Friday, July 12, 2013

CCM SIKU ZOTE WAFANYE WAO VYAMA VINGINE VIKIFANYA VINAMBIWA WAVUNJIFU WA AMANI

ccm
HAWA NDIO JANJAWILI WA CCM 
Wakati Rais Jakaya Kikwete wa nchi ya Tanganyika akiponda mpango wa Chadema kuanzisha kambi za mafunzo kwa ajili ya mafunzo ya ulinzi, imeelezwa kuwa Chama Cha Mapinduzi nacho kimekuwa kikiendesha mafunzo ya ukakamavu kwa vijana wake kwa siri kwa kipindi kikubwa sana.
Hata hivyo alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu kuendesha mafunzo hayo, Naibu Katibu wa CCM, Mwigulu Nchemba alisita kuzungumza na kumtaka mwandishi aangalie ukurasa wake wa Facebook ambako amefafanua.
Katika ukurasa huo, Mwigulu amekosoa Rasimu ya Katiba Mpya akisema muundo wake utaleta utata wa usalama. Mwigulu ametaja ibara ya 223(1) inayozungumzia uanzishwaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanganyika (Tanzania) Zanzibar (JWTZ), litakalokuwa na mamlaka ya kusimamia ulinzi na usalama, “Ibara ya 232(1) inasema bila kuathiri masharti ya Katiba hii, nchi Washarika wa Muungano wanaweza kuanzisha vikosi vya ulinzi na usalama …. katika maeneo yao.
Ametaja pia ibara ya 227(1) inayoeleza uundwaji wa Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano na ibara ya 232 inayozungumzia vikosi vya washirika kuhusika na ulinzi wa watu wao na ibara ya 233 (1) inayozungumzia Idara ya Usalama wa Taifa wa Jamhuri ya Muungano.
“Suala la usalama ni nyeti muundo huu utategemea tu mazingira na busara ya viongozi. Vinginevyo ni rahisi vikosi vya Muungano kupigana na vya nchi washirika kufuatia maelekezo ya viongozi wao siku wakitokea sio wataifa,”
Akifunga kongamano la amani lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanganyika (TCD) Dar es Salaam juzi, Rais Jakaya Kikwete wa nchi ya Tanganyika ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM pia alikosoa kitendo cha Chadema kususia mkutano. “Sasa hawa kweli wanapenda amani yetu wakati hawapendi tuzungumze,wanataka watu wauane,wapigane,” alisema.
Mbali na Rais Kikwete,Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, SSP Advera Senso limekionya Chadema kuhusu mpango huo. “Kitendo cha chama chochote cha siasa ikiwamo Chadema kuanzisha kikundi cha kujihami ni kinyume cha sheria za nchi na endapo watafanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Jeshi la Polisi nchini limeanza uchunguzi na litachukua hatua kulingana na ushahidi utakaopatikana.
“Jeshi la Polisi litamshughulikia mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha sheria bila kujali wadhifa wake,” alisema Senso katika taarifa yake.
Hata hivyo,mtindo wa kuanzisha vikundi vya ulinzi kwa vyama vya siasa unaonekana kuzoeleka huku vyama vikubwa vikiwa na makundi kama vile Red Brigade ya Chadema,Green Guard ya CCM na Blue Guard ya CUF.
Lakini hapa inaonyesha kuwa CCM wanataka kufanya wao tu wengine wakifanya basi inakuwa tabu pia sisi Wazanzibari tunajuwa sana kuwa hawa ndio wanao tumiwa siku za chaguzi kufanya fujo na kupiga watu na kuiba na kuuwa pia washauwa sana tu na ndio maana sasa CCM ina hofu kubwa maana inajuwa kama vyama vyote vitakuwa na walinzi wake basi sio rahisi kufanya ushenzi wao walio zowea kufanya siku za chaguzi.

No comments:

Post a Comment