Thursday, May 30, 2013

JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU YAMUWA KUNENA TENA

JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI)
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION

Bismillahir Rahmanir Rahiim

TAARIFA JUU YA HALI HALISI NA MATUKIO YA KESI
INAYOWAKABILI VIONGOZI WA UMOJA WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU NCHINI ZANZIBAR.25 MEI,2013

Jumuiya ya Uamsho na Mahadhara ya Kiislam-JUMIKI, ni Jumuiya iliyosajiliwa kihalali kufanya shughuli zake  hapa Zanzibar mwaka 2001.Kwa kipindi chote hicho hadi kufikia tarehe 21/10/2012 JUMIKI ilikuwa ikiendelea kufanya shughuli zake kwa utulivu na amani na kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi na taratibu zilizowekwa.

Wakati Jumuiya ikiendelea na kazi zake za kuhubiri, kutetea na kusimamia haki za Waislamu na kuelimisha jamii juu ya maswala mbali mbali ya kidini na kijamii, mnamo mwezi wa Ogasti 2012 ilitokea kadhia ya kukamatwa Sheikh Mussa Juma wa Msikiti wa Biziredi. Baada ya hapo Waislamu walijaribu kufuatilia sababu za kukamatwa kwake na kushindikiza kuachiwa huru kwa kuwa hakukuwa na sababu ya kuwekwa ndani.Lakini kilichofuata ni mfululizo wa mabomu ya machozi na pilipili kuwatawanya hali iliyozidisha mtafaruku katika mji wa Zanzibar.

Tarehe 19 Oktoba Sheikh Farid Hadi Ahmed alitekwa nyara na baadaye kuachiwa tarehe 22/10/2012.Tarehe 23Oktoba 2012 Sheikh Farid alitakiwa afike kituo cha Polisi, Madema kwa mahojiano kuhusu kutekwa nyara kwake.Masheikh wengine-Sheikh Msellem, Sheikh Azzan, Sheikh Mussa Juma na Sheikh Hassan walikwenda kumshindikiza.Bahati mbaya Polisi wakawakamata wote na kuwaweka ndani na kuwafungulia mashtaka mbali mbali ya uchochezi na uvunjifu wa amani na uharibifu wa mali na kupandishwa mahakamani Tarehe 20 Oktoba 2012; siku ambayo Masheikh wote walinyolewa ndevu zao,tukio lililowashangaza wengi kwa ule msingi wa Katiba kwamba hakuna mwenye hatia mpaka apatikane na hatia na mahakama iliyo huru ulishavunjwa tokea siku ya mwanzo kabisa.

 Baada ya hapo mashtaka kadhaa yakafunguliwa katika mahakama mbali mbali ikiwemo Kwerekwe(mahakama mbili za Wilaya) Mfenesini na Vuga (mahakama Kuu) Dhamana ziliwekewa masharti magumu mwanzoni lakini baadae mashrti yakalainishwa na washtakiwa kupewa dhamana, kesi moja ya mahakama ya Wilaya Kwerekwe ikafutwa na ile ya Mfenesini pia ikafutwa na Mkurugenzi wa mashtaka.

Kesi zote zinazowakabili Masheikh wa Uamsho ni kesi ambazo dhamana ni haki  ya washtakiwa kwani makosa wanayoshtakiwa si makosa ambayo hayana dhamana. Aidha kwa mujibu wa Sheria, Kesi hizo zinapaswa kuanza ndani ya miezi minne, vyengenevyo inabidi washtakiwa wapewe dhamana. Kinyume na misingi yote ya sheria na haki, washtakiwa wote kumi wameshakaa ndani kwa zaidi ya miezi saba sasa kinyume na sheria na taratibu zote za kuendesha mashtaka ya jinai. Jambo hili la kuendelea kuwawekwa mahabusu na kunyimwa dhamana kwa Masheikh ni dhulma, ukandamizaji na uvunjwaji wa makusudi wa haki za binadamu.Jee hii ndio demokrasia na utawala bora..???

Lengo la Jumuiya sio kuingilia kazi za mahakama, bali tuna haki ya kikatiba ya kupinga uvunjifu wowote wa Katiba ya Zanzibar ya 1984. Kwa kawaida inapotokea uonevu kama huu tumekuwa tukishuhudia Jumuiya za Kitaifa na za Kimataifa,Taasisis za kutetea Haki za Binadamu, Vyombo vya habari duniani,Asasi za Kijami, Vyama vya wanasheria na wengine wakipaza sauti zao kulaani, kushtumu na hata kukemea wazi wazi dhulma hizo; lakini kwa masikitiko makubwa hali imekuwa ni tofauti kwa Viongozi waliokumbwa na kadhia hii. Jee taasisi hizo ziko wapi..??? Au kwa sababu wahusika ni VIONGOZI WA KIISLAMUU....?????????????

Ikumbukwe kama hawa ni viongozi wa juu wa Jamii kubwa ya Kiislam nchini, hivyo kila mtu linamgusa na kumuuma na jambo ambalo likiendelezwa linaweza kusababisha uvunjifu wa amani usiotarajiwa.Kwa hali hii Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) imewaita Wanahabari,Mbalozi wa nchi za nje, na Wadu mbali mbali kuwaeleza jinsi ya dhulma, ukandamizaji, na uonevu unavyoendelea dhidi ya Viongozi wetu kama ifuatavyo.

