Saturday, November 23, 2013

SOTE WAZANZIBARI TUNAITAKIA TIMU YA NCHI YETU YA ZANZIBAR HEROES KILA LA KHERI


TIMU YA TAIFA YA NCHI YA ZANZIBAR HEROES WAKISHANGILIA BAO WALILO FUNGA

Nchi ya Tanganyika na Nchi ya  Zanzibar zimetangaza vikosi vya timu za Taifa zitakazoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji mwaka huu.
Michuano ya Kombe la Chalenji inayoshirikisha mataifa ya nchi za Afrika Mashariki na Kati imepangwa kufanyika Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12.
Timu hizo ambayo ya nchi ya Tanganyika ikiwa chini ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen na Timu ya nchi ya Zanzibar ikiwa chini ya Kocha wake, Salum Bausi ziko kambini zikijinoa kwa mashindano hayo.
 Zanzibar Heroes ya nchi ya Zanzibar na Kilimanjaro Stars ya Tanganyika  zimepangwa katika makundi tofauti katika michuano hiyo ambayo timu hizo zina uzoefu mkubwa.
Ikiwa  Zanzibar Heroes ni muanzilishi wa michuano hiyo ni matumaini yetu Wazanzibari  Zanzibar Heroes itatuwakilisha vyema na kurudi na kombe nyumbani nchini Zanzibar.
Litakuwa jambo la furaha iwapo kwa mara ya kwanza zote zitafanikiwa kucheza mchezo wa fainali kwani zitawahakikishia Watanganyika na kwa Zanzibar pia kisha katika mchezo wa fainali tuwapige bao Watanganyika na kombe litakuja nchini Zanzibar itakuwa furaha ya aina yake.
Zote mbili zina historia ya kutwaa kombe hilo kwa hiyo hakuna kitu cha ajabu kwa safari hii kurudia na kuiwezesha Zanzibar kuwa na heshima katika ukanda huu au Tanganyika kuwa na heshima katika ukanda huu.
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mashindano hayo kuanza Kenya ni wakati mwuafaka kwa Shirikisho la Soka la Tanganyika (TFF) na Chama cha Soka cha nchi ya Zanzibar (ZFA) kuhakikisha kwamba wanaziandaa vizuri timu hizo.
Vilevile ni muhimu kwa wadau mbalimbali wa mpira wa miguu nchini kuzisaidia timu hizo ili zisiwe na matatizo yoyote wakati zinakabiliwa na mechi ngumu za mashindano hayo.
Makocha Poulsen na Bausi nao wana kazi ya ziada ya kuhakikisha kwamba wanazinoa timu hizo na kuzipa makali ya kuweza kuhimili kishindo cha mashindano hayo makubwa kwa Afrika Mashariki na Kati.
Lakini, kazi kubwa zaidi iko mikononi mwa wachezaji wa timu hizo mbili ambao ndiyo wenye jukumu kubwa uwanjani la kuhakikisha kwamba nchi ya Zanzibar  inang’ara kwenye mashindano hayo na  Tanganyika inang’ara kwenye mashindano hayo pia.
Jambo la kwanza na la muhimu sana ni kwa wachezaji wote kuonyesha nidhamu ya hali ya juu katika kipindi hiki cha maandalizi na katika kipindi cha mashindano hayo. Nidhamu na kusikiliza na kufuata maelekezo ya makocha wao ndizo silaha kubwa zitakazowasaidia wachezaji hao na kuziwezesha timu zao kufanya vizuri katika mashindano ya Kombe la Chalenji.
Wachezaji wanapaswa pia kuonyesha uzalendo wa hali ya juu kwa kujituma kwa nguvu zao zote katika michezo yote watakayopambana katika mashindano hayo yanayofanyika Kenya.
Iwapo wachezaji watakuwa makini na kucheza kwa bidii kubwa huku wakiweka mbele mapenzi ya nchi zao bila shaka yoyote watarudi nchini Zanzibar wakiwa na furaha kubwa kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Ni vyema wachezaji wa timu zote mbili wakajiweka katika mazingira ya ushindani wakijua kwamba wanakwenda Kenya kupambana na timu zenye uwezo kwa hiyo wajiandae vizuri.
Wakati tunazitakia kila la kheri Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes itakuiwa furaha kubwa kwa Zanzibari au Watanganyika iwapo moja ya timu hizo italileta Kombe la Chalenji katika ardhi moja ya nchi hizi mbili ima nchini Zanzibar au nchini Tanganyika.

Wednesday, November 20, 2013

SHEIKHA AZZAN KHALID HAMDAN AMEREJEA NCHINI ZANZIBAR AKITOKEA NCHINI INDIA ALIKOKWENDA KWA JILI YA MATIBABU

SHeikh Azzan akiwa na familia yake nyumbani kwake Mfenesini, Zanzibar
 SHEIKH  AZZAN AKIWA NA FAMILIA YAKE NYUMBANI KWAKE HAPA MFENESINI NCHINI ZANZIBAR  

