Sunday, September 29, 2013

JE SHEIN NA SEREKALI YAKE YA GNU WAMELAANIWA NA M/MUNGU NA WAZANZIBARI PIA...???


Ndugu muandishi nakuomba utafute njia nyengine lakini si hii ya kupelekea salamu kwa Shein ama kwa serikali ya umoja wa kitaifa,,,kwa ufupi huyu Shein ameshapata laana za watu na keshalaaniwa na Mwenyezi Mungu pamoja na hiyo serikali yake ya umoja wa kitaifa, We Sheni huyo na serikali yake amefika kutoa amri ya kushushwa chini majina ya mwenyezi Mungu pale alipoamrisha ati bendera za uamsho zishushwe,, kwenye bendera hizo kuna nini...???

Kama wao walikebehi kushushwa kwa majina yale ya mwenyezi mungu na sifa zake, basi na yeye (wao) wamelaanika,,,Tulikuwa na maraisi wenye viburi na kejeli (salmin Amour) lakini hakufikia hatua za laana kama hizi, vurugu kwenye sikukuu za idd, kushushwa kwa majina ya mwenyezi Mungu, kuwatesa na kuwasweka ndani masheikhe tena zaidi ya wanne.

Salmini Amouri pamoja na kiburi chake alikuwa akitafuta njia nyengine yanapokuja mambo ya dini kwani nakumbuka wakati ule tulikuwa nao kina marehemu shehe Nassour Bachu, kina shehe Kurwa nk,,lakini hii ya huyu Shein na serikali yake ya kitaifa, imezidi mipaka,,sasa taabu yake anatupa mpaka sisi maana Mwenyezi mumgu adhabu yake ni kubwa na hushusha kwa wote…

Friday, September 27, 2013

PICHA ZA AL=SHABAB NA TUKIO WALILO FANYA NCHINI KENYA BAADA YA KUONYA KENYA NAKUTOKUSIKIA ONYO LAO


HAWA NDIO  AL-SHABAB WA NCHINI SOMALIA

a6
a7
a1
a2
a4
a5
a8
a9

NLD KUWAPELEKA ICC THE HAGUE MKAPA NA KARUME JE WALIO WAUWA WAZANZIBARI 1964 MAPINDUZI NAO WATAFIKISHWA ICC..???


CHAMA cha National League for Democracy (NLD) kimesema kina dhamira ya kuwafikisha kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) The Hague, Uholanzi marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Amani Karume.Ili liwe funzo kwa maraisi wengine wote wanao tawala ktk nchi ya Zanzibar na Tanganyika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho mjini magharibi nchini  Zanzibar, marais hao wanadaiwa wakiwa madarakani, kutumia nguvu kubwa za kijeshi na kusababisha vifo vya watoto 60 kisiwani Pemba, mwaka 2001.
Naibu Katibu Mkuu wa NLD nchini Zanzibar, Khamis Haji Mussa alimuambia muandishi wetu wa siri  kwamba utawala wa viongozi hao ulifanya uhalifu dhidi ya binadamu kwa kutumia helikopta na askari wa ardhini kuwamimiminia risasi wananchi wasio na hatia waliofanya maandamano Januari 26 na 27, 2001 kisiwani Pemba nchini Zanzibar.
Alisema Mkapa, akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na Karume akiwa Rais wa nchi ya  Zanzibar, walisababisha mauaji ya halaiki. Anashangaa kwanini hadi sasa hawajachukuliwa hatua za kisheria: alihoji
“Waliokufa ni watu akirudia tena waliokufa ni watu mbwana weee…Taasisi za kutetea haki za binadamu zinapaswa kuingilia kati na kuwafikisha mahakamani viongozi hawa na washirika wao,” alisema na kuongeza:
“Lakini pia Karume akiwa madarakani…alitumia vibaya madaraka yake kwa kuhodhi ardhi kubwa ya wananchi akitegemea kulindwa na Katiba mbovu isemayo Rais hatoshtakiwa akiwa madarakani na hata baada ya kuondoka madarakani,” alisema Mussa.
Alishangaa ni kwa nini Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata na Makamu wake, William Ruto walifikishwa ICC kwa madai ya kusababisha mauaji ya watu mwaka 2008 wakati Mkapa na Karume wakifumbiwa macho...???
Alipokumbushwa kwamba wakati wa mauaji hayo yakitokea Mkapa alikuwa nje ya nchi na aliyemwachia madaraka alikuwa ni Makamu wa Rais, hayati Dk Omar Ali Juma. Alijibu kwa mkato: “Kila kitu kitajulikana mahakamani,”.
Alisema miaka mingi baadaye, Karume aliamua kukutana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na kumrubuni kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) isiyo na tija kwa Zanzibar na Wazanzibari wanyewe:
“Alimrubuni kwa ghilba Maalim Seif ili tu kukwepa mashtaka…Karume akiwa madarakani alijiwekea chini yake Wizara ya Fedha kwa miaka 10 na kumuahidi Maalim kuwa angemsaidia kupata urais wa Zanzibar,” alisema na kuendelea:
“Miezi sita kabla ya kukutana Ikulu mwaka Novemba 2009…Maalim katika mkutano wa hadhara pale Kibandamaiti alisema. (Mussa anamnukuu Maalim Seif):
‘Karume na familia yake wanafanya ufisadi wa kupora mali…ardhi na fukwe za bahari huku watoto wake wakipata zabuni kinyume na utaratibu’:
“Leo inashangaza eti anasema Karume ni shujaa na Profesa wa siasa!,” alisema na kudai: “Hadi leo nnayo kanda ya video ya mkutano huo,” alisema Mussa.
Alidai pia kuwa Karume aliyatumia madaraka yake na kuipinda kama si kuivunja Katiba ya nchi yetu ya  Zanzibar ya mwaka 1984 na ile ya CCM kwa kuleta SUK kumlinda, dhidi ya mauaji yaliyotokea Pemba nchini Zanzibar.
Muandishi wetu  alipotaka kujua kama ana ushahidi wa madai hayo, alisema Mussa: “Nimejiandaa vya kutosha kuihakikishia ICC kuhusu hayo yote pamoja na ndugu na jamaa wa waliopoteza familia zao na sasa wanadai fidia,”.
Maandamano ya wafuasi wa CUF kupinga ushindi wa CCM nchini  Zanzibar, Januari 26 na 27 yalikumbana na rungu la dola na kusababisha mtafaruku mkubwa hadi watu kadhaa kwenda ukimbizini, Shimoni Mombasa  nchini Kenya.
Ingawa NLD inawasakama Mkapa na Karume, wadadisi wa masuala ya siasa walidai kuwa walioitisha maandamano yale, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu, Maalim Seif nao wanapaswa kuwajibika pia huko huko ICC:
“Lipumba na Seif wala hawakwenda kuyaongoza maandamano…Seif alikwenda ughaibuni eti kuwaomba wahisani waache kuisaidia nchi ya  Zanzibar wakati Lipumba alijificha Buguruni (Makao Makuu ya CUF) wakati wafuasi wao wakipambana na nguvu za dola na kupingwa na kutwangwa risasi,” alisema mwanachama mmoja wa CUF akitaka na viongozi hao pia wapelekwe  ICC ‘The Hague’.
Hata hivyo, mwanasheria mmoja mkongwe aliyewahi kuwa mwanachama mwandamizi wa CUF aliliambia Muandishi wetu kuwa hakuna uwezekano wowote wa Mkapa na Karume kupelekwa ICC The Hague:
“Ni uzushi tu na kutaka kufahamika kwa NLD…Huyo kiongozi angepaswa kwanza kufahamu Mkataba wa Roma (Rome Statute) uliounda ICC unasemaje?,” alihoji mwanasheria huyo.
Alisema Mkataba wa Roma, ulianza kisheria Aprili 11, 2002 pale idadi ya nchi wanachama ilipofika 60 na ICC ikaanza utekelezaji rasmi Julai 1, mwaka huo huo:
Anafafanua: “Kwa mujibu wa Mkataba…ICC ina uwezo wa kuchunguza na kupeleka mahakamani matukio ya uhalifu dhidi ya ubinadamu yaliyofanywa baada ya Julai 1, 2002.
“Maandamano na mauaji ya Pemba yalifanyika mwaka 2001 kwa hiyo ICC haina mamlaka ya kusikiliza wala kupokea malalamiko kama hayo,” alisema Mwanasheria huyo.....Muandishi wetu alipo muliza kwani hakuna viongozi wa nchi nyengine walio fanya mauwaji kabla ya mwaka huo na wamefikishwa mahakamni kama kosovo,bosnia na wengine alibaki ah ah ah mmmmm na kutoweka.

VIDEO-KOMBE LA DUNIA LITAKALO FANYIKA NCHINI QATAR LAGEUGA KUWA UTUMWA MAMBO LEO

JIONE UFAIDIKE ILI USIJEKUBALI MWANAO AKENDA
KATIKA UTUMWA NCHINI QATAR AU KOKOTE KULE
AMBAKO BADO WANAKILI ZA KUFANYA WATU
KAMA SIO BINADAMU ILA WAO TU NDIO
BINADAMU

Thursday, September 26, 2013

UHURU KENYATTA ASEMA AMEWASHINDA AL-SHABAB JE UHURU UMESHINDA NINI...???


