Tuesday, June 25, 2013

ASHA BAKARI NA MUNGU WAKE WA MWENGE-WAZANZIBAR NA M/MUNGU NA MAMLAKA KAMILI YA ZANZIBAR NANI ATASHINDA..???

SERIKALI ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar,inasikitisha sana sana baada ya kuanza kupata mpasuko kutokana na mawaziri wake kukosa umoja na kujitenga kwa baadhi ya shughuli za viongozi wa juu wa seriakli hiyo.
Aidha, imeelezwa katika mpasuko huo unaodaiwa kuikumba serikali hiyo, ni mawaziri wake kukosa ushirikiano kwa kushindwa kuwapa mapokezi stahiki, viongozi wake wa kitaifa.
Hayo yalielezwa juzi katika Baraza la Wawakilishi na Wajumbe kutoka vyama vya CCM na CUF wakati wakichangia Bajeti ya ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, iliyowasilishwa na waziri wa nchi wa ofisi hiyo, Mohamed Aboud.
Akichangia hotuba ya makadirio ya ofisi hiyo Mwakilishi wa viti maalumu, Asha Bakari (CCM) alisema lengo la kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar, limepoteza mwelekeo.
Alisema mawaziri wa serikali hiyo kutoka upande wa CUF, wamekuwa wakikwepa baadhi ya shughuli za kitaifa zinazofanywa na viongozi wa juu wa serikali hiyo, kwa kutoa mfano:
Mawaziri wote wa CUF ndani ya serikali hiyo, kushindwa kuhudhuria katika sherehe za uzinduzi wa MWENGE wa uhuru uliyowashwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohame Shein, Chokocho Pemba May 6, mwaka huu.
Alisema kitendo cha mawaziri hao kutokuhudhuria shughuli hiyo ya kitaifa, kinakwenda kinyume na lengo la kuundwa kwa serikali hiyo, iliyoazimia kudumisha amani na umoja wa Wazanzibari:
“Mawaziri wanafika kukimbia shughuli za MWENGE wa uhuru…hali hii ni kwenda kinyume na malengo ya kuanzishwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa,” alisema Asha Bakari. Hapa ndio muandishi wetu wa siri aliye ndani ya baraza la wawakilishi alipo pingwa na butwa kuona mama huyu badala yakuzungumza mambo ya maana kama maji,umeme,afya,madawa hospitalini,barabara,bei za vyakula n.k. yeye anazungumzia MWENGE  haswa katika kipindi hichi kigumu kabisa kwa wananchi wa Zanzibar kuwa wanataka nchi yao na kuwa na mamlaka kamili yeye ndio kwanza yuko katika miaka ya sitini MWENGE DAAAAAAAAAAAAH!!!!!!!!!!!!
Naye, Mwakilishi wa Kwahani, Ali Salum (CCM) ambaye alishadidia suala hilo alisema hofu ya wananchi kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa, kushindwa kufikia malengo yake, imetimia.
Alisema wananchi wa Zanzibar, mapema walionekana kuwa na wasiwasi wakati wa kubadilishwa kwa Katiba, na kuingizwa mfumo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa, kutokana na kutokuwepo kwa nia njema ya kujenga Zanzibar, yenye umoja:
“Wananchi wengi wa Zanzibar walikuwa na wasiwasi kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa nikiwemo mimi…leo wanaona wenyewe utendaji kazi wa viongozi wao wakiwemo mawaziri,” alisema Ali Salum.Na huyu nae badala ya kujenga anakuja kubomowa kabisa anajisema mwenye alikuwa na wasi wasi na serekali ya umoja wa kitaifa lazima uwe na wasi wasi maana hii sio ile serekali ya kufitinisha watu wala sio serekali ya kubaguwa watu na wewe hilo ndilo unalolijuwa sasa utafanya kazi gani na hupati kufitini wala kubaguwa watu..??? 
Hata hivyo, hoja hizo zilikumbana na kisiki, zilipingwa na Wawakilishi wa CUF, Hamad Masoud (Ole) pamoja na Ismail Jussa wa Mji Mkongwe, ambao waliibua hoja kali.
Jussa alisema viongozi wa CCM ndiyo chimbuko la tatizo, akidai kuwa: “Wameshindwa kumpa heshima Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kushindwa kujitokeza kumpokea wakati anaporudi safari za ndani na nje ya nchi,” alisema jussa:
“Ukipanda mbigiri utavuna mbigiri…mimi nimekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF wakati mwengine nilikuwa nakwenda kumpokea Makamo wa Kwanza wa Rais bila kuwapo mkuu wa mkoa wala mawaziri kutoka CCM,” alisema Jussa.
Kwa upande wake, Hamad Masoud alisema wapo watu hawana nia njema na serikali hiyo, lakini alisema malengo yao hayatatimia kwa sababu imewekwa kwa mujibu wa Katiba na kwa ridhaa ya wananchi wa Zanzibar:
Alifafanua: “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye aliyeanza kuzorotesha serikali ya umoja wa kitaifa kwa kitendo cha kutupilia mbali MAPENDEKEZO ya muundo na mfumo wa serikali hiyo,” alisema na kuongeza:
“Kukosekana kufuatwa kwa mapendekezo yale yaliyokuwa na sura halisi ya mfumo wa kitaifa kwa watendaji wa serikali kumesababisha serikali kuwa na viongozi wa kisiasa tu bila mfumo huo kuhusisha watenda wake,” alisema Hamad Masoud.
Hamad Masoud ambaye pia ni Mwakilishi wa Ole, akijadili na kuchangia Bajeti ya ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, alitilia shaka utendaji wa Tume mpya ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Na alisema:
“Ipo hatari kwa Tume ya uchaguzi ikarudisha migogoro ya kisiasa kwa sababu watendaji wake hawataki kubadilika,” alisema Hamad Masoud.

No comments:

Post a Comment