Tuesday, April 30, 2013

SHEIN ASEMA SIMUOGOPI MTU((HUYU KAEKWA ILI AWASHUGHULIKIE WAZANZIBARI WANAO DAI ZANZIBAR HURU


Waziri asiye na wizara maalum wa Zanzibar, Dk.Kumbi Ali Mohamed Shein amesema Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (JUMIKI) hawana ubavu wa kuwaamsha Wazanzibari kwa kuwa wananchi wake wamekwisha amshwa kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.
Dk. Kumbi Shein alitoa tamko hilo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika tawi la CCM Kinuni na kuwahutubia wananchi katika ziara yake ya kukagua uhai wa chama chake visiwani  nchini Zanzibar, juzi.
Dk Kumbi Shein alisema kuzinduka kwa wananchi na kupigania haki zao kasi yake iliongezeka kuanzia mwaka 1957 pale jumuiya mbili za Waafrika na Washiraz zilipoungana na kuzaliwa kwa chama cha Afro Shiraz Party (ASP).
“Uamsho unamuamsha nani, ni nani aliyelala wakati Wazanzibari waliamka kitambo na ilipofika mwaka 1964 wazee wakafanya Mapinduzi ya umma yaliyoongozwa na Mzee Abeid Karume,((karume hakuongoza alikuwa Tanganyika alikimbia ni john okello kama hujuwi historia kasome tena))”alisema Dk Kumbi Shein.
Alisema watu wanaofanya vitendo vya vurugu ikiwamo uharibifu wa mali na kuchomwa moto kwa matawi na maskani za CCM serikali yake haitawavumilia kwani mikono ya sheria itawakamata.((kwa kuwa mwanao ni jaji utafanya utakavyo))
Alisema nchi nyingi duniani zimesifia((tutajie majina ya hizo nchi))  muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ((Tanzania)) ikiendelea kupata sifa kutokana na kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, kuwapo kwa misingi ya demokrasia na kufuata utawala bora wa sheria.((wakuwaweka masheikh jela bila ya thamana na kuipiga kesi yao dana dana ndio utawala bora na sheria huwo kumbi shein..??))
Dk Kumbi Shein aliyasema hayo baada ya wananchi kulalamika mbele yake kuwa tawi moja la chama hicho katika eneo la Kununi kuchomwa moto na watu wasiojulikana zikiwamo na maskani kuu za Kisonge na Kachorora mjini Zanzibar.
“Siogopi mtu ila mimi hufanya kazi kwa mujibu wa katiba na sheria,((katiba ipi ya zanzibar au ya bwana wako Tanganyika mkoloni mweusi aliyekuweka madarakani..??)) sitomchelea kiongozi yeyote anayevunja sheria za nchi, Zanzibar ni yetu sote, ili tuishi kwa amani ni wajibu wetu kutii sheria zilizopo,”alisema.
Alisema watalii na wageni mbalimbali mashuhuri duniani huitembelea Zanzibar na kuingiza asilimia 80 ya fedha za kigeni kupitia sekta ya utalii na kwamba vitendo vya fujo na vurugu ni sawa na kuwafukuza watalii wakati ndiyo nguzo ya uchumi wa Zanzibar.
Alisema Zanzibar kwa asili yake haina historia ya matukio ya uchomaji moto kwa mali za serikali au watu binafsi na kuwaonya wanaofanya vitendo hivyo watafute kazi za kufanya kwa vile serikali yake imeshaamua kupambana nao kwa gharama yoyote.
Alisema vitendo vya vurugu na ghasia vilivyojitokeza mwaka jana haviwezi kukubalika katika nchi inayoongozwa kwa misingi ya utawala wa sheria na kuwaasa vijana wakatae kutumiwa na wanasiasa waliopoteza mwelekeo kwa kutafuta mafanikio ya kisiasa kwa njia za mkato.                        

((WEWE MWENYEWE HUKUSHINDA UCHANGUZI WA RAISI KILA MOJA ANAJUWA UKATUMIA NJIA YA MKATO YA MAJESHI YA KITANGANYIKA SASA UNAJIAMBIA MWENYEWE 

No comments:

Post a Comment