Tuesday, July 30, 2013

MASHEIKH WA UAMSHO HAWATA TOKA JELA KWA KUOMBEWA NA MTU BALI WATATOKA KWA UWEZO WA M/MUNGU

Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO wakiwa ndani ya gazi ya Polisi wakirejeshwa rumande baada ya kusomwa kwa kesi yao na kuahirishwa.
Sisi sote tunajuwa kuwa mahakama ya nchi yetu ya Zanzibar ni ya madhalim,matapeli,wezi,wasiojuwa haki wala batili,ni midudu tu imo ndani ya mahakama kutafuta tumbo lao lishimbe. ndio hapa nasema, pamoja na kuwepo sheria inayo waweka rumande Masheikh hao na kuzuilia dhamana zao, kuna haja ya kutizama upande wa pili: “Truth and Justice.” Ukweli na Haki.

Wapo watu waliwahi kukaa ndani miezi kadhaa au miaka kwa mashitaka ya kisiasa kule hapa nchini Zanzibar. Inasemekana kuwa watu waliokuwa karibu na Rais wakati ule Dkt. ‘Komandoo wa Udongo’ Salmin  Amur walimwendea na kumwomba awaachie watu wale. “Wacha wakae, kwani ni mapapai kwamba yataoza”, inasemekana hayo ndiyo yalikuwa majibu ya ‘Komandoo wa Udongo’ Mazungumzo yakaisha.

Watu wale wakati ule waliodaiwa sio mapapai na wakiona kuwa walikuwa wakidhulumiwa, kwamba sheria ilitumika vibaya dhidi yao, hivi sasa wapo madarakani katika nafasi mbalimbali. Swali ni je, kuna juhudi yoyote wanayofanya kuhakikisha kuwa haki kwa wote, ukweIi na uadilifu unakuwepo hilo la kwanza lapili wale wale walio kwenda kuwaombea wale wachiwe je wameshawaombea hawa masheikh pia wachiwe au walijuwa kuwaombea wale tu kwa kuwa ni wana wa siasa hawa wa dini wachwe waozee..???

FREE ZANZIBAR PEOPLE INAWATAKIA KILA LA KHERI MASHEIKH WETU WOTE WALIOKUWEPO JELA NA WALIOKUWEPO VIZUIZINI M/MUNGU AWAPE NYOYO ZA SUBIRA NA AWALIPE PEPO KWA KIJI ADHABU HICHI CHA DUNIA ABACHO WENGI WA VIONGOZI WANAFIKIRI NDIO MAFANIKIO YAO KWA NYINYI KUWEPO JELA WAO WAKATAWALA KWA RAHA HUKU NJE KUMBE NDIO KWANZA WANAJIPALILIA MKAA KATIKA DUNIA BILA KUSAHAU AKHERA NDIO KABISA.

BANDARI YA MALINDI YA BOTI DONGO ZA SAMAKI AINA YA VIBUWA KATIKA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI


Wafanyabiashara wa Uchuuzi wa samaki aina ya Vibuwa hapa nchini Zanzibar wakiwa katika bandari ya malindi wakipanga samaki hao kwa ajili ya wateja wao, katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa ramadhani samaki hutumika sana katika futari na daku, msimu ukiwa umeanza katika bandari hii ndoo moja ya kibua iliuzwa kwa shilingi 75000/= katika bandari hii.VIMETULEA

Friday, July 26, 2013

RAISI WA NCHI YA TANGANYIKA JK. KIKWETE AWACHIMBIA MIKWARA NCHI ZA JIRANI ASEMA WAKITHUBUTU WATAKIONA CHA MTEMAKUNI


Dar es Salaam nchini Tanganyika. Rais Jakaya Kikwete ametuma ujumbe kwa wale wanaoitishia Tanganyika. Amewaambia wakithubutu watakiona cha mtemakuni kama ilivyokuwa kwa Idd Amin wa Uganda.
Alisema mamlaka za ulinzi na usalama zilimdhibiti Amin alipofanya uvamizi katika ardhi ya Tanganyika mwaka 1978 na kwamba hazitashindwa kufanya hivyo kwa mtu mwingine yeyote atakayechezea usalama wa nchi.
Wakati Rais akisema hayo, Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange amewahakikishia wananchi kuwa wakati wote jeshi liko imara na kuwataka wasiogope lolote.
Viongozi hao walisema hayo jana katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa iliyofanyika katika Kambi ya Jeshi ya Kaboya iliyopo Muleba, Kagera.
“Sihitaji kusema tena, mmeshamsikia Mkuu wa Majeshi, atakayejaribu atakiona cha mtemakuni, laleni usingizi na msiwe na wasiwasi, msisikilize maneno ya mitaani,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Wakati wowote, saa yoyote tuko tayari kulinda nchi yetu. Hatuko tayari kuona amani inaharibika nchini, hatuwezi kuruhusu mtu yeyote kuimega au kuichezea nchi yetu kama alivyofanya Idd Amin.”
Katika siku za karibuni kumekuwa na kauli kadhaa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa nchi jirani ambazo zinatafsiriwa na wananchi kwamba ni za kuitisha Tanganyika.
Jenerali Mwamunyange alisema jeshi wakati wote liko imara kuwalinda wananchi na nchi kwa jumla hivyo wasiogope...“Endeleeni na shughuli zenu na msiogope mtu yeyote, fanyeni kazi zenu bila wasiwasi.”
Huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria maadhimisho hayo, Jenerali Mwamnyanye alisema yeyote atakayethubutu kuchezea usalama wa nchi atakiona cha mtema kuni.
Akizungumzia Siku ya Mashujaa, Rais Kikwete alisema ni siku ya kuwakumbuka mashujaa waliojitolea maisha yao wakati wa Vita ya Kagera kuilinda nchi yao ili iwe salama na yenye amani.
“Kuhakikisha usalama wa nchi kuna gharama yake kwani kuna wengine walikufa na wengine wakabaki na vilema kwa ajili ya hilo. Wale ambao wamebaki na wana matatizo lazima tuwaangalie vizuri na vile ambavyo havijafanyika tutavishughulikia kwani kutetea taifa ni kazi ngumu.”
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo, Makamu wa Rais, nchi ya Tanganyika Dk Gharib Bilal, Dk Mohammed Shein, Jaji Mkuu wa Tanganyika, Othman Chande na Jaji Mkuu wa nchi ya Zanzibar, Omar Othman Makungu ambao wote walipewa nafasi ya kuwasalimia wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo.  Awali, viongozi wa dini, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba Methodius Kilaini, Shehe wa Mkoa, Haruna Kichwabuta na Mwakilishi wa Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo, Askofu Elisa Buberwa walitoa wito kwa Watanganyika kuthamini amani iliyopo na umuhimu wa kuwa na mshikamano katika kuilinda na kuhakikisha kwamba haivurugwi kwa misingi ya imani, itikadi au ukabila.
Matatizo Muleba
Awali, Rais Kikwete wa nchi ya Tanganyika aliwahakikishia wananchi wa Muleba kuwa matatizo ambayo wabunge wao wameyawasilisha kwake mbele yao atayashughulikia.
“Nimesikia yale waliyoyasema hapa ; suala la mpaka kati ya eneo la wananchi na jeshi, Waziri wa Ardhi yupo hapa, kaeni na jeshi na vijiji ili tatizo liishe ni jambo ambalo linawezekana hivyo litatuliwe,” alisema Rais Kikwete.
Alisema suala la umeme na madaraja litashughulikiwa na viongozi wa mkoa wakishirikiana na wabunge na watakapokwama wafikishe kwake... “Mimi ndiye ninayetoa fedha za maendeleo hivyo hayo masuala yakikwama waniambie nitayashughulikia.
ANANZA KUCHOKONOWA KISHA VITA VIKIANZA WAZANZIBARI MSTARI WA MBELE WAULIWE VIZURI HAYA KIDOLE NA MACHO HICHO WAZANZIBARI.

