Monday, June 10, 2013

PAPISS CISSE MCHEZAJI ANAYE MUOGOPA M/MUNGU NA KUIPENDA DINI YAKE SIO VIONGOZI WA ZANZIBAR WANAFIKIRI MATUMBO TU.


Klabu ya New Castle inayosakata kabumbu kwenye ligi ya primia nchini Uingereza, ambayo katikati ya msimu uliopita ilimpoteza mshambuliaji wake mahiri Demba Ba ambaye alitimkia klabu ya Chelsea ya mjini London, hivi sasa kuna hati hati inaweza kumpoteza mchezaji wake mwingine mashuhuri Papiss Cisse raia wa Senegal, baada ya kukataa kuvaa jezi ya timu hiyo yenye tangazo la WONGA.COM, wadhamini wapya wa klabu hiyo msimu ujao. Papiss Cisse ni muumini safi wa dini tukufu ya Kiislamu na aliwaambia viongozi wa klabu hiyo juu ya kutokuwa tayari kwenda kinyume cha maadili ya dini yake ya Kislamu kwa kuvaa jazi ambayo itakuwa na matangazo ya biashara za kampuni hiyo ya mikopo. Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, waumini wa dini ya Kislamu hairuhusiwi kunufaika au kujinufaisha na riba kutoka kwa mtu mwingine. Wachezaji wengine Waislamu wa klabu hiyo ya New Castle ambao ni Waislamu kama vile, Cheick Tiote na Hatem Ben Arfa, huenda nao wakachukua uamuzi kama huo wa Cisse wa kugomea jezi hizo. Hivi sasa klabu hiyo iko njia panda, kwani haiko tayari kumuacha mchezaji huyo inayomtegemea atimkie klabu nyingine, na kuna uwezekano mkubwa kwa klabu hiyo kufanya kama ilivyokuwa kwa Freddie Kanoute raia wa Mali aliyegoma kuvaa jezi yenye nembo ya tovuti ya 888.com alipokuwa akiichezea Seville ya Uhispania miaka kadhaa iliyopita, kwa sababu ya kamari.sio hapa kwetu zanzibar timu nzima waislamu lakini jazi za tusker na mijitu inavaa tu almuradi ipate kulaa hata kama kula hiyo ni ya haramu.mawaziri, wabunge, masheha ndio usiseme kabisa wao ndio toka kunakucha wanachuma moto wakila moto mpaka wanalala na kuwathulumu wanyonge haki zao. hata kufikiri haifikiri kuwa kuna kiyama na m/mungu hakuna kabisa hebu angaliyeni mifano hii au jitu limo tu muungano lazima uwepo wee muungano lazima uwepo hata kama kuwauwa Wazanzibari wote yuko tayari ili muungano uwepo lipate kujaza tumbo mkaye mkijuwa tumbo halijai chumeni halali musije chelewa mukenda kutana na athabu ya m/mungu.

No comments:

Post a Comment