Nianze kwa kutoa pole zangu za dhati kwa jirani zetu wa Kenya kufuatia Kichapo  kilichowakumba kwa muda wa siku nne huku  likiacha yatima, wajane, na wafiwa kadhaa, kutokana na kupotea kwa roho za raia wa Kenya na wakigeni, wengi wao wakiwa hawana hatia.
Kenya kuwa jirani zetu haswaa, impekana nasi kwa kila upande, iko mpakani mwa nchi zote mbili Tanganyika na Zanzibar. Kenya wamepakana na Tanganyika kwa upande wa Kaskazini mwa nchi ya Tanganyika (Namanga), na wamepakana na nchi ya Zanziabar kwa upande wa kisiwa cha Pemba (Msuka). Pamoja na ujirani wetu mwema, wakenya ni ndugu zetu, ukirudia historia utang’unduwa kwamba, Mombasa ilikuwa sehemu ya dola ya nchi ya Zanzibar kabla ya kugawanywa na kupelekwa Kenya (mainland). Mbali ya hilo, udugu wa Kenya na Zanzibar au na Tanganyika ni zaidi ya udugu wa kihistoria. Wakenya na Wazanzibar/ na Watanganyika, wanaowana, kuuziana, na kusaidiana wakati wa majanga mbali mbali. Itakumbukwa Wazanzibar mwaka 1964 katika mapinduzi ya kupinduliwa nchi ya Zanzibar na kuingia utawala wa MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA Wazanzibari wengi walikimbilia Mombasa na hata hivi karibuni tu siku za uchanguzi kwa mara nyengine tana Wazanzibari wenye asili ya kisiwa cha Pemba walipewa hifadhi ya ukimbizi na ndugu zao wakenya (Shimoni-Mombasa) wakati yalipotokea machafuko na mauwaji kule Pemba, January,2001. Hivyo basi tunakila sababu yakuguswa na msiba huu  uliolitokea majirani zetu wa nchi ya Kenya (Westgate), msiba wao ni msiba wetu….!
Nimeisikiliza hotuba ya Rais wa Kenya aloitoa siku ya nne baada ya wanamgambo wa Al-shabab kuvamia Westgate,kuuwa, kujeruhi na kuleta hofu kwa wakazi wa Kenya. Hotuba ilijaa maneno ya faraja, pongezi, ujasiri, kujiamini na ushujaa. Pamoja na ukweli kwamba yeye kama Rais (kiongozi wa nchi) hatakiwi kukiri kushindwa au kugofywa….bado haiondoi ulazima wakukubali kukosea au hata kushindwa kama ni hivyo. Usipokubali kuona ulipokosea au kushindwa kamwe huwezi kurekebisha makosa!!! Unahitaji uone aliposhindwa ndipo Utaweze kuipanga serkali yako kisera na kiulinzi ili kuzuia mauwaji ya watu wa sio na hatia kutokea tena katika ardhi yako msimo wa kiswahili asiyekubali kushindwa sio mshindani.
Kenyatta amehutubia taifa, akielezea kwamba Kenya imeshinda, na imewatia aibu Al-Shabab. Hii ni lugha ya kisiasa, kwangu haina nafasi unapohusisha maisha ya watu wasio na hatia na mali zao. Unasema umeshinda, umeshinda nini wakati kutokana na mfumo wako m’baya wa kisera umesababisha Al-Shabab wawafanye raia wako wasio na hatia na wasiohusika na chochote wala kunufaika na lolote katika sera hiyo wawe waathirika wa Al-Shabab na kuwafanya kuliwa kama kachiri rai wako na Al-Shabab Umeshinda nini, wakati udhaifu wa vyombo vyako vya ulinzi na usalama vimeshindwa kuzuia Al-Shabab hawa kuingia na kufanya uhalifu ndani ya ardhi ya nchi yako..?? Umeshinda nini, wakati serkali yako ilisimama kwa muda wa siku nne mfululizo..?? Umeshinda nini wakati raia wako na wageni wameshindwa kufanya  shughuli zao za kujieletea maendeleao kwa muda wa siku nne..?? umeshinda nini wakati rai wako na rai wa kigeni wameuliwa kama kuku..?? Ushindi uko wapi wakati Al- Shabab  wamepelekea kuuvuruga uchumi wa Kenya kwa muda wa siku nne tu..?? Ushindi upi wakati tayari Wakenya wenye asili ya somalia wanaishi kwa hofu ya kulipiziwa kisasi, ushindi upo wapi wakati Westgate sio ile tena ya awali, imebaki gofu….sioni ushindi hapo, labda kujifariji tu..!!! Wakenya na wapenda amani duniani hatujashinda..!!
Ni kweli Al-Shabab hawapo tena Westgate, na sasa Westagate ipo chini ya vikosi vya ulinzi vya Kenya, lakini kila mtu anajuwa kwamba halikuwa lengo la Al-Shabab  kuhamia Westgate au kuivamia Kenya na kufanya ndio makazi yao..!! Wala haikuwa lengo lao kutoka wakiwa hai, ndo maana kupitia msemaji wao (Abuu Omar), waliweka wazi kwamba hawatafanya makubaliano (negotiation) juu ya mateka, kama wangetaka watoke salama na roho zao, wangewacha njia hii ya makubaliano wazi..!!
Nikikumbuka hesabati  nilizojifunza shule ya msingi japo kuwa nilikuwa sio mkali sana katika hisabati (hesabu za milinganyo) nilijiuliza swali hili ; Ikiwa Al-Shabab 10 walovamia Westgate imewachukuwa Jeshi la Kenya na polisi wa Kenya na vyombo vyake vyote vya ulinzi na usalama (plus wataalamu kutoka USA/Israel ) siku 4 kupambana nao, jee ingekuwa  Al-Shabab 100 ingewachukuwa siku ngapi...??? musitufanye kuchaka wakati sio mahali pa kucheka.
Kwa kutumia kanuni rahisi ya mlinganyo (tulikuwa tunaita kwa kimombo “cross multiplication”), utaona Kenya ingesimama kwa zaidi ya mwezi mmoja (siku 40!) Na ingepoteza watu wasio na hatia wasiopunguwa 700, majeruhi 1700 kama Kenya kungekuwa na ”Shopping malls” mfano wa Westgate 10….kwa wapenda amani ya kweli hakuna tulichoshinda..!!!
Viongozi wa nchi zetu lazima mujuwe kwamba hotuba zenu nzuri, zilizojaa majigambo na ujasiri hazitusaidii sisi raia wakawaida wakati usalama wetu upo mashakani. Hazina maana yoyote kwetu wakati tunaendelea kupoteza maisha, na kuishi kwa hofu ndani ya nchi zetu. Sisi raia tunahitaji suluhisho la kudumu, tunahitaji usalama wetu uwe wa asili sio wakuwekwa na kulindwa na mitutu ya bunduki, maana mwenye bunduki hiyo akisinzia usalama wetu haupo tena…
Al-Shabab  ni viumbe kama sisi, ni watu wenye kutumia akili, kupanga,wananda,kukusoma wapi wewe ni mwepesi wa kukuvamia,vipi wakuvamiye.sio kama ni watu wapumbvu kama wengi wa watu wanavyo fikiri.hatufurahi wanacho kifanya hata siku moja sio sawa kabisa lakini Pamoja na ubaya wao huo Al-Shabab  ni sawa na kirusi  cha maradhi hatari kilichotengenezwa maabara (lethal genetically engineered virus).Al-Shabab,boko haramu na wengineyo   tunawatengeneza wenyewe kutokana na sera zetu mbaya na mbovu...!!! Nchi za afrika zimeingia katika mkumbo wakuiga nakumbuka siku za nyuma au miaka ya nyuma watu walivyo anza kurap nchini Tanganyika na nchini Zanzibar moja wa warap alikuja na rap yake akisema musii igee ovyo musii igee ovyo ndio nyinyi viongozi wa afrika na kuja na sera na kuiga ovyo sera za mataifa ya Magharibi (USA na UK). Tumeanza kucheza ngoma za mabwana wakubwa hao, wakati ngoma za asili yetu na midundo na aina ya uchezaji hatujui...!!!!!!!
Binafsi, kama muumini wa amani na utulivu, naamini kwamba hakuna vita yoyote (hasa inayohusisha ndugu) ambayo inamalizwa kwa vita..!!! Hakuna m’badala wa mazungumzo katika kutafuta suluhu. Itakuwa kitendo cha ajabu, jirani yako watoto wake wanagombana na  wewe unampeleka mwanao mkubwa akamsaidie jirani yako huyo kumpiga mwanawe moja wapo, kwa jina atiii la kuleta amani..!!! Kama ambayo hakuna sababu yoyote itakayo halalisha Al-Shabab  kuuwa raia wasio na hatia, vile vile hakuna sababu yoyote itakayo halalisha Jeshi la nchi moja kuingia nchi nyengine kusaidia upande mmoja unaovutana na mwengine. Usinambie eti unasiaidia serekali halali hakuna serekali halali…my foot! Afrika na serekali halali wapi na wapi....? wacheni kujidanganya nafsi zenu Njia wanazotumia serekali zetu nyingi za Afrika kuingia madarakani tunazijuwa, chaguzi zetu ziitwazo ”free and fair” tunazijuwa, kwa hiyo ikitokea kuna kundi linalalamika au kukataa uongozi uliopo madarakani, huo ni sawa na ugomvi wa ndugu wanaogombania mirathi…si juu yako kupeleka jeshi kupigana dhidi ya kundi moja kwanza nchi yako yenyewe ina walala hoi wangapi..? omba omba wangapi...? watu wasio na kazi wangapi..? watu wasio jeweza wangapi….? leo wewe ndio wakwenda kusaidia nchi nyengine wakati nyumba yako mwenyewe imeja nyufa unamzuga nani...???
Serekali za Afrika badala ya kupeleka majeshi kuendelea kuuwa na kuharibu hicho kidogo kilichobakia nchini somalia, ingekuwa jambo la maana sana kama wangekuwa wanapeleka wana ”diplomasia” na wataalam wa kutatua migogoro, ili kuwaleta wanaogombana kwenye meza ya mazungumzo. Naamini kwenye mazungumzo na utayari wa msuluhishaji kutoegemea upande wowote, lazima kutapatikana suluhisho la kudumu. Nasisitiza, lazima anaesuluhisha awe tayari kuyasikia na kuyakubali mapungufu ya kila upande, lakini pia awe tayari kuyasikia na kuyakubali yenye mantiki kutoka kila upande. Haiwezekani kikundi cha watu katika jamii kipaze sauti zao kulalamika halafu iwe hakuna lamaana wanalodai...!!!! Lazima wasikilizwe na wazingatiwe. Sikubaliani na falsafa ya ”wacha walo wachache wasikike na walo wengi waamuwe” Mimi nasema wacha wote (minority and majority) wasikike na wote wazingatiwe katika maamuzi.