Thursday, July 25, 2013

VIJANA WA JKU NCHINI ZANZIBAR NI WAZANZIBARI AU NI MITWANA,MISHENZI,MACHONGO,MIHUNI KUTOKA NCHI YA TANGANYIKA WAKOLONI WEUSI...??


WEWE MPUMBAVU SUJUDIA M/MUNGU SIO BENDERA NA MITWANA YA KITANGANYIKA.
Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad alipotembelea soko kuu la Darajani, mjini Unguja wiki iliyopita.

Maalim Seif alisema, kama ilivyo sheria ya nchi ya Zanzibar ya tokea siku za ukoloni, ya watu kuwa huru kufanya biashara wakati wa mwezi wa Ramadhani katika eneo hilo, basi mamia ya vijana wanaotafuta rizki hapo waachiwe kufanya hivyo mpaka utapomalizika mwezi huu.
Kauli hiyo imeonekana kuwakera baadhi ya wakubwa katika serikali, kama vile na wao hawauheshimu na kuutukuza mwezi wa Ramadhani.

Vijana wa linaloitwa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ambalo wengi wa wananchi wanaliona ni Jeshi la Kutesa Umma na kuwakandamiza Wanzibari ndani ya nchi yao ya Zanzibar walivamia eneo hilo siku ya pili yake kuonyesha dhihaka na jeuri kwa agizo la Makamo wa Pili wa Rais ambaye alifuatana na viongozi kadhaa katika safari yake.

Vijana hawa walionesha uhuni uliokubuhu. Kwanza kama kawaida yao, walipiga watu ovyo ovyo na hata kupora bidhaa zao. Ni aibu kwa nchi yetu ya Zanzibar kuwa na jeshi lenye wahuni wa kiwango hiki pia tunajiuliza kila siku jeshi hili kweli ni vijana wetu wa kutoka Zanzibar au niwanyamulenge machogo wa bara waliojanzwa katika kambi za nchi yetu ya Zanzibar...?? Inasikitisha, na zaidi kuona ushenzi huu unafanyika katika mwezi ambao Waislamu wanaamini ni wa rehma, kuoneana imani na kusaidiana.

Lakini kilichoonekana hapa huu uhuni wa askari wa JKU ndio aina ya rehma na msaada ambao wamepewa mafunzo ya kuutumia.

Ninaamini kwa dhati kabisa vijana hawa hawakwenda pale Darajani na kufanya uhuni ule bila ya kutumwa na wakubwa zao. Walitekeleza amri ya viongozi wanaojijua na ambao wajuwe wananchi wanawajua vilevile.
Uhuni huu unaonesha dhahiri kuwepo kundi la watu wasioitakia mema serikali ya umoja wa kitaifa pamoja na nchi yetu ya Zanzibar. Waniona serikali ya mfumo huu inasumbua uwezo na utashi wao wa kupora mali za watu, kupiga na hata kuua.

Ama kweli washairi wa karibuni, kama walivyo wale wahenga, hawakukosea waliposema: Aliyezowea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi.

Huu si ustaarabu, hasa ukitilia maanani kwamba nchi ya Zanzibar ilianza kutulia baada ya kuwa katika kipindi kilichojaa zahma za kisiasa baada ya kupatikana maridhiano ambayo baadhi ya viongozi kwa kuwa sasa wapo madarakani wanaonesha jeuri.

Watu hawa wanasahau kuwa kama siyo maridhiano ingelikuwa vigumu kwao kufika hapo walipo na ambapo wanapatumia kuhujumu wananchi. Ni vyema watazame hali inavyokuwa mbaya na nchi kutokalika kwa utulivu wakati pakikosekana siasa za maridhiano zinazohusisha kuvumiliana sana kisiasa.

Ni vizuri wahusika wa kufitini wakaacha mara moja mtindo wa kila mmoja kupiga kasia lake na tupige makasia kwa pamoja. Njia nzuri ya kuanzia ni kuwatia adabu wale wote waliotoa amri kwa askari wa JKU kwenda Darajani kufanya uhuni ulioonesha kukejeli agizo la Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad.

Ninaamini kwa dhati hao waliotoa amri hiyo hawatawaelekeza hata siku moja hao wanaoitwa askari wa JKU kwenda kukejeli amri ya Rais au ya Makamo wa Pili wa Rais wala kuongombowa nchi ya Zanzibar iliyo mezwa na Mkoloni Mweusi Tanganyika.

Lakini wamefanya hivyo kwa sababu wanayo ajenda yao ya siri ambayo sasa ipo dhahir shahir na kwa uwezo wa Mwenyeezi Mungu haitafanikiwa kuwarejesha Wazanzibari katika siasa za kupigana na kuuwana.

Ni vyema watu hao wakajirudi. Warudi kwenye mstari. Watu hawa mahodari wa kutumia vyombo vya habari vilivyo chini ya Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC) kufanya kile ambacho kwa wengi kinaokena kama ni kutaka kuwarejesha Wazanzibari walikotoka kwa sauti za upande mmoja tu kusikika zikishutumu watu wengine.

Watendaji wahafidhina hawa wasiotaka kuona Wazanzibari wanaishi kwa raha mustarehe ndani ya nchi wanayoipenda huku wakishindana bila ya kupigana, wametuma waandishi wa gazeti la Zanzibar Leo, kituo cha redio kilichokuwa Sauti ya Tanganyika Zanzibar (STZ) na televisheni ya TVZ kutafuta habari zilizolenga kujenga picha kwa umma kwamba agizo la Makamu wa Kwanza wa Rais halikuwa la busara. Waoneshe kuwa kiongozi huyu alikurupuka.

Siku ya pili tu baada ya agizo lile, ZBC Redio na televisheni zilikuja na taarifa za kuonesha utekelezaji wa agizo umeharibu taswira ya eneo la Darajani. Umewavimbisha kichwa wafanyabiashara na mbaya zaidi umewachochea wafanyabiashara walioko Saateni kugoma kulipa ushuru kwa madai kuwa wanabaguliwa kushikiliwa kubaki huko ilhali wenzao wanadekezwa kukaa Darajani na hivyo kupata wateja bila shida.

Kinachosababisha yote hayo mabaya ni mipango mibaya ya serikali tangu hata serikali ya umoja haijaingia. Serikali wakiwemo na viongozi wa Baraza la Manispaa wenyewe wameshindwa kutafutia ufumbuzi tatizo la matumizi mabaya ya eneo hilo.

