Sunday, July 21, 2013

BENDERA YA NCHI YA ZANZIBAR ILIPO PANDISHWA U.N.NEW YORK 1963 MIAKA 50 BAADAYE CCM MUME FANYA NINI ZAIDI YA KUITIA UMASIKI NCHI YA ZANZIBAR



BADALA YA KULETA MAENDELEO KWA WANANCHI WEWE NI MATUSI,UBAGUZI,KEJELI,MIPASHO NA NYINYI MAJUHA MULO KAA NA KUSIMAMA KUMSIKILIZA SIJUWA MUTAZINDUKA LINI.NYUMBA MUNAZO ISHI MPAKA LEO 2013 HAMUNA MAJI WALA UMEME,CHOO NA CHOO CHA BAFUU NDIO HICHO HICHO KIMOJA, ISITOSHE CHOO CHENYEWE KIKO NJE YA NYUMBA,MLO MOJA KWA SIKU, MIHOGO YA KUCHEMSHA HAMNA HATA KIBUWA MUKISHA PEWA UPANDE WA KANGA NA PANGA NDIO MUNAONA MAISHA KUMBE MUMELIWA

Hii benderaa pili kutoka mkono wa kulia na ya nne kutoka mkono wa kushoto ndio bendera ya nchi ya Zanzibar baada ya kupata UHURU. Siku bendera ya Nchi ya Zanzibar ilipopandishwa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, mwezi Disemba 1963. Wazanzibari sasa wanataka kurudisha mamlaka kamili ya nchi yao ya Zanzibar baada ya miaka karibuni 50 ya nchi yao kutolewa katika muungano wa U.N. na kupelekwa katika  Muungano wa mkoloni mweusi Tanganyika na chama cha ccm chama cha majuha,choyo,waroho wa madaraka,wabaguzi,wasio juwa kufikiri,wasio juwa nini maendeleo isipokuwa matumbo yao kwa wake zao na familia zao,miroho na tamaa,wauwaji,mathalim,majambazi,wala haramu wasio ogopa siku ya kiyama,wakotayari kuuwa kwa matumbo yao.

