Tuesday, April 23, 2013

SHEIN NA KIKWETE WAKO HAMUNA UWEZO WAKUWATESA MASHEIKH ILA MUNAJIPALIA MKAA WENYEWE WAKWENDA KUWACHOMA VIZURI SIKU YA KIYAMAA.


makame silima
Wazanzibar wengi wanashindwa kufahamu matatizo ya Muungano hasa yapo wapi..???
Wengi husema ni Tanganyika yani (Watanganyika) mimi sikubaliani na hili moja kwa mmoja, Chanzo hasa cha Muungano ni Wazanzibar wenywe .
Nasema hivi kwa ushahidi kamili na kama kuna wakunipinga alete hoja zake hapa zifanyiwe kazi.
Wazanzibar tumejigawa ndio maana Watanganyika wakautumia mwanya huu na vivuli hivi kufanya watakavyo,Kama isingelekuwa hivyo basi tungekuwa na Zanzibar yenye heshima nje na ndani na Tanganyika yenyewe ingeliheshimu Zanzibar kama nchi na sehemu Moja kuu kubwa ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Lakini wapi..?? tumeyatupa wenyewe yani wahafidhina walitupeleka ovyo na wanazidi kutupeleka ovyo kwa kukumbatia  CCM na kuuwacha Uzalendo na Mapenzi ya nchi yao Zanzibar, hili limewapa Mwanya hata Watanganyika na wenye asili ya Tanganyika kujiona wao ni Bora zaidi kuliko Wazanzibar ndio mzanzibar yoyote mwenye asili ya Tanganyika huwa yuko Tayari kuisaliti Zanzibar kwa kuipigania Tanganyika Ijitayo ((Tanzania)) kuendelea kuibinya Zanzibar.
Ikiwa Wazanzibar wenyewe wana wapa priort ya hali ya juu na kuwapa hata nafasi kubwa wageni na kuwapa kipau mbele huku wakiwanyima Wazanzibar asili tutegemee nini mbeleni..?? nikutoka katika Bad kuingia katika Warst.
Kilicho tawala Zanzibar ni ubaguzi,Chuki , Husda na Choyo , hizi ndio kero kubwa za Muungano na tutashindwa kufanya lolote kama tutaendelea nazo hizi , nyiyi hamuoni kila heri ikija na ikichanua hufuia kwa mambo haya.
Ndani ya nafsi za Wananchi wa Zanzibar mambo haya ndio yenye kututeketeza na kuiteketeza Zanzibar , Zanzibar imekuwa kama mtoto yatima asie na walezi.
Chuki zinapaliliwa hasa na hao wajitao Wahafidhina wengi wao wana nundu za Sijda lakini nafsi zao ni wabaguzi wakubwa na chuki na fitna ndani ya nyoyo zao huyu nani huyu nani.
Katika Serekali ya SMZ-GNU  na baraza lake la Wawakilishi takribani % 100 ni Waslima lakini % 100 hio hio ni Wanafiki na wasio juwa hata uislamu ni nini na jambo hili ni aibu kwa hulka ya Wazanzibar kuwa asilimia ya Viongozi wake ni Wanafiki tena Unafiki wao hivi sasa umeshika kasi na Ubaguzi.
Leo mtu anasthamini Sera za Chama na itikadi za Chama kuliko Dini ya Mwenyewe M/mungu.?? na mtu huyo ana chukuwa chuki za kisiasa kwa kuwahilikicha Mashekh wetu na maulamaa wetu kwa misimamo tu ya chuki za kisiasa..?? ama kweli Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un (إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ).
Tuangalie mifano hai hapa hapa Zanzibar ya viongozi wetu walivyo mbali na Dini ya Allah na wafuasi wake na wajumbe wake.!!!  Wanapokufa Mashekh kiongozi unae muona ni mmjo huyo huyo siki zote lakini Wakifa Mapadri hata Mikowani Tanganyika basi viongozi nusu ya SMZ-GNU huenda akiwemo Shein.
Padri akifa hapa Zanzibar tena ndio usiseme Serekali yote huenda kuzika kisha wakaja kukaa matanga, Lakini wakifa Mashekh hata habari hawana ,kafa Sheikh Nassor Bachu zaidi ya Ummati wa Wananchi viongozi wa Serekali ni Maalim Seif huyo huyo na Waheshimia wa-CUF .
Lakini Kafa Bi Kidude angalia Serekali ya Muungano yote ilikuweko Mazikoni na Matangani Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un (إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ).