Kupeleka jeshi kwenye nchi ya jirani kwa minajili ya kuisadia serekali au kikundi kinachopigana na serekali ni kujijengea maadui katika nchi yako hivi kweli ingelikuwa Kenya ndio somalia iko katika hali mbaya sana ya kivita yenyewe kwa wenyewe Mkikuyu na Mjaluwo wanapigania kuongoza Kenya kisha somalia wakaleta majeshi wawasaidiye Wajaluwo je nyinyi Wakikuyu,Wakamba n.k. mungelionaje...???,hii ni kuwatengenezea mazingira hatarishi raia wako wasiofaidika kwa lolote na sera hiyo ya kibabe, sera ambayo hata muanzilishi mwenyewe (USA) AMECHEMSHA, ameshaanza kujifunza kwamba haina faida zaidi ya hasara na kuongeza maadui. Upinzani anaoupata rais Obama kutoka kwa raia wake na Maseneta wake  dhidi ya nia yake ya kutaka kuivamia nchi ya Syria kijeshi ni ushahidi tosha juu ya kuanza kung’amua ubaya wa sera hii. Lazima tujifunze kwamba mauwaji ya aina yoyote huzaa visasi. Mtu anaeshuhudia mzazi wake au jamaa, iwe mama, baba, dada au mtoto wake au hata rafiki anauliwa kwa bomu, risasi au rocket na majeshi wa nchi ya kigeni, anaharibiwa mfumo wake mzima wa maisha, iwe kwa nia njema au mbaya iliyofanywa na majeshi hao, ni rahisi sana kwa mtu huyo kujenga kisasi dhidi ya jeshi au hata raia wa nchi hiyo. Ni rahisi kushawishika kuungana na vikundi vyenye nia ya kulipiza kisasi ( Al-Shabab)! Lakini lazima pia tukubali kwamba, hakuna amani iletwayo kwa vita....!!! Ashindae kwenye vita hupata utulivu wa muda tu, alieshindwa kwenye vita, akijijenga na kupata nguvu atarudi tena na tena na tena kupambana, maana visasi hurithishwa kizazi mpaka kizazi….!!! Tutatue migogoro yetu kwa mazungumzo yenye nia ya kweli ya kuleta suluhisho au tuwachiye wenyewe wana ndugu msimo wa kiswahili wanadungu wakigombana chukuwa jembe ukalime. Viongozi wetu ubabe wenu unaoishia kwenye majukwaa kwa hotuba za kuandikiwa hautusaidii kitu, mwisho wa siku tunaokufa na kuumia ni sisi raia wakawaida au wachini sio nyinyi muliojificha katika IKULU na MAJUMBA YA KIFAHARI NA ULIZI MKALI..!!!!
Mwisho narudia tena kusema sikufurahishwa na hatua ya kundi Al-Shabab  hao kuuwa, kujeruhi na kugofya raia wasio na hatia. Kwa kitendo chao hicho hawastahili kuheshimika hata ikiwa wao ndio wanajita wakombozi wa nchi ya somalia pia sifurahishwi na nchi za Burundi,Uganda,Kenya na wengine kuugana na kuwapiga wasomalia wa upande moja na kusaidia upande mwengine. Naungana na familia zilizopoteza wapendwa wao katika mkasa huu, Allah awajaalie mioyo ya subra,  na nawaombea wapowe haraka wale walopata majaraha...!!!!!

Huu ni mtazamo wangu tu….lakini kwa kujihami natembea ”alkali” kujikinga na wanaomwagia wenzao ”asidi” au TINDI KALI hapa nchini Zanzibar natumai nitakuwa sio nazalisha chumvi, na kuepusha masikini za mungu kung’olewa meno bila ganzi nawashauri wajichoma  ”lidocaine” kabisaaa!

KAMISHNA MUSSA ALI MUSSA WACHA KUJIFICHA NJOO UELEZE UKWELI AU DOMO LAKO LIMEKUPONZA..???


JESHI la Polisi nchini Zanzibar limekaa kimya na halitoi maelezo yoyote ya kinachendelea katika uchunguzi wa madai yake kuwa huenda watu wenye uhusiano na kikundi cha Al Shabaab cha Somalia wanahusika katika mashambulizi ya tindikali nchini Zanzibar.

Lakini wakati polisi wakiwa kimya, kelele zinasikika kila pembe zote za nchi ya Zanzibar na kutoka nje, zikiwemo taarifa za habari za kimataifa, mitandao ya jamii na ya taasisi za nje, kutaka kujua zaidi juu ya habari hizi.

Hali imeonekana kuwa tete zaidi na mijadala kuwa mingi kila pembe ya nchi ya Zanzibar, mijini na vijijini, baada ya shambulio kali la Al Shabaab mwishoni mwa wiki katika Jiji la Nairobi, nchini Kenya, lililosababisha watu zaidi ya 62 kuuawa na wengi kujeruhiwa.

Baadhi ya watu, kwa sababu zao tofauti, wanaonyesha shaka kubwa, na wengine hawataki kabisa kuamini taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Polisi nchini Zanzibar, Mussa Ali Musa.

Mjadala mkubwa umezuka juu ya picha ambazo Kamisha Mussa mwenyewe anaonyesha mageloni madogo meusi ya tindikali zilizokamatwa, na kwamba watu 15 walikuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi. Mengi yamezuka juu ya kauli ya kamishna na hiyo picha inayoonyesha tindikali.


Kwanza watu wanataka kujua nini kimetokea katika kuwachunguza watu hao 15, wangapi wanashikiliwa na polisi na wangapi wameachiliwa...?

Jingine ni wasi wasi kama hicho kilichoonyeshwa ni tindikali au maji ya betri za magari kwa vile hizo chupa zilikuwa na maandishi ya “distillery water”. Je, ni kweli hayo ni maji ya betri au hayo maandishi ni bandia..??

Wataalamu wanaofahamika kujua vizuri masuala ya tindikali na wanaotumia katika kazi zao katika maabara mbalimbali wanasema maji ya betri hayana madhara makubwa kiasi cha kuweza kubabua mwili wa mtu.

Jingine ni kwamba hizo chupa zilikuwa na chapa, maandishi ya wenye maduka. Je, katika uchunguzi imegundulika watu hao wamezipata kihalali..??

Vile vile inasemekana palifanyika uchunguzi katika maabara mbalimbali, zikiwemo za utafiti. Je, nini kilichogunduliwa huko..??

Ni muhimu wananchi kujua ili kila raia mwema ambaye huenda akawa anajua chochote juu ya suala hili aweze kulisaidia Jeshi la Polisi katika uchunguzi wake, kwa sababu linafanya kazi ya kunusuru maisha ya wananchi.

Unapoisoma mitandao mbalimbali ya kijamii na ile ya taasisi za kimataifa ndiyo utaona upo mkorogo juu ya suala hili.

Jamaa mmoja katika mtandao amekwenda mbali zaidi na kuhoji ikiwa maji ya betri ni kosa la jinai. Akasema basi kama ni kosa madereva wote wa magari Unguja na Pemba (pamoja na polisi) wanafanya kitendo cha uhalifu kwa kuendesha gari ambazo betri zake zina maji hayo.

Maelezo haya, kwa vyovyote vile, huenda yakawa ya kejeli, lakini ni ishara ya kuonyesha namna ambavyo watu hawaridhiki na jinsi polisi wanavyolichunguza suala hili.

Ukimya uliopo ndio unatoa mwanya zaidi wa uvumi na hata kusingizia polisi mambo yasiyo ya kweli katika hii kadhia ya mashambulizi ya tindikali.

Kwa vyovyote vile, Kamishana Mussa halitendei haki Jeshi la Polisi, Wazanzibari na Watanganyika kwa ujumla kwa kukaa kimya au kukwepa kujibu maswali ya waandishi wa habari.

Kwa taarifa yake, wanachojaribu kufanya waandishi ni kuwafahamisha wananchi kinachoendelea na hawana ajenda ya siri na wala sio wao waliotaka ajiuzulu kwa madai ameshindwa kazi.

Kama kamishna alikuwa hataki kuulizwa maswali ili atoe ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali, basi asingelitoa habari hizo hadharani.

Hapa nigelipenda kukumbusha kwamba Inspekta Jenerali Saidi Mwema, mara tu alipoingia madarakani alifika Zanzibar na kuwataka waandishi wa Tanganyika kulitendea wema na haki Jeshi la Polisi na kutaka pawepo mashirikiano kwa maslahi ya nchi.

IGP Mwema alitoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Habari Tanganyika (MCT)lilopo Shangani, mbele ya Hoteli ya Serena.

Kauli hii ya IGP ilifuatiwa na Jeshi la Polisi kuweka hadharani kwa waandishi wa habari namba za simu za wakuu na makamanda wa polisi wote wa mikoa. Sasa huu mwenendo wa kukwepa waandishi wa habari unatoka wapi au Jeshi la Polisi limeamua kwenda kinyume na wito wake..??

Kamishna wa Polisi Mussa anapaswa kufahamu kwamba kauli yake ya kuwepo Al Shabaab Visiwani imewashitua sana Wazanzibari wengi ndani na nje na kuanza kujiuliza kama visiwa vyao vipo salama, hasa wakitilia maanani waliyosikia kutokea Somalia na sasa Kenya.

