Wednesday, May 1, 2013

TUMUOMBE M/MUNGU KATIKA KILA JAMBO LETU WAZANZIBARI

Viongozi wa Taasisi za Kiislamu ambao wamewekwa ndani na kunyimwa dhamana wakiwa katika moja ya sala na dua ya pamoja siku chache baada ya kutokea ajali ya meli ya Mv. Skagit iliyosababisha vifo kadhaa, dua hiyo ilifanyika katika Msikiti wa Mbuyuni Zanzibar

JUMAZA katika kikao chake cha Jumamosi tarehe 27/4 kiliafikiana kuwa ni muafaka kwa hivi sasa kuiombea dua ya kheri na amani nchi yetu na kuwaombea Masheikh wetu pamoja na Wazanzibari wote kwa kutanguliza kufunga siku ya Alkhamis ya tarehe 2 Mwezi wa 5 (Mei) sawa na mwezi 21 mfunguo 9. Baadae itafuatiwa na Qunuti kuanzia swala ya Ijumaa ya tarehe 3 mwezi wa 5 sawa na mwezi 22 mfunguo 9 itakayofanyika mfululizo  kwa muda wa siku 21 katika kila swala, kama mafunzo tuliyoyapata kutoka kwa Mtukufu wa Daraja (S.A.W) kheri zote ziwe juu yake.
Inasisitizwa waislamu wote katika misikiti yote kushirikiana katika jambo hili.

No comments:

Post a Comment