Friday, July 5, 2013

WAZANZIBARI MILLIONI MOJA NA NUSU TUNASHINDWA KUISHINDIKIZA SEREKALI HII KUWACHIYA WAKOMBOZI WA ZANZIBAR


Amir Farid MKOMBOZI WA WAZANZIBARI.3 ZIMEBAKI RAMADHANI WAO WAKO JELA

Sheikh MSELLEM MKOMBOZI WA WAZANZIBARI. 3 ZIMEBAKI RAMADHANI WAO WAKO JELA

Sheikh Mussa MKUMBOZI WA WAZANZIBARI. 3 ZIMEBAKI RAMADHANI WAO WAKO JELA

Sheikh Azan MKOMBIZI WA WAZANZIBARI. 3 ZIMEBAKI RAMADHANI WAO WAKO JELA

Hawa ni masheikh,wazazi,viongozi,wakombozi,ambao wamejitolea kwa hali na mali kuikombowa nchi yetu ya Zanzibar iliyo ndani ya tumbo la CHATU Tanganyika.wametuelimisha na kutufundisha mambo mbali mbali ambayo wengi wetu tulikuwa hata hatujuwi tuta anzia wapi.wameleta umoja wa wazanzibari baada ya nusu karne ya kubaguwana na kuchukiana kulikoletwa na Watanganyika ili wazidi kututawala na kuimeza nchi yetu ya Zanzibar.

kwa bahati mbaya viongozi hawa wamefahamika vibaya na waroho wa madaraka,viongozi wanaopenda kutenda mathambi,viongozi walio weka dunia na raha za dunia mbele zaidi kuliko akhera,wanajiona ni viongozi kumbe ni watumwa,vitimbakwiri,vibaraka,wasaliti,wajinga wa kufikiri,waoga wa mabadiliko,mijizi ya mali za rai wanyonge,wabaguzi,wanafiki,viongozi wanao jali MATUMBO YAO TU NA YAWAFALME WAO TANGANYIKA.

Je wewe ukiwa kama Mzanzibari ushawahi kujiuliza ni nini umefanya katika uhai wako kuikombowa nchi yako ya Zanzibar..?
je wewe ukiwa kama Mzanzibari umefanya nini ili hawa Mashekh wetu viongozi wetu walio tumpwa jela bila ya kosa lolote wanatolewa huko jela na kuja nyumbani kwenye familia zao.
je Mzanzibri ushawahi kujiuliza ingelikuwa wewe uko je sisi tuko nje tumenyamaza kimya ungelifikiria vipi wakati ulipokuwa nje tulikuambia tuko pamoja na wewe leo upo jela sisi tumebana kimya..? wao wametetea nchi yetu ya Zanzibar kwa faida yetu sote leo wamefungwa kwa kutetea nchi yetu je sisi tumeshindwa kuwatete wao huko jela waliko tupwa na tunajuwa kuwa hakuna haki katika mahakama zetu za wajaza matumbo yao.
je ingelikuwa wawe ndio uko jela na ramadhani inakuja ungelifikiria vipi..? nchi yetu ya Zanzibar ina watu zaidi ya millioni moja na nusu sasa kweli tunashindwa kuishindikiza serekali kuwachia MSHEIKH,WAKOMBOZI WA ZANZIBAR.?? 
KATIBA YA ZANZIBAR INASEMA NCHI YA ZANZIBAR ITAONGOZWA NA WANANCHI WENYEWE NINI TUNASHINDWA KUISHINIKIZA SEREKALI TULIO ICHANGUWE WENYEWE KUFANYA TUNAVYOTAKA SISI NA KAMA HAIFANYI BASI SIO SEREKALI YA KUKA MADARAKANI TUTABURUZWA MPAKA LINI...?????

No comments:

Post a Comment