Wakiulizwa viongozi hao ni kwa nini mpaka leo imeshindikana kutekeleza mpango wa kuendeleza mji (Master Plan) uliohusisha ramani ya kuvutia machoni mwaa mtu iliyowahi kupachikwa pale Darajani..??? Mbona hakuna maelezo yoyote mpaka leo ya ulikotokomea mradi ule..?? Viongozi waadilifu wangetoka hadharani na kuwaambia wananchi kilichotokea kuhusu mradi ule.

Hakika tunajua Maalim Seif hakukurupuka kutoa agizo lile. Alikuwa ameamua hasa kutoa ujumbe mzito tangu mwanzo wa ziara yake ile. Alikuwa anajua vizuri hali iliyopo. Anaijua hali inayowakumba wafanyabiashara hao ya kila siku kukimbizana na askari wanaojificha nyuso zao kwa soksi zinazotoa harufu mbaya. Anayajuwa yote haya.

Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad anajuwa mtindo huo umekuwa ukiumiza wananchi wanaohangaika kupata chejio. Anajuwa hawana kazi nyingine ya kufanya ili kumudu uwezo wa kuhudumia familia zao. Ndio, Maalim Seif anajuwa wanaohangaikia maisha Darajani wana familia zao zinazowategemea kimaisha.
Sasa wanaponyanyaswa kila kukicha, wanapopigwa na kudhalilishwa kila kukicha huku wakiporwa bidhaa zao, ndio serikali yao iliyopo kuwatumikia wao itakuwa inajenga au inabomoa..??? Itakuwa inawasaidia kumudu maisha au inawakandamiza na kuwavunja moyo..??

Ukweli Maalim Seif Shariff Hamad anajuwa fika kwamba serikali ambayo haijafanikiwa kuondoa tatizo kubwa la ajira linaloongezeka kila mwaka kwa maelfu ya vijana kuingia katika soko la ajira wakitafuta maisha baada ya kushindwa kuendelea na masomo, wana haki ya kufanya kazi. Wataishije bila ya kufanya kazi..?? Na serikali haipaswi kuvunja haki hii ya binadamu kwa visingizio visivyo mashiko.
Haya ya fikra za upande mmoja yanaonekana katika mjadala wa rasimu ya katiba na wanaopanga njama hizi wanajulikana.

 Ni pamoja na wale wanaoweka vizingiti na kutaka kuzuwia magazeti huru yasisajiliwe Zanzibar. Kwa kweli wamechelewa, kila wanachofanya dhahiri na siri kinajulikana. Hawana nafasi hata chembe ya kufanikiwa.
Watu hawa wanapaswa kujua sasa kuwa wanachokifanya ni sawa na simulizi ya mtu kulivunja daraja linalowaunganisha Wazanzibari lengo likiwa ni kuwaangamiza. Sasa ninawauliza, kama walivyotuasa wahenga: Jee, wameshajifunza kuogelea..??? Kama bado, ni kwa nini basi wanafanya hima na njama za kulibomoa daraja..???

Nijuavyo mimi wengi wao hawajuwi kuogelea kwa vile si wana kindakindaki wa nchi ya Zanzibar. Nchi ambayo watu wake wengi hujuwa kuogelea. Kwa hivyo ni vizuri waelewe kuwa Wazanzibari kindakindaki si watakaozama kwani wanazijua mbinu za kujiokoa pale jahazi la kisiasa likizama, ikiwa pamoja na kuogelea.

Wenyewe Wazanzibari wana wa kindakindaki yakitokea tu hujisemea: “Poo…simo.” Jee wao wenzangu na mie waliopo mbele kuchochea fitna na idhilali watajiokoaje wasikumbwe na madhara ya idhilali hiyo..???

Tumuombe Mungu aiepushe nchi yetu ya Zanzibar na hawa mahasidi wasiovitakia kheri visiwa vya Unguja na Pemba. Mungu ajaalie watu wake waendelee kuishi kwa amani, raha, furaha na maelewano yenye maridhiano ya kweli na siyo ya kinafiki.

Wednesday, July 24, 2013

MAKAMO WA KWANZA WA RAISI NCHINI ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMADA KATIKA ZIARA YAKE YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI YA KUTEMBELEA WAGONJWA NA WAFIWA.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali na kumfariji mzee Muombwa Rashid wa Kajengwa Makunduchi, wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika  Mkoa wa Kusini Unguja
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif 

Sharif  Hamad, akimjuilia hali na kumfariji mzee Muombwa 

Rashid wa Kajengwa Makunduchi, wakati wa ziara yake ya 

kutembelea wagonjwa katika Mkoa wa Kusini Unguja
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali  na kumfariji Bi. Mkasi Jihadi wa Kijini Makunduchi wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika  Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif 

Sharif  Hamad, akimjuilia hali na kumfariji Bi. Mkasi Jihadi 

wa Kijini Makunduchi wakati wa ziara yake ya kutembelea 

wagonjwa katika Mkoa wa Kusini Unguja nchini Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na wananchi wa Makunduchi wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika  Mkoa wa Kusini Unguja
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif 

Sharif  Hamad, akisalimiana na wananchi wa Makunduchi 

wakati  wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Mkoa 

wa  Kusini Unguja nchini Zanzibar
Wananchi mbali mbali wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni Zanzibar
Wananchi mbali mbali wakijumuika katika futari 

iliyoandaliwa na Makamo wa Kwanza wa Rais nchini 

Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake 

Mbweni nchini  Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad akimfariji mzee Ali Juma Makame wa Mkwajuni, baada ya kumjuilia hali ikiwa ni ziara ya kiongozi huyo ya kutembelea wagonjwa na wafiwa
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif 

Sharif  Hamad akimfariji mzee Ali Juma Makame wa 

Mkwajuni,  baada ya kumjulia hali ikiwa ni ziara ya Makamo 

wa Raisi wa nchi ya Zanzibar ya  kutembelea wagonjwa na 

wafiwa.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali mzee Faraji Mziwanda wa Chaani, ikiwa ni ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif 

Hamad, akimjuilia hali mzee Faraji Mziwanda wa Chaani, 

ikiwa ni ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wafiwa 

katika Mkoa wa Kaskazini Unguja nchini Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali Haji Makame Sangire wa Kigunda, ikiwa ni ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.  Picha zote na Salmin Said, OMKR.
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif 

Sharif  Hamad, akimjulia hali Haji Makame Sangire wa 

Kigunda, ikiwa ni ziara yake ya kutembelea wagonjwa na 

wafiwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja nchini Zanzibar.

Masheikh mbali mbali walio jumuika katika nyumba ya Makamo wa Raisi Maalim Seif Shariff Hamad nchini Zanzibar katika futari aliyo wandalia Masheikh hao.
 
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif Sharif 

Hamad akiitikia dua wakati akimjuilia hali Bi. Maryam Omar wa 

Kilimahewa Msikiti ngamia, wakati wa ziara 

yake kwa wagonjwa Mkoa wa Mjini Magharibi nchini Zanzibar.

Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amewahimiza waislamu kushirikiana na kusaidiana ili kudumisha umoja miongoni mwao.
Amesema umoja na mshikamano ndio nguzo ya kuzidisha mapenzi miongoni mwa waislamu, na kutaka utamaduni huo uendelezwe kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo alipokuwa akitoa shukrani kwa masheikh na wananchi waliojumuika nae katika futari aliyoiandaa kwa ajili ya viongozi hao wa dini, nyumbani kwake mbweni.

