Wednesday, May 22, 2013

KESI YA WAKOMBOZI WA NCHI YA ZANZIBAR UAMSHO SASA KUNGURUMA KATIKA MAHAKAMA YA WAKOLONI WEUSI NCHINI TANGANYIKA

                                                                                                                                                                                        
Dar es Salaam. Kesi ya kusingiziwa na kutaka kuwatesa wakombozi wa nchi ya Zanzibar inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu ya nchi ya Zanzibar (Jumiki),Sheikh Faridi Hadi Ahmed (41), na wenzake 9, sasa imepangwa kuunguruma katika Mahakama ya Serekali ya Wakoloni Weusi nchini Tanganyika ya Rufani Dar es Salaam, Juni 10, mwaka huu.
Sheikh Faridi na wenzake wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama Kuu ya Zanzibar. Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mselem Ali Mselem, Mussa Juma, Azzan Khalid Hamdani, Suleiman Juma, Khamis Ali na Hassan Bakari, Ghalib Hamada Juma, Abdallah Saidi na Fikirini Fikirini.
Washtakiwa hao kupitia kwa mawakili wao, wamewasilisha maombi katika Mahakama ya Rufani ya Mkoloni Mweusi  Tanganyika, wakiomba mahakama hiyo itupilie mbali rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP MASHUZI ASIYEJUWA KAZI YAKE),nchini  Zanzibar, dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, wa Machi 11, mwaka huu.
Mahakama hiyo, katika uamuzi wake uliotolewa na Jaji Abrahamu Mwampashi, ilitengua mwenendo wa maombi ya dhamana ya washtakiwa yaliyotolewa na mawakili wao kwa Msajili wa Mahakama Kuu, Oktoba 25, siku washtakiwa hao waliposomewa mashtaka.
Pia Mahakama hiyo ilitupilia mbali maombi ya marejeo ya washtakiwa hao kuhusu uamuzi wa Msajili wa Mahakama Kuu kuwakatalia dhamana na kuamuru warejeshwe rumande hadi tarehe iliyopangwa kutajwa kwa kesi hiyo, pamoja na pingamizi la awali (PO) la upande wa mashtaka.
Katika maombi yao kwa Mahakama ya Rufani, washtakiwa hao wanaiomba Mahakama ya Rufani kutupilia mbali rufaa hiyo ya (DPP MASHUZI,) kwa madai kuwa hakuna rufaa iliyofunguliwa na mjibu maombi (DPP) dhidi ya uamuzi na amri ya Mahakama Kuu anayoipinga.
Washtakiwa hao wanabainisha kuwa taarifa ya kusudio la kukata rufaa iliyowasilishwa mahakamani hapo na mjibu maombi haihusiani na uamuzi huo wa Mahakama Kuu wa Machi 11, mwaka huu.
Wanafafanua kuwa uamuzi huo wa Mahakama Kuu wa Machi 11, mwaka huu hauwezi kupingwa kwa rufaa wala kwa maombi ya marejeo katika Mahakama ya Rufani.
 
yamepangwa kusikilizwa na jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani ya Wakoloni Weusi Tanganyika, Juni 10, mwaka huu, jijini Dar es Salaam sasa ndio labda Wazanzibari mutazidi kuamka na kujuwa kuwa munatawaliwa na Mkoloni Mweusi maana hii ni kesi ya nchi ya Zanzibar vipi yapelekwa katika nchi ya Tanganyika..??? kama sio Zanzibar ni koloni lao na sasa wanawahukumu masheikh ili wasidai Zanzibar yanye mamlaka kamili na kuka kimya nakuwa mkowa wa pwani Zanzibar ndivyo wanavyotaka Wakoloni Weusi Tanganyika.
Jopo hilo la majaji watakaosikiliza maombi hayo linaongozwa na Jaji January Msiffe, akisaidiana na Jaji Salum Massati na Jaji William Mandia.
Maombi hayo yamewasilishwa chini ya hati ya dharura wakiomba mahakama iyasikilize mapema .

No comments:

Post a Comment