Thursday, March 21, 2013

MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU!!! WAKATI MAITI ZA WANAWAKE ZILINAJISIWA HALIYAKUWA WANAWAKE WASHAKUFA.


John Okello alitoka kwao Uganda, Injin aliyetoka kwao Kenya na Mfaranyaki aliyetoka Tanganyika,wote hawa sio wazanzibari ni mitwana ya kutoka bara au nchi jirani na kuja kuivamia nchi huru usiku wa manane watu wamelala wa kuamkia tarehe12 Januari 1964. Wananchi, mafisadi kwa sababu ya maslahi ya nafsi zao hawakuhisi uchungu kuipoteza nchi yao, wala kuzipoteza roho za wazee wao, za ndugu zao na za marafiki zao. Kwa mujibu wa kitabu cha huyo aliyejipa ujamadari wa hayo 'mavamizi' ya Januari 12, 1964, John Okello, amesema kuwa watu waliyokufa katika 'mavamizi' hayo ni 13,000. Hii ni idadi ndogo kabisa aliyopenda kuitaja ila tukumbuke walikuwa ni Wazanzibari walio uliwa na mitwana ya kutoka Uganda,Kenya na Tanganyika. 

Ukatili, ushenzi na unyama uliofanywa katika visiwa hivi ulikuwa haujapata kutokea ulimwenguni kote kabisa kabisa tofauti na nchi hii ya Zanzibar ilivyokuwa na ustaarabu wa kupigiwa mfano, hauwezi hata kuhadithika. Wengi waliokuwa wanaijua Zanzibar, waliona taabu kuyaamini waliyokuwa wameyasikia yametokea Zanzibar kutokana na hayo yenye kuitwa 'mapinduzi matukufu astahafiru allah na anaeyaita ati ni muislamu'. Ilifika hadi, siku hiyo ya 'mavamizi' washenzi na makatili hao kuwanajisi maiti wa kike. Kitendo hicho hakijawai kufanyika katika nchi nyingi ulimwenguni za kunajisi maiti za kike lakini hapa zanzibar yametokea hayo na ni nchi moja katika nchi zenye ubinaadamu na ustaarabu wake. Lenye kuzidi kushangaza na kusikitisha ni kumsikia mwananchi mwenye kujulikana kuwa yeye ndiye mwongozi wa hao wenye kujiita "progressives" akasema kuwa, watu waliyouliwa katika hayo yenye kuitwa 'mapinduzi' ni 491! Duh! 

Mwenyewe Okello alieongoza hayo mauwaji amesema kuwa wamekufa wananchi 13,000. Hata wangekuwa watano tu, bali ni binaadamu, ni wananchi, jee, ndio wawe wamestahiki kuuliwa kwa kuvamiwa nchi yao na wageni ambao wewe na wenzio kama wewe mmechanganyika na hao wageni katika kuifisidi nchi na wananchi wake..? La kustaajabisha zaidi - ni pale ilipojulikana kuwa haya yote yalipangwa kabla - kwa siku 30 tu yaaani Desemba 10 mpaka Januari 11 ilitosha kujuwa uovu wa Serikali hata ikastahiki kupinduliwa..? Hata ingelikuwa ni ovu hivyo, bali njia za kuiondowa za kikatiba zilikuwepo ambazo zingaliweza kutumika, khasa na hao Wapinzani. Haikuhitaji hata kidogo kutumia nguvu. Lakini hakika khasa ni kuwa mambo yalikwisha pangwa zamani kuwa nchi ya zanzibar ivamiwe na washenzi na wafanye uchafu wao waliotaka kufanya na mumefanikiwa,na hayo yalikuwa ni matekelezo tu!!

mbona hamuwataji tena kwenye historia yenu kina 
1)Abdulwahid 
2)Ally Sykes 
3)Hamza Mwapachu,
4) Tewa Said Tewa,
5)Ali Migeyo , 
6)Suedi Kagasheki,
7)Dossa Azizi,
8)Abdulkarim Karimjee,
9)Chifu Abdieli Shangali wa Machame, 
10)Kleist Sykes,
11)Abdulwahid Sykes,
12)Othman Shariff KABURI LAKE LIKO WAPI TUMTILIYE UBANI..?
13)Kassim Hanga,KABURI LAKE LIKO WAPI TUMTILIYE UBANI..?
14)Twala,
15) Ringo,
16) Majura,
17) Saadalla, 
18)Aboud Nadhif, 
19)Mdungi Usi.
20)Luteni Hamoud Hamoud KABURI LAKE LIKO WAPI TUMTILIYE UBANI..?
21)Kanali Seif Bakar,
22)Jenerali Said Natepe,
23)Kanali Ali Mahfudhi  au ukipenda utamwita  Komandoo.
24)Faki Mohamed Faki,
25) Abdurahman Mohamed Babu,
26) Said Iddi Bavuai,
27) Saidi Washoto,
28)Ramadhan Haj.
29)mzee hassan nassor moyo,
30)mzee aboud jumbe,
31)mzee abeid amani karume.
wote hawa wako wapi sasa..? jibu ni wazee na wengine washakufa haswa hata hawapo tena duniani je Dr Kumbi Shein na kundi lako munajifunza nini kwa hawa watu wote waliokuwa wakijivuna na kupinga watu na kuuwa watu na kuthulumu mashamba ya watu na mali za watu na kuowa watoto wa kike bila ya ridha zao au wazee wao au hata kuwanajisi na kuwapiga bakora majela na kutesa watu kinyama wote wako wapi sasa..?? wako wapi sasa..?? mbona hata kidole chao hatukioni hapa ZANZIBAR..? basi mukae mukijuwa na nyinyi mtapita tu kama mvuwa ya masika.

No comments:

Post a Comment