Friday, May 31, 2013

KWANZA ILIKUWA MIAKA,MIEZI,WEKI,SIKU,SASA NI MASAA TU IWE NI SIKU YA MAMLAKA DAY YA NCHI YETU YA ZANZIBAR.

mamlaka day
Je unayo habari..?? Je umesahau..?? ni wazanzibari, wapenda nchi yao, wazalendo, wanaharakati, wana kindakindaki, makureishi wa zenji na wale wanaosema kwa yakini ya mioyo yao na kuthibitisha kwa vitendo vyao mapenzi makubwa ya nchi yao. Wale wanaoamini kwamba “vyovyote na iwe lakini Zanzibari ibaki huru yenye mamlaka yake kamili”. Umma huo utakusanyika kesho Jumamosi tarehe 01/06/2013 katika viwanja vya Demokrasia Kibanda Maiti. Uwanja wa Kibanda Maiti utageuka “Tahrir Square” ya wazanzibari kama ilivyokuwa Misri na kuudhihirishia ulimwengu kwamba wazanzibari kwa amani kabisa wanataka mamlaka kamili ya nchi yao tukufu na kuwaonyesha ulimwengu kuwa Wazanzibari wanataka nchi yao. Unamuogopa nani ewe Mzanzibari? Ogopa nchi yako kuendelea kuwa chini ya ukoloni. Hapa ni Zanzibar kwanza, itikadi ni baadae. Viongozi mbali mbali wa vyama mbali mbali wazalendo wenye uchungu na nchi yao wanatarajiwa kuhudhuria.
Shime Shime wazanzibari tujitokeze kwa wingi. Mambo yataanza saa 2:00 za asubuhi mpaka saa 12:00 jioni. Mgeni Rasmi ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
TUNATAKA NCHI YETU SASA TUMECHOKA TAFRANI HII TAFRANI HII TUNATAKA NCHI YETU SASA TUMECHOKA
ZANZIBAR KWANZA!

TUNAPATIKANA LIVE: http://www.ustream.tv/channel/mazruimedialive

FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI INAFURAHA KUBWA NA PIA KUWAOMBA VIONGOZI NA WATU WOTE WANAO PIGANIA NCHI YETU YA ZANZIBAR KUWA HURU KUWA MAMLAKA DAY KESHO NI UNGUJA ILA TUNAOMBA IANDALIWE SIKU NYENGINE PIA KWA JILI YA PEMBA MAMLAKA DAY IFANYIKE PIA PEMBA ILI KWA WALE AMBAO HAWATAWEZA KUJA KESHO UNGUJA BASI NA WAO WAPATE UTAMU HUKO HUKO PEMBA IN SHAA ALLAH HILI NI OMBI KUTOKA KWA WAFANYAKAZI WOTE NA FUNDI MITAMBO WOTE WA FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI.

No comments:

Post a Comment