Friday, July 19, 2013

NCHINI TANGANYIKA MAJOZI,SIMANZI,MASIKITIKO,VILIO VYA KWIKWI VYATAWALA NCHINI TANGANYIKA



JESHI LA WATANGANYIKA NA TISHA TOTO ZAO UWANJA WA TAIFA

DARFUR SUDAN WATU HAWATISHI TOTO WANAFANYA KWELI TU
Songea. Vilio na simanzi vimetawala katika baadhi ya familia za  wanajeshi la Wananchi wa Tanganyika (JWT) ambao waliuwawa katika eneo la Darfur, Sudan ambako wanashiriki katika ulinzi wa amani.

Mamia ya waombolezaji walionekana katika makazi ya familia za marehemu; Songea mkoani Ruvuma na Nachigwea mkoani Lindi ambako ziko kambi ambazo baadhi ya wanajeshi hao walikuwa wakifanya kazi.

Imefahamika kuwa wanajeshi waliouwawa Jumamosi iliyopita wanatoka katika vikosi vya, 42KJ Chabruma, Songea,  44KJ Mbeya, 36KJ Msangani, 92KJ Ngerengere, 94KJ cha Mwenge, Dar es Salaam, 41KJ Nachingwea na Makao Makuu ya JWT- Upanga, Dar es Salaam nchini Tanganyika.

