya kuwashangaza wengi chama cha CHADEMA kupitia kurugenzi yake ya Ulinzi na Usalama kimekua kikiandaa utekaji nyara wa watu na kuwapa mateso mabaya kwa watu kadhaa kwa malengo tofauti ya kujitafutia umaarufu na kuwapumbaza watanganyika. Hili halina tofauti na vitendo walivyovizoea watanganyika vinavyofanya na dola na wanamgambo wa CCM vya kuwavamia watu na kuwapiga, kuwanyanyasa na hata kuwauma bila ya sababu za msingi.
Matokeo kadhaa ya utekaji nyara na utesaji hapa nchini yamekuwa yakiumiza haswa wazanzibari mpaka kufikia kuomba ukimbizi Kenya na nchi nyengine. vichwa vyao na mara kadhaa kutupiwa lawama idara ya usalama wa Taifa kuwa inahusika. Imebainika kuwa si idara ya usalama wa taifa pekee kumbe na idara ya usalama ya CHADEMA ni mwanafunzi aliyehitimu kutekeleza vitendo hivyo vya kimafia vya CCM. Mkanda wa video uliochukuliwa kwa utaalamu wa hali ya juu uliomrekodi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA sura halisi ya msingi wa utekaji nyara wa watu kadhaa hapa nchini na kuwatesa vibaya. Kiongozi wa Jumuiya ya madakatari Dr Ulimboka, mwanahabari mashuhuri Bwana Absalom Kibanda na wengine ni miongoni mwa watu waliotekwa nyara na kuteswa vibaya katika matukio tofauti.
Tanganyika na Zanzibar zimeshtushwa mno baada ya kupatikana ushahidi wa kutosha wa jambo hili kwamba kumbe CHADEMA na viongozi wake wanahusika katika kuratibu matukio haya kwa malengo binafsi na maslahi binafsi ya kisiasa ili kuwapumbaza watu. Inasemwa kwamba malengo makuu ya CHADEMA katika kufanya umafia huu ni 1. Kuyahusisha matukio hayo na idara ya usalama wa taifa kwa kuwa ndio iliyokuwa imezoeleka kufanya hivyo ili wananchi wazidi kuichukia serikali na CHADEMA izidishe matarajio umaarufu wake kupitia hadaa hiyo. 2. Kuwakomoa, kuwatisha na kuwaweka katika hali ya hofu na kutojiamini waandishi wa habari na wahariri ambao wanaonekana kuandika ukweli, kashfa na mwenendo usiofaa wa chama hicho na chama cha CCM pia.'
 
Mkurugenzi wa ulinzi na Usalama wa CHADEMA akiwa katika mpango wa utekaji nyara na umafia
natuone hatamu yake kama kweli ataishia jela au geresha tu kisha anachiwa na kula kuku wake
 
Watanganyika wanataka uchumi badala ya umasikini, wanataka amani badala ya mitafaruku na migogoro, wanataka umoja badala ya utengano na mifarakano, wanataka haki na usawa badala ya upendeleo na ubaguzi na ufisadi na wanataka kusonga mbele badala ya kurudi nyuma. Siamini hata chembe kama vita hivi vinaweza kushindwa kwa kufanya dhambi mbadala. Hivi ni kweli tunaweza kushinda rushwa kwa kuendesha vitendo vya rushwa mbadala..??? Kama hapana ndio hivyo hivyo hatuwezi kushinda vita dhidi ya maonevu na unyanyasaji unaofanya na CCM na dola kwa kufanya unyanyasaji mbadala tena dhidi ya wasio na hatia yeyote. Hivi ndivyo inavyofanya CHADEMA katika mwenendo wake mpya wa kufanya siasa zake za matayarisho ya kuchukua dola la TANGANYIKA na KULIONGOZA MWAKA 2015.
Siasa hizi za kigaidi na kijambazi za CHADEMA na viongozi wake ndio zinazopangwa kuitawala Tanganyika kigaidi na kijambazi pale watakaposhinda uchaguzi wa mwaka 2015. Watanganyika amkeni, si CHADEMA si CCM, vyote hivi si vyama vya kuyatetea maslahi ya watanganyika wanyonge. Vyote ni vyama vya unyanyasaji, mateso, uonevu, ukosefu wa huruma na ubinafsi. Tuviepuke kama ukoma. Mbadala wa siasa safi za Tanganyika na Zanzibar ni chama cha wananchi CUF chenye misingi imara ya kutetea haki sawa kwa watu wote vilivyo baki ni kufurisha matumbo yao na familia zao.


No comments:

Post a Comment