Kama Jeshi la Polisi litafanya utafiti wa haraka haraka litagundua kwa kiasi gani hali imekuwa mbaya na watu kujaa hofu juu ya kuwepo Al Shabaab Visiwani.

Kwa upande mwingine, wataalamu kadha wanaoelewa kwa undani na kufuatilia kwa karibu masuala yenye kuhusu mashambulizi ya kigaidi duniani, wanasema hawana kumbukumbu zinazoonyesha kuwa Al Shabaab wanatumia tindikali katika mashumbulio yao.

Badala yake hutumia silaha za moto, maroketi na mabomu. Hili pia limeonekana katika shambulio liliofanyika Nairobi mwishoni mwa wiki nchini Kenya.

Vile vile sio kawaida kwa Al Shabaab kumlenga mtu mmoja mmoja au wawili, bali hutafuta eneo lililojaa watu na kufanya mashambulio  yao.

Katika hali hii wapo watu wanaouliza je, hawa Al Shabab wanaosemekana kuwepo Visiwani na kufanya mashambulizi kwa kutumia tindikali ni tofauti na hao wanaodaiwa kuwa wenzao waliopo Somalia na wale wanaofanya mashambulizi kwengineko..??

Haya ni masuala mazito ambayo Kamishna Musa anawajibika kwa kila hali kuja hadharani na kuyatolea maelezo, na katika zama hizi za kutafuta ukweli na uwazi, ni vizuri akawa muwazi na kuwa tayari kujibu maswali na sio yeye tu kutaka kuzungumza na kusikilizwa.

Ni vizuri akafahamu kuwa kwa hili hakuna anayemuonea, ni upande wa pili wa sarafu wa kazi ngumu na jukumu alilokuwa nalo kama Kamishna wa Polisi wa nchi ya Zanzibar.

Katika dunia yetu ya leo, hata katika shule, wanaoambiwa jambo au kufundishwa na mwalimu huwa na haki ya kuuliza, tofauti na hali inavyokuwa katika ibada misikitini au kanisani ambako kila anachotamka kiongozi wa dini hupokelewa kimya kimya au kuitikiwa kwa watu kutamka “Amin”.

Ni vizuri kwa Jeshi la Polisi Zanzibar likavunja ukimya na kuuleza umma kinachoendelea.

Hii itaepusha uvumi ambao kwa kawaida haujengi bali unabomoa. Pia kutoa nafasi kwa umma kuchangia kwa njia moja au nyengine kuwanasa hawa wanaotukosesha raha usiku na mchana kwa matumizi ya tindikali kushambulia watu wasiokuwa na hatia na kutuharibia jina la nchi yetu ya Zanzibar.

Tuache ukimya na tuelezane kinachoendelea

MADISCO,BAA NA KUMBI ZA STAREHE VYATIA FORA YA UFUSKA NA KUSABABISHA VIJANA 30 KUAMBUKIZWA UKIMWI PAJE NCHINI ZANZIBAR


Wananchi wa Kijiji cha Paje Mkoa wa Kusini Unguja nchini Zanzibar wamewalalamikia wamiliki wa baa na kumbi za starehe na madisco zilizomo katika kijiji hicho kutokana na vitendo viovu vinavyo kwenda kinyume na heshima na maadili ya kijiji hicho na nchi ya Zanzibar.
Wananchi hao wametoa malalamiko yao katika mkutano wa pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk na wamiliki wa baa na madisco zilizomo kijiji hapo uliofanyika Ofisini kwa Waziri Kikwajuni.
Walisema wamiliki wa baa na kumbi za starehe wamekua wakiwasumbua kwa kupiga disco usiku kucha na kusababisha kushindwa kulala majumbani mwao kabisa.
Waliongeza kuwa tabia hiyo inapelekea vishawishi kwa watoto wao na kujiingiza katika mambo maovu yanayokwenda kinyume na mila silka na utamaduni wa kijiji chao na nchi ya Zanzibar pia.
Disco linatuletea usumbufu mkubwa kwa watoto wa kijiji chetu wapo baadhi hawalali makwao usiku mzima,” alisema Mbaraka Salum askari Jamii wa kijiji hicho.
Mbaraka alisesema vitendo vya ngono na kubakwa kwa watoto wa kiume vimekuwa vikifanywa bila woga na vijana 30 wa kijiji hicho tayari wameshaambukizwa virusi vya ukimwi.
Wananchi hao wa Paje wameishauri Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kuzuia vibali vya kupiga Disco kumbi zote za starehe ndani ya kijiji hicho kwa kuhofia kutokea madhara makubwa zaidi.
Wamiliki wa Baa na kumbi za starehe kwa upande wao wameitaka serikali iwaangalie kwa jicho la huruma kwa sababu burudani ya ngoma ndiyo inayopelekea kupata wateja na kuongeza kipato chao kinyume chake ni hasara katika biashara yao.
‘’Tunaiomba Serikali ituruhusu japo siku moja kwa wiki tupige ngoma ili tuweze kuingiza mapato,”alisema Mariyam Simba Mkwasi mmiliki wa baa la Vuvuzela. astahafiru allah kisha jina lake ni mariyam
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe, Said Ali Mbarouk alisema kuwa vibali vya musiki vitaendelea kuzuiliwa ikiwa wamiliki wa sehemu hizo watashidwa kufuata taratibu ziliziowekwa .
‘’Ni bora tukose mapato Serikalini kuliko kuendelea kuwanyima uhuru wananchi wetu tutaendelea kuzuiya vibali vya disco mpaka mujenge kumbi zisizotoa sauti,‘’alisema Waziri wa Habari.
Alisema iwapo kuimarika kwa sekta ya utalii Zanzibar kutasababisha Utamaduni wake kumongonyoka hilo halitawezekana na hatuwezi kupanda mbegu ya ufuska katika visiwa vyetu.
Alisema Zanzibar ina ustaarabu na utamaduni wake, hivyo ametaka kila mmoja ahakikishe kuwa utamaduni huo unalindwa, unadumishwa na kurithishwa kwa vizazi vijavyo.
Kumbi za starehe na burudani zilizolalamikiwa zaidi na wananchi wa kijiji cha Paje ni pamoja na Vuvuzela, Jambo, Gereje na Deman Loge

Monday, September 23, 2013

NCHINI TANGANYIKA HAKUKALIKI FAMILIA YAUWAWA NA KITOTO KICHANGA PIA

mauaji
Mwanza. Familia ya watu watatu akiwamo baba, mama na mtoto wa miezi saba, wameuawa kikatili usiku wa kuamkia jana Kata ya Buhongwa, Kijiji cha Ihila,Wilaya ya Nyamagana, mkoani huko nchini Tanganyika.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia miili ya marehemu hao ikiwa sakafuni, huku imetapaaka damu. Hadi sasa haijafahamika sababu ya watu hao kuuawa.
Waliouawa ni Jonas Luhinga, Rusia Jonas na mtoto Eliud Jonas.
Akisimulia tukio hilo, mtoto wa marehemu, Debora Jonas (12), alisema tofauti na baba, mama yake na mdogo wake ambao wameuawa, kulikuwa na mgeni nyumbani kwao kwa muda siku tatu ambaye asubuhi ya tukio alitoweka.
Debora alisem saa 10:00 usiku, akiwa amelala na mdogo wake ghafla alianza kulia sana na kumbembeleza, baada ya muda mgeni huyo aliingia chumbani kwake na kumwomba mtoto huyo ili ampeleke chumbani kwa mama yake.
Alisema alimpatia mtoto huyo na yeye kulala mpaka asubuhi na kwamba, aliamka kwenda kufungua mlango wa chumbani kwake na kukuta umefungwa kwa nje ndipo alipoanza kuomba msaada kwa kupiga kelele na majirani walikwenda kufungulia.
“Nilipofika mlangoni nilijaribu kuufungua bila mafanikio, baadaye niligundua umefungwa kwa nje,” alisema Debora.
Alisema baada ya kufunguliwa aliona maiti ya baba yake ikiwa sebuleni, huku ikiwa imechinjwa na alikimbia chumbani kwa mama yake na alimkuta amekufa na mdogo wake huyo wa miezi saba.
Pia, tukio hilo lilishuhudiwa na majirani waliokwenda kumfungulia mlango.
Debora alisema alikimbia chumbani kwa wazazi wake moja kwa moja akiwa na majirani hao na kukuta miili ya mama na mdogo wake ikiwa chini, hakukuwa na damu bali waliona kamba ikiwa pembeni yao na kuhisi huenda ndiyo ilitumika kumnyongea mama na mtoto wake.
Kuhusu mgeni ambaye alikaa nyumbani kwao kwa siku tatu, alisema alikuwa hamfahamu zaidi ya kumtambua kwa jina moja la Lameck na kwamba, muda mwingi alikuwa akimwona anaongea na baba yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Erenst Mangu, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, polisi wanafuatilia waliohusika na mauaji hayo.
Akizungumza eneo la tukio, Ofisa Upelelezi Makosa ya Jina Mkoa Mwanza, Joseph Konyo, alisema waliouawa ni familia ya Jonas Luhinga.
Konyo alisema ni mapema kwa polisi kuzungumzia mauaji hayo kwamba, watakapokuwa tayari watatoa taarifa.
Baadhi ya wananchi walisema hivi sasa upokeaji wa wageni unatakiwa kuratibiwa kama ilivyokuwa zamani, mwenyeji akitakiwa kutoa taarifa kwa mjumbe wa nyumba kumi.
Walidai inawezekana mgeni huyo akawa amehusika na muda aliokaa hapo alikuwa anasoma mazingira ya nyumbani.
Pia, walitaka ulinzi shirikishi kuimarishwa kwa sababu inawezekana wakati mauaji hayo yalipokuwa yanafanyika, kungekuwa na doria ingeweza kusaidia. Hata hivyo, baadhi ya wananchi wamekuwa wakipinga kushiriki ulinzi shirikishi, huku wakidai kazi hiyo inatakiwa kufanywa na polisi.