Nchini Zanzibar
Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu nchini Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Azzan Khalid Hamdan amerejea nchini Zanzibar akitoke India alikokwenda kwa ajili ya matibabu na kutakiwa kurejea tena Desemba 15, mwaka huu .
Sheikh Azzan aliaachiwa kwa dhamana ya matibabu akiwa miongoni mwa washtakiwa kumi waliofunguliwa kesi atii ya uharibifu wa mali na kuhatarisha Usalama wa Taifa, kesi ambayo inaendelea Mahakama Kuu nchi ya  Zanzibar
Akihojiwa na muandishi  nyumbani kwake Mfenesini nchini Zanzibar, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Sheikh Azzan alisema baada ya kufanyiwa uchunguzi wa figo, madaktari bingwa wamemtaka kurejea tena nchini India Desemba 15, mwaka huu kwa ukaguzi wa mwisho wa afya yake.
Sheikh Azzan alirejea nchini Zanzibar Novemba 8, mwaka huu baada ya kukamilisha matibabu yake katika Hospitali ya Manipal nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu na baadaye kupumzika Muscat Oman kwa muda wa wiki kabla ya kurejea hapa nchini  Zanzibar.
Akitoa tathmini ya maendeleo ya afya yake, Sheikh Azzan alisema alipofika Hospitali jambo la kwanza alifanyiwa uchunguzi na kuonekana ana matatizo makubwa matatu moja likiwa ni kupatikana na mawe 17 katika figo zake zote mbili, alitibiwa kwa mionzi na kuvurugwa mawe.
Sheikh Azzan anasema “Walinipiga mionzi katika figo langu la kwanza na kisha wakanipiga la pili na kuyavuruga mawe yote na kutoka mwilini kwa njia ya mkojo,”
Katika uchunguzi wa daktari aliofanyiwa, Sheikh Azzan alipatikana akiwa na tatizo la maumivu ya kichwa ambapo awali alikuwa akilalamika kuwa na maumivu makali pamoja na kukosa usingizi kwa muda mrefu.
Alisema daktari alimshauri apunguze matumizi ya simu ya mkononi (mobile phone) ili kujaribu kutuliza hali hiyo pamoja na kumpa dawa za kupunguza maumivu kwa muda wa miezi miwili mfululizo.
Akitaja tatizo la tatu, Sheikh Azzan alisema madaktari waligundua ana michubuko na vidonda katika tumbo na kutakiwa katika hatua ya awali kujipangia mlo na kuacha kula baadhi ya vyakula vikiwamo vile vyenye virutubisho vya Protein kama nyama ya ng’ombe, kuku, samaki, zabibu na maboga.
Alipoulizwa kama atarejea rumande Sheikh Azzan alisema, hakuna masharti ya kutakiwa kurejea gerezani lakini alisema Jaji Mkuu wa nchi ya Zanzibar alisema ripoti na uamuzi wa daktari utaheshimiwa kulingana na tatizo la kiafya linalomkabili.
“Sijapewa muda maalumu wa kurudi gerezani, kauli ya Jaji Mkuu, madaktari ndiyo watakaoshauri kama nipumzike kwa muda gani kabla ya kurejeshwa rumande na nina imani ripoti itakapowasilishwa watajadiliana,” aliongeza kusema Sheikh Azzan. 

Friday, November 15, 2013

HAWA NDIO MARAISI WAZI WA NCHI ZA AFRIKA WANAO IBAA PESA ZA AFRIKA NA KUZIFICHA USWISI, JERSEY, BAHAMAS N.K.

