Monday, March 18, 2013

NCHI YA TANGANYIKA TOKA IPATE UHURU MPAKA SASA MIAKA 50 MAJI SAFI YAMEWASHINDA KUWAPATIA RAI WAO.



Kwa miaka 25 iliyopita, Tanganyika imekuwa ikiadhimisha Wiki ya Maji hahahah bora ni cheke kwanza hahaha wiki ya maji, tukio ambalo mwaka huu limeanza juzi, Machi 16 na linafanyika Mkoani Lindi kwa kaulimbiu, ‘Mwaka wa ushirikiano wa maji kitaifa’.
Kihistoria, Wiki ya Maji huadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kuwaelimisha, kuwahamasisha na kuwashirikisha wananchi katika utekelezaji wa sera ya maji, mikakati na mipango iliyopo katika sekta ya maji.
Maadhimisho hayo pia hutumika katika kupima mafanikio yaliyopatikana katika mwaka uliopita ambayo hapa nchini Tanganyika hayapo, matatizo na changamoto zinazoikabili nchi na mikakati iliyowekwa ili kupata ufumbuzi wa matatizo hayo katika kuboresha utoaji wa huduma ya majisafi, usafi wa mazingira na pia katika usimamizi wa rasilimali za maji zinazopatikana mijini na vijijini.
Kwa jumla, maadhimisho hayo hufanyika nchini kote katika ngazi ya kitaifa, mkoa na wilaya.
Chanzo cha wiki hiyo
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) mwaka 1992 lilipitisha Azimio Namba 47/193 likipendekeza kuwa  Machi 22 kila mwaka iwe Siku ya Maji Duniani.
Mwaka huu maadhimisho  hayo yanafanyika mkoani Lindi kwa kaulimbiu ya ‘mwaka wa ushirikiano wa maji kitaifa’.
Lakini, je, wewe kama Mtanganyika mjini au kijijini unaweza kujiuliza, je, hali ya upatikanaji maji nchini ikoje hadi sasa..?
Jibu lake ni rahisi, kwamba wengi wa watu nchini Tanganyika,kuanzia mijini na vijijini wanaishi, kutumia maji yasiyo safi na salama.
Azma  ya kuwapatia huduma ya maji iliyowekwa tangu awamu ya kwanza ya utawala wa Tanganyika, chini ya Mwalimu Julius Nyerere na kufuatiwa na awamu nyingine tatu zilizofuata ya kumfikishia mwananchi maji kwa umbali wa mita 50, inaonekana imeshindikana na zimegonga ukuta maana sasa ni 2013 miaka 50 ni nusu karen hiyo na mpaka leo mijini maji hakuna wachilia mbali vijijini.
Watalaamu wa sekta ya maji, afya nchini, kwa upande wao wanaeleza kuwa upatikanaji wa maji salama ni muhimu katika kupigana na umaskini na matatizo ya afya.  
Wanaeleza kuwa watu maskini wengi wao ambao huishi vijijini wana nafasi finyu ya kupata maji safi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kwa ajili ya mazao na matumizi ya afya.
Faida za uchumi zinaweza kupatikana siyo kwa njia ya moja kwa moja tu, bali kwa kuwa na afya bora na kuokoa muda unaotumika kuhangaika na kazi za kuchosha za kubeba maji kwa umbali mrefu kwa mageleni.  
Tatizo kubwa la wanawake, watoto kufuata maji kwa umbali mrefu ni sugu linawakumba wananchi wengi mijini na vijijini ambako upatikanaji wa maji si wa uhakika, miaka 50 baada ya uhuru, haupo uhuru hata enzi za mkoloni basi maji hayakuwa na tabu hii sasa nchi ina uhuru na inadidimia kila siku maji na umeme vimo midomoni mwa watu na wala matatizo hayatatuliki.
Takwimu zinaonyesha kuwa magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya maji hupatikana zaidi katika sehemu ambapo watu wanatumia zaidi maji yaliyoambukizwa au hawana maji ya kutosha kwa matumizi yao ya kila siku.

No comments:

Post a Comment