KAMANDA WA CHAMA CHA MAPINDUZI ASEMA TUTAWAKATA SHINGO ZENU NA KUWAMWANGIA TINDI KALI WACHINA WOTE WALIO NCHINI TANGANYIKAMaisha ya raia wa China wanaoishi nchini Tanganyika, yako hatarini, kutokana na mtu anayejiita kuwa ni ‘Kamanda wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Asilia’, kusambaza ujumbe kwenye mtandao wa kompyuta unaotishia kuwaua akiwatuhumu kwa makosa 21 dhidi ya nchi yao ya Tanganyika.
Ujumbe huo ulioandikwa kwa lugha ya Kiingereza wenye kichwa cha habari: “Yah: Killing of all Chinese citizens in Tanganyika” (Yah: Kuwaua raia wote wa China walioko Tanganyika), umeelekezwa kwa Balozi wa China nchini, Lu Younqing, ambaye umemtaja kimakosa kwa jina la Liu Xinsheng.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba, aliahidi kufuatilia taarifa hizo.
Mtu huyo anaanza kudai katika ujumbe huo kuwa wamekasirishwa na kile alichokiita “Matusi ya Balozi Younqing dhidi ya Watanganyika” kwa kuingilia siasa za Tanganyika na kujifanya msemaji wa CCM.
“Tukiwa ni wananchi wa Tanganyika, tunatangaza kwamba, tumekasirishwa na hilo. Hivyo, tunataka raia wote wa China waondoke haraka nchini na iwapo hawatafanya hivyo watakuwa walengwa wa mauaji,” ulieleza ujumbe huo na kuongeza:
“Tutawakata shingo zenu, kuwamwagia tindikali popote pale kutoka Mtwara hadi Moshi. Serikali na Uhamiaji hawawezi kufanya lolote. Ni lazima tuwashughulikie.”
Ujumbe huo unadai watatekeleza maovu hayo kwa madai kwamba, Balozi Younqing ndiye aliyesababisha kwa kuingilia mambo ya ndani ya Tanganyika, baada ya kuwaibia Watanganyika kila kitu.
Mbali na balozi kudaiwa kufanya hayo, ujumbe huo unasema pia raia wa China wamekuwa wakiingiza nchini samaki waliooza kwa nia mbaya ya kuwaua Watanganyika.
Unadai kuwa maneno ya balozi huyo yameonyesha kuwa ni adui mkubwa kuliko kundi la Al-qaeda.
“Raia wa China watakuwa ndiyo lengo letu kubwa, tutawaua wote kwa wakati mmoja. Tunashauri uchukue taarifa hii kwa umakini kwa sababu CCM Asilia tutawaua nyote na vichwa vyenu kuvilisha mbwa,” unasema ujumbe huo.
Unadai CCM-Asilia ni watu wanaoendesha mambo yao chini kwa chini, wana mafunzo na mpangilio na wamejiunga na wanajeshi wastaafu wazalendo kukomboa nchi yao.
“Ni kundi ambalo lina sumu ya kukabiliana na tishio la Wachina nchini,” unaeleza ujumbe huo.
Ujumbe huo unaeleza kuwa CCM-Asilia wanamiliki silaha za kutosha na pia wana uwezo wa kiufundi wa kuua kila Mchina nchini kwa sababu mbalimbali, ikiwamo Wachina kuvamia hifadhi za Taifa na kuchimba dhahabu na madini mengineyo.
Sababu nyingine ni Wachina kuharibu misitu, kujihusisha na ukahaba jijini Dar es Salaam, vitendo ambavyo vinapingwa na Waislamu .
Unataja sababu nyingine kuwa ni Wachina kupora ardhi iliyopo kwa ajili ya chakula cha Watanganyika na kuitumia kwa manufaa yao na kuwatesa Watanganyika kila mahali wanakokwenda.
Sababu nyingine ni kuchafua mazingira, kuharibu uchumi wa nchi, kuuza dawa za kulevya, kupora ajira ya Wamachinga Kariakoo, kupora ajira ya ujenzi na kwamba, sasa wanataka pia kupora kazi zote za gesi.
Unadai sababu nyingine ni Wachina kuuza chakula kibovu kinachohatarisha maisha ya Watanganyika, kuua tembo na vifaru, kujihusisha na rushwa kubwa, ambayo haikubaliki katika nchi yao.Pia kutumia vibali bandia, kujenga barabara na majengo mabovu nchini.
Alipoulizwa na wandishi wa habari jana kuhusiana na ujumbe huo, Kamishna Manumba alisema bado hajaupata, lakini akaahidi kuwa atafuatilia.
“Nashukuru kwa kunipa taarifa hiyo. Tutafuatilia,” alisema Kamishna Manumba.
Hata hivyo, jitihada za wandishi wa habari  kumpata Balozi wa China ili azungumzie vitisho hivyo, hazikufanikiwa baada ya simu yake kutopatikana.

Sunday, September 15, 2013

POLISI MUNAWAJUWA WANAO MWANGIA WATU TINDI KALI NCHINI ZANZIBAR ACHENI KUZUGA WATU


Huenda kuna watu wanashangaa inakuwaje polisi hadi leo kushindwa kuwakamata wahalifu wanaohusika na kuwamwagia watu tindikali na vitendo vyengine viovu. Hili halishangazi kutokana na utendaji wa kazi wa polisi wa nchi hii ya Zanzibar.
Kwanza polisi walio wengi wanahusika na baadhi ya vitendo vya uhalifu kama hivi karibuni wameweza kuuiba upanga wa kipolisi aliokabidhiwa kamanda wa polisi wa nchi ya Zanzibar. Ilikuwaje kitu cha thamani kama hicho kuweza kuibiwa kirahisi..???  Pia uhalifu wanaoufanya polisi kwa kupiga watu kama wanyama nani ambae hajawahi kushuhudia..???

Siku za nyuma polisi hawakuwa na tabu kuweza kuwakamata angalau washukiwa au masikini za Mungu ambao hubambikiwa kesi.Wafuasi wengi wa CUF walikumbwa na kukamatwa kutokana na fitna za majirani zao CCM ambao waliwaambia polisi kuwa hao MACUF ndio wanaowashuku hapo mtaani kufanya vitendo vyote vya hujuma. Hili kwa sasa kidogo lina tabu.Maana Wazanzibari wameungana na kuwa kitu kimoja hakuna tena hao MACUF wala hao MACCM. isipokuwa hao wahafidhina na vitimbakwiri wa MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA tu ndio bado wamo.

Ingekuwa kuna kiongozi wa UAMSHO ambae hajakamatwa basi polisi wangekuwa kila akimwagiwa mtu tindikali basi wangekamata mmoja mmoja. Lakini kwa bahati mbaya wote washawakamata na kuwasweka jela. Nadhani wanatamani wawatoe ili wawe wanawakamata kwa design hii lakini wapii. Polisi hupata tabu sana kuwakamata wafuasi wa CCM wanaposhukiwa kufanya uhalifu. Hili haliuziki kwa wakubwa wa polisi hata kwa mzizi wa muarubaini. Alipouliwa yule padre kule Beit al Ras kulikuwa na kila aina ya makeke kuwa mhusika atakamatwa kwani maafisa waliobobea wa polisi kutoka nchi ya Tanganyika na hawa wetu hapa nchini Zanzibar mbumbumbumatari wakisaidiwa na FBI wanafanya uchunguzi. Kilichotokea ni kuwa FBI waliondoka kimya kimya baada ya kuona polisi hawakuwa tayari kutoa ushirikiano wa kweli. Baadae ikawa anatafutwa mtu abambikiziwe kesi ili angalau hili jambo lizimike kwanza. Kwa hiyo polisi katika pekura pekura zao wakaona video ya Bwawani ya jamaa aliesema kuwa wako tayari kuunda vikundi vya msituni kupinga muungano.
Baada ya kumuona wakamchora picha yake kisha wakaitangaza kila mahali(ilhali wanamjua huyo jamaa) na kusema atakaesaidia kukamatwa kwa huyo jamaa atapata donge nono.Wakaishia kumkamata wenyewe pale Kariakoo na donge nono wakalichukuwa wenyewe na kulila na kumuacha Jamaa yuko Kiinuamiguu bila hatia lakini imesaidia polisi kulizima hilo na kula donge nono.

Walikomwagiwa tindikali wale kina dada wa UK kukazuka zogo la wakuu wa nchi na polisi kulaani na kusema kuwa waliohusika watakamatwa haraka sana. Hiyo kisiasa ilisaidia kuzima hilo jambo.
Na hivi leo baada ya uhalifu huo kurudiwa tena kwa kumwagiwa tindikali padre mwengine, wakuu wa nchi na wa polisi wanaruka wakitoja kulaani na kuhimiza waliohusika na unyama huu wakamatwe lakini polisi wamechachiwa. Wanazo fununu za kujua waliohusika lakini hawana ubavu wa kuwakamata. It is very simple! Wanaohusika ni watu ambao hawataki nchi ya Zanzibar iwe na mamlaka kamili. Kwa hiyo wanawatishia watu wenye asili ya nchi ya Tanganyika ili ikitokezea kupiga kura ya maoni wakatae mfumo wa serikali tatu au chochote kupelekea nchi ya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili. Sasa niambie ni polisi gani mwenye ubavu wa kuwakamata watu hawa...???
Hili litapigiwa kelele na magazeti kisha litaisha na litazimwa kisiasa na baadae tutasahau mpaka litokezee jengine. Unyama wanaoufanya hawa jamaa hauna tofauti na ule waliokuwa wakiufanya KMKM enzi zile.Kwa hiyo hakuna jipya. Patasemwa kisha watu watasahau.

