Sunday, April 28, 2013

SHEIN HABU KUBALI YAISHE KAMA WEWE SIO RAISI HEBU KUBALI DAAAAAAAAAH


MARAISI WATANO WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI WAKUTANA JIJINI ARUSHA NCHINI TANGANYIKA ZOMBI SHEIN UKO WAPI..?? AHAA NIMEKUMBUKA WEWE SI RAISI NI WAZIRI USIYE NA WIZARA UMEWEKWA HAPO UWATESE WAZANZIBARI WANAO TAKA NCHI YAO YA ZANZIBAR KUTOKA KATIKA MAKUCHA YA TANGANYIKA NDIO KAZI YAKO.
Arusha. Marais watano wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, wanakutana jijini hapa Arusha nchini Tanganyika katika mkutano wa dharura, ambapo pamoja na mambo mengine watajadili itifaki ya umoja wa fedha katika nchi za Afrika ya Mashariki, kabla ya kutiwa saini Novemba mwaka huu.
Marais hao ni Yoweri Kaguta Museveni Rais wa Uganda, ambaye ndiye Mwenyekiti, Jakaya Kikwete wa Tanganyika, Pierre Nkuruzinza wa Burundi, Paul Kagame wa Rwanda ambaye hayuko pichani na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta,je ((Dr Kumbi Shein Zombi..??)) wote walitarajiwa kuanza kuwasili jana Arusha.
Kenyatta anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa leo, kwani atakuwa anahudhuria kwa mara ya kwanza katika vikao vya EAC jijini Arusha nchini Tanganyika kama Rais wa Kenya.
Katika kikao cha marais hao, ambacho kitafanyika kwenye Hoteli ya Ngurdoto, pia anatarajiwa kuapishwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki anayetokea Kenya, Charles Njoroge na pia kuapishwa majaji wawili wa Mahakama ya Afrika ya Mashariki, Dk Faustin Ntezilyayo kutoka Rwanda na Liboire Nkuruzinza kutoka Burundi.
Kikao cha marais hao, kilitanguliwa ni kikao cha makatibu wakuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na pia Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari ya Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Richard Sezibera, alisema mawaziri wa jumuiya hiyo, pia walijadili itifakiwa umoja wa fedha kwa nchi hizo na taarifa yao itapelekwa kwa marais leo.
Pia mawaziri hao, walijadili bajeti ya jumuiya hiyo ya mwaka 2013/14 ya Dola 117,238,966, walijadili pendekezo la kuongezea wigo na mamlaka Mahakama ya Afrika ya Mashariki na pia undaaji wa itifaki ya haki na kinga kwa watumishi wa jumuiya ya Afrika ya mashariki.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa Afrika ya Mashariki wa Tanganyika, Samweli Sitta alisema tayari baraza la mawaziri, limepitisha bajeti ya jumuiya hiyo na taasisi zake zote.
Sitta alisema kuhusiana nauuamuzi wa masuala mbalimbali ambayo yalijadiliwa na mawaziri hao, taarifa rasmi itatolewa leo na marais baada ya kuyapitia .
Hata hivyo, alisema katika kikao cha mawaziri, Kenya iliwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Kenya kwa kuwa bado Waziri wa Kenya hajathibitishwa na bunge.((je mwanasheria mkuu wa Zanzibar anaejikuna kama anaupele wa ukurutu mbona hajatuwakilisha Wazanzibari..??))

No comments:

Post a Comment