Amewashukuru masheikh kwa kujitokeza kwa wingi katika futari hiyo, na kwamba kitendo hicho kinaashiria mapenzi waliyonayo viongozi wa dini kwa viongozi wao wa kitaifa.
Wakati huo huo Maalim Seif amehitimisha ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wafiwa kwa upande wa Unguja nchini Zanzibar, baada ya kufanya ziara katika Mkoa wa Mjini Magharibi.

Katika ziara hiyo ametembelea maeneo mbali mbali ya Wilaya za Mjini na Magharibi na kuonana na wagonjwa na wafiwa katika mitaa tofauti ikiwemo Mbweni, Tomondo, Magogoni na Mji Mkongwe.

Akiongozana na viongozi mbali mbali wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib Ferej na Naibu Waziri wa Elimu Zahra Ali Hamad, Maalim Seif alianza ziara mapema asubuhi katika mitaa wa Mbweni matrekta, Kiembe samaki na Mwanakwerekwe, kabla ya kusitisha ziara hiyo na kujumuika katika mazishi ya wanajeshi wawili wa Zanzibar waliouliwa Darfur nchini Sudan.

Alihitimisha ziara hiyo kwa kutembelea Jimbo la Mji Mkongwe alipokwenda kuwajuilia hali na kuwafariji mzee Salim Mzee wa Darajani na mzee Ali Yussuf wa Mkunazini.
Ziara kama hiyo inatarajiwa kufanyika katika mikoa ya Pemba nchini Zanzibar hivi karibuni, ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Tuesday, July 23, 2013

VIDEO-ANGALI UFAIDIKE KATIKA MASWALI TUNAYO JIULIZA NA MAJIBU YAKE ZANZIBAR KWANZA


NCHINI ZANZIBAR WALIO KWENDA KUTAKA KUWAZIKA WANAJISHE WETU WA ZANZIBAR WALIOULIWA DARFUR NCHINI SUDAN NA WAO WAPATA AJALI


Madaktari katika hospitali ya mnazi moja wakitowa huduma kwa wananchi na wanajeshi walio pata ajali wakati wakienda katika maziko ya wanajeshi waliouliwa darfur nchini sudan ajali hiyo imetokea mwanakwerekwe sokoni

daktari katika hospitali ya mnazi moja ikitowa huduma ya kwanza ya moja wa wanajeshi walio pata ajali wakati wakiende mazikoni kuwazika wanajeshi wa zanzibar waliouliwa darufur  nchi sudan
06
Moja katika majeruhi akiteremshu katika lori la jeshi wa nchi ya Zanzibar walio pata ajali walipokuwa wanakwenda kuwazika wanajeshi waliouliwa Darfur Sudan

daktari katika hospitali ya mnazi moja akitowa huduma ya kwanza kwa mahatuti aliyefikishwa hospitalini baada ya kupata ajali na gari walilo kuwa wanakwenda kuwazika majeshi wa zanzibar waliouliwa darfru nchini sudan

Moja wa majeruhi waliokuwa katika gari lililo pata ajali akipewa huduma ya kwanza baada ya kufikishwa hospitali ya mnazi moaja

Madaktari wakimpokea na kumkibizi ndani ya hospitali ya mnazi moja. moja wa rai wa Zanzibar nchi Zanzibar baada ya kupata ajali walipokuwa wakiende kuwazika majeshi waliouliwa Darfur nchini sudan

Madaktari na manasi wakitayarisha mabendeji ya kutowa huduma ya kwanza mnazi moja


WAMEKWENDA KUULIWA DARFUR SUDAN SI BORA MUNGELIULIWA KWA JILI YA NCHI YENU YA ZANZIBAR IWE HURU ILIYO MEZWA NA JOKA KUBWA TANGANYIKA




Ni moja katika vizuka akitokea jijini Dar es salaam nchini Tanganyika kupokea maiti ya mume wake aliye kuwa ni moja katika wanajeshi saba waliouliwa Darfur nchini Sudan hapa ni kiwanja cha denge nchini Zanzibar huu msiba unatukumbusha dungu zetu walio pelekwa Uganda na kuliwa sisi Wazanzibar hatusomi.

Na huyu ni kizuka wapili na familia ya wanajeshi wa nchi yetu ya Zanzibar waliouliwa Darfur nchini Sudan

DR Shein akisaini katika maziko ya wanjeshi wawili wa Kizanzibari waliouliwa Durfur nchini Sudan

majeneza ya wanajeshi wa Kizanzibari waliouliwa Darfur nchini Sudan wakisomewa hitma na duwa kabla ya kuswaliwa swalati maiti nchini Zanzibar

Makamo wa raisi nchini Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akisoma hitma ya wanajeshi waliouliwa Darfur nchini Sudan

Hii ni swalati maiti viongozi na rai wa Zanzibar wakiwaswalia wanajeshi wawili waliouliwa Darfur nchini Sudan.

Majeneza yakitoka msikitini na kupakiwa katika malori ya kijeshi tayari kuelekea katika makaburi ya mwanakwerekwe nchini ZanzibarMoja katika majeneza ya wanajeshi wa nchi yetu ya Zanzibar yakiwasili katika makaburi ya Mwanakwerekwe tayari kwa maziko moja katika wanajeshi waliouliwa Darfur nchini Sudan

Wanajeshi wakifyatuwa risasi agani kuashiria maziko ya moja wa wanajeshi wa Zanzibar waliouliwa Darfur nchini Sudan

Viongozi na majeshi na rai wa nchi ya Zanzibar wakiwa katika makaburi ya mwanakwerekwe kusubiri mazisha ya kuwazika wanajeshi wawili wa hapa nchini kwetu Zanzibar waliouliwa Darfur nchini Sudan.

Dr Shein akitia mchanga katika kaburi moja la mwanajeshi wa yetu ya Zanzibar aliyeuliwa Durfur nchini Sudan

Jenerel wa nchi ya Zanzibar akitia mchanga katika kaburi moja la wanajeshi waliouliwa Darfur nchini Sudan

Dr Shein akitowa pole na kuwasalimu rai wa nchi ya Zanzibar kwa msiba wa wanajeshi wao waliouliwa Darfur nchini Sudan.

PUMBAVU LIKI PUMBA BASI PUMBA NALO


Sambamba na hayo Salim Suleiman Ameir kutoka shehia ya Donge alisema Muundo wa serikali tatu si makubaliano ya Waasisi Abeid karume na Mwalimu Nyerere na kudai kuleta mfumo mpya ni kuvunja heshima yao.

MANENO YA HUYU MZEE NI KAMA HILI JOKA
“Tukiwa na Muungano wa shirikisho lazima kuwe na mkataba maalumu mmoja akiukiuka ndio Muungano ushavunjika uoo, kwa hiyo ni vyema tuendelee na mfumo wetu huu uliasisiwa na wazee wetu ili tupate radhi zao” alieleza Ameir.

