Thursday, April 4, 2013

KANZA NAHODHA KUFITINISHA WAZANZIBARI SASA VUAI ALI VUAI ANAENDELEA ILI WAWAFURAHISHE WAFALME WAO MACHOGO YA TANGNYIKA.



Maridhiano yaliyofikiwa Zanzibar kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) na kuwezesha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa yako hatarini baada ya CCM kumtupia lawama nzito Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, kwamba amekiuka makubaliano hayo yaliyofikiwa mwaka 2010.
Aidha, CCM kimemtupia lawana Maalim Seif kwamba anafanya vitendo vya kuhatarisha amani nchini humo.
Akihutubia mamia ya wanachama na mashabiki wa CCM vichwa vya samaki waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika Jumba la Vigae huko Jang’ombe mjini hapa jana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alidai kuwa Maalim Seif ameanza kufanya vikao vya siri vinavyotishia kuvuruga amani na umoja wa kitaifa visiwani humo.
Vuai ambaye ni kati ya wajumbe walioshiriki katika mchakato wa mazunguzmzo yalioleta upatanishi na kufikia muafaka wa kisiasa Zanzibar, alisema kama angejua mapema dhamira ya Maalim Seif katika mazungumzo ya kundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, angekuwa radhi kujitoa katika mazungumzo ya kufikia muafaka.
Alisema kwamba hivi karibuni Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF, aliitisha kikao maalum cha vijana wa chama chake na kusema kuwa ikiwa chama chake kitawaamrisha vijana kufanya vurugu, nchi haitatawalika na ikibidi jahazi litote na kujaa maji.
“Msingi wa mazungumzo yetu katika awamu zote za kusaka maridhiano ya kisiasa yalihimiza kujengeka kwa amani, utulivu kuimarisha misingi ya umoja wa kitaifa,” alisema.
Vuai aliita kauli hiyo ni ya kichochezi na kwamba haikubaliki mbele ya jamii hivyo aliwatolea wito viongozi wa kisiasa na kiserikali kuchunga ndimi zao ili kuyaenzi mazingira yaliyoleta amani, umoja na utulivu uliopo visiwani hapa.
“Kama anahitaji jahazi litote tugawane mbao ni kheri akachukua mapema ubao wake na kuelekea Mtwambwe (Pemba), lakini hatuko tayari kuona amani ya Unguja ikichezewa na kupotezwa kwa maslahi binafsi,” alisema Vuai.
Vuai aliendelea kudai kuwa miongoni mwa mambo waliokubaliana katika mchakato wa mazungumzo ya kusaka muafaka ni kuwaasa wanasiasa wasitoe kauli na matamshi makali yanayoweza kuibua mpasuko wa kisiasa.
Alisema kwa muda wa mwaka mmoja CCM kimekuwa hakifanyi mikutano ya hadhara kwa kuheshimu makubaliano hayo, lakini cha ajabu viongozi wa CUF wamekuwa wakiendesha mikutano yenye lengo la kuirudisha nyuma Zanzibar.
Akizungumzia madai ya kuwepo kwa utata katika Muungano, Vuai alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni halali na kuwataka wanasiasa wanaopotosha jambo hilo kukaa na kutafakari kwa kina faida zitokanazo na kuwapo kwake na athari ikiwa Muungano huo utavunjika.
“Ikiwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utavunjika, nafikiri huenda hata utulivu na maelewano kati ya Unguja na Pemba nayo yanaweza kutetereka, wanaopigia debe na kulishabikia jambo hilo litokee wanahitaji kupima pepo za nyakati na ikibidi waepukwe badala ya kuwashabikia,” alisema Vuai.
Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu, alisema sera ya CCM katika Muungano ni kuendelea na mfumo wa serikali mbili na kwamba hakuna mpango wa kuwa na serikali ya mkataba au kuvunja Muungano uliopo.
Muandishi wetu wa siri alijaribu kumtafuta Maalim Seif jana ili kujibu madai hayo, lakini mara zote alizopigiwa simu yake iliita bila kupokelewa.
Katibu wake, Issa alipoulizwa na Muandishi wetu wa siri jana alisema hawezi kujibu lolote kwa kuwa madai hayo yalitolewa katika jukwaa la siasa na yeye ni msaidizi wa Maalim Seif upande wa serikali.
Hivyo akashauri aulizwe Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF, Salim Bimani.
Baadaye, Muandishi wetu wa siri alimtafuta Bimani, lakini simu yake ilikuwa imezimwa.mpaka hapo tukawa hatuna la kusema ila kurudi mitamboni na kusema kuwa nahodha na vuai wameanza choko choko zao maana wanaona ni kimya sasa mashekhe washawafunga sasa wanatafuta la kuiangamiza CUF hawa kweli wanaitakia Zanzibar mema hawa..??? kwanza wewe ni kama nani usime kuwa hakuna cha muungano wa mkataba kwani hii Zanzibar na ya baba yako au ya marehemu babu yako kakuandikia au ndio unatowa maoni yako kwa jili ya katiba mpya ya wafalme wako Tanganyika..???
Zanzibar ni yetu sote na sote ndio tutakao amuwa kama ni mkataba,kuvunja au kubaki katika muungano musijidai kusimama majukwani na kupiga debe ili mkoloni wenu mweusi Tanganyika aone mnafanya kazi vizuri tuungeni au tupigeni vita lakini mujuwe nchi hii ni ya Wazanzibari wote sio ya vuai wala nahodha wala CCM na mukiendele na fitna zenu basi mujuwe siku tukivunja muungano nyinyi muwe mushakwenda dodoma kuishi huko la sivyo nyote tutawashataki kwa kuwasaliti Wazanzibari na kuizamisha nchi ya Zanzibar katika makucha ya wakoloni weusi Tanganyika kwa jili ya faida yenu na mitumbo yenu isiyo shimba baada ya kuiba kote mliko ibaa.

No comments:

Post a Comment