SHEIN ASEMA KITENDO CHAKUMWANGIWA TINDI KALI PADRI NI KITENDO CHA KIKATILI JE SHEIN CHA WEWE KUWAFUNGA JELA MASHEIKH WA UAMSHO JE...???


Nchini Tanganyika jijini Dar. Siku moja baada ya Padri wa Kanisa Katoliki Parokia, Mkoa wa Kusini Unguja nchini Zanzibar, Joseph Mwang’amba kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana,ameamuwa kurudi kwao nchini Tanganyika pia inasemakana kuwa atii alitishiwa kuuwawa miezi mitatu kabla ya kukutwa na tukio hilo chaa jabu mbona hakuripoti polisi na kusema kuwa kuna watu wamemtishia kuumuwa kwa mara nyengine tena tunaona kuwa ni mbinu za MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA Kutaka kuwatia ubaya Wazanzibari na kufitinisha ili kuuanzisha vita vya kidini.

Wakati Padri huyo akieleza hayo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ali Mohamed Shein, ameijia juu polisi kwa kushindwa kudhibiti matukio ya viongozi wa dini na serikali nchini humo Zanzibar, kushambuliwa kwa kumwagiwa tindikali huku akilitaka kuwakamata waliohusika na tukio hilo swali Shein hutaki akamatwe alimpiga mapanga Sheikh wa KITOPE mpaka kufa ila aliyemrushia padri ndio wakamatwe uko wapi uwadilifu wako....???

Kiongozi huyo wa dini, aliyejeruhiwa maeneo ya usoni, mikononi na kifuani baada ya kumwagiwa tindikali alisafirishwa jana na ndege ya kukodi ya Shirika la Coastal kutoka nchini Zanzibar hadi nchini Tanganyika jijini Dar es Salaam kwao alikotokea na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa ya nchi yao ya Tanganyika Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.

Shein alisema Polisi inatakiwa kuongeza nguvu za uchunguzi ili kukabiliana na matukio ya kikatili ya umwagaji wa tindikali, yanayoshamiri nchini humo Zanzibar hivi sasa.
“Hatuwezi kuviacha vitendo hivi viendelee … ni lazima Jeshi la Polisi lijitahidi kuwatafuta wahusika ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Shein.

Sheni alisema, kitendo hicho ni cha kikatili na kisichovumilika na kuongeza kuwa wahusika lazima wasakwe na kuchukuliwa hatua za kisheria tunamuliza shein kitendo cha kuwafunga Masheikh wa Uamsho bila kosa ni kitendo cha burudani...??? au pia ni kitendo cha kikatili na chakishenzi na wewe ndio umewafunga basi wewe shein katili mkubwa kuliko wa tindi kali.

Kwa upande wake, Padri, Thomas Assenga aliyefuatana na kiongozi huyo mpaka MNH, alisema siku za nyuma Padri Mwang’amba alitolewa vitisho na mtu ambaye hamfahamu wakati akienda kutoa huduma katika kituo cha wazee cha Welezo.

Alisema kabla ya kufika kituoni hapo, kuna eneo ambalo nyakati za asubuhi watu hufanya mazoezi barabarani ambapo kuna mtu mmoja alimtolea maneno ya vitisho.

“Unajua kawaida ya watu wa Zanzibar hufanya mazoezi barabarani, sasa kipindi anapita eneo hilo katika kilima, kuna mtu alimwambia atamfanyia kitu kibaya ambacho hatujui ndiyo hiki au laa,” alisema Padri Assenga na kuongeza:

Alisema Juni mwaka huu mara baada ya kupewa vitisho hivyo alikwenda kutoa taarifa kwa Sheha wa eneo hilo na. “Mara baada ya kutolewa vitisho hivyo Juni mwaka huu, alichukua jukumu la kwenda kutoa taarifa kwa mkuu wa eneo hilo (Sheha)

Akielezea tukio la kumwagiwa tindikali Padri Mwang’amba, alisema alimwagiwa saa 9:45 alasiri juzi wakati akizungumza na simu nje ya internet cafĂ© iliyopo eneo la Mlandege
Padri Assenga alisema kabla ya kumwagiwa tindikali, Padri huyo alikuwa ndani ya internet akitoa ‘photocopy’ za nyaraka. Alipokuwa akitoa ‘photocopy’ (nakala) alipigiwa simu na mtu ambaye anamfahamu hivyo ikabidi atoke nje kuongea naye, lakini alivyokuwa akiongea alimwona kijana akija na kikopo alichokishika mkononi na kummwagia na kukimbia kuelekea katika mitaa ya eneo hilo,” alisema Padri Aseenga.

Alisema mara baada ya hapo, alipelekwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, kwa matibabu baada ya kujeruhiwa usoni, kifuani na mikononi ambapo hivi sasa afya yake inaendelea vizuri.

Naye , Msemaji wa Jeshi la Polisi, nchini Zanzibar Mohamed Muhina alisema, hana taarifa hizo za vitisho na kuahidi kulifanyia kazi. “Tukio limetokea mchana kweupe na watu walikuwapo lakini wananchi wamekuwa hawatupi ushirikiano hivyo tunawaomba kutupa ushirikiano ili kukomesha vitendo hivi,” alisema Muhina.

Tukio lilivyokuwa

Akifafanua zaidi kuhusu tukio hilo, Padri Mwang’amba alisema kwamba lilitokea nje ya duka linalotoa huduma za mawasiliano ya mtandao (Sun Shine Internet Caffee) liliopo eneo la Mlandege Wilaya ya Mjini Unguja nchini Zanzibar, ndipo alipotokea kijana mmoja na kumwagia tindikali.

Padri Mwang’amba akimweleza Dk Shein kuwa hali yake ni nzuri na anaweza kuona vizuri, lakini anatarajia kupata nafuu zaidi baada ya uvimbe kupungua katika sehemu za usoni na machoni mwake.

“Hali yangu ni nzuri lakini natarajia uvimbe ukipungua nitaona vizuri zaidi,” alisema Padri Mwang’amba na kuongeza kuwa ilikuwa ni bahati kwake kwa kutoathirika sana.

Uwanja wa Ndege

Katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Kiongozi huyo aliwasili saa 4.16 asubuhi na ndege ya Shirika la Costal akiongozana na Padri Assenge.

Kiongozi huyo aliyekuwa akitembea taratibu, huku akijitahidi kujifunika mwili wake na kanga kuzuia mwanga wa Jua kutokuathiri zaidi mwili wake ulioathiriwa na tindikali.

Saturday, September 14, 2013

SHEIN AMTEMBELEA PADRI ALIYE MWANGIWA TINDI KALI MNAZI MMOJA HOSPITAL SHEIN AZZAN JE UTAMTEMBELEA...???

Padri Joseph Magamba amemwagiwa acid maeneo ya Sunshine Internet Cafe hapo Mlandege, mjini Zanzibar.
Padri Joseph Magamba baada ya kumemwagiwa tindikali maeneo ya Sunshine Internet Cafe  Mlandege, nchini Zanzibar.

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba, wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika
Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,Mjini Unguja,baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi jana jioni nchini Zanzibar, Padri alimwagiwa Tindikali alipokuwa akitoka kupata huduma ya Mtandao nchini Zanzibar

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba,akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kumwagiwa Tindikali jana na watu wasiojulikawa,katika mtaa wa Mlandege Mjini Unguja nchini Zanzibar, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,ambapo amelazwa na kupatiwa matibabu. ambayo pia ndio hospitali hii hii ambayo amalazwa Sheikh Azzan na Shein hakuja kumtembelea na bado yuko humu hospitali M/Mungu anatuonyesha vipi huyu Shein na unafiki wake Wazanzibari funguweni macho kikulocho....

Mmoja wa Ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba na,Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein, akimueleza Shein hisia zake kwa Uchungu kutokana na kitendo hicho cha kumwagiwa Tindikali na watu wasiojulikana kwamba zilichukuliwe hatua za kisheria na kukomeshwa Vitendo kama hivyo.

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,akiwafariji jamaa na wafuasi wa Padri Joseph Monesmo Magamba,waliofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikana jana jioni Mtaa wa Mlandege Mjni Unguja nchini Zanzibar je huyu Shein ashawahi kuwafariji wake na watoto na dungu na jamaa wa Masheikh walio fungwa jela wa UAMSHO au wake na watoto na jamaa wa Sheikh Nassor Bachu alifariki....???

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,akiwafariji jamaa na wafuasi wa Padri Joseph Monesmo Magamba,waliofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikana jana jioni nchini Zanzibar.

