Thursday, April 4, 2013

DPP MASHUZI NCHINI ZANZIBAR ALITUPILIA MBALINI FAILI LA UCHUNGUZI WA MAUWAJI YA PADRI MUSHI MBONA LA UAMSHO BADO UNALIKUMBATIA.????Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP MASHUZI) wa nchi ya Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim, ametupilia mbali uchunguzi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na kusema mtuhumiwa hana kesi ya kujibu mahakamani.
Padri Mushi ambaye alikuwa Paroko wa kitanganyika ishie hapa nchini Zanzibar wa Kanisa Katoliki Minara Miwili aliuwawa akiwa ndani ya gari lake.
Baada ya mauaji hayo, Rais Jakaya Kikwete alitoa kibali cha kukaribisha maafisa wa (FBI) kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa mauaji hayo na Machi 17, mwaka huu Jeshi la Polisi lilimkamata Omar Mussa Makame ati kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo ila ukweli ni kuwa pengo aliwatolea ukali polisi ndio wakaona bora wambambikia kesi hii Omar Mussa Makame na cha ajabu Kikwete alipouliwa sheikh kitope kwa kupigwa mapanga hakuita (FBI) wala (CIA) KABANA KIMYA .
Uchunguzi wa free zanzibar people from mkoloni mweusi umebaini kuwa (DPP MASHUZI) wa nchini Zanzibar baada ya kulipitia jalada la uchunguzi aliyesingiziwa mauaji hayo, juzi alitoa mwongozo kwa Jeshi la Polisi kuendelea kumtafuta muuaji wa Padri Mushi.!!!!!! sasa huyu aliyesingiziwa kauwa vipi achiwe au...??
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, (DPP MASHUZI) aliliandikia barua Jeshi la Polisi na kukabidhiwa juzi ikieleza sababu za ofisi yake kutofungua hati ya mashtaka hadi sasa dhidi ya mtuhumiwa wa mauaji hayo.
Jeshi la Polisi limethibitisha kuipokea barua ya (DPP MASHAZU) ambayo inaeleza kuwa ushahidi uliokusanywa katika jalada la kesi hiyo hauna mashiko na kwamba mtuhumiwa hahusiki na mauaji hayo. VICHEKESHO NA AIBU KWA POLISI NA DPP MASHUZI PIA.
Chanzo cha habari kutoka Jeshi la Polisi kilieleza kuwa (DPP MASHUZI) hajaridhishwa na uchunguzi wote uliokusanywa dhidi ya mtuhumiwa pamoja na watuhumiwa watatu wanaotuhumiwa kwa mauaji ya askari polisi, Said Abdulrahman aliyeuawa kwa kupigwa mapanga na watu wanaosingiziwa kuwa wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar Oktoba 17, mwaka jana hii ni thahiri shahiri kuwa polisi (DPP MASHUZI) na serekali zinazidi kuibika na kufetheheka na zaidi watu kuwaelewa kuwa wote sio wasomi bali ni mashaghala bala walio pachikwa vyeo kwa hiyo hawajuwi kazi zao ila wanajuwa kumbambikia watu kesi zisizo wahusu kabisa.
Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini Zanzibar, Mussa Ali Mussa na mijino yake, alithibitisha hatua ya (DPP MASHUZI) kutupa uchunguzi wote wa jalada la mauaji ya Padri Mushi na kuwataka waandishi wa habari kumtafuta (DPP MASHUZI) azungumzie sababu za uamuzi wake wa kutokubaliana na uchunguzi wa Polisi kwa kesi hiyo na sisi wandishi wa habari tunataka kujuwa pia faili la uamsho je linaushahidi ndio maana bado wako gerezani na kama ndio mbona sasa kesi zinafutwa kwa kuto kamilika uchunguzi na kama sio je mbona hawawachi na wakiwawachia wako tayari kuwalipa kwa kuwaweka gerezani miezi yote hii hali wakijuwa kuwa hawana makosa...??????????
Hata hivyo,Mussa Ali Mussa mtumwa wa Watanganyika alisema kwamba Jeshi la Polisi bado linaamini uchunguzi walioufanya kwa kushirikiana na FBI hauna shaka na kwamba mtuhumiwa huyo ana kesi ya kujibu mahakamani na wataendelea kumshikilia!!!!!! swali letu sisi kwa Mussa ni kuwa (FBI) waliondoka nchini hata wewe mwenyewe hukujuwa kama wameondoka sasa huo unchunguzi mulio fanya nao mumefanya vipi ikiwa watu wenyewe hujuwi kama wameondoka....????
