Saturday, May 18, 2013

MAIMAMU NCHINI ZANZIBAR WAHOJI UDHALILISHWAJI WA MASHEIKHE WA UAMSHO NA WENGINEO

Muislamu ni ndugu yake Muislamu ni haramu kumdhulumu na ni haramu kuacha kumnusuru akidhulumiwa.Wamenuku hadithi hiyo maimamu nakisha kumkabili.Mwanasheria Mkuu kwa kusema kuwa wanafikisha malalamiko yao kwa sababu ndiye" msimamizi Mkuu wa Sheria katika Serekali na utendaji wake kisheria"

Wakasema wanashangazwa sana;kuiona serekali ya umoja wa kitaifa (SUT) ikiridhia kwa kuka kimya juu ya thulma na ukiukwaji wa kisheria na udhalilishwaji wanaofanyiwa Viongozi wa Taasisi za Kislamu nchini akiwemo Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar.Sheikh Farid Hadi Ahmed pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislamu na Mashekhe(wengine).

Jumuiya ya Maimamu Zanzibar(JUMAZA) inasema kuwa Viongozi hao kumi wa Kiislamu wamezuiliwa na jeshi la Polisi tokea tarehe 20/10/2012 mwaka jana na kufikishwa Mahakamani kwa kesi za bandia zenye sura ya kutengenezwa ili kuwaweka ndani kwa muda mrefu kadiri itakavyowezekana."

Jumaza wakiendelea kusema kuwa ushahidi wa hayo ni kuwa tokea siku waliofikishwa Mahakamani hadi leo huu  sasa unaanza ni mwenzi wa saba,hakuna haki yoyote waliyotendewa zaidi ya udhalilishwaji na usaani wa kudanganya Umma wa Wazanzibari kuwa Mashekhe na viongozi wao hao wanakabiliwa na kesi kubwa ili wananchi waongope na warudi nyuma waachane na madai yao ya kudai mamlaka kamili ya Nchi yao Zanzibar."

''Mh,Mwanansheria Mkuu,kwa upande wa Mahakama,hadi hii leo imeshindwa hata kuwapangia Jaji kama taratibu zilivyoelekeza na kwa kipindi hicho chote kesi ya msingi imebaki kwa mrajisi wa Mahakama ambaye amekuwa akiitaja kila wanapofikishwa Mahakamani.kutokana na kutokuwa na nia nzuri ya kutoa haki kama ambavyo Mahakama inatakia ifanye,Mrajisi huyu alijipa uwezo wa kuzui dhamana ya mashekhe na Viongizi hao licha ya kuwa hana uwezo kisheria wa kufanya hivyo.

Jambo ambalo limebainishwa wazi na katika hukumu ya Ombi la dhamana lililotolewa tarehe 11/3/2013."imesema sehemu ya barua ya (JUMAZA) iliyosainiwa Katibu Mtendaji wake Sheikh Muhidini Zuberi.Barua hiyo ikaongeza kudai kuwa ''kwa upande wa Ofisi ya Mkurungenzi Mashitaka nao umekiuka utaratibu kwa hati ya kupinga dhamana na huku wakijuwa kuwa hawana sheria wala mamlaka ya kufanya hayo na kwamba kinacho onekena wazi ni kujaribu kuridhisha utashi bi nafsi wa kisiasa ambao unaonekana kuwa umelengwa kufanisha kuwaweka ndani Viongozi hao kwa muda mrefu na kuwanyima haki yao ya dhamana kwa kulifanya kosa ambalo halipo kuwa ni kosa kubwa na lakutisha kinchi.''

Wakimtupia lawama Mwanasheria Mkuu, JUMAZA wamemkabili wakisema Wewe ni mweledi zaidi wa mambo ya sheria na hivyo unafahamu fika kuwa dhamana ni haki ya mtuhumiwa kwa kesi kama hiyo, lakina bado Mashekhe wanaendelea kunyimwa  dhamana hiyo na kupigwa dane dane. Sheria zinachezewa huku Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikibariki ukiukwaji huo kwa ukimya wake na kupongeza Jeshi la Polisi. Mbali ya kuwa dhamana ni haki yao, kesi yenyewe unafahamu wewe na Serikali kuwa kisheria kesi hiyo ililazimika isikilizwe ndani ya miezi minne na sheria inaelekeza ikishindikana,basi kesi ifutwe,laa kusikitisha leo ni mwezi wa sita udhalilishwaji unaendelezwa huku wananchi wakifanywa waamini nchi hii in Utawala Bora na Kuheshimu Sheria.''

Wakikamilisha maelezo yao JUMAZA wakasema kuwa ''Waislamu wa Zanzibar hawajawahi kuona viongozi wa dini ya Kikiristo wakidhalilishwa kwa namna yoyote ile kama wanavyofanyiwa viongozi wa Waislamu.Na wakamaliza kwa kuwataka wananchi kuungana na kutowa sauti moja ya kupinga dhulma,uonevu na udhalilishwaji kwa sababu hiyo sio yaliyotarajiwa kuletwa na kufanywa na Serekali ya Umoja wa Kitaifa.Jumuiya ya Maimamu inatowa wito kwa Serekali na Wawakilishi wa wananchi kusimamia Utawala wa Haki na Sheria bila ya ubaguzi na kushirikiana pamoja na wananchi utangulizi utetezi wa maslahi ya nchi kwanza.

Maslahi ya vyama,vikundi vya watu na mtu binafsi yatafuatia baadaye.''Walimaliza JUMAZA katika barua yao walioinakili kwa Waziri wa Sheria,Baraza la Mapinduzi,Jaji Mkuu,Baraza la Wawakilishi na Mkurugenzi wa Mashtaka.Wengine waliopewa nakala ni Sherika la Kimataifa la kutetea wafungwa (Amnesty International),Umoja wa Majaji na Makadhi Zanzibar,East Africa Law Society,Zanzibar law Society na Wandishi wa Habari.

No comments:

Post a Comment