RAISI KIKWETE ASEMA TANGU UHURU NI SERA YA NCHI YETU KUTETEA WANYONGE DHIDI YA UKOLONI,UBAGUZI,UONEVU,DHULMA-HAYA YOTE ULIOSEMA NCHI YA TANGANYIKA INAIFANYIA NCHI YETU YA ZANZIBAR!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Dar es Salaam.nchini Tanganyika Rais Jakaya Kikwete ameutaka Umoja wa Mataifa (UN), kuruhusu kutumika kwa mtutu katika operesheni za kulinda amani zinazoendelea.
Alitoa kauli hiyo jana baada ya kutoa heshima zake kwa wapiganaji saba wa Tanganyika waliouliwa Darfur, Sudan katika operesheni ya kulinda amani ya U.N na Afrika (Unamid) ambao waliouliwa.
Wapiganaji waliouawa ni Oswald Chaula kutoka 42KJ Chabruma, Songea, Peter Werema (44KJ Mbeya), Fortunatus Msofe (36KJ Msangani, Pwani), Rodney Ndunguru (92KJ Ngerengere), Mohamed Juma (94KJ Mwenge), Mohamed Chukilizo (41KJ Nachingwea) na Shaibu Othman (MMJ- Upanga).
“Raisi wa Tanganyika alisema lazima nikiri kuwa taarifa hiyo ya vifo vya vijana wetu ilinihuzunisha, kunisikitisha na kunikasirisha. Kwa nini watu wa Darfur wawaue wanajeshi wetu ambao wamekwenda kule kuwasaidia wapate utulivu ili kunusuru maisha yao, kuwaondolea wasiwasi na kuwawezesha wafanye shughuli zenye tija kuendesha maisha yao..???
“Moja kwa moja sikusita kuamini kuwa waliofanya hivyo ni watu wahalifu. Tangu uhuru ni sera ya nchi yetu kutetea wanyonge dhidi ya ukoloni, ubaguzi, uonevu, dhuluma na watu wote walioko katika mazingira hatarishi Afrika na duniani.(swali tunamuliza kikwete mbona huwatetei Wazanzibar au wao sio wanyonge..? Zanzibar hatuoni muungano tunaona ukoloni au wewe huwoni...? mumetubaguwa Wazanzibari mpaka tumechoka sasa tunataka nchi yetu au unakata kuwa hamutubaguwi..? munatuoneya katika kila kitu cha muungano nyinyi munatuoneya au hamutuonei..? mumetudhulumu mpaka nchi yetu ya Zanzibar imekuwa kama kijiji tu cha Tanganyika tulipeni basi pesa zetu tulizo towa katika benk kuu tulipeni wanajeshi wetu walio uliwa uganda mpaka leo hamujawalipa tulipeni pesa zote mulizo omba nchi za nje kwa mgongo wa Tanzania kisha mukazitia katika mfuko wa Tanganyika n.k. hiyo sio thulma..? sasa nyinyi wenyewe thulma kisha ati munakwenda nchi nyingeni kusitisha thulma sivichekesho. U.N ifanyie marekebisho sheria ili majeshi yanayolinda amani yawe na nguvu za kujihami ili kuzuia maafa yanayoweza kujitokeza.”
Hivi karibuni, Msemaji wa Unamid, Chris Cycmanik alimwambia mwandishi wetu wa siri: “Majeshi ya U.N mjini Darfur yanaweza kufanya kazi chini ya Kifungu cha VII ambao inaruhusu kutumia nguvu lakini kwa hali iliyopo hawafanyi hivyo,” alisema.
Rais Kikwete alisema eneo hilo ni hatarishi kwa sababu hadi sasa watu 41 kutoka katika nchi mbalimbali wameuawa wakati wakilinda amani huku wengine 55 wakijeruhiwa tangu mpango wa kulinda amani ulipoanza mwaka 2007.
“Tumeshawasilisha U.N maombi kutaka Kifungu namba Sita cha kulinda amani kibadilishwe na kitumike Kifungu namba Saba ambacho kinawataka wanajeshi kujihami pindi wanapovamiwa na maadui,” alisema.
Alisema tayari amewasiliana na Rais al-Bashir akimtaka kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua kali wote waliohusika na tukio hilo huku akiwataka wanajeshi kutokata tamaa kwa tukio hilo na kulichukua kama changamoto katika kujilinda na kuwabaini maadui.
Aliwapa pole wafiwa na kusema Serikali na wananchi wote wapo pamoja katika kipindi hiki kigumu na kuwataka kuwa na subira. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha alisema kitendo cha waasi kuwaua wanajeshi saba wa Tanganyika ni mkakati wa vikundi vya waasi kuhakikisha kuwa jitihada za kuleta amani zinagonga mwamba.
Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanganyika (JWT), Jenerali Davis Mwamunyange alisema askari hao pamoja na wengine walikuwa wakisindikiza msafara wa walinzi wa amani uliokuwa ukitoka katika kambi yao karibu na Mji wa Nyala.
Alisema walipofika kilometa 25, katika eneo la Khor Abeche walivamiwa kwa kushtukizwa na kikundi cha watu wachache na kwa sababu hawakuwa na silaha za kujihami, walishindwa kujitetea na kusababisha vifo hivyo.  Simanzi, vilio vyatawala
Rais Kikwete aliwasili katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa saa 11.10 asubuhi na kupokewa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Jenerali Mwamunyange.
Muda mfupi baadaye, malori saba kila moja likiwa na mwili wa wanajeshi hao yaliwasili katika viwanja vya wizara hiyo.
Wakati miili hiyo ikiteremshwa kwa ajili ya kuaga, wafiwa ambao awali, walikuwa wametulia kwenye viti walianza kulia.
Rais na mkewe, Salma walianza kutoa heshima zao na kisha kuwapa mkono wa pole wafiwa.
Askari wawili wa JWT walizirai wakati utoaji huo wa heshima za mwisho ukiendelea na walibebwa na wenzao kwenda kupatiwa huduma ya kwanza.
Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam walijitokeza katika viwanja hivyo kiasi cha wengine kukosa nafasi ya kuingia ndani hivyo kulazimika kukaa nje hadi miili hiyo ilipoondoshwa tayari kwa kusafirishwa sehemu mbalimbali kwa maziko.

Sunday, July 21, 2013

BENDERA YA NCHI YA ZANZIBAR ILIPO PANDISHWA U.N.NEW YORK 1963 MIAKA 50 BAADAYE CCM MUME FANYA NINI ZAIDI YA KUITIA UMASIKI NCHI YA ZANZIBAR



BADALA YA KULETA MAENDELEO KWA WANANCHI WEWE NI MATUSI,UBAGUZI,KEJELI,MIPASHO NA NYINYI MAJUHA MULO KAA NA KUSIMAMA KUMSIKILIZA SIJUWA MUTAZINDUKA LINI.NYUMBA MUNAZO ISHI MPAKA LEO 2013 HAMUNA MAJI WALA UMEME,CHOO NA CHOO CHA BAFUU NDIO HICHO HICHO KIMOJA, ISITOSHE CHOO CHENYEWE KIKO NJE YA NYUMBA,MLO MOJA KWA SIKU, MIHOGO YA KUCHEMSHA HAMNA HATA KIBUWA MUKISHA PEWA UPANDE WA KANGA NA PANGA NDIO MUNAONA MAISHA KUMBE MUMELIWA

Hii benderaa pili kutoka mkono wa kulia na ya nne kutoka mkono wa kushoto ndio bendera ya nchi ya Zanzibar baada ya kupata UHURU. Siku bendera ya Nchi ya Zanzibar ilipopandishwa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, mwezi Disemba 1963. Wazanzibari sasa wanataka kurudisha mamlaka kamili ya nchi yao ya Zanzibar baada ya miaka karibuni 50 ya nchi yao kutolewa katika muungano wa U.N. na kupelekwa katika  Muungano wa mkoloni mweusi Tanganyika na chama cha ccm chama cha majuha,choyo,waroho wa madaraka,wabaguzi,wasio juwa kufikiri,wasio juwa nini maendeleo isipokuwa matumbo yao kwa wake zao na familia zao,miroho na tamaa,wauwaji,mathalim,majambazi,wala haramu wasio ogopa siku ya kiyama,wakotayari kuuwa kwa matumbo yao.

LETE MAENDELEO SIO MLIPI MREFU, POROJO,MATUSI,CHUKI,UBAGUZI,FITINA,MIYAYUSHO,UWONGO,UKALI,KEJELI.HOSPITALI MPAKA LEO HAKUNA DAWA,VITANDA,MZEE KARUME KAJENGA VIWANDA NYINYI MIAKA 50 MUMESHINDWA HATA KUVIENDELEZA WACHILIAMBALI KUJENGA VYEPYAA,MPAKA LEO BADO KUNA WAZANZIBARI MLO MOJA UNAWASHINDA WAKATI NYINYI VIONGOZI NA WAKE ZENU NA WATOTO WENU MUNAMWANGA VYAKULA.
Wazanzibari wanatoa maoni yao kwa uhuru kamili. Wanafanya hivyo wakitambua kwamba fursa waliyonayo sasa huenda wasiipate tena.
Wanaelewa vyema umuhimu wa kuwa na msimamo mmoja ili waweze kuigomboa nchi yao kutoka katika tumbo la chatu mkoloni mweusi Tanganyika. La sivyo, wakichezacheza na wasipoungana kifikra basi fursa hiyo inaweza ikawaponyoka, wakajikuta wamekwenda kapaa. Katika hayo majadiliano kuhusu mustakabali wa nchi ya Zanzibar suala la Muungano feki ndo jambo kubwa linalozungumzwa nchini Zanzibar. Muungano feki unajadiliwa mijini, vijijini na kwenye vitongoji Unguja na Pemba.
Ukiwasikiliza wananchi wa nchi ya Zanzibar utawasikia wanataka irejee Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, ikiwa ni dola kamili iliyo huru kama ilivyokuwa awali pia Wazanzibari wanataka ujirani mwema na nchi ya Tanganyika,Kenya,Uganda pamoja na nchi nyingine za eneo hili. Tofauti ya mahusiano yaliyopo sasa na hayo wayatakayo ni kwamba wangependelea huo mfumo mpya wa mahusiano ya kufungamana uwe wa mikataba na si wa Katiba lakini baada ya kuwa na nchi yao ilio huru ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Msimamo huo ni sehemu ya ile iitwayo Ajenda ya Zanzibar niliyowahi kuizungumzia miezi kadhaa iliyopita. Ni ajenda inayopigiwa debe na wengi wa Wazanzibari wakiwa pamoja na viongozi wao kutoka vyama tofauti vya kisiasa na asasi isipokuwa CCM baadhi ya viongozi wasio shiba na uroho wao bado.
Wengi wao wanaamini kwamba kutokana na Hati za Muungano huu feki na mambo mengine yaliyoingizwa kuwa ni ya Muungano raisi aliyewekwa hapa nchini Zanzibar na giningi DODOMA SIO RAISI ALIYE CHANGULIWA NA WAZANZIBARI. Pia  baraza letu la kutunga sheria (Baraza la Wawakilishi) na Mahakama yetu. Mamlaka ya taasisi zote hizo tatu za Zanzibar, ambazo ni mihimili mikuu ya dola, yamepunguzwa katika kipindi cha miaka 47 ya Muungano feki.
Kilichotokea ni kwamba kwa muda wote huo unaokaribia nusu karne mamlaka au madaraka yote ya nchi ya  Zanzibar yaliyo muhimu yamehamishwa nchini Tanganyika kwa mkoloni mweusi. Ujanja ulitumika kulifanya Bunge la nchi ya Tanganyika liwe Bunge la Muungano feki na kuigeuza Katiba ya nchi ya  Tanganyika iwe Katiba ya Muungano feki. Ujanja vilevile ulitumika kuifanya Serikali ya Muungano feki iwe ndiyo Serikali ya nchi ya Tanganyika na ya Tanganyika iwe ya Muungano feki.ikawa nchi ya Tanganyika imeva koti na kujiita ya muungano feki. Shughuli za Jamhuri ya Muungano ya ((Tanzania)) na za Jamhuri ya Tanganyika zimekuwa zikiendeshwa na Serikali moja.
Kwa upande mwingine, Zanzibar na Serikali yake hazina jukumu kubwa au la maana katika utawala na uongozi wa Muungano feki. Ingawa kwa mujibu wa Sheria za Kimataifa na kwa mujibu wa Hati za Muungano, Zanzibar na Tanganyika ni washirika wenye hadhi sawa ndani ya Muungano feki, mambo yanavyokwenda ni kwamba Zanzibar imewekwa kando au maneno ya mtaa imepingwa bao.
Zanzibar imetoweka hata kutoka kwenye ramani ya dunia na haina jukumu lolote la maana katika shughuli za eneo letu la Afrika Mashariki au la Afrika au ulimwenguni kwa jumla. Wala Zanzibar haipati manufaa yoyote inayopata nchi yenye kushiriki katika uchumi wa dunia; isitoshe, hairuhusiwi kujihusisha na taasisi za kimataifa ni kusema nchi ya Zanzibar iko jela chini ya nchi ya Tanghanyika mkoloni mweusi.
Hii leo wanasiasa wa Tanganyika hawawezi tena kuyapuuza manung’uniko na matakwa ya Wazanzibari kwa sababu wamekwishatanabahi kwamba Muungano feki kwa namna ulivyo sasa, uko kwenye njia panda na wakati umefika wa kufanya uamuzi muhimu kuhusu mustakabali wake.
Kwa sasa hakuna anayeweza kutabiri nini yatakuwa matokeo ya nchi ya Zanzibar je itakuwa huru au itaendelea kuwa chini ya mkoloni mweusi Tanganyika.
Mnamo miaka ya 1990 palitolewa pendekezo la kutaka pawepo na mfumo wa serikali tatu, yaani Serikali ya Tanganyika, ya Zanzibar na ya Muungano. Waliopendekeza hivyo waliamini kwamba mfumo huo wa serikali tatu ndio ulio bora na utaokubaliwa na washirika wote wawili, yaani Tanganyika na Zanzibar.
Kwa hakika, baadhi ya wanasiasa mashuhuri wa Tanganyika nao walifanya jaribio la kuifanya nchi yao iwe na serikali yake ndani ya Muungano. Jaribio hilo halikufika mbali kwani Julius Nyerere alitumia nguvu zake za turufu na kulizima suala hilo.
Pendekezo hilo liliibuka tena lilipotolewa kwa mara nyingine na Tume ya Muungano feko iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Robert Kisanga. Rais wa Muungano feki wa wakati huo, Benjamin Mkapa aliye uwaa wapemba wengi siku za changuzi. naye alilipinga. Hatujui ikiwa huo ndio mwisho wa pendekezo hilo au iwapo Serikali ya Muungano feki italikubali kuwa njia murua ya kuunusuru Muungano feki usiporomoke.
Iwapo Serikali ya Muungano feki hatimaye italikubali pendekezo hilo hatujui kama Wazanzibari nao wataliridhia kwa vile pendekezo hilo ukiliangalia kwa undani haliipi nchi yao ya Zanzibar uhuru wake kamili bali linauwekea mipaka. Muungano  huo wa serikali tatu utakuwa Muungano utaojengwa juu ya misingi ya mkataba na sio Katiba.
Ndio maana siku hizi huko Zanzibar mazungumzo kuhusu Muungano ni ya kutaka serikali tatu sio mbili labda hawa wafidhina ndio wanataka mbili. Au kama hawataki nchi ya Tanganyika basi kila moja abaki na nchi yake. Wazanzibari wengi wanahisi kwamba ule mfumo wa serikali mbili za Muungano umekwishapitwa na wakati. Wanapotoa hoja zao wanasema kwamba mfumo huo labda ungekubalika katika miongo iliyopita lakini si mnamo mwaka 2015.
Hata wale wenye kuunga mkono mfumo wa serikali tatu sasa wanasema kwamba ile serikali ya tatu, yaani ya Muungano, isiwe na mamlaka mengi kwani wanachotaka ni Zanzibar kuwa na uhuru zaidi ndani ya mfumo mpya wa Muungano.
Hao Wazanzibari wenye kutaka Muungano utaoundwa juu ya misingi ya Mkataba na sio Katiba wanahoji kwamba mfumo wa Muungano wa Mkataba ndio ufaao kwa mataifa yaliyo huru. Wanaendelea kuhoji kwamba hakuna haja ya kuwepo Serikali ya ((Tanzania ambayo ni Tanganyika imeva joho)). Badala yake, wanasema, pawepo Tume Maalumu ya Muungano itayokuwa na nguvu hafifu au mamlaka machache na itayosimamia vifungu vya Mkataba wa Muungano.
Mfano wanaoutaja mara kwa mara ni ule wa Tume ya Muungano wa Ulaya. Wanataka Muungano wao uwe mithili ya ule wa Ulaya ambao umeundwa kwa mikataba ya kimataifa kati ya nchi 27 zilizo huru. Majaribio ya kutaka pawepo Katiba moja ya Muungano huo yalikataliwa pale palipofanywa kura za maoni katika baadhi ya nchi wanachama. Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa Muungano huo kila nchi ina kura ya turufu, na inaweza kujivuta na kujitoa kutoka kwenye Muungano kwa vile maamuzi yote makuu hukatwa kwa nchi kukubaliana.
Wazanzibari wenye kuupigania mfumo huo wanasema kwamba mfumo huo si kwamba unazifaa nchi ya Zanzibar na Tanganyika tu bali pia ni mujarab kwa bara zima la Afrika. Bara hilo nalo linahitaji kuwa na chombo kitachoziunganisha nchi zake zote kwa maslahi ya nchi wanachama.

