Friday, May 17, 2013

JUA KALI BADO WAYA MKALI ZAIDI YA SEREKALI YA MADHALIM SMZBaraza la Mji wa Zanzibar limezidi vituko, dhulma na unyanyasaji wa wafanya biashara ndogo ndogo (ambao kimtazamo, sio “halali’ lakini wanatozwa kodi ya sh 500 kwa kila siku; na kwa kila wanapokaa na kupanga biashara zao.
Juzi ile baada ya kufanya operesheni ya kuchukua vitu vya watu, kuharibu mali za watu; baadae walikwenda pale Vikokotoni, ambako wale jamaa wa “Jua Kali”/Dada Njoo wanaweka vitu vyao katika godown. Askari wa ZMC, Janjaweed, KMKM, KVZ na wote unaowajua wewe — walikwenda na kulivunja na hatimaye kuiba vitu vyote. Watu wote walijiuliza: je, kule kumewakera nini BLM/ZMC??
ZMC na hao askari wao — walikwenda na FUSO na kupakia vitambaa na nguo na vitu vyenginevyo na kuondoka navyo. Hakuna anayejua vitu hivyo vimepelekwa wapi?? na mpaka leo hakuna ‘news’ juu ya tukio hilo; ila ZMC wanadai kuwa eti sio wao waliovunja ila ni ‘majambazi/wezi’. Ahhhhh……….mengine enh…na mengine ni kinehe!
Najua kuwa pengine Mkurugenzi Mpya wa ZMC, Maalim Ebeid Kombo au umaarufu wake ‘Maalim Abeid’ — anataka kuonyesha kuwa ‘anafanya kazi vizuri’ na kuwakomoa jamaa zake wenyewe.
Hayo kama hayatoshi. Wiki iliyopita, kulikuwa na kikao cha madiwani, eti wanataka kupitisha miswada na kubinafsisha ZMC. Kilichojiri ni kuwa mjumbe mmoja alisimama kutoka CCM, na kudai kuwa kabla hatujasonga mbele, tuangalie tulipo na tunakotoka. Akasimama Diwani wa CUF na kudai aonyeshwe risiti za parking zote.

Likatolewa buku kubwa (ledger book) huko yakazuka mambo: receipts zote za Darajani parking na maeneo tunalipa sh.500 kwa saa; lakini katika buku hilo kubwa kinachoandikwa ni malipo ni sh 250/=.
Je, hizo 250/= nyengineo – zinakwenda wapi..??? na kwa nini hakuna mtu anayewajibika au anayewajibishwa kwa dhulma kama hii, wizi wa wazi wazi..??? Baada ya mkasa huu, madiwani wa CCM, walimgeukia diwani wa CUF kuwa ndiye ‘mbaya’. Aliyeiba sio mbaya, ila aliyesema Fulani kaiba ndiye mbaya.
Ama kama parking yako utaifanyia kule forodhani na maeneno kama hayo — huko unalipa 1000/= na karibuni sana itapanda na kuwa 1500/=. Hiyo value ya parking ya 1500/ au 500/= kweli ipo pale Darajani..??
Naomba nifafanue kidogo: ninaposema haya, haina maana ninatetea ufanyaji biashara pale Darajani, la hasha. pale ni illegal kufanya biashara; ila ninakosema mimi kwa nini ZMC inafanya dhulma ya namna hii, at the same time, wanatoza pesa watu na huku wanawageukia na kuwapiga, kuwanyanganya mali zao n.k.                                                                       
Na kama ni illegal, kwa nini uwaruhusu wengine (wamachinga kutoka Mtwara, Wamasai wanaouza dawa, na wale wanaouza njugu kwenye nyungo, korosho n.k); lakini unawasumbua wauza samaki kutoka Nungwi, Fumba, Kidoti, Vitongoji n.k..??

No comments:

Post a Comment