Wednesday, March 13, 2013

SEREKALI YA DR KUMBI SHEIN YASHINDWA HATA KUZIBA MITARO NA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO


MVUA kubwa imenyesha mjini hapa kuanzia usiku wa kuamkia jana na mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi amepoteza maisha…
Mwanafunzi huyo alikufa baada ya kutumbukia kwenye mtaro ambao haujajengewa toka serekali hii ya madhali kuingia madarakani na mwenzake wakati walipokuwa wakilipisha gari lilolokuwa likienda kwa kasi karibu na shuleni kwao Kijitoupele nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Kaimu Kamnda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Haji Abdallah Hanna alimtaja mwanafunzi aliyekufa kuwa ni Munaifat Abdallah Mussa wa Maili Nne kati ya Mwanakwerekwe na Fuoni.
Alisema tukio hilo lilitokea saa 1 asubuhi wakati wanafunzi hao wakitoka nyumbani kwenda shuleni.
Kamanda alisema baada ya watoto hao wawili wa shule ya msingi kutumbukia mmoja aliokolewa hapo hapo na aliyekufa alichukuliwa na maji na maiti yake ilipatikana baada ya msako uliofanywa na Zimamoto, Polisi na wananchi.je waziri wa miundo mbinu atajiuzulu kwa tukio hili..?
Alieleza kuwa maiti iliyokuwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja jana ilikabidhiwa kwa ndugu wa marehemu na ilitarajiwa kuzikwa siku hiyo hiyo.
Kamanda aliwataka wazazi kuwachunga watoto wao katika kipindi hiki cha mvua na kuwataka madereva wa magari kuchukua hadhari wanapowaona watoto wako barabarani

No comments:

Post a Comment