Saturday, August 31, 2013

MARA CHINA MARA UHOLANZI FAIDA GANI WANAYO IPATA RAI WA ZANZIBAR..???

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein, na Ujumbe wake wakiteremka  mlima wakati walipotembelea  Makumbusho ya Kihistoria ya Dr.Sun Yat-sen’s  yaliyopo juu ya Mlima  Nje ya Mji wa Nanjing,katika Jimbo la Jiangsu nchini China,atii wakiwa katika ziara ya Kiserikali yagujuuuu sema kweli umekwenda china kutia raundi tu serekali gani..?

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mwanamwema Shein, wakisalimiana Waongoza Wahusika wa FAya Dr.Sun Yat-sen’walipofika na ujumbe wake kupata historia ya makumbusho hayo huko Nje ya Mji wa Nanjing,katika Jimbi la Jiangsu nchini China.
IMG_2496
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mitambo ya usambazji wa Gesi inayotumika katika nchi za ulaya,(GATE TERMINAL) Dick Meurs,alipokuwa akiwafuta ujinga kwa Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,ukioongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ali Mohamed Shein,katika ziara nchini Uholanzi.
IMG_2524
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,(katikati)na ujumbe wake wakitolewa ujinga  kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mitambo ya usambazji wa Gesi inayotumika katika nchi za ulaya,(GATE TERMINAL) Dick Meurs,walipofika katika Ofisi za Kituo hicho huko katika Bandari ya Rotterdam,nchini Uholanzi.
IMG_2542
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,(katikati)na Mawaziri pamoja na Balozi Dr.Diadorus B. Kamala wa nchi ya Tanganyika,Mzanzibari jiulizi huyu Balozi wa nchi ya Tanganyika anafanya nini..? na haya ni mafuta ya Wazanzibari yanayojadiliwa hapa(wa pili kulia)wakizungumza na Makamo wa Raisi pia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Rotterdam, Rene Van Der Plas,walipokuwa katika Boti walipoitembelea Bandari ya Rotterdam Nchni Uholanzi.

Balozi wa nchi ya Tanganyika nchini Belgium na Holland Diodorus Kamala akifungua mkutano uliojumuisha Watanganyika wanaoishi nchini Holland kuzungumza na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein hapo  katika hotel ya Hilton iliyopo jijini Den Haag. 

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ali Mohamed Shein akizungumza na Watanganyika wanaoishi nchini Holland Shein yupo huko nchini Holland kwa ziara atii ya kikazi wadanganyeni hao hao CCM.

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,akisalimiana na  Mkurugenzi wa Kituo cha habari kwa wafugaji wa Ngo’mbe wa maziwa Reimond Van Gent,alipofika kuangalia familia ya ufugaji wa Ngo’mbe wa maziwa na utengenezaaji wa Jibini (Cheese) akiwa huko nchini Uholanzi .

Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,akibadilishana hati ya makubaliano baada ya kutia saini na  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mafuta ya   Shell ya uholanzi na Serikali za Afrika Mashariki Axel Knospe,(kushoto)makubaliano ya ushiriano katika sekta ya gesi na mafuta katika ukumbi wa ofisi ya kampuni hiyo Mjini Uholanzi alipokuwa katika ziara ya Kiserikali,ujumbe ulioongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi AliMohamed Shein je Wazanzibari mushambiwa...??

Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,baada ya kumaliza kutia saini na  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mafuta ya   Shell ya uholanzi na Serikali za Afrika Mashariki Axel Knospe,(kushoto)makubaliano ya ushiriano katika sekta ya gesi na mafuta katika ukumbi wa ofisi ya kampuni hiyo Mjini Uholanzi alipokuwa katika ziara ya Kiserikali,ujumbe ulioongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi  Ali Mohamed Shein.

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,akifutwa ujinga kutoka kwa Frank Captein,wakati alipotembelea katika eneo maalum lililohifdhiwa Jibini (cheese) iliyokuwa imehifadhiwa tayari kwa mauzo haya Wazanzibari Shein akirudi tu atawafundisha na nyinyi muanze kutengeza cheese tartibuni tu asije akawatia uchizi badala ya kutengeza cheese.

