Wednesday, June 12, 2013

EWEE MOLA KAMA WALIVYO TUSIKIA KWA HILI VIONGOZI HAWA NA WATUSIKIA KUHUSU ZANZIBAR YENYE MAMLAKA KAMILI AMIIIN AMIIN.

Viongozi mbali mbali wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa ZECO, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa uimarishaji Miundombinu ya umeme Zanzibar, Mtoni
FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI TUNAFURAHA SANA SANA KUONA HII MIONGOZI YETU MITUMBO ISIO SHEBA MIJAHIL ISIO FAHAMU SAS INAAZA KUSIDUKA TUME TANGAZA HAPA MARA NYINGI TU KUHUSU ZANZIBAR HAIHITAJI UMEME WA TANESKO UNAWEZA UKATUMIA JUA AU UPEPO AU MAWIMBI YA BAHARI AMBAYO YOTE MAMBO MATATU YAPO ZANZIBAR. TUKAIFUNDISHA HII MIONGOZI NA KUYAMBIA LAKINI WAPI MIBICHWA YAO KUFAHAMU SIO RAHISI LAKINI ALHAMDULILAHI M/MUNGU KAWAZUNDUWA NA SASA WAMEONA NA YALIYO BAKI PIA M/MUNGU AWAZINDUWE. KWA MFANO KAMA MAJI TUMEZUNGUKWA NA BAHARI MAJI HAYO HAYO YA BAHARI YANAWEZA KUSAFISHWA NA KUWA MAJI YA KAWAIDA KAMA DUBAI NDIVYO WANAVYO ISHI NA HAKUNA SHIDA YA MAJI WALA MFEREJI MOJA KIJIJI KIZIMA HAKU NA SISI PIA TUNAWEZA IKIWA HIYO MIONGOZI ITAWACHA KUIBA PESA NA KUJAZA MATUMBO YAO PIA TUNAWEZA KUWA NA MAJI SAFI NA LAA MWISHO HATUTAKI RASIMU,KATIBA WALA SEREKALI TATU HATUTAKI HATUTAKI TUNATAKA NCHI YETU YA ZANZIBAR KWANZA KISHA SHENGESHA NYENGINE BAADAYE M/MUNGU WAFUMBUWE MACHO NA AKILI MIONGOZI HII YENYE VICHWA VIGUMU KUFAHAMU ILA WASHIRIKIANE NA SISI RAI KUIKOMBOWA NCHI YETU ILI ZANZIBAR IWE HURU KAMA NCHI NYENGINE SIO CHINI YA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.
Dr shein nchini Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema licha ya Zanzibar kupata umeme wa uhakika kutoka Bara(Tanganyika) Serikali yake inatarajia kuanzisha uzalishaji wa umeme mbadala ili kujitegemea katika huduma hiyo.
Amesema Serikali imefanya upembuzi yakinifu ambapo tayari wataalam wamethibitisha uwezo huo kwa Zanzibar kujitegemea katika huduma hiyo ambapo muda si mrefu taratibu zitaanza kufanywa.
Dkt Shein ameyasema hayo leo alipokuwa akizindua Mradi wa Uimarishaji Miundo Mbinu ya Usambazaji umeme huko Mtoni nchini Zanzibar uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japan JICA.
Amesema Utafiti uliofanywa umebainisha kuwa nchi ya Zanzibar inaweza kutumia njia ya Upepo na Jua na kuweza kuzalisha Megawati 50 ambazo zitasaidia pale tatizo la umeme litakapotokea nchini Tanganyika.
“Serikali imekuwa ikitafuta njia mbadala za kuzalisha umeme hapa hapa na utafiti umeonesha matokeo mazuri kuwa njia ya Upepo na Jua zinaweza kuzalisha hadi Megawati 50 ambazo zitatupa uhakika ili kule Bara hata kama kutatokea tatizo tuweze kuwa na umeme wetu ” Alisema Dkt. Shein.
Aidha ametaja njia nyingine mbadala ambazo Zanzibar inaweza kuzitumia kuzalisha umeme kuwa ni pamoja na njia ya Mawimbi ya bahari, Gesi na Takataka.
Dkt Shein ameelezea matumaini yake ya umeme wa uhakika unaopatikana kupitia msaada wa Japani kwamba utachochea sekta za maendeleo na ukuaji wa Uchumi.
Aidha amewataka viongozi wa Shirika la Umeme ZECO kutumia fursa hiyo ya upatikanaji wa umeme kudai madeni wanayowadai wateja wao wa Sekta binafsi, Taasisi za umma na Wananchi kwa ujumla.
“Tumuieni fursa hii kuwadai wote iwe ni Tasisi binafsi au Taasisi za Umma lakini mutumie njia za kistaarabu kudai madeni yenu ” Alieleza Dkt. Shein.
Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Tanganyika (Tanzania) Masaki Okada amesema nchi yake itaendelea kuisaidia nchi ya Zanzibar katika Sekta mbalimbali ili kudumisha urafiki wa muda mrefu baina ya nchi ya Zanzibar na nchi ya Japan.
Amesema ana matumaini kuwa Umeme wa uhakika ulipo nchini Zanzibar utakuwa ni kichocheo kikubwa cha Maendeleo na fursa ya kukabiliana na umasikini nchini.
Awali akimkaribisha Drk Shein, Waziri wa Ardhi,Makazi, Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban amewataka wananchi kuitunza na kuwa walinzi wa miundo mbinu ya umeme kwa kuepuka kujenga katika maeneo yaliyopita nyaya za umeme ili kuinusuru nchi kupata hasara.
Mradi wa Uimarishaji Miundo Mbinu ya Usambazaji umeme kwa kisiwa cha Unguja na pemba umefadhiliwa na Serikali ya Japan kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambapo jumla ya Shl. Bilioni 57 zimetumika kugharamia ujenzi huo.

No comments:

Post a Comment