Monday, July 1, 2013

WATU WA KITOPE WAKIAMBIA CHAMA CHA CCM BYE BYE BYE BYE BYE bye bye bye bbbbbyyyyyeeeee

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha kadi ya CCM ikiwa ni miongoni mwa kadi zilizorejeshwa na baadhi ya vijana wa Mgambo jimbo la Kitope walioamua kujiunga na CUF.
Katibu Mkuu wa CUF na Makamu wa Raisi wa nchi ya Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha kadi ya CCM ikiwa ni miongoni mwa kadi zilizorejeshwa na baadhi ya vijana wa Mgambo jimbo la Kitope walioamua kutoka katika chama cha CCM na kujiunga na chama cha CUF.
Upenja, jimbo la Kitope.
Vyombo vya dola vimeshauriwa kutoa fursa sawa kwa vyama vya siasa katika kuendesha shughuli zao za kisiasa, ilkiwa ni hatua moja ya kutekeleza kwa vitendo dhana ya demokrasia nchini Zanzibar.
 
Ushauri huo umetowa na Katibu Mkuu wa CUF na Makamo wa Raisi wa nchi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika viwanja vya Upenja jimbo la Kitope.
Kada wa CCM ajulikanae kwa jina la Mzee Mabati wa Mgambo, akivua uanachama wa chama hicho huku akiashiria kwa t.shirt ya CCM kuwa kakivuwa na kujiunga na CUF katika mkutano wa hadhara uliofanyika Upenja jimbo la Kitope.

Amesema kila chama cha siasa kilichopata usajili, kina haki ya kuendesha shughuli zake za kisiasa popote Tanganyika (Tanzania), Zanzibar bila ya kujali eneo hilo linadhibitiwa na chama gani.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo kufuatia kile alichokiita tabia ya baadhi ya vyama vya siasa kushirikiana na vyombo vya dola kuvinyima haki ya kufanya mikutano vyama vyengine katika baadhi ya maeneo ya nchi ya Zanzibar.

Wazanzibari walio toka katika usingizi waliopewa na chama cha CCM wakirundisha kadi za chama hicho cha CCM ambacho kimewatia katika umasikini,ufukara,kuto kutambulika kitaifa na kimataifa,kimewafanya wazeeke kabla ya umri wao kimewanyima uhuru wakusafiri na kuwadanganyka kuwa maendeleo yanakuja wala hayafiki N.K.wote hawa wameungana na chama cha CUF kuendele kupigania nchi yao itoke katika tumbo la joka kubwa aliyo wameza nalo ni Tanganyika.
 
“Samahani sana rafiki yangu Balozi Seif, leo nimekuja katika jimbo lako na wala sikuvamia, lakini hii ndio demokrasia inayotakiwa, na wewe nakukaribisha Mtambwe kufanya mikutano, na jimbo langu la uchaguzi ni Mtoni Unguja, njoo ufanye mikutano tafadhali”, alisema Maalim Seif.

Alitanabahisha kuwa wakati wa kuvizuia baadhi ya vyama kufanya shughuli zake za kisiasa umepitwa na wakati, na kwamba chama chake hakizuiliki tena kufanya mikutano ya kisiasa pahala popote ndani ya Tanganyika (Tanzania.) Zanzibar

Katika mkutano huo jumla ya wanachama 435 wengi wao wakitokea shehia ya Mgambo jimbo la Kitope, walijiunga na CUF na kukabidhiwa kadi za chama hicho huku baadhi yao wakirejesha kadi za chama cha CCM na t.shirt za chama hicho cha CCM.

No comments:

Post a Comment