Tuesday, July 30, 2013

MASHEIKH WA UAMSHO HAWATA TOKA JELA KWA KUOMBEWA NA MTU BALI WATATOKA KWA UWEZO WA M/MUNGU

Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO wakiwa ndani ya gazi ya Polisi wakirejeshwa rumande baada ya kusomwa kwa kesi yao na kuahirishwa.
Sisi sote tunajuwa kuwa mahakama ya nchi yetu ya Zanzibar ni ya madhalim,matapeli,wezi,wasiojuwa haki wala batili,ni midudu tu imo ndani ya mahakama kutafuta tumbo lao lishimbe. ndio hapa nasema, pamoja na kuwepo sheria inayo waweka rumande Masheikh hao na kuzuilia dhamana zao, kuna haja ya kutizama upande wa pili: “Truth and Justice.” Ukweli na Haki.

Wapo watu waliwahi kukaa ndani miezi kadhaa au miaka kwa mashitaka ya kisiasa kule hapa nchini Zanzibar. Inasemekana kuwa watu waliokuwa karibu na Rais wakati ule Dkt. ‘Komandoo wa Udongo’ Salmin  Amur walimwendea na kumwomba awaachie watu wale. “Wacha wakae, kwani ni mapapai kwamba yataoza”, inasemekana hayo ndiyo yalikuwa majibu ya ‘Komandoo wa Udongo’ Mazungumzo yakaisha.

Watu wale wakati ule waliodaiwa sio mapapai na wakiona kuwa walikuwa wakidhulumiwa, kwamba sheria ilitumika vibaya dhidi yao, hivi sasa wapo madarakani katika nafasi mbalimbali. Swali ni je, kuna juhudi yoyote wanayofanya kuhakikisha kuwa haki kwa wote, ukweIi na uadilifu unakuwepo hilo la kwanza lapili wale wale walio kwenda kuwaombea wale wachiwe je wameshawaombea hawa masheikh pia wachiwe au walijuwa kuwaombea wale tu kwa kuwa ni wana wa siasa hawa wa dini wachwe waozee..???

FREE ZANZIBAR PEOPLE INAWATAKIA KILA LA KHERI MASHEIKH WETU WOTE WALIOKUWEPO JELA NA WALIOKUWEPO VIZUIZINI M/MUNGU AWAPE NYOYO ZA SUBIRA NA AWALIPE PEPO KWA KIJI ADHABU HICHI CHA DUNIA ABACHO WENGI WA VIONGOZI WANAFIKIRI NDIO MAFANIKIO YAO KWA NYINYI KUWEPO JELA WAO WAKATAWALA KWA RAHA HUKU NJE KUMBE NDIO KWANZA WANAJIPALILIA MKAA KATIKA DUNIA BILA KUSAHAU AKHERA NDIO KABISA.

No comments:

Post a Comment