Monday, July 8, 2013

CCM YA NCHINI ZANZIBAR YASEMA CHAMA KWANZA NCHI BAADAYE DUUUUUUUUH


Mawaziri na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar toka CCM Zanzibar wametakiwa kuanza kujibu mapigo kwa nguvu ya hoja dhidi ya madai na upotoshaji unaofanywa na chama cha upinzani cha CUF kama wanavyo dai CCM.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka BICHWA LA SAMAKI, wakati akifungua tawi jipya la Mambobado katika kijiji cha Kijini Mkoa wa Kusini Unguja mbele ya Mwakilishi wa Makunduchi CCM, Haroun Ali Suleiman.
Shaka BICHWA LA SAMAKI alisema kukaa kimya kwa mawaziri na wawakilishi toka CCM huku upande wa CUF ukiishambulia na kuisulubu bila huruma Serikali ya CCM!!!!!!! si jambo linalowafurahisha wanachama wa chama hicho.
“Wawakilishi na mawaziri wetu ni mahiri na hodari, kukaa kwao kimya bila ya kujibu mapigo huku upande wa CUF ukitupa makombora na kuisulubu serikali, ukimya huo umeanza kutia shaka na kujenga hofu,”alisema shaka BICHWA LA SAMAKI.
Alisema UVCCM katu hairidhishwi na ukimya unaoendelea kujitokeza katika Baraza hilo na hukera hata pale mafaniko ya Serikali yaliofikiwa yanapobezwa kwa makusudi na upinzani. Hata hivyo kiongozi huyo alisema pamoja na kuwapo kwa serikali yenye mfumo wa umoja wa kitaifa Zanzibar bado kila chama kina misimamo yake, sera na itikadi yake.
“Haikuundwa SUK Zanzibar na kuviunganisha vyama vya sera za CCM na CUF, kila chama na mipango yake, mfumo unaojitegemea kiuendeshaji hivyo propaganda ya nchi kwanza na chama baadaye, haipaswi kufuatwa na wawakilishi wa CCM,” alifafanua.
Alisema siasa ni mchezo wa mapiku hivyo kuendelea kunywamaza kwa wawakilishi hao na mawaziri bila ya kujibu mapigo ya neno kwa neno mahasimu wao huutumia vibaya mwanya huo na kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

No comments:

Post a Comment