Saturday, June 1, 2013

WALOZOWEA KUFANYA UCHAFU WAO NCHINI ZANZIBAR SASA BASI MIAKA 30 AU MAISHA JELA CHAGUWA KUSUKA AU KUNYOWA


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (GNU), imetunga sheria ya kupiga marufuku 

ndoa za  watu wa jinsia moja.Waziri wa Katiba na Sheria wa nchi ya Zanzibar, 

Bwana Abubakar Khamis Bakar, aliyasema hayo kwenye Kikao cha Baraza la 

Wawakilishi Zanzibar. 

wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Nassor Juma kutoka 

Chama cha Wananchi (CUF).Katika swali lake, Bw. Saleh Nassor Juma alitaka kujua ni lini Serikali ya Zanzibar 

itatunga sheria ya kukataza ndoa hizo na kuweka adhabu kali kwa watu ambao 

watabainika kufanya vitendo hivyo vichafu. 

Waziri Abubakar amesema, ndoa za watu wa jinsia moja ni kinyume na 

utamaduni wa Zanzibar na kwamba sheria hiyo imeweka adhabu ya kifungo cha 

miaka saba kwa wale wote watakaopatikana na hatia hiyo.

Pia alisema kama ninavyomnukuu: "Sheria hii inahusu makosa mengi 


yakiwemo ya ubakaji, zinaa, usagaji na umalaya ambayo yote yana 

adhabu ya kifungo cha maisha au miaka isiyopungua 30 gerezani," 

mwisho wa kunukuu.

1 comment:

  1. That was up..keep it up ur country will be clean..u the best!

    ReplyDelete