LETE MAENDELEO SIO MLIPI MREFU, POROJO,MATUSI,CHUKI,UBAGUZI,FITINA,MIYAYUSHO,UWONGO,UKALI,KEJELI.HOSPITALI MPAKA LEO HAKUNA DAWA,VITANDA,MZEE KARUME KAJENGA VIWANDA NYINYI MIAKA 50 MUMESHINDWA HATA KUVIENDELEZA WACHILIAMBALI KUJENGA VYEPYAA,MPAKA LEO BADO KUNA WAZANZIBARI MLO MOJA UNAWASHINDA WAKATI NYINYI VIONGOZI NA WAKE ZENU NA WATOTO WENU MUNAMWANGA VYAKULA.
Wazanzibari wanatoa maoni yao kwa uhuru kamili. Wanafanya hivyo wakitambua kwamba fursa waliyonayo sasa huenda wasiipate tena.
Wanaelewa vyema umuhimu wa kuwa na msimamo mmoja ili waweze kuigomboa nchi yao kutoka katika tumbo la chatu mkoloni mweusi Tanganyika. La sivyo, wakichezacheza na wasipoungana kifikra basi fursa hiyo inaweza ikawaponyoka, wakajikuta wamekwenda kapaa. Katika hayo majadiliano kuhusu mustakabali wa nchi ya Zanzibar suala la Muungano feki ndo jambo kubwa linalozungumzwa nchini Zanzibar. Muungano feki unajadiliwa mijini, vijijini na kwenye vitongoji Unguja na Pemba.
Ukiwasikiliza wananchi wa nchi ya Zanzibar utawasikia wanataka irejee Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, ikiwa ni dola kamili iliyo huru kama ilivyokuwa awali pia Wazanzibari wanataka ujirani mwema na nchi ya Tanganyika,Kenya,Uganda pamoja na nchi nyingine za eneo hili. Tofauti ya mahusiano yaliyopo sasa na hayo wayatakayo ni kwamba wangependelea huo mfumo mpya wa mahusiano ya kufungamana uwe wa mikataba na si wa Katiba lakini baada ya kuwa na nchi yao ilio huru ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Msimamo huo ni sehemu ya ile iitwayo Ajenda ya Zanzibar niliyowahi kuizungumzia miezi kadhaa iliyopita. Ni ajenda inayopigiwa debe na wengi wa Wazanzibari wakiwa pamoja na viongozi wao kutoka vyama tofauti vya kisiasa na asasi isipokuwa CCM baadhi ya viongozi wasio shiba na uroho wao bado.
Wengi wao wanaamini kwamba kutokana na Hati za Muungano huu feki na mambo mengine yaliyoingizwa kuwa ni ya Muungano raisi aliyewekwa hapa nchini Zanzibar na giningi DODOMA SIO RAISI ALIYE CHANGULIWA NA WAZANZIBARI. Pia  baraza letu la kutunga sheria (Baraza la Wawakilishi) na Mahakama yetu. Mamlaka ya taasisi zote hizo tatu za Zanzibar, ambazo ni mihimili mikuu ya dola, yamepunguzwa katika kipindi cha miaka 47 ya Muungano feki.
Kilichotokea ni kwamba kwa muda wote huo unaokaribia nusu karne mamlaka au madaraka yote ya nchi ya  Zanzibar yaliyo muhimu yamehamishwa nchini Tanganyika kwa mkoloni mweusi. Ujanja ulitumika kulifanya Bunge la nchi ya Tanganyika liwe Bunge la Muungano feki na kuigeuza Katiba ya nchi ya  Tanganyika iwe Katiba ya Muungano feki. Ujanja vilevile ulitumika kuifanya Serikali ya Muungano feki iwe ndiyo Serikali ya nchi ya Tanganyika na ya Tanganyika iwe ya Muungano feki.ikawa nchi ya Tanganyika imeva koti na kujiita ya muungano feki. Shughuli za Jamhuri ya Muungano ya ((Tanzania)) na za Jamhuri ya Tanganyika zimekuwa zikiendeshwa na Serikali moja.
Kwa upande mwingine, Zanzibar na Serikali yake hazina jukumu kubwa au la maana katika utawala na uongozi wa Muungano feki. Ingawa kwa mujibu wa Sheria za Kimataifa na kwa mujibu wa Hati za Muungano, Zanzibar na Tanganyika ni washirika wenye hadhi sawa ndani ya Muungano feki, mambo yanavyokwenda ni kwamba Zanzibar imewekwa kando au maneno ya mtaa imepingwa bao.
Zanzibar imetoweka hata kutoka kwenye ramani ya dunia na haina jukumu lolote la maana katika shughuli za eneo letu la Afrika Mashariki au la Afrika au ulimwenguni kwa jumla. Wala Zanzibar haipati manufaa yoyote inayopata nchi yenye kushiriki katika uchumi wa dunia; isitoshe, hairuhusiwi kujihusisha na taasisi za kimataifa ni kusema nchi ya Zanzibar iko jela chini ya nchi ya Tanghanyika mkoloni mweusi.
