Sunday, October 13, 2013

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA NCHI YA ZANZIBAR ABUBAKAR KHAMIS BAKARI ASEMA NCHI YA ZANZIBAR HAIKUSHIRIKISHWA MUSWADA WA KATIBA


WAZIRI wa Katiba na Sheria wa wa nchi ya  Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari ameliambia Baraza la Wawakilishi kwamba muswada wa mabadiliko ya Katiba, uliyopitishwa na Bunge la nchi ya Tanganyika na kuzusha malumbano kwa Wabunge wa upinzani, wa nchi ya Zanzibar haikushirikishwa katika marekebisho ya vifungu 12 vilivyoingizwa kinyemela  baadaye.
Abubakar alisema hayo wakati alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu ushirikishwaji wa nchi ya  Zanzibar katika mchakato wa marekebisho ya Katiba, ambao katika siku za hivi karibuni umezusha malumbano zaidi kwa kambi ya upinzani.
Mwakilishi wa Mji Mkongwe, Unguja Ismail Jussa (CUF), alimtaka Waziri wa Katiba na Sheria kufafanua kuhusu kauli zinazotofautiana kuhusu nchi ya  Zanzibar, kushirikishwa au kutokushirikishwa katika mchakato wa Katiba.
Akifafanua, Waziri Bakari alisema awali muswada huo uliletwa serikalini na kufanyiwa marekebisho katika maeneo ya mambo manne ambayo nchi ya  Zanzibar, iliyatolea mapendekezo yake na kupelekwa mbele.
“Marekebisho ya awali yaliletwa serikalini…ambapo mimi binafsi nilitoa mapendekezo kwa niaba ya serikali katika maeneo manne,” alisema Waziri Bakari.
Hata hivyo, alisema ilipofika mwezi wa Mei, kulikuwa na utaratibu mwingine wa kuongeza jumla ya vifungu 12 ambavyo hivyo nchi ya  Zanzibar, haikushirikishwa wala haikuonyeshwa:
“Mimi Abubakar Khamis Bakari…Waziri mwenye dhamana ya Katiba na Sheria katika marekebisho ya muswada huo ambapo jumla ya vifungu 12 viliingizwa…sisi nchi ya  Zanzibar hatukushirikishwa,” alisema Waziri Bakari.
Alisema alifanya juhudi za kutafuta muswada huo uliyopitishwa Bungeni na kuona mabadiliko hayo ambayo nchi yetu ya  Zanzibar, haikushirikishwa pamoja na kuingizwa kwa vifungu 12 vipya ndani ya Katiba.
Waziri huyo alisema Septemba 13, mwaka huu alimuandikia barua Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balosi Seif Ali Idd ambaye naye, aliandika barua kwa ofisi ya Waziri Mkuu, lakini hakuna majibu yaliyotolewa.
Waziri Bakari alisema amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo kwa kauli mbalimbali zenye utata, ambapo baadhi ya watu pamoja na viongozi wa vyama vya siasa, wamekuwa wakipotosha ukweli huo katika majukwaa ya siasa.
Zanzibar kwanza Zanzibar kwanza Zanzibar kwanza jino kwa jino mpaka kieleweke.

No comments:

Post a Comment