The_African_Presidents
UROHO na UTAPIA fedha unawafanywa na watawala wetu wacheze na moto. Tunachoshuhudia siku hizi ni jinsi watawala wetu na matajiri wetu wanavyosaidiana kujitajirisha bila ya kikomo huku mamilioni ya wananchi wenzao wakizidi kuwa mafukara,masiki,mayatima ndani ya nchi yao wasijuwe wapi paa kukimbilia.
Utajiri, tena utajiri mkubwa, umeangukia kwa njia za haramu katika mikono ya watu wachache sana nchini humu. Si dhamiri yangu kuwazungumza wafanyabiashara waliotumia ubunifu wao wa kibiashara kujipatia utajiri mkubwa kwa njia za halali. Hawa tunaweza kuwatia kwenye kiganja kimoja.
Wala siwazungumzi wafanyabiashara wa kawaida wanaohangaika usiku na mchana kujipatia faida katika biashara zao wakiwa, kwa mfano, ama na maduka au magari ya kusafirisha abiria,wauza mitumba,nyanya,mama ntilia n.k.
Ninaowakusudia ni ile mitajiri, iliyo mijivi au ni ite majizi mengwegwe, inayotumia ulaghai kulighilibu taifa kwa manufaa yao wenyewe bila ya kujali madhara makubwa wanayowasababishia walio chini katika jamii.
Ufisadi wote huu unarahisishwa na mfumo wa uchumi tulionao. Huu ni mfumo unaotumia kisingizio cha utandawazi na uchumi wa soko huru ili kuwapururia majambazi waweze kulinyonya taifa hili.  Mfumo huu ni mfumo mwovu.
Tumeona katika miaka na miezi ya hivi karibuni jinsi mfumo huo ulivyozusha taharuki na mahaniko katika nchi mbalimbali zikiwa pamoja na zile zinazotajwa kuwa ziko safu ya mbele miongoni mwa nchi zilizoendelea.
Chumi za nchi hizo zimetikiswa na zikatikisika kwa sababu mwingi wa utajiri wao umo mikononi mwa waroho wachache katika nchi hizo. Na wao ndio wenye kuzusha mfarakano na mpambano baina ya matajiri na wafanyakazi.
Ukweli wa mambo kwa sasa wanauhisi zaidi walio maskini na hata walio katika tabaka la kati katika nchi za Ulaya ya Magharibi na Marekani.  Wanaoishi katika nchi hizo wanaona jinsi hali za uchumi katika nchi hizo zilivyodidimia, jinsi wasio na ajira wanavyohangaika bila ya mafanikio ya kupata ajira, jinsi bei za bidhaa zilivyoruka, jinsi huduma za afya na za kijamii zilivyoanguka na jinsi maisha kwa jumla yalivyo magumu.
Mwezi Septemba mwaka jana taasisi moja ya kiuchumi mjini Washington iitwayo Economic Policy Institute ilichapisha takwimu za mapato ya wafanyakazi wa Marekani.  Kwa mujibu wa takwimu hizo mapato ya wastani ya mfanyakazi wa kiume wa Marekani aliyeajiriwa kikamilifu mwaka 2011 yalikuwa madogo yakilinganishwa na mapato aliyokuwa akipata mfanyakazi kama huyo mwaka 1973.
Takwimu hizo pia zimeonyesha kwamba asilimia 74 ya mwongezeko wa utajiri baina ya mwaka 1983 na 2010 uliwanufaisha asilimia 5 tu ya Wamarekani ambao ndio matajiri wakubwa kabisa.  Hali za asilimia 60 ya wasiojiweza zilizidi kudidimia.
Hali kama hiyo haina budi ila kuzusha mapambano. Huo huwa ni mpambano wa kitabaka, baina ya maskini na wafanyakazi wanaonyonywa na matajiri wachache wanaoishi kama kupe kwa kuwanyonya walio wengi.
Mpambano huo wa kitabaka ndio moto wanaouchezea waroho wetu. Tuliacha kuzungumzia kuhusu mapambano ya kitabaka katika miaka ya mwisho ya 1980 pale Ukuta wa Berlin ulipoporomoka na Muungano wa Jamhuri za Kisoshalisti za Kisovieti ulipo sambaratika.
Lakini ni dhahiri kwamba mapambano hayo bado tungali nayo. Na yana hatarisha hata uthabiti wa kisiasa nchini China ambako wafanyakazi, hasa katika sehemu za kusini mwa nchi hiyo, wanakabiliana na matajiri wao wakidai mishahara zaidi na hali bora za kufanyia kazi.
Wenye kutunga sera zetu za uchumi wanafaa wakumbuke kwamba kuna majeshi ya wasio na ajira na majeshi ya wenye vipato vya chini — walio kwenye majeshi yote hayo wanaghadhibika wakiwaona wachache katika jamii yetu wakiichezea rasilimali ya taifa hili.
Wanaghadhibika wakisikia jinsi mabilioni ya fedha yalivyohaulishwa na kufichwa katika akaunti za nje zilizo kwenye benki za ama huko Uswisi au Jersey au Bahamas.  Wanaghadhibika wakiona kwamba serikali na taasisi zake zinazohusika ama zimelala au zimekhiyari kuvifungia macho vitimbi hivyo vya kifisadi kwa kuwa na wao wanakula humo humo.
Wanaghadhibika zaidi na kukirihishwa wakisikia, kwamba miongoni mwa wanao ukorofesha uchumi wa taifa kwa vitendo vyao vya kifisadi ni aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, waziri wa zamani wa nishati na madini pamoja na waziri wa zamani wa ulinzi. Wote hao walitajwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ambaye ameyavalia njuga mas’ala haya ya waroho wetu wenye kutorosha mabilioni kwa matrillioni ya fedha nje ya nchi na kwenda kuyaficha nchi hizo nilizozitaja na kwengenako.
Kwa sasa hakuna vuguvugu linalowaunganisha wananchi kuupinga mfumo uliopo wa kiuchumi na sera zake.  Lakini watawala wetu wasifikiri kwamba walio chini katika jamii wataendelea kuvumilia wakinyonywa na kunyanyaswa bila ya kuchukuliwa hatua dhidi ya wanyonyaji na wanyanyasaji au bila ya hatua kuchukuliwa kurekebisha hali za walio chini, ambao ndio wengi wa wananchi wa taifa hili wanao umia.
Yote hayo yanaweza yakachukuliwa hatua endapo wakuu wa serikali kweli wamejizatiti kuung’oa ufisadi katika jamii sambamba na misingi ya utawala bora.  Ni muhimu kwamba tuna yatafakari haya sasa wakati nchi yetu ya Zanzibar iko mbioni kudai mamlaka kamili na Tanganyika wakiwa mbioni katika mchakato wa kulipatia taifa lao Katiba mpya.
Lazima watawala na sisi watawaliwa tujikumbushe kwamba mamlaka kamili hayatoshi sasa na nchi ya Tanganyika kupata Katiba pekee haitoshi na kwamba tunapaswa tuwe na utamaduni wa kisiasa utaowazuia mafisadi kutorosha mabilioni ya fedha kutoka nchini. Ikiwa utamaduni huo wa kisiasa hatunao basi Katiba kwa nchi ya Tanganyika na mamlaka kamili kwa nchi ya Zanzibar hata yawe mamlaka kamili ya utamu namna gani haitoweza kuhakikisha kwamba vitendo vya kifisadi kama hivyo havitoweza kutokea tena., kwa Tanganyika ndio hivyo hivyo katiba na iwe nzuri namna gani, haitoweza kuhakikisha kwamba vitendo vya kifisadi kama hivyo havitoweza kutokea tena.
Ugumu uliopo ni kwamba inachukua muda mrefu kuulea utamaduni wa kisiasa utaotuwezesha tuutumie kuimarisha demokrasia na utawala bora ili ufisadi usiwe na nguvu ya kutuvurugia uchumi.
Inatupasa tutafakari na tujiulize iwapo ni siasa au utamaduni wa kisiasa utaotuwezesha tufanikiwe kuung’oa ufisadi wa hali ya juu wa akina huyo Mkuu wa Jeshi mstaafu, aliyetajwa bila ya kutajwa jina na Kabwe.
Iwapo tunataka maendeleo hatuwezi kuwaachia watawala wetu waendelee na utamaduni wao wa kuvumiliana na kulindana.  Lazima wajirekebishe. Wazitumie siasa kuubadili utamaduni wao. Demokrasia wanayosema kuwa wanaijenga haiwezi kuwa kitu iwapo haitoandamana na utawala wa sheria.
Na ni huo utawala wa sheria tu utaoweza kuwazuia mafisadi wasiendelee na ufisadi wao unaozusha mpasuko mkubwa wa mapato katika jamii baina ya matajiri wachache na mamilioni ya wananchi wenzao wanaozidi kusononeka kwa hali zao duni. Wasipo usimamisha huo utawala wa sheria basi watawala wetu wataendelea kucheza na moto.  Kuna siku utakuja waunguza haba dunia bado kwenye kaburi wakifukiwa na siku ya kiyama wala musijidanganye kuwa ni mbali hata sio mbali Nyerere yuko wapi..? Mzee Karume yuko wapi..? Mabutu yuko wapi..? Mzee Kinyata yuko wapi..? Iddi Amini yuko wapi..? Kabila yuko wapi..? Savimbi yuko wapi..? Said Baree na Jeneral Aidid wako wapi..? Gaddafi yuko wapi n.k. n.k. basi na nyinyi mtakwenda mtaziwacha hapa hapa.