Alisema kwamba kwa mujibu wa sheria, Jeshi la Polisi jukumu lake ni kuchunguza kesi na ofisi ya (DPP MASHUZI) jukumu lake ni kufungua hati ya mashtaka na kutetea kesi mahakamani je mussa unamfundisha (DPP MASHIZI) KUFAANYA KAZI YAKE....????
Hata hivyo,Mwandishi wetu wa siri wa free zanzibar people from mkoloni mweusi alipofika katika ofisi ya (DPP MASHUZI), Katibu muhtasi wake alisema amepokea maagizo kutoka kwa bosi wake kuwa waandishi wote wa habari wanaofuatilia suala hilo, wamuone Kamishna wa Polisi kwa vile kazi aliyopewa ya kupitia jalada la uchunguzi kabla ya kufungua kesi ameikamilisha hapa tukaona kuwa tunapingwa danadana (KAMISHNA MIJINO) anasema nendeni kwa (DPP MASHUZI) na (DPP MASHUZI) anasema nendeni kwa (KAMISHNA MIJINO).
Katibu muhtasi akiendelea kusema Kamishna ndiye aliyeitisha mkutano na waandishi wa habari au sio alihoji kisha akaendelea kusema kuelezea hatua iliyofikiwa pamoja na kukamatwa kwa mtuhumiwa, sasa awaite tena amalizie kazi yake ya kuwaeleza hatua iliyofikiwa baada ya Mkurugenzi kurejesha jalada la mauaji,” alisema Katibu muhtasi huyo ILIBIDI TUCHEKE KIDOGO HAHAHA maana imekuwa kama watoto wa darasa la kwanza au la pili.
Katika hatua nyingine, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Yusuph Ilembo, jana alifika katika Mahakama Kuu ya Zanzibar, kufuatia ombi lililofunguliwa mahakamani na wakili anayemtetea mtuhumiwa wa mauaji, Abdallah Juma Mohamed.
Abdallah Juma amefungua ombi katika Mahakama Kuu kwa kutumia kifungu cha sheria 390 cha sheria namba 7 ya mwenendo wa makosa ya jinai ya mwaka 2004, akitaka Jeshi la Polisi litoe maelezo kwa nini mteja wake hajafikishwa mahakamani ndani ya saa 24 tangu alipokamatwa Machi 17, mwaka huu.
Wakili Abdallah Juma akisaidiwa na mawakili Shaban Juma Bakari na Shaibu Ibrahim Shaibu waliitaka Mahakama Kuu itoe amri ya kuachiwa kwa mteja wao kutoka mikononi mwa Jeshi la Polisi. Hata hivyo, Ilembo alisema kuwa kutokana na uzito wa kesi hiyo, anaomba kupewa muda wa kutayarisha majibu ya hati ya kiapo kwa maandishi na kuuwasilisha kwa upande wa utetezi na mbele ya mahakama hiyo kabla ya ombi hilo kuanza kusikilizwa na kutolewa uamuzi.
“Tunaomba mtuhumiwa aendelee kushikiliwa na Polisi, wakati tukifanya matayarisho ya kujibu hati ya kiapo,” alisema Ilembo.
Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu, Mkusa Isaack Sepetu, alisema baada ya kusikiliza pande zote mbili, alimtaka Ilembo awe amejibu kwa maandishi hati ya kiapo ya maombi hayo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo Aprili 8, mwaka huu.
Aidha, Jaji alisema wakati wa kusikilizwa kwa shauri hilo, ametaka mtuhumiwa huyo afikishwe mahakamani, baada ya hoja za upande wa mawakili wanaomtetea kutaka dhamana kwa mteja wao, kwa vile bado hajafikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.
Kutupwa kwa uchunguzi wa jalada la mauaji hayo pamoja na jalada la uchunguzi wa mauaji ya Polisi kunadhihirisha kuwapo kwa mvutano mkubwa baina ya Jeshi la Polisi nchini Zanzibar na ofisi ya DPP MASHUZI pia inatuonyesha sisi wazanzibari kuwa wote hawajuwi walifanyalo na wala hawajuwi kazi zao ila ni fitna na chuki na kubambikiana kesi kwa kutumia vyeo vyao basi ila mkae mkujuwa mwenye kuthulumiwa duwa yake haina pazia nyinyi jidanganyeni na vyeo vyenu wenzenu walikuwa kama nyinyi wako wapi sasa...??

No comments:

Post a Comment