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Frank Captein,wakati alipotembelea ndama wadogo jinsi wanavyolelewa katika famili ya BW.Captein,huko Nchini Uholanzi
IMG_2640
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na Mfalme wa Uholanzi Willem Alexander,alipomtembelea katika makazi yake  huko nchini Uholanzi.
IMG_2649
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi

wawakilishi wa Makampuni wakati alipowasilim katika Chakula cha jioni kilichoandaliwa na

 Famili ya Mfalme pamoja na makampuni nchini Uholanzi.
Ushirikiano katika kuendeleza sekta ya mafuta na gesi.
Makubaliano hayo yametiwa saini juzi tarehe 28 Agosti, 2013 mjini The Hague ambapo Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Ramadhani Abdalla Shaaban alitia saini makubaliano hayo kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwakilishi wa Kampuni Shell Tanganyika Axel Knospe alitia saini kwa niaba ya  Kampuni hiyo.
Makubaliano hayo yamefikiwa mjini The Hague wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ali Mohamed inayoendelea nchini huko Uholanzi.
Kabla ya kusainiwa kwa makubaliano hayo  Shein alifanya mazungumzo na Uongozi wa juu wa kampuni ya Shell  yaliyojielekeza katika kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Zanzibar na Kampuni hiyo.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo Kampuni ya Shell itaisaidia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujenga uwezo wa kitaalamu, katika hatua za awali za uendelezaji wa sekta hiyo.
Sambamba na hatua hiyo Kampuni ya Shell itasaidia pia shughuli za maendeleo ya vijana katika kuwajengea uwezo kwa kuwapatia elimu na mafunzo mbalimbali yakiwemo ya stadi za ujasiriamali.
Akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano hayo Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Ramadhani Abdalla Shaaban alisema “kutiwa saini kwa makubaliano hayo ni hatua moja kubwa na mwelekeo sahihi katika jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuendeleza sekta ya nishati nchini Zanzibar” je Wazanzibari mushambiwa kama mafuta yenu yashatiwa saini huko Uholanzi..??
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni ya Shell Tanganyika Bwana Axel Knospe alieleza kuwa wakati mashauriano yakiendelea kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Tanganyika juu ya kuliondoa suala la mafuta na gesi katika mambo ya muungano, Kampuni hiyo itaendelea na dhamira yake ya ushirikiano na nchi ya Zanzibar hadi hapo muda utakapokuwa tayari kuanza kazi ya shughuli za uchimbaji mafuta na gesi ambapo itaifanya kazi hiyo kwa kuzingatia uwajibikaji kiuchumi, kijamii, kimazingira na  kuifanya sekta hiyo kuwa endelevu
“wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika zikishughulikia kwa pamoja suala la kisheria na kisera kuipatia nchi ya Zanzibar haki pekee ya kuendeleza sekta ya mafuta na gesi nchini Zanzibar, Kampuni ya Shell itaendelea na dhamira yake ya kushirikiana na nchi ya Zanzibar hadi hapo muda muafaka utakapofika kuanza shughuli za uchimbaji wa mafuta na gesi” alieleza bwana Axel Knospe.
Wakati akizungumza na Shein Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Zanzibar nchini Uholanzi juzi Waziri wa Biashara ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Uholanzi Bibi Lilianne Ploumen alimueleza Shein kuwa Serikali ya nchi hiyo iko tayari kutumia utaalamu na uzoefu wake katika sekta ya mafuta na gesi kuisaidia nchi ya Zanzibar kuendeleza sekta hiyo.
Bibi Ploumen alieleza kuwa Serikali ya nchi hiyo iko tayari kutoa fursa za mafunzo kwa watumishi wa Serikali ya nchi ya Zanzibar katika sekta ya nishati ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na uzoefu katika kusimamia rasilimali hizo,(haya natuone achanguliwe mzanzibari kwenda kusomea yagujuuu)  utunzaji wa mazingira na ushiriki wa wananchi katika matumizi ya rasilimali hiyo kuepusha migogoro.
“Mambo ya msingi ya kupewa kipaumbele ni pamoja na namna ya uendeshaji, usimamizi na matumizi bora ya rasilimali hizo, ushirikishwaji wananchi na utunzaji mazingira”alieleza bibi Ploumen na kusisitiza haja ya nchi ya Zanzibar kujifunza kutoka nchi nyingine kuepuka makosa yaliyofanywa na baadhi ya nchi ikiwemo Uholanzi yenyewe.
Shein anamaliza  ziara yake ya siku tano nchini Uholanzi leo  na anatarajiwa kurejea nyumbani nchini Zanzibar Jumapili.
Katika ziara hiyo Shein amefuatana na Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ramadhani Abdalla Shaaban, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim na Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa, Uwekezaji na Uchumi, Balozi Mohamed Ramia.

No comments:

Post a Comment