Wednesday, November 13, 2013

BREGEDIA JENERALI WA NCHI YA ZANZIBAR NI LINI WEWE UTAITETE NCHI YA ZANZIBAR..??


 Bregedia Jenerali Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Sharif  Shekh. Othman,

DKT MVUNGI AFARIKI DUNIA NCHI YA TANGANYIKA HAIKALI WALA HAITEMBELEKI KWA MAJAMBAZI WALIO KITHIRI NCHINI HUMO

Dkt. Mvungi akisindikizwa kupanda ndege kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Hii ni picha ya Dkt. Mvungi akisindikizwa kupanda ndege kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
kumbe huko ndio anako kwenda kumalizika.

Wakati ikiwa ni jana tu ambapo Waziri wa mambo ya ndani wa nchi ya Tanganyika Dkt . Emmanuel Nchimbi alitangaza kushikiliwa kwa watu tisa wanaotuhumiwa kuhusika na ujambazi na kumkatakata kwa mapanga Dkt. Sengondo Mvungi aliyekua mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Mpya na kiongozi wa NCCR-Mageuzi.
Habari zilizopatikana jioni hii zinasema kwamba mjumbe huyo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dakta Sengodo Mvungi amefariki dunia majira ya saa tisa alasiri; katika hospitali ya Mill Park huko Afrika ya Kusini alipokuwa akipata matibabu ya majeraha ya mapanga.
Dkt. Mvungi alijeruhiwa kwa kukatwa katwa  mapanga kichwani usiku wa kuamkia Jumapili Oktoba 3 Mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Mill Park, Johannesburg, Afrika Kusini.

SHEIN KAMA WEWE SIO MNAFIKI NI NINI...???


SHEIN WEWE KAMA SIO MNAFIKI NI NINI....????

Shein alisema kila mwananchi ana haki kikatiba(UAMSHO SIO WANANCHI WAO HAWANA HAKI YA KIKATIBA..?) kufanya jambo analolitaka ukiwamo uhuru wa  kutoa maoni:(MBONA UAMSHO WALIVYO TOWA MAONI YAO UMEWESWEKA JELA IKIWA NI UHURU KUTOWA MAONI..? )
“Kama Makamu wa Kwanza wa Rais anayo maoni yake kuhusu  muundo wa Muungano ni maoni yake au ya chama chake (UAMSHO PIA YALIKUWA MAONI YAO MBONA UME WASWEKA JELA..?)…Lakini siyo msimamo wa  serikali…Isitoshe msemaji wa serikali ni mimi labda atoe msimamo wa serikali  kwa maelekezo yangu,”.SHEIN WEWE SIO MSEMAJI WA SEREKALI WEWE NI MSIMAJI WA DODOMA ASIYEJUWA NI NANI KATIKA ZANZIBAR HII UMELALA BADO HII NI 2013.

Shein amemtetea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,  Maalim Seif Sharif Hamad kwamba hajakiuka utaratibu wa kuendesha serikali ya  umoja wa kitaifa kwa kutoa kauli za kutaka kuwepo mfumo wa Muungano wa serikali tatu na Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili.
Akizungumza Ikulu mjini Zanzibar jana, Shein  aliwaambia wandishi wa habari kwamba Maalim Seif hajawahi kutoa kauli ambazo zinahusu msimamo wa serikali  kwa mambo mbalimbali na kwamba kama ametoa kauli ni maoni yake binafsi  ama ya chama chake.
Shein alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa swali kwamba  inakuwaje Maalim Seif anatoa kauli tofauti na msimamo wa serikali hususan mfumo  wa Muungano kwa kusema kwamba uwe wa mkataba.
Shein alisema kila mwananchi ana haki kikatiba kufanya jambo analolitaka ukiwamo uhuru wa  kutoa maoni:
“Kama Makamu wa Kwanza wa Rais anayo maoni yake kuhusu  muundo wa Muungano ni maoni yake au ya chama chake…Lakini siyo msimamo wa  serikali…Isitoshe msemaji wa serikali ni mimi labda atoe msimamo wa serikali  kwa maelekezo yangu,”.
Aliongeza:  “Waziri yeyote wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hawezi kuisemea serikali juu ya Katiba…Mimi sijamsikia Maalim Seif anazungumza hivyo kwa niaba ya serikali,” alisema  Shein.
Hata hivyo,  Shein alisema mawaziri wote wanaounda serikali hiyo wanafanya kazi kwa  ushirikiano mkubwa na kwamba hawajawahi kuvutana:
“Tunajadili maslahi ya  watu wetu…ukija katika vikao vya Baraza la Mawaziri huwezi kujua nani anatoka  chama gani…La msingi ni kuvumiiana na kila mmoja kufuata Katiba,” alisema  Shein.
Pia Shein alisema amefanikiwa kuiongoza serikaliya umoja wa kitaifa kwa  mafanikio, ingawa alisema kuna wanachama wa CCM ambao wakati inaundwa walimuuliza  kama ataweza kuiongoza.
Alipoulizwa kuhusu kutofautiana kwa kauli kati  Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,  Balozi Seif Ali Iddi kuhusu mchakato wa Katiba mpya baada ya Waziri Bakari kusema kuwa nchi ya Zanzibar haikushirikishwa na Balozi mdogo wa nchi ya Tanganyika Balozi Iddi kusema kuwa ilishirikishwa,  Shein hakuwa  tayari kujibu hilo na alisema: “Suala hilo limemalizika,”.
Shein  aliwashukuru Maalim Seif na Balozi mdogo wa nchi ya Tanganyika Balozi Iddi kwa jitihada na kazi zao kubwa  walizofanya katika kipindi cha miaka mitatu kwa kumsaidia kuiongoza nchi ya Zanzibar: “Umahiri wao na uadilifu wao umesaidia sana katika kuwatumikia wananchi,” alisema Shein.