1)Kuwatupia shutma kali na malalamiko Serekali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar na Serekali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuvunja sheria za nchi walizozitunga na kuzilia viapo na kuzipitisha wenyewe na kudai kuwa hakuna MTU ALIE JUU YA SHERIA.

2)Jumuiya ya Kimataifa;wakiwemo'.
Mabalozi wa Jumuiya ya nchi za Ulaya,Marekani, na Magharibi kwa ujumla kwa kuka kimya kinyume na kawaida yao ya kutetea haki za binaadamu.

3)Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali ndani na nje ya nchi-kwa kutoripoti au kuripoti kwa kuegemea upande mmoja wa Serekali huku ikiihusisha Jumuiya na ufanyaji wa fujo, na pili kutoa habari kwa mitazamo yao wenyewe mfano;Kulihusisha tukio la Maandamano ya Morogoro na matukio ya Zanzibar.

4)Raisi wa Zanzibar kuendelea kuingilia uhuru wa Mahakama kwa kutoa misimamo yake mikali dhidi ya Masheikh wa Uamsho waliopo MAHABUSU.

5)Kuvunjwa kwa katiba ya nchi mfano ;kuingiliwa na uhuru wa habari na maoni kwa Jeshi la polisi kukama CD za mawaidha ya kiislamu na kuzuia redio kutangaza matangazo ya jumuiya na Kamisheni ya Habari ya Zanzibar na Waziri wa Mambo ya ndani  Mhe; Emanuel Nchimbi kuzuia kutoa taarifa za JUMIKI katika vyombo vya habari.Mfano; Redio Nour na Adhana FM.

Shutma kwa vyombo vya dola hususan Jeshi la polisi, Usalama wa Taifa, na Vikosi vya SMZ, kwa kupachuliwa kwa nguvu bendera za Jumuiya katika sehemu mbali mbali nchini kwa lengo la kuudhalilisha UISLAMU, kupingwa na hata kuuliwa baadhi ya watu kwa kukataa kupachua bendera hizo.

Matumizi ya nguvu kubwa, kuweka hali ya hatari, taharuki na kuzuia hata jamaa za washtakiwa kukaribia mahakamani ambapo hata kesi ya uhaini ndugu na jamaa waliruhusiwa kuhudhuria na kusikiliza kesi za ndugu na jamaa zao.

Unyanyasaji wa watuhumiwa na uingiliaji wa uhuru wa kuabudu kwa majibu wa katiba; Mfano; kuwanyoa ndevu kwa lazima, kuwazuia kusoma quraan,kupata habari,kuswekwa na kutengwa katika chumba cha kila mtu peke yake (katika siku za mwanzo za mahabusu)

Kuwatenga na mahabusu wengine hata katika ibada kinyume na utaratibu wa sheria na haki za binadamu.

Mwisho, Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu inatoa TAMKO RASMI  kuhusiana na kadhia yote tangu ilipoanzia hadi leo hii kama ifuatavyo;                                     

1.Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) inakanusha vikali propaganda zote zinazoenezwa na vyombo vya habari, wanasiasa na watu mbali mbali kuihusisha Jumuiya na vurugu na vitendo vyovyote vile vya uvunjifu wa amani kama vile uchomaji wa makanisa, maskani na upotevu wa maisha ya watu.Fujo sio sera ya Jumuiya wala haihusiki nazo.

2.Kwa vile Msingi mkuu wa katiba zote za nchi zinazoendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia ikiwemo Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ni kuheshimu na kulinda haki za binaadamu ikiwemo uhuru wa kuabudu na kujikusanya na kujieleza, kwahiyo, JUMIKI inalaani vikali wale wote wanaotoa kauli za vitisho na matamko ya uvunjifu wa katiba na kuipeleka nchi katika utawala wa KIDIKTETA

3.JUMIKI itaendelea na shughuli zake za kuelimisha, kutetea na kusimamia haki na wajibu wa kila raia kama kawaida yake,ilimradi haivunji sheria wala taratibu za nchi. Itaendele kutetea,kudai na kuelimisha umma wa Wazanzibari juu ya haki yao ya kuidai Zanzibar huru yenye mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa.

4.JUMIKI inashangazwa na kauli za  nchi za magharibi kwa kuipongeza serekali ya Umoja wa Kitaifa; serikali ambayo inavunja na inakandamiza wananchi wake wenyewe kwa kudai haki yao ya kujitawala.

5.JUMIKI itaendelea kusimamia agenda yake ya msingi ya kudai Zanzibar huru kinyume na jitihada zinazofanywa na Serekali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) na vyama vya kisiasa za kututoa katika lengo kwa kuanzisha agenda za pembeni ikiwemo kukamata viongozi wetu,kuanzisha mchakato wa katiba na kueneza uvumi na propaganda usio na ukweli wowote.

6.JUMIKI itaendelea kusisitiza kama ni kuendelea na muungano au laa kwa kuheshimiwa matakwa ya wananchi pia kupewa fursa ya kutoa maoni kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar. Jumuiya tayari imekusanya majina ya watu sitini elfu kwa niaba ya Wazanzibari kwa ajili ya kupeleka mbele agenda ya kudai kura ya maoni na kudai mustakbali wa NCHI YETU YA ZANZIBAR.

WABILLAHI TAUFIQ


IMETOLEWA NA;
OFISI YA KATIBU MKUU
JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAM
ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment