Sunday, September 15, 2013

POLISI MUNAWAJUWA WANAO MWANGIA WATU TINDI KALI NCHINI ZANZIBAR ACHENI KUZUGA WATU


Huenda kuna watu wanashangaa inakuwaje polisi hadi leo kushindwa kuwakamata wahalifu wanaohusika na kuwamwagia watu tindikali na vitendo vyengine viovu. Hili halishangazi kutokana na utendaji wa kazi wa polisi wa nchi hii ya Zanzibar.
Kwanza polisi walio wengi wanahusika na baadhi ya vitendo vya uhalifu kama hivi karibuni wameweza kuuiba upanga wa kipolisi aliokabidhiwa kamanda wa polisi wa nchi ya Zanzibar. Ilikuwaje kitu cha thamani kama hicho kuweza kuibiwa kirahisi..???  Pia uhalifu wanaoufanya polisi kwa kupiga watu kama wanyama nani ambae hajawahi kushuhudia..???

Siku za nyuma polisi hawakuwa na tabu kuweza kuwakamata angalau washukiwa au masikini za Mungu ambao hubambikiwa kesi.Wafuasi wengi wa CUF walikumbwa na kukamatwa kutokana na fitna za majirani zao CCM ambao waliwaambia polisi kuwa hao MACUF ndio wanaowashuku hapo mtaani kufanya vitendo vyote vya hujuma. Hili kwa sasa kidogo lina tabu.Maana Wazanzibari wameungana na kuwa kitu kimoja hakuna tena hao MACUF wala hao MACCM. isipokuwa hao wahafidhina na vitimbakwiri wa MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA tu ndio bado wamo.

Ingekuwa kuna kiongozi wa UAMSHO ambae hajakamatwa basi polisi wangekuwa kila akimwagiwa mtu tindikali basi wangekamata mmoja mmoja. Lakini kwa bahati mbaya wote washawakamata na kuwasweka jela. Nadhani wanatamani wawatoe ili wawe wanawakamata kwa design hii lakini wapii. Polisi hupata tabu sana kuwakamata wafuasi wa CCM wanaposhukiwa kufanya uhalifu. Hili haliuziki kwa wakubwa wa polisi hata kwa mzizi wa muarubaini. Alipouliwa yule padre kule Beit al Ras kulikuwa na kila aina ya makeke kuwa mhusika atakamatwa kwani maafisa waliobobea wa polisi kutoka nchi ya Tanganyika na hawa wetu hapa nchini Zanzibar mbumbumbumatari wakisaidiwa na FBI wanafanya uchunguzi. Kilichotokea ni kuwa FBI waliondoka kimya kimya baada ya kuona polisi hawakuwa tayari kutoa ushirikiano wa kweli. Baadae ikawa anatafutwa mtu abambikiziwe kesi ili angalau hili jambo lizimike kwanza. Kwa hiyo polisi katika pekura pekura zao wakaona video ya Bwawani ya jamaa aliesema kuwa wako tayari kuunda vikundi vya msituni kupinga muungano.
Baada ya kumuona wakamchora picha yake kisha wakaitangaza kila mahali(ilhali wanamjua huyo jamaa) na kusema atakaesaidia kukamatwa kwa huyo jamaa atapata donge nono.Wakaishia kumkamata wenyewe pale Kariakoo na donge nono wakalichukuwa wenyewe na kulila na kumuacha Jamaa yuko Kiinuamiguu bila hatia lakini imesaidia polisi kulizima hilo na kula donge nono.

Walikomwagiwa tindikali wale kina dada wa UK kukazuka zogo la wakuu wa nchi na polisi kulaani na kusema kuwa waliohusika watakamatwa haraka sana. Hiyo kisiasa ilisaidia kuzima hilo jambo.
Na hivi leo baada ya uhalifu huo kurudiwa tena kwa kumwagiwa tindikali padre mwengine, wakuu wa nchi na wa polisi wanaruka wakitoja kulaani na kuhimiza waliohusika na unyama huu wakamatwe lakini polisi wamechachiwa. Wanazo fununu za kujua waliohusika lakini hawana ubavu wa kuwakamata. It is very simple! Wanaohusika ni watu ambao hawataki nchi ya Zanzibar iwe na mamlaka kamili. Kwa hiyo wanawatishia watu wenye asili ya nchi ya Tanganyika ili ikitokezea kupiga kura ya maoni wakatae mfumo wa serikali tatu au chochote kupelekea nchi ya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili. Sasa niambie ni polisi gani mwenye ubavu wa kuwakamata watu hawa...???
Hili litapigiwa kelele na magazeti kisha litaisha na litazimwa kisiasa na baadae tutasahau mpaka litokezee jengine. Unyama wanaoufanya hawa jamaa hauna tofauti na ule waliokuwa wakiufanya KMKM enzi zile.Kwa hiyo hakuna jipya. Patasemwa kisha watu watasahau.

No comments:

Post a Comment