WANAJESHI WA JWT NCHI TANGANYIKA WALITHANI DARFUR NI KAMA MTWARA NA ZANZIBAR WATAPIGA WANAVYOTAKA NA KUUWA WANAVYOTAKA


HAWA NI VIONGOZI WA CUF NCHINI TANGANYIKA WAKIONYESHA ALAMA ZA VIPIGO WALIVYO PEWA NA JESHI LA LA NCHI YAO JWT HUKO NCHINI KWAO TANGANYIKA
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) mkoani Mtwara nchini Tanganyika wakiwaonyesha waandishi wa habari majeraha yanayodaiwa waliyapata baada ya kupigwa na wanajeshi wa JWT.
Viongozi watano wa Chama cha Wananchi (CUF), wamesimulia mateso na vipigo walivyovipata wakati wakiwa mikononi mwa Jeshi la Wananchi (JWT) mkoani Mtwara nchini Tanganyika.
Viongozi hao ni Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi (Taifa) Shaweji Mketo, Mwenyekiti Jumuiya ya Vijana (JUVICUF) wilaya ya Mtwara Vijijini, Ismail Njalu na Mwenyekiti wa wilaya ya Mtwara Mjini, Salum Mohamed.
Wengine ni Mwenyekiti wa wilaya ya Mtwara vijijini, Ismal Jamal, Katibu wa wilaya ya Mtwara Mjini, Said Kulagwa na dereva wa gari walilokuwa wakilitumia siku ya tukio, Kashinde Kalumbwana.
Pamoja na taarifa hizo kwa wanahabari, wameeleza kusudio lao la kwenda mahakamani baada ya kuwasiliana na mwanasheria wao pamoja na asasi zinazotetea haki za binadamu.
Viongozi hao wanadai kukamatwa Juni Juni 27, mwaka huu na kupata mateso yaliyowasababishia majeraha, wakiyaonesha kwa waandishi wa habari, kwamba yalifanywa na wanajeshi wa JWT.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mketo, alidai kuwa siku ya tukio walikuwa wakitoka kufuatilia madai yaliyowafikia kuhusu kuwapo wanajeshi watatu wa JWT hapa hapa nchi waliombaka mtoto (jina kapuni).
“Taarifa tulizopata nyumbani kwa mtoto huyo ni kwamba wanajeshi hao walifika hapo na kumkuta (mtoto huyo) akiwa jikoni, wakamdanganya kuwa watampa Shilingi 3,000, wakamkamata kwa nguvu wakambaka walitumia mipira, (kondom)” alidai.
Mketo alisema katika kufuatilia zaidi tukio hilo, alibaini uchunguzi wa daktari uligundua kuharibika sehemu zake za siri za mtoto huyo vibaya sana.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo, aliamua kulikabidhi suala hilo kwa viongozi wa chama eneo husika ili kuendelea kufuatilia hatma yake.
Alisema baada ya kulikabidhi, wakati wakirudi Mtwara mjini, walikutana magari mawili ya JWT yakiwa yameziba barabara.

Alisema eneo hilo kulikuwa na wanajeshi zaidi ya 50 ambao baada ya wao kusimama, walikamatwa na kuanza kupigwa.
“Nilikuwa na Shilingi 85,000 mfukoni wakati tunatembezewa kipigo, mmoja wa wanajeshi alitaka kuzichukua katika kupambana naye, mwanajeshi huyo alinihoji kwa nini nagombana na kanali wa jeshi,” alidai.
Alieleza kuwa baada ya kipigo hicho, walichukuliwa kupelekwa katika kambi ya jeshi ya Lembele, ambapo waliposhushwa, mmoja wa wanajeshi aliwataka wenzake waandae peni na panadol kwa ajili yao, lakini hawakujua ilimaanisha kitu gani.
“Tulivuliwa nguo zote na kuanza kupigwa bila kujali unapigwa wapi, tulipata majeraha na kuvuja damu nyingi, “ alidai na kuongeza:
“Cha ajabu kilichofuata, yalitengenezwa maji yenye barafu ambayo ndani yake yaliwekwa pilipili na ndimu, tukawa tunamwagiwa kwenye majeraha.”
Mketo alidai kuwa kwa upande wake, aliwahi kufanyiwa upasuaji eneo la ubavuni, hivyo kutokana na mateso hayo, aliamua kuwaweka wazi wanajeshi hao juu ya tatizo lake.
Alisema licha ya kufanya hivyo, kilichotokea ni kwamba aliitwa mwanajeshi (daktari) ambaye baada ya kudhibitisha hilo, waliamriwa wanajeshi wengine wawili wamshike mikono juu na kuambulia kipigo eneo lililofanyiwa upasuaji.
“Ilifikia hatua nikatamka maneno haya, nipigeni najua mmetumwa na Pinda, baada ya mateso makali, walimuita Mkuu wa upelelezi Mtwara na polisi ili watuhoji,” alisema.
Mketo alisema baada ya mahojiano, siku iliyofuata jioni walisomewa mashtaka yao na kupelekwa gerezani ambapo huko walikataliwa kutokana na majeraha waliyokuwa nayo.
“Jeshi la magereza liliamua kutuchukua kutupeleka hospitali ya Igula kwa matibabu na baadaye waliturudisha gerezani, hadi hapo tulipoachiwa,” alisema.