Vijana wa Umoja wa Kitaifa (VUK) kupitia Kaimu Mwenyekiti wa umoja huo ndugu Salum Abdallah Salum, wametoa tamko lao kama linavyosomeka hapa chini.
Kwa mara nyengine tena tukio la kinyama na la aibu limetokea kwa matumizi ya tindi kali dhidi ya binaadamu ambapo leo hii Kiongozi wa Kidini akiwa ni Padri Joseph Magamba, alieshambuliwa akiwa maeneo ya Mlandege, Nchini Zanzibar.
Vijana wa Umoja wa Kitaifa Zanzibar (VUK) lina laani tukio hilo kwa nguvu zote na hakuna sababu yoyote ile ya kutumia tindi kali kama silaha dhidi ya binaadamu.
VUK inasikitishwa na matendo kama haya ambayo yanazidi kujenga uadui baina ya Wazanzibari ambapo huu ni wakati wa Wazanzibari kuwa pamoja zaidi na wazuie vishawishi vyovyote vya kuwagawa.
Kama ambavyo inalaani matumizi kwa binadaamu yoyote pia inalaani matumizi ya tindi kali dhidi ya viongozi wa kidini na inasimama kuwa hakuna sababu yoyote ile ya kufanya hivyo ama kwa njia ya kisasi, mgogoro kwa sababu njia za amani hazijafungwa na kwa hakika zimezoeleka kutumika na Wazanzibari.
VUK inawataka wananchi kushikamana, lakini hasa vijana wasikubali kuingizwa katika matukio kama hayo lakini pia wasishabikie na zaidi wasiwafiche waovu kama hawa kwa kuwatolea ripoti kwa mamlaka za ulinzi na usalama.
VUK inawataka wananchi kujua matukio kama haya sio tu ya hatari, lakini pia wanachafua jina na amani ya nchi na kwa hivyo wakati huu ndio muwafaka kwa kila mwananchi kuwa macho na kuwa mlinzi wa watu ambao wanataka kuiharibia sifa na jina jina la nchi yetu ya Zanzibar.
VUK inalitaka Jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa itoe majibu ya matukio kama haya ambayo sasa yanachafua akhlaki na utengamano wa Wazanzibari, na majibu hayo tunayataka leo kabla ya kesho maana kuanzia kesi ya Sheikh Fadhil Soraga, Sheha wa Tomondo na pia vijana wawili wa Kiingereza ambao ni Katie Gee (18) na Kirstie Trup (18).
VUK inavitaka vyombo hivyo virudishe imani ya Wazanzibari ambao wamezoea jamii inayoishi kwa kupendana na kusaidiana na ambapo sasa inafisidika kwa kuchukina na unyama.
Pia VUK inatoa wito kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutumia kila aina ya uwezo iliyonayo, na kwa umma kuona uwezo huo unatumika, kuhakikisha kuwa wahusika wanakamatwa na kuchukuliwa hatua.
Vilevile SMZ ihakikishe inadhibiti upatikanaji na usambazaji wa tindi kali, ambayo hivi sasa inaonekana kupatikana kwake ni rahisi na matumizi yake ni hatari kwa umma.
Kila mtu ajue na aone kuwa anaweza kuwa hatarini kushambuliwa kwa silaha hii na hivyo wajibu wa kuchukia na kuchukua hatua ni wa kila mtu lakini hasa vijana ambao wao huwapo mitaani saa zote.
VUK ina mpa pole Padri Joseph Magamba na inamuombea Mungu ampe afueni ya haraka na tunaungana na jamaa na waumini wake katika kipindi hiki kigumu.

Friday, September 13, 2013

JK AKITIA SAINI TU JI SWADA LA KATIBA FEKI NDIO ISHA PITA JE JK NA SHEIN NI NINI NIA ZENU KULAZIMISHI HILI JISWADA..???

Rais Jakaya Kikwete Ali Shein
Wakati Rais Jakaya Kikwete wa nchi ya Tanganyika akisubiriwa asaini Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa 2013 ili kuwa sheria kamili, wasomi, wanasiasa na wanaharakati wamemshauri asifanye hivyo, wakisema itapatikana Katiba Mpya isiyo na tija.

Wananchi hao kutoka nchini Tanganyika na nchini Zanzibar walisema kwa nyakati tofauti kuwa, Rais Kikwete wa nchi ya Tanganyika anatakiwa kutumia busara ya kushauriana na kupata maoni ya watu wa kada mbalimbali ili kujua nini kifanyike, kabla ya kuamua kusaini muswada huo.

Mjadala wa muswada huo uliopitishwa Ijumaa iliyopita na wabunge wengi wakiwa wa CCM chama cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA, ulizua tafrani bungeni iliyosababisha Kiongozi wa Upinzani Bungeni huko nchini Tanganyika, Freeman Mbowe na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) kutolewa nje na askari. Katika tafrani hiyo iliyozuka huko nchini Tanganyika, baadhi ya wabunge wa upinzani walirushiana makonde na maofisa usalama, huku wabunge wote wa upinzani, isipokuwa Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema, wakiususia.

Wapinzani walisema Serikali iliubadili kwa nguvu muswada huo kwa kuondoa maoni muhimu ya wadau, pia walilalamikia kitendo cha wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge kutokwenda nchini Zanzibar kuchukua maoni ya wananchi wa nchi ya Zanzibar ambayo ndio upande huo wa muungano na nchi ya Tanganyika katika Muungano huu feki.

Wasomi
Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanganyika (UDSM), Gaudence Mpangala alisema mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya ulikuwa ukienda vizuri… “Lakini umebadilika vibaya, tena katika kipindi muhimu. Kupitishwa kwa muswada na kusubiri saini ya Rais kunaweza kuleta Katiba Mpya, ikawa siyo ile ambayo Watanganyika wanaitarajia.” Alishauri busara itumike kabla ya kusainiwa kuwa sheria kamili.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tunguu nchini Zanzibar, Ali Uki alisema hakuna haja ya muswada kukimbiliwa kusainiwa kwani katiba ni mali ya wananchi na kuupitisha ili uwe sheria bila kuyashirikisha makundi mengine, kutaendeleza malalamiko na kurudisha nyuma malengo ya kupatikana kwake. Uki alisema upo wasiwasi kwamba Katiba Mpya itatokana na utashi wa kisiasa badala ya matakwa ya wananchi, jambo ambalo alisema linaweza kuathiri malengo ya kuandikwa kwake.

“Utashi wa vyama umeanza kujitokeza, huku chama kimoja kikiwa na uwakilishi mkubwa kwenye Bunge hilo lililokuwepo nchini Tanganyika, chama kimoja kina uwakilishi wa asilimia 72 katika Bunge la Katiba,” alisema Uki.
Alikosoa Kifungu cha 8 na Kifungu kidogo cha 4 na 5 cha muswada huo kwamba vina kasoro kwa kuruhusu wabunge wa Bunge la Katiba kufanya uamuzi kwa wingi wa kura badala ya kutumika utaratibu wa theluthi mbili kutoka nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika.

Profesa mwingine wa UDSM, Chris Peter Maina alisema ikiwa kuna nia njema ya kupata Katiba bora, lazima suala la uwiano wa idadi ya wabunge katika Bunge la Katiba litazamwe upya.
“Rasimu ya pili ikishatolewa na kukabidhiwa kwa Bunge la Katiba, kazi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ndiyo itakuwa imekwisha. Sasa inakuwaje Bunge linajadili Rasimu ya Katiba huku waliyoiandaa hawapo, hiki kitu kinashangaza,” alisema Profesa Maina.

Mhadhiri Mwandamizi wa chuo hicho, Dk Frank Tilly alisema hakuna umuhimu wa kukimbiza muswada kutiwa saini wakati kuna mambo mengi ya msingi ambayo hayajapatiwa ufumbuzi… “Watanganyika hawajakubaliana kwa pamoja, ili jambo liwe zuri ni lazima pande mbili au zaidi zenye masilahi na kitu husika zikubaliane, sasa hilo halijafanyika tunakimbilia wapi?” alihoji.

Tuesday, September 10, 2013

PELE WA NCHI YA ZANZIBAR MAJHAM NI ALMASI ISIYO THAMINIWA NCHINI MWETU ZANZIBAR

Timu ya Zanzibar kwenye Kombe la Gossage la mwaka 1952.
 

Timu ya Zanzibar kwenye Kombe la Gossage la mwaka 1952.
 
