Sunday, July 21, 2013

SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YATAKA KUMRUDISHA SULTANI NA KUWAUZA VIJANA WA KIZANZIBARI KAMA WATUMWA WA WARAABU KATIKA NCHI ZA FALME ZA KIARABU

                                                                                                                                                                                                      
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanza kutekeleza mpango wa vijana kwenda kuwauza nje ya nchi katika nchi za Falme za Kiarabu wakiwa kama watumwa baada ya serekali hii ya mapinduzi kushindwa kabisa kuleta maendeleo kwa wananchi na haswa vijana wamekuja na mpango mpya wanao dai ati ili kukabiliana na wimbi la ukosefu wa ajira Nchini Zanzibar.

Sasa ikiwa ndio hivyo wakulaumiwa ni nani..? pia sisi rai tumewachanguwa nyinyi matulete maendeleo sasa haya ndio maendeleo kutuu uzaa katika nchi za Falme za Kiarabu kwenda kuosha sahani na masufuria, si tunasema kila siku tume PINDUWA ILI TUSIWE WATUMWA NA TUJITEGEME mbona sasa tunapelekwa  nchi za Falme za Kiarabu twende tu kapige diki huku tumeinama..? kama mumeshindwa kutulete maendele hapa hapa kwetu basi achiliyeni madara mkalime konde sio mutu uze nchi za kiarabu kisingizio ati ajira.

Mzee Karume mwana mapinduzi hakupeleka vijana kwenda kupiga deki,kuosha masufuria,miko na pawa na sahani katika nchi za kiarabu bali alijenga viwanda vidogo vidogo,kuwapeleka vijana masomoni sio kwenda kuosha mavi ya watoto wa kiarabu, kisha ikifika wakati wa uchanguzi muarabu weee muarabu weee wanafiki wakubwa nyie sasa mbona munataka kutuza huko huko kwa waraabu..?
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji wa Wananchi, Kiuchumi na Ushirika, Haoroun Ali Suleiman, alisema hayo wakati akiwasilisha makadirio na matumizi ya bajeti yake ambapo kazi ya kuorodhesha majina ya vijana iliyoanza kufanyika mwaka jana.
Haroun alisema kati ya vijana 464 vijana 350 wameshanufaika na ajira katika nchi za Oman ambapo vijana 148, Qatar imewechukua vijana nane, Dubai 54 na Djibout watano hadi kufikia Machi, mwaka huu.
Alisema kwamba vijana hao wamekuwa wakifanyakazi katika nchi hizo kwenye viwanda na majumbani na hatua hiyo alisema itasaidia kupunguza ukosefu wa ajira nchini.
Alisema Wizara yake imekusanya takwimu toka soko la ajira la sekta binafsi na kubaini katika mwaka uliopita vijana 1529 wameajiriwa katika sekta binafsi za utalii, mashirika ya ndege, kampuni za mafuta, afya na kampuni za ulinzi.
Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Fedha na Uchumi sekta ya Viwanda Zanzibar, pato la Taifa limeanguka toka asilimia 12.0 hadi asilimia 11.7, mwaka jana.
Hata hivyo alisema Wizara yake imeanza mchakato wa kurasimisha shughuli za sekta isiyo rasmi kwa kuanzia na sekta ya usafiri wa umma kwa malengo ya kuongeza ajira kupitia nyanja ya usafiri na usafirishaji.
Alisema chini ya mpango huo madereva wa daladala na utingo watalazimika kusajiliwa na kupewa mikataba ya kazi na waajiri wao ili waweze kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii na kupata fursa anazostahiki kupata mfanyakazi mbali na msharaha na huduma za matibabu.
Haroun alisema mkutano huo ulijadili namna ya kurasimisha sekta hiyo ili iweze kuchangia katika kukuza ajira za staha na uchumi wa Taifa na kwamba wajumbe wa mkutano huo walikubaliana kwa kuanzia na mikataba ya wafanyakazi katika sekta ya usafirishaji pamoja na kujiunga na mifuko wa hifadhi ya jamii.
Madereva na utingo wa daladala wamekuwa wakifanya kazi kwa muda mwingi bila ya kuwa na mikataba ya kazi na waajiri wao hali inayoonyesha kupoteza kwa nguvu zao na kukosa hifadhi ya malipo yao ikiwa watapata ajali kazini na kukosa mikataba ya kisheria.

No comments:

Post a Comment