Hii leo wanasiasa wa Tanganyika hawawezi tena kuyapuuza manung’uniko na matakwa ya Wazanzibari kwa sababu wamekwishatanabahi kwamba Muungano feki kwa namna ulivyo sasa, uko kwenye njia panda na wakati umefika wa kufanya uamuzi muhimu kuhusu mustakabali wake.
Kwa sasa hakuna anayeweza kutabiri nini yatakuwa matokeo ya nchi ya Zanzibar je itakuwa huru au itaendelea kuwa chini ya mkoloni mweusi Tanganyika.
Mnamo miaka ya 1990 palitolewa pendekezo la kutaka pawepo na mfumo wa serikali tatu, yaani Serikali ya Tanganyika, ya Zanzibar na ya Muungano. Waliopendekeza hivyo waliamini kwamba mfumo huo wa serikali tatu ndio ulio bora na utaokubaliwa na washirika wote wawili, yaani Tanganyika na Zanzibar.
Kwa hakika, baadhi ya wanasiasa mashuhuri wa Tanganyika nao walifanya jaribio la kuifanya nchi yao iwe na serikali yake ndani ya Muungano. Jaribio hilo halikufika mbali kwani Julius Nyerere alitumia nguvu zake za turufu na kulizima suala hilo.
Pendekezo hilo liliibuka tena lilipotolewa kwa mara nyingine na Tume ya Muungano feko iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Robert Kisanga. Rais wa Muungano feki wa wakati huo, Benjamin Mkapa aliye uwaa wapemba wengi siku za changuzi. naye alilipinga. Hatujui ikiwa huo ndio mwisho wa pendekezo hilo au iwapo Serikali ya Muungano feki italikubali kuwa njia murua ya kuunusuru Muungano feki usiporomoke.
Iwapo Serikali ya Muungano feki hatimaye italikubali pendekezo hilo hatujui kama Wazanzibari nao wataliridhia kwa vile pendekezo hilo ukiliangalia kwa undani haliipi nchi yao ya Zanzibar uhuru wake kamili bali linauwekea mipaka. Muungano  huo wa serikali tatu utakuwa Muungano utaojengwa juu ya misingi ya mkataba na sio Katiba.
Ndio maana siku hizi huko Zanzibar mazungumzo kuhusu Muungano ni ya kutaka serikali tatu sio mbili labda hawa wafidhina ndio wanataka mbili. Au kama hawataki nchi ya Tanganyika basi kila moja abaki na nchi yake. Wazanzibari wengi wanahisi kwamba ule mfumo wa serikali mbili za Muungano umekwishapitwa na wakati. Wanapotoa hoja zao wanasema kwamba mfumo huo labda ungekubalika katika miongo iliyopita lakini si mnamo mwaka 2015.
Hata wale wenye kuunga mkono mfumo wa serikali tatu sasa wanasema kwamba ile serikali ya tatu, yaani ya Muungano, isiwe na mamlaka mengi kwani wanachotaka ni Zanzibar kuwa na uhuru zaidi ndani ya mfumo mpya wa Muungano.
Hao Wazanzibari wenye kutaka Muungano utaoundwa juu ya misingi ya Mkataba na sio Katiba wanahoji kwamba mfumo wa Muungano wa Mkataba ndio ufaao kwa mataifa yaliyo huru. Wanaendelea kuhoji kwamba hakuna haja ya kuwepo Serikali ya ((Tanzania ambayo ni Tanganyika imeva joho)). Badala yake, wanasema, pawepo Tume Maalumu ya Muungano itayokuwa na nguvu hafifu au mamlaka machache na itayosimamia vifungu vya Mkataba wa Muungano.
Mfano wanaoutaja mara kwa mara ni ule wa Tume ya Muungano wa Ulaya. Wanataka Muungano wao uwe mithili ya ule wa Ulaya ambao umeundwa kwa mikataba ya kimataifa kati ya nchi 27 zilizo huru. Majaribio ya kutaka pawepo Katiba moja ya Muungano huo yalikataliwa pale palipofanywa kura za maoni katika baadhi ya nchi wanachama. Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa Muungano huo kila nchi ina kura ya turufu, na inaweza kujivuta na kujitoa kutoka kwenye Muungano kwa vile maamuzi yote makuu hukatwa kwa nchi kukubaliana.
Wazanzibari wenye kuupigania mfumo huo wanasema kwamba mfumo huo si kwamba unazifaa nchi ya Zanzibar na Tanganyika tu bali pia ni mujarab kwa bara zima la Afrika. Bara hilo nalo linahitaji kuwa na chombo kitachoziunganisha nchi zake zote kwa maslahi ya nchi wanachama.

No comments:

Post a Comment