Jana muandishi wetu wa siri wa FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI Alibaini kuwapo kwa maombolezo katika baadhi ya familia za wanajeshi hao walio uliwa huko Darfur baada ya kupokea taarifa za vifo vyao kutoka JWT.
Katika Kambi ya Chabruma, Songea mkoani Ruvuma kulikuwa na umati wa waombolezaji nyumbani kwa mmoja wa wapiganaji hao, Koplo Oswald Chaula ambaye alikuwa katika Kikosi cha Mizinga Chabruma na ndugu zake walikiri kupokea taarifa za msiba huo.
Hali kama hiyo ilikuwa nyumbani kwa Koplo Mohamed Chukilizo katika Kambi ya Majimaji, Nachingwea ambako baadhi ya ndugu na jamaa zake wakiwamo mkewe na baba mkwe wake walikutana jana jioni kujadiliana kuhusu msiba.
Mwandishi wetu wa siri mwengine pia alishuhudia waombolezaji wakiwa wamekusanyika eneo la Mjimwema, Songea Mkoani Ruvuma ambako ni nyumbani kwa Komandoo Rodney Ndunguru aliyetoka kikosi cha 92KJ Ngerengere, Morogoro, baada ya kupokea taarifa za msiba huo. 
Vilio, majunzi, Simanzi, huzuni.
Katika kambi ya Chabruma, mke wa marehemu Koplo Oswald aliyejitambulisha kwa jina la Maria alikuwa akilia kwa simanzi baada ya kupata taarifa kuwa miongoni mwa waliofariki ni baba watoto wake huku akilia alisema. 
“Ninamuomba Mungu ampumzishe mume wangu...nimekosa nini jamani, mume wangu kaondoka...alikuwa tegemeo langu. Sijui kama wanangu watasoma, dunia imenigeuka... imekuwa ghafla mno, Chau kaondoka bado nampenda,” alisikika akisema Maria huku akiwa amewakumbatia wanawe. Ndugu na jamaa walikuwa wakimfariji.
Maria anatarajiwa kuondoka Songea leo kwenda katika kijiji cha Kilolo, mkoani Iringa kusubiri mwili wa mume wake ambaye atazikwa huko. Chaula ameacha watoto wanne, mmoja akiwa na umri wa miezi minne.
Katika eneo la Mjimwema mama wa marehemu Ndunguru, Lucy Ndunguru aliyekuwa akilia muda wote, alisema: “Mwanangu Rodney kaniacha...nilikuwa namtegemea, alikuwa ananitunza na mimi ni mjane sasa kaniacha...ee Mungu nimekosa nini mimi....”
Sauti yake ya mitetemo na kwikwi za simanzi viliwafanya baadhi ya waombolezaji nao kujikuta wakibubujikwa na machozi, huku kukiwa na taarifa kwamba wanapanga marehemu kama atazikwa Kijiji cha Myangayanga alikozikwa baba yake 
Mwandishi wetu wa siri  iliyokuwapo karibu na nyumbani kwa marehemu na kushuhudia vilio na simanzi na wengi wamekuwa wakizidisha vilio hasa kutokana na mke wake kuwa na kichanga kwani alikwenda kujifungua nchini  Zanzibar.
Kwenye Kambi ya Majimaji, Nachingwea ilifahamika kuwa Koplo Chukilizo ambaye alikwenda Darfur kama fundi wa magari ya deraya, ni mwenyeji wa Kigoma na kwamba huenda akasafirishwa kwenda huko.
Baba mkwe ambaye marehemu alizaa na mwanawe alisema: “Taarifa nimezipata jioni hii, tulikuwa na wasiwasi lakini tukathibitishiwa na ndiyo tuko hapa tunasubiri taarifa zaidi...hata hivyo tunataka kwenda Dar es Salaam ili kuupokea mwili.”
Katika kambi ya Msangani mkoani Pwani, habari zinasema jana jioni matangazo yalibandikwa kueleza kifo cha Private Fortunatus Msofe ambaye alitajwa kuwa mwanajeshi wa kikosi cha ardhini aliyehamia Kibaha, Pwani akitokea Moshi mkoani Kilimanjaro.
“Huyu alikuwa akiishi katika mahanga ya askari, lakini familia yake bado iko Visiga, Pwani sasa imeelezwa kuwa msiba uko kwa mke wake Visiga,” kilisema chanzo chetu katika kambi hiyo.
Habari zilizopatikana baadaye zilidai kuwa mwanajeshi walielezwa kuwa kwa anayetaka kuifariji familia ya marehemu aende Visiga kwa kuwa hakuna utaratibu wa kuweka msiba kwenye mahanga.
Marehemu wachunguzwa
Wakati hayo yakiendelea miili hiyo jana ilisafirishwa kutoka Darfur kwenda Mji Mkuu wa Sudan, Khartoum ambako madaktari wa nchi ya Tanganyika na wale wa Umoja wa Mataifa wataifanyia uchunguzi utakaochukua siku mbili. 
Msemaji wa Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa na Afrika (UNAMID), Chris Cycmanick aliwambia wandishi wa habari jana kuwa miili ya askari hao ilipelekwa jana mjini Khartoum, Sudan kwa shughuli hiyo.
Cycmanick alisema kuwa kazi hiyo ya uchunguzi inatazamiwa kuchukua siku mbili na baada ya hapo ndio miili itarejeshwa nchini Tanganyika.
“Haitakuwa kazi ya kuchukua siku moja. Pengine nahisi itachukua siku mbili hivi. Miili hii inaweza kuletwa Tanganyika. Ila tuwasiliane zaidi niweza kukutajia siku ya kuja,” alisema Cycmanick.
Hata hivyo, Kanali Mgawe alisema miili ya marehemu hao imepelekwa Khartoum kwa ajili ya maandalizi ya kusafirishwa kesho.
Alisema maiti watakapowasili itakapofika watahifadhiwa Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam na kwamba wamepanga Ijumaa kwa ajili ya kuwaaga kwenye Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi, Upanga. 
Alisema baada ya hapo kila moja atasafirishwa kwenda maeneo yaliyopangwa na familia zao kwa ajili ya maziko.
Jumamosi iliyopita, wanajeshi saba wa nchi ya Tanganyika waliuliwa na wengine 19 walijeruhiwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa walikuwa wakifuatilia magari yao yaliyokuwa yametekwa na kundi mojawapo la wapiganaji wa Darfur huko Sudan.
Mji wa Nyala ambao ndio mkubwa zaidi katika eneo la Darfur umekumbwa na tatizo la ukosefu wa usalama katika siku za hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment