Saturday, March 2, 2013

MCHANGO KWA AJILI YA WANAFUNZI WA F4/F6 PEMBA YETU NA NDIO KWETU


President
Pemba Yetu Organization
CHANGIA ELIMU PEMBA, CHANGIA GHARAMA ZA WALIMU WALIOJITOLEA
KUFANYA TEACHING PRACTICE PEMBA
Assallam alaykum Warahmatullah Wabarakatuh!
Kwanza kabisa hatuna budi kumshukuru Allah SW kwa kila kitu ambacho ameturuzuku nacho sisi viumbe vyake, Alhamdulillah.
Kwa muda mrefu sasa wanafunzi wa Pemba wenye kumaliza Form 4 na Form 6 wamekuwa wakipata matokeo mabaya sana kama vile ambavyo tumewahi kutoa statistics katika wall ya Pemba Yetu.
Hivyo basi, uongozi wa Pemba Yetu kwa kupitia kiongozi wake ndugu yangu Sheikh Said Yunus au Abuu Yunus al Micheweny, ulifanya kazi kubwa ya kuwashawishi wanafunzi wanaosomea ualimu kwenda kufanya teaching practice kisiwa cha Pemba. Alhamdulillah, wanafunzi 115 wamekubali ombi hilo. Kati ya hao 105 ni wenye asili ya Pemba na 10 waliobaki ni wageni. Kuwalete wanafunzi hao Pemba kunahitaji gharama na Pemba Yetu imetathmini zoezi zima kugharimu kiasi cha 9,050,000/
(Milioni tisa na elfu hamsini)
Fedha hiyo itatumika kuwagharimia wale wageni 10 na pia kusaidia nauli kwa wale wanafunzi mia wa Pemba kwani wengi wao hawana pesa za mkopo na wanajisomesha wenyewe.
Ndugu yangu muislam, ndugu yangu Mpemba popote ulipo ulimwenguni, tunaleta ombi hili kwako, changia ulichonacho kufanikisha zoezi hili na jaza yako utaikuta kwa Allah SW. Kidogo ulicho nacho ni muhimu sana kwa shughuli hii. Haba na haba hujaza kibaba.
Wanafunzi hao wanatakiwa wafike Pemba mwanzoni mwa mwezi wa MARCH na kwa sasa siku zilobaki ni chache sana.
Pelekeni michango yenu kupitia wajumbe wafuatao hapa chini:
1. Arif Suleiman Mohammed - Dar es alaam……………0773-556-688​
* Mbarak Said – Dar ……………………………………………………..0773-60068
2. Maalim said Yunus - Zanzibar………………………………0776-399-494​
3. Mohammed al-Nabhany – Canada………………………..(416)854-1386​
4. Seif al-Khuzeiry – UK……………………………………………0794-053-4815
5. Nasser al-Ismaily – Gulf States………………………………….994-98306
Kwa watu wa Ghuba wanaweza kumwasiliana na Nasser al-Ismaily au waende kwenye
www.pembayetu.wix.com/pembayetu
kisha wachangie kwa kutumia PayPal na zitanifika hapa na kuziwasilisha pamoja na nitakazokusanya awamu ya pili. Au Tumia WorldRemit.com uzitume Dar Moja kwa moja kwa kutumia jina la Arif Suleiman Mohammed (PBZ- DAR), na namba yake ya simu iko hapo juu kwenye list. Njia hii ya Worldremit ni rahisi na haraka na pia charge siyo kama ya Western Union, yao ni ndogo sana.
Tunakuombeni mujitahidi kuchangia kwani muda haupo.
Tunatanguliza shukrani kwentu nyote.
NDIO KWETU TUKUTHAMINI TUKUJENGE.
 

No comments:

Post a Comment