Huu ndio ubaguzi na Jambo jengine wananchi angalia Mashekh wetu wanavyo teseka Magerezani huu hivi sasa ni mwenzi wa 5 kama sikosei wanakosa kutowa dawa ,wanakosa kusomesha ,wanakosa hata sala za ijumaa kusali na kutowa dawa hizo sala na kusoma masahafu naskia mwanzo walinyimwa humo ndani walivyo fanywa ni sistem ile ile ya Wantanamo Cuba.
Jee kweli Huyu Shein ni Muislamu kweli huyu na anaongoza jamii ya waislamu wa Zanzibar au anafuata itikadi za kitahuti na ubaguzi wakidini.??
Maana ikiwa anafuata sera na itikadi za Chama chake basi hata hizo sera za chama chake hazifuati!!! Wao viongozi wanafiki si wanasema Serekali haina dini yani Zanzibar na Tanganyika ((Tanzania)) haina dini..?? Sasa tuangalie kweli Serekali haina dini au inayo dini ina ikingia kifua Serekali.
Rais wa Muungano wa ((Tanzania)) Mrisho Jakanya Kikwete Jee huyu si Muislamu.?? Rais wa Zanzibar aliye wekwa na mkoloni mweusi Tanganyika  Dr Kumbi Ali Mohammed Shein , Jee huyu si Muislamu..??
Sasa marais wote hawa hawajuwi kuwa kusema Na Bii Issa Nabii Issa (Alayhis salaam) kuwa ni Muungu ni kosa kubwa kwa uislamu na Waislamu na nisawa na kuibua hasira mbele ya Waislamu mbona Maskofu na Mpadri na wanao wachunga makanisani na mitani huhubiri na kusema Hazarani kuwa Nabii Issa ni Mungu.!!! jee hawa mbona hawachukuliwi hatuwa zozote za uchochezi..??
Bali kuna Kijana Yule alofungwa Miezi 6 eti kakashifu dini ya watu na kuleta uchochezi wa kidini kusema Nabii Issa( Yesu sio Mungu ni Nabii wa M/mungu.)
Jee Ali Mohammed Shein kuna Padri yoyote uliomchukulia hatua hapa Zanzibar kwa uchochozi wa kukacshifu dini ya waislamu ambayo pia ni dini yako na Wazanzibar kusema Nabii Issa ni Mungu..?? au ndio chama kwanza na itikadi zake..??
Leo wewe na viongozi wenzako muujitao waislamu munakaa raha mustarehe huku Mashekh wako magerezani kwa ushauri na chuki za kisiasa tu ama kweli wewe Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un (إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ).
Wewe kwa mawazo yako unaona unawakomowa wale na kuwatesa lakini maskini hujuwi kuwa unajikomowa wewe na kujitesa wewe mbele ya Allah, kumbuka kuwa roho ya mumini haifi na hio imetokea mifano sehemu nyingi tu za dunia ikiwepo Saudia.
Kuna watu wa litaka kujenga wakanunua eneo na bada ya kuchimba eneo kwa kujenga wakogonga kaburi na kuona damu na kitambaa cheupe kiko vile vile na katika ufuatiliaji nikuwa hapakuwa na mava pale kipindi cha karne nyingi baada ya kuona mkasa huo ukaingiliwa na watafiti kujuwa vipi kaburi lile na kuwa bado maiti mbichi na sanda yake..??
Kuangalia kumbukumbu za karne za nyuma nikuwa eneo lile lilipiganwa Jihadi na wapiganaji Jihadi wengi walizikwa pale kwa hio Shein Roho ya Mumini haifi hua iko hai siku zote na aya zipo za M/mungu kusibiticha hayo.
Kwa hio na hawa Masheikh wetu ni watu waliojitolea kupigania haki na maonevu wanayofanyiwa waislamu wa Zanzibar kwa hio Shein na Kikwete wako mujuwe tu kuwa maisha ya dunia niyakupita tu na yana muda mfupi mbele ya Allah.
Kuna watu wakiishi miaka mirefu na kuwa majabari lakini baada ya kukaribiwa na mauti walijihisi maisha waloishi ni kupwesa na kupwesua tu na wakajuta na wakaomba waongezewe angalau siku ili waitumiliye kwa kutubu na kufanya ibada wapi..??yalaitani.
Wewe Shein huna mateso yakuwatesa wachamungu uwezo wako wakuwatesa ni mdogo na huna, Wachamungu ni watu waliozichukuwa nafsi zao na kumkabidhi Allah kwa hio utawatesa na wakishakufa huwezi kuwatesa tena huo ndio uwezo wako tu.
Lakini kumbuka na wewe jee baada ya kufa wao wewe una muda gani wakuishi.?? na jee ukionana na Mola wako na Uliowatesa tena wajumbe wake Allah utamwambiaje Dr Kumbi Shein Mollah wako..???
M/mungu walinde masheikh zetu na wakorofi hawa.

No comments:

Post a Comment