Akielezea zaidi hali ya Mtwara, Mketo alisema kuwa, sio shwari na kwamba wananchi wamekuwa wakipigwa bila hatia.
Kufuatia mateso hayo, CUF imemtaka Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati suala hilo kwa sababu kazi ya polisi ni kulinda sio kutesa raia.


WAMEKWENDA DARFUR SUDAN KWA MIGUU YAO WANARUDI KWENYE MASANDUKU WANAJESHI WA NCHI YA TANGANYIKA
Dar es Salaam.nchini Tanganyika Makamu wa Raisi wa nchi hiyo ya Tanganyika, Dk Mohamed Gharib Bilal jana aliwaongoza mamia ya waombolezaji kupokea miili saba ya wanajeshi wa Tanganyika wa nchi hiyo waliouliwa Darfur, Sudan, Julai 13, mwaka huu.

Miili ya wanajeshi hao saba iliyowasili jana ni Sajeni Shaibu Sheha Othman, Koplo Osward Paulo Chaula, Koplo Mohamed Juma Ally, Koplo Mohamed Chukilizo, Private Rodney Ndunguru, Private Peter Werema na Private Fortunatus Msofe.

Wanajeshi hao walikuwa sehemu ya Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa (Unamid), kusini mwa Darfur imeelezwa kuwa wanajeshi hao waliouliwa na kikundi cha waasi, huku wengine 19 wakijeruhiwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa walikuwa wakifuatilia magari yao yaliyokuwa yametekwa na kundi hilo.
 
Hali ilivyokuwa

Baada ya miili hiyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Jeshi saa 10:40 jioni na ndege ya Antlantis iliyotolewa na Umoja wa Mataifa(UN), mamia ya watu waliokuwapo uwanjani hapo walionekana kuingiwa na huzuni baada ya kuona miili ya marafiki, ndugu na jamaa zao ikishushwa kwenye ndege hiyo.

Baada ya ndege hiyo kuwasili, viongozi wakuu wa Serikali pamoja na wambolezaji wengine waliisogelea ndege hiyo kwa ajili ya kupokea miili ya wanajeshi hao.

Miili hiyo ilishushwa na kuingizwa kwenye magari saba ya jeshi, na kupelekwa katika Hospitali ya Jeshi la Lugalo kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Wanajeshi hao wanatarajiwa kuagwa kesho Jumatatu katika viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi Upanga, baadaye miili hiyo itasafirishwa kwenda kuzikwa katika maeneo yaliyotengwa na familia zao.

Waombolezaji

Baadhi ya ndugu wa marehemu waliofika kwenye viwanja hivyo walisema kuwa walikuwa wakiwategemea sana ndugu zao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema mara baada ya kupata taarifa za vifo hivyo, walishtuka na kutoamini kilichotokea huku wakieleza kuwa walikuwa wanawasiliana nao mara kwa mara wakati wakiwa Darfur.
“Tuliwasiliana na baba (Koplo Mohamed Chukilizo wa kikosi cha 41KJ, Majimaji, Nachingwea), siku chache kabla ya kifo chake, aliniambia anarudi hivi karibuni na kunitaka niendelee vizuri na masomo,” alisema Amina mtoto wa marehemu Chukilizo.

Aliongeza, “Baada ya wiki mmoja tulipewa taarifa za kifo chake, jambo hili lilitustua sana na hatukuamini kabisa.”

Amina ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne, Shule ya Sekondari Nachingwea alisema mpaka sasa hajui hatima yake katika elimu kwa sababu alikuwa akimtegemea baba yake kwa kila kitu.

Binti huyo aliyekuwa ameongozana na mama yake, hawakuwa na ndugu yeyote wa familia ya baba yake waliomsindikiza.

Chukilizo atazikwa mkoani Kigoma mara baada ya kukamilika kwa taratibu za mazishi.

Naye Msemaji wa familia wa marehemu, Sajini Shaibu Othman kutoka Makao Makuu ya Jeshi Upanga (MMJ) jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika, Mohamed Sadiki alisema kuwa marehemu ameacha mjane na watoto watatu.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo, walishtuka na kutoamini kilichotokea.

“Tumeshtushwa sana na tukio hilo, hatukuamini kabisa kwa sababu tulikuwa tukimtegemea kwa kiasi kikubwa, na ameacha mama yake mzazi, mjane na watoto watatu,”alisema Sadiki.

Aliongeza, marehemu alikuwa anaishi Kigamboni, kwamba atazikwa nchini  Zanzibar kwa maelezo kuwa ndiko familia ilikopendekeza kumzika.

Naye mke wa marehemu, Oswald Chaula kutoka kikosi 42KJ Chabruma, Songea, Maria Chaula alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo walipatwa na mshangao na walikusanyika nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kupanga taratibu za mazishi.

“Nilipopata taarifa za msiba huu wa mume wangu nilihisi kuchanganyikiwa. Mume wangu tegemeo langu niliomba arudi salama ili tuweze kupanga maisha yetu, lakini Mungu amempenda zaidi,” alisema kwa uchungu Maria.

Hata hivyo, waombolezaji wengine walishindwa kuongeza chochote katika eneo hilo, huku wakionekana kulia wakati wote tangu walipofika kwenye eneo la uwanja huo hadi miili ya wapiganaji hao ilipowasili.
Hata hivyo, Kaimu Msemaji Mkuu wa JWT, Meja Joseph Masanja alisema kuwa, miili ya wapiganaji hao imehifadhiwa katika hospitali ya jeshi kwa ajili ya kusubiri utaratibu wa kuagwa ifikapo Jumatatu ili iweze kusafirishwa vijijini kwao.

“Ratiba iliyopo ni kupokea miili ya marehemu na kwenda kuihifadhi katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, na ifikapo Jumatatu majira ya saa 2:30 asubuhi itapelekwa kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi kwa ajili ya kuaga,”alisema Meja Masanja.

Dk Bilal aliongozana na mke wa Rais, Salma Kikwete,Balozi mdogo wa nchi ya Tanganyika kutoka nchini Zanzibar Balozi Seif Idd, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa nchi ya Tanganyika, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanganyika (IGP)Said Mwema.