Thursday, April 11, 2013

UHURU KENYATTA ASEMA NITATUMIA SIKU 100 TU KUTIMIZA AHADI NILIZO WAHIDI RAI WA KENYA JE KWELI..??


Ataanza kwa ahadi ya matibabu bure kwa wanawake wanaofuata huduma za uzazi
Nairobi. Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kwamba atatumia siku 100 tu kutekeleza ahadi zake zote ambazo ameziahidi kipindi cha kampeni.
Alisema kwanza atatumia miezi mitatu tu kuondoa kabisa malipo ya Afya ya uzazi kwa kina mama katika zahanati zote na hospitali za umma.
Alisema kwamba Serikali yake itatoa kiasi cha Sh bilioni 6  zilizotengwa kwa ajili ya mfuko wa vijana na wanawake .
Pia alikumbushia ahadi ya kutoa ‘laptop’ kwa wanafunzi wote wa shule za msingi watakaojiunga na shule za serikali mwakani.
Uhuru alisema kwamba kutekeleza ahadi hizo ni katika suala la utekelezaji wa sera na misimamo wa Muungano wa Jubilee.
“Mimi nina fahari kubwa kuwajali wanyonge waliokubali kunipa nafasi hii ya uongozi na nimekubali kulivaa vazi hili la uongozi hivyo nitasimamia sera za Jubilee kama tulivyoahidi Wakenya wakati wa kampeni,’’ alisema Uhuru.
Aliongeza kwamba yupo kwa ajili ya Wakenya wote waliompigia kura na hata wale
waliowapigia wapinzani wake.
Uhuru alisema atawasaidia Wakenya pamoja na taifa zima kuelekea katika mizizi imara ya kiutajiri kwa njia ya amani, hali ambayo alisema inawezekana ikafanikiwa kwa kiasi kikubwa baadaye.
Naye mtaalamu wa Uhusiano wa Kimataifa, Profesa Munene Macharia alipokuwa akifanya mahojiano na Kituo cha Habari cha Xinhua ,alisema kwamba kuchaguliwa kwa Rais Uhuru Kenyatta, kuna uwezekano mkubwa kubadilika kwa sera za kiuchumi.
Alisema kwamba Rais huyo ambaye awali alikuwa katika Baraza la Mawaziri la awamu iliyopita akiwa Waziri wa Fedha anatakiwa kujenga uhusiano wa karibu na mataifa ya nje ili aweze kubadili sera za kiuchumi.
Pia alimtaka waziri huyo kuangalia suala la kuimarisha uhusiano wa kibiashara na nchi jirani za Afrika na Afrika Mashariki.
Profesa Macharia alisema baada ya kuitumikia Serikali ya Kibaki, Kenyatta ana uwezo mkubwa wa kudumisha sera hiyo ya kiuchumi.
“Lengo la msingi kwa Serikali ya Kenyatta inatakiwa kuimarisha mahusiano yake na Jumuiya ya Afrika Mashariki nchi wanachama (EAC) Kama majirani wa karibu,” Macharia alibainisha.

No comments:

Post a Comment