Sunday, June 9, 2013

ABBU JAHAAL WA ZANZIBAR ARUDI KUTOKA CHINA NA KUSEMA SIITAMBUI KAMATI YA MARIDHIANO ZANZIBAR

                                                                                                                                                                                                 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amesema haitambui kamati ya maridhiano inayotetea Zanzibar kuwa na mamlaka kamili kama taifa linalojitegemea na kuwa na kiti katika Umoja wa Mataifa.
Dk. Shein alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume baada ya kukamilisha ziara ya kikazi nchini China juzi.
Alisema kwamba haitambui kamati hiyo lakini alikiri kukutana nayo mara tatu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ilikwenda kumpongeza Ikulu baada ya kuibuka na ushindi, mara ya pili walifika kumpa mkono wa pole kufuatia ajali ya meli ya Spice Islanders kabla ya kukutana nao kwa mara ya mwisho.
Alisema shughuli zinazofanywa na kamati hiyo hazina baraka zake na wala hatambui mtu aliyeunda au kuteua kamati hiyo ambayo imekuwa ikifanya kampeni kubwa za Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili na kuwahusisha viongozi wastaafu akiwemo Rais wa Awamu ya Tano, Dk. Salmin Amour Juma ‘Komandoo’ na Rais wa Awamu ya Sita, Dk. Amani Abeid Karume.
“Waulizeni nani aliyeunda kamati hiyo na nani aliyeteua kama wakishindwa nitawaeleza mimi katika mkutano nitakaouitisha kuzungumza na waandishi wa habari, na walipokuja kwangu wanajua nini nilichowaeleza waseme,” alisema Dk. Shein.
Kamati hiyo ambayo ilikuwa ikitetea sera ya Muungano wa mkataba inaundwa na wanachama watatu kutoka CCM na watatu kutoka CUF, ikiongozwa na waziri wa kwanza wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hassan Nassor Moyo(CCM), Makamu Mwenyekiti Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Abubakar Khamis Bakari(CUF), Katibu wake ni Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu(CUF) na wajumbe ni pamoja na Waziri wa zamani wa SMZ na Mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki, Mansour Yusuph Himid(CCM) na Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma Salim Bimani(CUF).
Hivi karibuni, kamati hiyo iliandaa mkutano wa hadhara na kutangaza mambo 10 yanayopaswa kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano, ikiwa ni siku chache kabla ya Mwenyekiti wa tume ya katiba Jaji Joseph Warioba kuzindua rasimu ya katiba ya awali.
Kutokana na hali hiyo joto la kisiasa na vuguvugu la mabadiliko ya katiba mpya limechukua sura na mitizamo mbalimbali kutoka kwa wanasiasa, wanaharakati na wasomi ambao wengi walikuwa wamelala na sasa kuamka na kujuwa umuhimu wa kudai nchi yao ya Zanzibar lakusikitisha ni huyu kibaraka wa watanganyika dr kumbi shein kufikiri kuwa hii nchi labda kandikiwa kuwa ni yake,ila muda sio mrefu Wazanzibari watamuonyesha huyu kuwa hii ni nchi ya Wazanzibari sio ya Dodoma.pia ajiulize hii serekali ya (GNN) anayo jivunia na kumpa tiketi kwenda mpaka china kama sio hiyo kamati ya maridhiano huyu kumbi anathani angelikuwa hiyo alivyo kuwa..??

No comments:

Post a Comment