Saturday, April 6, 2013

TUME YA KATIBA YATOA RASIMU MAONI YA WAZANZIBARI YA KUTAKA MUUNGANO WA MKATABA YATUPILIWA MBALIHATIMAYE Tume ya Mabadiliko ya Katiba, imekamilisha mwelekeo wa Katiba mpya, na kupendekeza mfumo wa Muungano wa Serikali mbili au tatu.
Hii ni kwa mujibu wa rasimu ya Katiba inayotarajiwa kutoka Jumatatu Aprili 8, mwaka huu kabla ya kujadiliwa na wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.
Taarifa za uchunguzi kutoka ndani za Tume, zimesema Makamishna wa Tume hiyo wamefikia muafaka wa mapendekezo hayo, baada ya uchambuzi mkubwa wa maoni ya wananchi kutoka mikoa ya nchi ya Tanganyika (Tanzania) na nchi ya Zanzibar.
Rasimu ya Katiba hiyo, inatarajiwa kufikishwa katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, ambayo wajumbe wake waliteuliwa hivi karibuni katika shehia mbalimbali.
Wajumbe wa wilaya ya Mabaraza ya Katiba, wanatakiwa kufanya uchambuzi wa maoni, kupitia mwelekeo wa rasimu hiyo na hatimaye kuirejesha tena kwa Tume ya marekebisho ya Katiba mpya.
Muungano wa ((Tanzania)),nchi ya Tanganyika na nchi ya  Zanzibar umekuwa katika mfumo wa Serikali mbili tangu ulipoasisiwa, Aprili 26, 1964 na viongozi wa wili tu bila kuwauliza wananchi wa nchi hizi mbili kama wanautaka au hawautaki muungano wa nchi zao hizo mbili.
Hata hivyo: Historia inaweza kubadilika endapo turufu mbili zilizopendekezwa na Tume ya Katiba, moja itashinda, hasa mfumo mpya wa serikali tatu.
Aidha, habari zaidi zinafahamisha kuwa Tume hiyo, imetupilia mbali maoni ya Muungano wa MKATABA maana ndio unao takiwa haswa na Wazanzibari walio wengi je nini haswa Tanganyika anathamiri kuitendea nchi ya Zanzibar.???
HAPA NYERERE AKIWAPIKA VIJANA WAKE PAMOJA NA KICHO CHA KOROSHO WARIOBA JINSI YA KUIMALIZA ZANZIBAR JE KWELI WARIOBA ATAITAKIA MEMA ZANZIBAR..?????

No comments:

Post a Comment