Na Hamza Z. Rijal. WENGI wanamjua kwa jina lake la mkato: Majham. Kuna wanaomwita ‘Pele wa nchi ya  Zanzibar’.  Angelikuwa amezaliwa Ulaya, Marekani au hata Amerika ya Kusini hii leo angelikuwa anaenziwa.  Hakujaaliwa bahati ya akina Boby Charlton, Geoff Hurst, Johan Cruyff, Platini, Pele, Blokhin, Hadji, Latto, Tostao, Gerson, Romario.
Angelijaaliwa bahati hiyo basi angelikuwa fahari ya nchi ya  yake Zanzibar  kwani zama zake Majham alikuwa amebobea katika michezo miwili — soka na hoki (mpira wa magongo).  Viwanja vya soka vikimjua, viwanja vya hoki vikimtambua.
Siku hizi ukimtafuta Majham hutompata kwenye viwanja vya soka wala vya hoki.  Kwanza vya hoki haviko tena ndani ya nchi ya Zanzibar kwani hoki haichezwi tena nchini mwetu.  Mchezo huo ulipigwa marufuku baada ya Mapinduzi ukionekana kuwa ni spoti ya kibwanyenye.
Siku hizi ukimtaka Majham itakubidi wende Mchangani. Zikate kona mbili tatu hadi nyumbani kwake. Ukibahatika utamkuta amekaa barazani. Saa zote anakuwa mpweke hapo barazani kwake akitafuta rubaa la washabiki wa spoti wa kuweza kuzungumza naye. Ingawa ni mpweke hataki kujinasibisha na chochote kile.
Hii leo Majham — jina kamili Abdul Majham Omar — amekuwa mfano wa lulu iliyotupwa. Pamoja na uzee, ana umri wa miaka 79,  Majham siku hizi ni dhaifu, ganzi ya miguu inamsumbua na haoni sawasawa. Mwandishi aligundua kitu kimoja cha ki-Majham pekee: kinapotokea kitu katika mazungumzo kinachomkuna husema ‘awii’.
Mwandishi: Je unakumbuka mwaka uliozaliwa?
Majham: Miye sikumbuki lakini labda uwaulize wale niliocheza nao watu kama kina Sayyid Ali Soud, lakini ninachoweza kukisema kuwa ninafahamu fika kuyajuwa yaliokuwa yanaendelea kwenye Vita Vikuu vya Pili  wakati huo ni mtoto wa makamo naenda chuoni kusoma Qur’an.
Mwandishi: Itakuwa labda una umri wa miaka 9 hivi wakati huo wa Vita Vikuu vya Pili vya dunia?
Majham: Zaidi, labda miaka 11 au 12.
Mwandishi: Nikifanya mahesabu unafikia umri wa miaka 79.
Majham: Nakubaliana na wewe.
Mwandishi: Nielezee maisha yako kwa mukhtasar?
Majham: Mimi ni mzaliwa wa mtaa wa Malindi na ndipo nilipokulia. Nalianza masomo yangu ya Qur’an chuo cha Maalim Jeledi.  Nilisoma hapo mpaka nikahitimu na huku nikiendelea na masomo ya msingi katika skuli ya Gulioni.  Naikumbuka Gulioni na nina masikitiko kuwa jengo la skuli hiyo halipo. Nawakumbuka baadhi ya walimu wetu ambao walikuwa sio walimu wenye kusomesha lakini walikuwa ni wazazi wetu. Unaposomeshwa na Maalim Burhan au Maalim Buda au Maalim Badi unajikuta kuwa upo na sehemu ya wazazi wako. Sijabahatika kusoma na kufika mbali, nalimaliza masomo hapo Gulioni skuli nilipofika chumba cha 5.
Mwandishi: Baada ya masomo ya msingi ulikuwa unafanya nini?
Majham: Zamani sio leo, kila mtu alikuwa ni mzee.  Nilitafutiwa kazi [na wazee] na kupata kazi sehemu ya Umeme pale Public Works Department (PWD) na nilifanya kazi hapo kwenye miaka ya 1950 hadi kufikia Mapinduzi. Halafu nikawa nafanya kazi katika Shirika la Umeme na nimefanya kazi hapo hadi kufikia kustaafu.
Mwandishi: Baada ya kuzungumzia maisha yako kwa jumla hebu tugeukia michezo. Kitu gani kilikuvutia kucheza soka, hoki (mpira wa magongo) na kriketi (cricket)?
Majham: Nimeanza kucheza soka nikiwa na umri wa miaka sita na nilikuwa hodari wa kupiga chenga tangu umri huo. Ninapocheza na watoto wenzangu kila mtu huvutiwa namna ninavyochukua mpira na kuwapiga chenga wenzangu. Nilipokuja kuona filamu ya Garincha pale Ofisi ya Filamu ya kina Mohammed Kassim, hapo ndipo ikawa nikichocheo kikubwa kwangu kuwa nakokota mpira na kuhesabu wachezaji, ingawa Mwalimu wetu ‘Mr. Mazal’, huyu ni Ahmed Iddi Mjasiri. alikuwa hapendi kumuona mtu anakaa na mpira kwa muda mrefu.
Mwandishi: Majham wewe ni mzaliwa wa Malindi, verejee ukachezea Vikokotoni?
Majham: Ukweli miye sipendi mambo ya kifahari wala kujiweka mbelembele. Miye mambo yangu ni kutopenda mambo ya kifakhfakh. Kwa sababu hizo ndio nikenda  Vikokotoni, ingawa nilicheza muda mfupi katika timu inayoitwa Hadhrami.  Haya mambo ya Hadhrami yawache kwani yana hikaya refu.
Mwandishi: Kwa nini isiwe Kikwajuni, Mwembeladu, Miembeni?
Majham: Miembeni au Kikwajuni zama hizo kulikuwa ni sawa kwa leo kama upo maeneo ya Mwanakwerekwe,. Doooh, ingekuwa taabu kwangu.
Mwandishi: Taabu ya nini?
Majham: Uwwih, alaaa, [kacheka sana bila ya kutaka kuendeleza].
Mwandishi: Ulianza kuchezea Gossage mwaka gani?
Majham: Nakumbuka nilianza kucheza Gossage 1952 nakupa na hiyo picha uone .  Nilikuwa na kina Mzee Mwinyi(Mpiringo) Mzee Ahmed Islam, Seif Rashid, Maulidi Mohamed (Machaprala) na wengineo. Tulicheza Nairobi tulikuwa washindi wa pili. Tuliwafunga Waganda na Tanganyika, tulilala kwa Kenya na ukweli Kenya ikitupa tabu sana, kwani wakitumia nguvu za hali ya juu na sisi tulikuwa na wachezaji wachache ambao wakitumia nguvu.  Sisi mchezo wetu ni dama, mfano wa Brazili. Unaweka karata kwenye bao, unaanza nyuma unafika kati, unachezewa kidogo, unapelekwa wingi, unawekwa kati, haooo, tunarudi, huo ndio mtindo wetu. Kenya wao pasi tatu wako golini.
Kutoka hapo niliendelea kuchaguliwa kwenye timu ya Gossage mpaka mwaka wa 1968 ndio nikamalizia kucheza timu ya taifa. Nimecheza na kina Kassim bin Mussa, Sururu, Khalid Kessi, Boti mkubwa wa Malindi, nikaja nikacheza na vijana kina Boti mdogo, Abdimout Ajmi, Saad, Hijja Saleh, Seif Rashid, Seif Nassor (Mshumaa).  Kisha nilikuwa na fowad nikistaladha kucheza nao, huku Ahmada Mwanga, huku Mossi Kassim, Mkweche kushoto, Ahmada Mwanga na mfalme wa hewani Mohammed Kassim, uwwih, alaaa. Hapo nakwambia kigoma tukikipiga, waulize Warusi waliokuja na kuzifunga timu zote za Afrika Mashariki na kuja hapa tukenda suluhu nao, Warusi hawajaweza kuamini, siku hiyo mpate Ahmada Mwanga na Mkweche watakuelezea kigoma tulivyokipiga, ilikuwa kila mtu anazungumza juu ya game hii.

Timu ya Zanzibar kwenye Kombe la Gossage la mwaka 1962.

 
 
Timu ya Zanzibar kwenye Kombe la Gossage la mwaka 1962.
 
Mwandishi: Mchezo gani unaoukumbuka na hutousahau?
Majham: Gossage Zanzibar mwaka wa 1966, timu yetu ilikuwa 1. Bobea. 2. Sleiman Amour 3. Tindo 4. Ahmed Himidi London 5. Majham 6. Kitwana Rajab 7. Mossi Kassim, 8.Mohammed Kassim. 9. Peter 10. Ahmada Mwanga 11. Maalim Seif Nassor (Mshumaa). Tulifungwa na Kenya, tukalala kwa Tanganyika na tukenda suluhu na Uganda.  Natamani kungekuwa na filamu yake ungeona namna tunavyocheza. Yule kocha wa Tanganyika aliwahi kusema lau ningeipata timu hii ya Zanzibar ningekuwa juu.
Mwandishi: Tuzungumzie hoki (mpira wa magongo) na kriketi (cricket).
Majham: Kriketi sijacheza. Nilijaribu nikaona mchezo haunifai, kwani unachukua muda mrefu, lakini mpira wa magongo nilicheza baada ya kushauriwa kuwa nitasaidia hoki ambayo ilianza kupotea baada ya Mapinduzi. Nikasema kuwa nipo tayari lakini naogopa kucheza mbele, nikapendekezwa nicheze golikipa na nikakubali. Ukipa wangu ulikuwa nachanganya na utaalamu wa soka nikawa natoa pasi nacheza kijanja, nikapata sifa nikawa nachaguliwa timu ya taifa miye, kijana Islam Ahmed Islam nimecheza mpira na babake, halafu huyu Daktari Mohamed Jidawi tukicheza pamoja timu ya Taifa ya Tanzania.
Umetaja kriketi, nikipenda kuwaangalia vijana wawili wazalendo wakichezea Comorian, Zaghalouli na Ahmed Himidi. Wakikutana hao, basi utaona raha. Zaghalouli anapiga mipau, mipira kaokote jumba la Makumbusho, lakini Ahmed Himidi kutwa yupo kiwanjani anazuia tu, akiwapa taabu kwelikweli warushaji mipira.
Mbona leo umeazimia kutaka kuniliza? Leo wapi… nchi hii watu wakicheza futuboli, hoki, kriketi, tenis hata gofu. Michezo yote imekufa isipokuwa soka. Kuna wachezaji kama Ahmed Himidi London akicheza michezo yote hio, sio kucheza tu, lakini akichaguliwa katika timu ya taifa kwa kwa kile mchezo.
Mwandishi: Una nyongeza?
Majham: Nyongeza ninayo. Kwanza mbona hujaniuliza kuwa timu ya kwanza kucheza kombe la klabu la Afrika ilikuwa ni Cosmopolitan chini ya Mwalimu Mansour Magram. Tulicheza na timu ya Somalia tulikwenda suluhu 1-1 pale kiwanja cha Ilala Dar-es-Salaam na tukashindwa kwenda Somalia kwa mbinu za FAT kutotaka twende. Silisahau hili. Tupo klabu tunasubiri safari na mabegi yetu tunaambiwa hamna safari. Tulikuweko pale kina Abdimout, Msuba, Msomali, Emil Kondo, Marandu, Abuu, Kitwana Douglas, Masiku, Rajabu, Iddi Balozi, Makanda. Tulikuwa tuelekee Somalia zikafanywa hila na haya yanakwenda na kujirejea.
Jengine, kama unavyoniona nipo mgonjwa. Nashukuru nimepata kuonana na Rais [Ali Mohamed Shein] nikaambiwa nitapatiwa matibabu nje ya nchi, lakini hadi leo hakuna lilofanyika na hali yangu ya kiafya inakwenda chini. Aidha namshukuru Waziri Mohammed Aboud na ile kamati ya mtoto wa muuza magazeti [Farouk Karim] na wewe mwandishi naambiwa umo, kufanyisha mchango wakuweza kunisaidia nashukuru sana, sana.
Wito wangu Serikali ijuwe sisi tulilitumikia Taifa basi tuangaliwe kama wenzetu huko Ulaya na kwengineko. Tumetupwa useme kanda la usufi, puuuu!