SHEIKH FARID,SHEIKH AZZAN,SHEIKH MUSSELEM,SHEIKH MUSSA NA WENZAO WACHIWE BASI MAANA WAO PIA NI WANANCHI NA WANAHAKI KIKATIBA WACHIWE BASI. WACHIWEEE WAPUMUWEEE

Monday, November 11, 2013

HAYAWI HAYAWI MBONA YAMEKUWA WANANCHI WA DONGE WAIKARIBISHA CUF NDANI YA DONGE


Wafuasi wa CUF wakiingia Donge na kubeba ujumbe wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.

Wafuasi wa CUF wakiwa wakibeba ujumbe mzito katika eneo la Donge.

Vijana wa CUF Donge, wakighani utenzi katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika viwanja vya Muwanda Donge.

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Muwanda Jimbo la Donge.

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akipandisha bendera katika moja ya matawi mapya ya chama hicho katika eneo la Donge.

Wafuasi wa CUF wakiwa tayari kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi kadi kwa mmoja wa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho katika Jimbo la Donge.

Picha na Salmin Said, OMKR
Na Hassan Hamad, OMKR
Hatimaye Chama Cha Wananchi (CUF) kimeingia katika kijiji cha Donge kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Muwanda na kuhutubiwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
Maelfu ya wafuasi wa Chama hicho kutoka maeneo mbali mbali ya Mjini na Vijijini walijitokeza katika mkutano huo ili kushuhudia kile kilichokosekana kwa muda mrefu kuingia katika eneo hilo la Donge kwa ajili ya Mkutano wa hadhara.
Akizungumza katika mkutano huo, Maalim Seif amesema anajisikia fahari kuzungumza na wananchi wa Donge katika eneo la ndani la jimbo hilo.
Amesema Donge ni kijiji chenye historia ndefu na ambacho kimejipatia umaarufu mkubwa Zanzibar baada ya kutoa wanazuoni kadhaa, pamoja na kutajwa kwao kushiriki kikamilifu katika Mapinduzi ya mwaka 1964.
Kuhusu mamlaka kamili amesema suala hilo limeanza kudaiwa tangu wakati wa marehemu mzee Karume, na kwamba wanaobeza kudai mamlaka ya Zanzibar wanabeza kauli za Mzee Karume ambapo katika mkutano huo pia iliwekwa sauti ya Mzee Karume alipokuwa akitaja malengo ya Mapinduzi.
Maalim Seif aliingia Donge mapema asubuhi ambapo kabla ya mkutano huo alifanya shughuli za kuimarisha chama ikiwa ni pamoja na kufungua matawi ya Chama hicho, barza pamoja na kuweka jiwe la msingi katika tawi la CUF Donge Muwanda.
Katika Mkutano huo Maalim Seif pia alikabidhi kadi kwa wanachama wapya 234, baadhi yao wakiwa wanachama na viongozi waliokihama Chama cha Mapinduzi kwa sababu tofauti, mmoja wao nd. Salim Khamis Nassor akiwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya (CCM).

Sunday, November 10, 2013

HUTBA YA RAISI WA NCHI YA TANGANYIKA KUHUSU MATATIZO WALIYO NAYO NA EAC JE IMEWATOWA TAKA ZA MASHIKIO NA TONGO ZA MACHO WAHAFIDHINA NA VIBARAKA WA WATANGANYIKA MULIO ZANZIBAR AU NDIO KWANZA MELALA..??


