Sunday, May 12, 2013

NDUGU MUISLAM CHANGIA UJENZI WA MSIKITI ULIOPO FUONI IJITIMAI-KWA JILI YA AKHERA YAKO

TANGAZO LA MSIKITI
Asalam Alaikum,
Ndugu Waislam, munaombwa kufungua account isiyoliwa na wadudu wala kufilisika kwa kuchangia ujenzi wa msikiti ulioko huko Ijitimai Fuoni.
Eneo hili limekuwa na uhaba wa nafasi yakusalia baada ya kijisikiti chao kidogo kilichojengwa kwa miti na kuezekwa kwa makuti kuwa hakitoshelezi mahitaji na matakwa ya wingi wa watu wanahamia na kuishi kwenye mtaa huo mpya.
kwa jitihada za wakaazi wa eneo hilo wamefanikisha kupata kiwanja kipya cha kujenga msikiti huo ambacho kiko pembeni mwa msikiti mkogwe, wamefanikiwa kuanza na ujenzi kwa kuanza kujenga foundation na kukwama kwenye  kumwaga janvi.
Tunatowa wito kwa Waislamu wote popote walipo Duniani, wanakaribishwa kwa hali na Mali ikiwa watatowa Pesa au watataka kujenga mwenyewe ruhusa hiyo inatolewa na Kamati Msikiti.
WABILLAH TAUFIQ

No comments:

Post a Comment