VIONGOZI HAWA NDIO KIBOKO NA MUARUBAINI WA NCHI YA TANGANYIKA SIO VIONGOZI WA NCHI YETU YA ZANZIBAR KILA ASEMALO MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA HEWALA BWANA MTANGANYIKA
Yeyote ambaye ni Mzanzibari na anaipenda nchi yake ya Zanzibar aliyefuatilia kwa umakini hotuba ya Rais Jakaya Kikwete raisi wa nchi ya Tanganyika alipohutubia katika Bunge la nchi yake mjini Dodoma juzi, bila shaka atakuwa siyo tu ameshangazwa bali atakuwa na maswali mengi yasiyo na majibu kuhusu hotuba hiyo, pia jinsi alivyozungumzia masuala mazito kwa kuipambapamba nchi yake ya Tanganyika kuwa ndio nchi nzuri haina ubaya inapenda mashirikiano bla blablabla.
Rais wa nchi ya Tanganyika alizungumzia masuala mengi yanayohusu mustakabali wa Tanganyika na nchi hizo za jirani, lakini hapa tutajielekeza tu kwa maelezo yake kuhusu nafasi ya nchi ya Tanganyika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), bila kuizunguzia nchi ya Zanzibar na nyenginezo. baada ya nchi ya Kenya, Uganda na Rwanda kuendesha mambo ya jumuiya hiyo bila kuihusisha nchi ya Tanganyika na kuiweka nchi ya Tanganyika ubao.
Pamoja na kwamba hotuba hiyo ilikuja ikiwa imechelewa, kwa maana ya watendaji wa Serikali wanaohusika na masuala ya nchi za nje, ikiwamo EAC kuachwa kwa muda mrefu wakitoa kauli tata na danganyifu kuhusu mustakabali wa nchi ya Tanganyika katika jumuiya hiyo, kujitokeza kwa Rais Kikwete juzi watanganyika wengi wamethani kuwa Raisi wao kaweka rekodi sawa kuhusu hali ya baadaye ya nchi yao ya Tanganyika katika jumuiya hiyo. Dhana ilikuwa imejengwa na watendaji hao kuwa, kutokana na nchi ya Tanganyika kutengwa na nchi hizo za EAC, kujiondoa kwa nchi ya Tanganyika katika jumuiya hiyo sasa lilikuwa jambo lisiloepukika.
Hivyo, kujitokeza kwa Rais Kikwete Raisi wa nchi ya Tanganyika juzi kulizungumzia suala hilo na kuliwekea msimamo bado kuwa Watanganyika wengi wanadhani kuliondoa wasiwasi uliokuwa umetanda miongoni mwa wananchi wa nchi ya Tanganyika siyo tu hapa nchini Tanganyika, bali pia Watanganyika wanafikiri katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo.Pia kuna Watanganyika wengi wanao jidanganya kuwa hakuna asiyejua kwamba nafasi ya nchi ya Tanganyika katika jumuiya hiyo ni kubwa na kwamba kujitoa kwake kutaiachia jumuiya hiyo ombwe ambalo kamwe haliwezi kuzibika nacheka kwanza hahahahahah maana haya ndio wanayojidanganya Watanganyika kila siku kuwa nyinyi Wazanzibari mukijitenga mutakuwa hamupati batata,vitugu,umeme utafikiri wanatupa bure nchi yenu itatikisika cha jabu tukiwambiya vunjeni basi Muungano Feki ili Wazanzibari tuteseka wanaogeza majeshi katika kambi za jeshi za nchi yetu. Kwa upande mwingine, Watanganyika wanajuwa kuwa lazima waungane na nchi nyengine la sivyo wao ndio watakao teseka ndipo walipokuja na usemi kuwa nchi ya Tanganyika tayari imewekeza sana katika jumuiya hiyo, hivyo kujitoa katika mazingira ya sasa ni sawa na kumsusia nguruwe shamba la mahindi.
Ni jambo la kheri kwamba Rais Kikwete ameweka wazi msimamo kwamba nchi ya Tanganyika imo, itaendelea kuwamo na haina mpango wa kujitoa katika jumuiya hiyo kama anavyosema mwenyewe licha ya vitimbwi vinavyofanywa na viongozi wa nchi hizo tatu. Hii ni ishara tosha kuwa nchi ya Tanganyika ndio muhitaji zaidi katika nchi hizo tatu kuliko hizo nchi nyengine maana kama sio muhitaji basi wangelijitoa tu lakini wanajuwa wazi kuwa wao ndio wahitaji zaidi nchi ya Tanganyika ndio maana wamengangania kubaki.hakuna na tafauti yoyote na ila ya nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar wakitaka wasitake nchi ya Tanganyika inahitaji zaidi nchi ya Zanzibar kuliko nchi ya Zanzibar inavyo ihitaji nchi ya Tanaganyika ila huta sikia hata siku moja Watanganyika wakisema hilo siku zote wao ndio wahitajiwa hahahahahaha bora nicheke hahahahaahahah.
Ni hotuba iliyojaa uwazi na kweli kuwa wao hawataki kuamuliwa mambo yao au ya nchi yao ya Tanganyika mpaka waamuwe wenyewe. Sasa tunajua kwamba sababu kubwa ya viongozi hao kuitenga nchi ya Tanganyika ni kuwa wanabadilika kama kinyonga pia kuhusu Raisi wa nchi ya Tanganyika msimamo wake wa kupinga kuharakisha kuundwa kwa shirikisho la kisiasa, hasa katika maeneo ya umiliki wa ardhi, uhamiaji na ajira. Msimamo huo umechukuliwa na nchi hizo tatu kama kikwazo kinachochelewesha maendeleo ya jumuiya hiyo, ingawa nchi ya Tanganyika imekuwa ikisisitiza umuhimu wa nchi wanachama kuheshimu mkataba ulioanzisha jumuiya hiyo.hapa ndipo tunawauliza Watanganyika mbona mnakereka Wazanzibari wakikata na Mafuta yao na Gas..?? mbona mnakereka Wazanzibari wakitaka kurudisha Paspoti zao...??  mbona mnakeraka Wazanzibari wakitaka kujuwa kila Mtanganyika anaikuja Nchini Zanzibar awe na sababu malum sio kuingia na kutoka kama chooni..?? mbona mnakeraka Wazanzibari wakitaka kuanzisha Pesa zao..??  mbona mnakereka tukiwauliza Hati ya Muungano Feki iko wapi ili tujuwe mkataba na mambo tulio ungana..?? n.k  n.k. bora nisite hapa maana ni mengi,
Nataka na nyinyi viongozi wa nchi ya Zanzibar mipumbavu mutowe takataka za mashikio na tongo za macho musikilize na muone anavyo juwa kujiweka katika miungano ya nchi nyengine huku wakiendelea kutukandamiza Wazanzibari amkeni amkeni walevi nyieee.Namnuku Raisi wa nchi ya Tanganyika  Kwa maana hiyo, sisi hatuoni tatizo kama msimamo wa Tanganyika ni kuona jumuiya hiyo ikijengwa hatua kwa hatua kama ilivyoainishwa katika mkataba, badala ya kuruka baadhi ya hatua. Hatua hizo zilizoainishwa katika mkataba ni; Umoja wa Forodha, Soko la Pamoja, Sarafu ya Pamoja na hatimaye Shirikisho la Kisiasa litakalopatikana baada ya wananchi katika nchi wanachama kupiga kura ya maoni. Hivyo, tunadhani Serikali ya Tanganyika iko sahihi kutounga mkono kuharakisha kuunda Shirikisho la Kisiasa ambalo linapaswa kujengwa juu ya misingi imara ya kiuchumi.
Hoja hapa ni kwamba tukiharakisha Shirikisho la Kisiasa Jumuiya itavunjika, kwani kama alivyosema Rais Kikwete, mambo yanayozua mitafaruku siku zote ni ya uchumi wala siyo ya kisiasa. Bahati nzuri huo pia ndiyo msimamo wa wananchi wa nchi ya Tanganyika.

Saturday, November 9, 2013

SIO INDIA TU HATA HAPA NCHINI KWETU HAYA YAKO WANAJIDAI WAKO BIZI KUMBE WANACHEZA KARATA KTK KOMPYUTA

JAJI FREDERICK WEREMA JE WANDISHI NASI TUAZISHE SHERIA KUWA KIONGOZI YOYOTE MWIZI BASI ANYONGWE UTAKUBALI..???


Nchini Tanganyika jijini Dodoma. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya nchi ya Tanganyika (AG), Jaji Frederick Werema jana ameangukia pua baada ya Bunge kukataa mapendekezo ya Serikali ya kubadili baadhi ya vipengele vya Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, ya kuongeza adhabu kwa waandishi wa habari watakaopatikana na hatia ya makosa ya uchochezi mwanasheria mkuu ndio jizi,jambazi na jiuwaji KUU.
Kadhalika Spika wa Bunge, Anne Makinda, aliungana na wabunge wengine kukataa mapendekezo hayo na kudai kuwa wakati umefika kwa Serikali kupeleka bungeni muswada wa sheria ya vyombo vya habari, badala ya kutoa ahadi zisizo na majibu kila wakati.
Kukataliwa kwa mapendekezo hayo ni pigo kwa Serikali na Jaji Werema ambaye juzi wakati akijibu hoja za wabunge alijigamba kwamba yeye anasimamia amani ya nchi kwa hiyo vifungu hivyo haviwezi kuondolewa, kwani anafanya kazi kwa masilahi ya taifa na hategemei magazeti kwa ajili ya kuwa mbunge.
“Sitegemei magazeti kuwa mbunge nafanya kazi ya taifa. Walio wangu watanikataa na wasiokuwa wangu watanikataa. Nipo kwa ajili ya taifa sitamwangukia mtu yeyote miguuni,” alisema Werema, kauli ambayo iliwachefua wabunge.
Hata hivyo, jana baada ya Spika kuwahoji wabunge na kukataa mapendekezo ya Serikali, Jaji Werema alionekana kukereka hivyo alisimama na kutaka Spika aruhusu kura zihesabiwe katika kifungu hicho.
“Mheshimiwa Spika, nimesimama kuona hata wa upande wangu wamenisaliti, duh, basi naomba kura zihesabiwe kwa kuita majina mmoja, mmoja ili tujiridhishe,” alisema Werema.
Hata hivyo, Spika alikataa na kusema: “Kama kuna eneo ambalo tumefanyia utani Serikali ni katika eneo hili, naomba Serikali mtuletee muswada bungeni siyo porojo za maneno.”
Katika marekebisho hayo, Serikali ilikuwa ikipendekeza katika sheria hiyo mabadiliko ya kuongeza adhabu kwa waandishi wa habari watakaopatikana na hatia ya kuandika habari za uchochezi, kutoka faini ya Sh15,000 hadi kiasi kisichozidi Sh5 milioni.
Hata hivyo, wakati Bunge lilipoketi kama kamati wabunge walikataa kupitisha marekebisho hayo ambayo yalikuwa sehemu ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2013, wakisisitiza kwamba Serikali ipeleke bungeni muswada wa sheria ya habari.
Kasheshe Bunge
Moto wa wabunge hao uliwashwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM), ambaye alipendekeza sehemu ya nane ya muswada iliyokuwa na vipengele vya 39, 40 na 41 iondolewe ili kuishinikiza Serikali kupeleka bungeni sheria nzima inayohusu vyombo vya habari.
Mbunge huyo alisema kuwa sehemu hiyo na vipengele vyake kama vingepitishwa vingeifanya Serikali kuwa kimya na kushindwa kupeleka bungeni Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari kama ilivyoahidi kwa muda mrefu. Mimi nimekuwa mbunge hapa huu mwaka wa nane, lakini kila siku Serikali imekuwa na kigugumizi cha kuleta muswada huo. Kila mara tunaambiwa kuwa utaletwa, lakini hauletwi sasa mpango wa kuleta vitu nusu-nusu haufai,” alisema Selukamba.
Mbunge huyo alilalamika kuwa baadhi ya viongozi walishapendekeza kuwa watu wote wanaopigia kelele sheria hiyo waangaliwe hati zao za kusafiria kwa madai kuwa zinatia shaka jambo alilosema kuwa yuko tayari kufanya hivyo ilimradi ahakikishe anasimamia kweli.
Jenista Mhagama
Baada ya Serukamba kutoa hoja hiyo, wabunge wengi walisimama kumuunga mkono ndipo akapewa nafasi ya kuchangia Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama ambaye pia alisisitiza kwamba lazima sheria ya vyombo vya habari ifikishwe bungeni.
Mhagama alisema kutokana na kigugumizi cha Serikali, tayari kuna gharama ambazo zimekuwa zikijitokeza ikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii kutumwa India kwa ajili kujifunza mambo mbalimbali yanayoendana na sheria hiyo, lakini bado hata hivyo haijasaidia kitu.
Mhagama na Serukamba tangu wakati mjadala wa  sheria ulipoanza juzi walisisitiza kuunga mkono kuletwa kwa sheria ya vyombo vya habari. Serukamba alisema akichangia muswada huo alihoji: “Kuna nini hapa..?? Maana hii tabia ya kuchomoa vipande vipande na kutuletea hapa haina tija.”
“Tukatae vipengele hivi, nawaomba wabunge wenzangu mniunge mkono katika hili na ikiwa tutavikataa vipengele hivi Serikali italeta sheria nzima hapa, mimi sina tatizo na adhabu hata ingekuwa mara tatu, lakini tuleteeni sheria nzima, mnaogopa nini..??” alihoji Serukamba.
Mhagama yeye alisema kwa muda mrefu wadau wa vyombo vya habari wamelalamikia kuwapo kwa sheria hiyo itakayolinda tasnia ya habari, lakini Serikali mara zote imekuwa ikipiga danadana.
“Kwa nini Serikali inachelewa kuwasilisha muswada wa sheria bungeni..?? Hebu sasa tukae na wadau tukubaliane mambo ya msingi, tuwe na sheria ili kuinusuru tasnia ya habari, sheria itasaidia kuwadhibiti makanjanja, wapo watu wanaoidhalilisha tasnia ya habari bila sababu za msingi,” alisema.
Taarifa ya Serikali iliyotolewa bungeni jana ilisema Muswada wa Vyombo vya Habari uko tayari na kwamba wakati wowote unaweza kupelekwa bungeni kwa ajili ya kupitishwa kuwa sheria.
Wabunge wengine
Vipengele hivyo vilipingwa na wabunge wengi tangu mwanzo, akianza Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu Lissu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) pamoja na Wabunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya na Martha Mlata (CCM). Tundu Lissu
Katika maoni ya Kambi ya Upinzani, Lissu alisema mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Magazeti hayana msingi kwa sababu; hakuna ushahidi wowote kwamba adhabu zilizoko katika vifungu vya 36(1) na 37(1)(b) zinazopendekezwa kuongezwa zimeshindwa kudhibiti makosa ya uchochezi.
“Tangu sheria hiyo ilipotungwa miaka zaidi ya 37 iliyopita, hakuna mwandishi wa habari au mchapishaji wa gazeti lolote ambaye amewahi kufikishwa mahakamani na kupatikana na hatia ya makosa hayo. Badala ya kuwapeleka wakosaji mahakamani,  Serikali imejenga utamaduni wa kufungia magazeti na kutisha waandishi habari,” alisema Lissu na kuongeza:
“Hii peke yake inathibitisha hoja kwamba sheria ilitungwa kwa malengo ya kisiasa ya kudhibiti wakosoaji na wapinzani wa Serikali na watawala na si kuzuia makosa ya jinai”.
Bulaya
Bulaya kwa upande wake alisema, Serikali inafanya makosa makubwa kwa kutaka kuwaadhibu waandishi wa habari, pasipo kujenga msingi imara wa uandishi wenyewe kama taaluma katika nchi.
“Kwa nini Serikali inawaza adhabu kali tu..?? Kuongeza faini kutoka Sh15,000 hadi Sh5 milioni, hapo kuna nini, lazima tujiulize maana kwa kufanya hivi tunawaumiza waandishi wa habari ambao wengi wao hawana uwezo wa kulipa hizo fedha,”alisema Bulaya na kuongeza:
“Sheria nzima ikiletwa hapa, tutakuwa na uwezo wa kuangalia mambo mengi yakiwamo masilahi ya waandishi wa habari, lakini pia kuwabana watu ambao hawataki kutoa habari ila wanasubiri waandikwe ndipo wajitokeze kulalamika.”
Mlata
Naye Martha Mlata katika mchango wake alisema wanasiasa ndio wamekuwa wakiwatumia waandishi wa habari na kwamba faini iliyowekwa na Serikali ni mbaya kwani ni mzigo kwa waandishi wa habari.
“Na sisi wanasiasa tuache kuwatumia waandishi wa habari na ninyi waandishi wa habari msikubali kutumiwa na wanasiasa, tukitaka kuwatumia mkatae na mfanye kazi kwa kumwogopa Mungu kila mtu kwa dini yake,” alisema Mlata.
Walioishabikia sheria
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Pindi Chana na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM) walishabikia kuwapo kwa adhabu kali kwa waandishi wa habari, kwa maelezo kwamba wamekuwa wakitumiwa kuwachafua watu.ila ukweli wa mambo ni kuwa tunafichuwa siri zao za kuiba mamillioni kwa mamillioni na kutumia na kuzivuruga pesa za serekali wao na wake zao na watoto wao sasa wanaona mambo yao yako nje kila moja anayasoma ndio maana wakafurahia adhabu hiyoo.
Chana alisema: “Katika malengo ya Serikali ilipoleta marekebisho haya wametuambia kwamba malengo yake ni kuongeza adhabu ili kulinda matumizi ya lugha ya matusi, makosa haya yanajumuisha matumizi ya lugha za uchochezi zinazoweza kusababisha machafuko katika jamii.
“Ni ukweli kila Mtanganyika anafahamu kuwa magazeti yetu kuna wakati yanatumika na kikundi fulani, kuwabeba kikundi fulani au mtu fulani na kuangamiza mtu fulani au kikundi fulani.
Aliliomba Bunge litoe majibu pale magazeti yanapomdhalilisha mtu kwa kuandika jambo ambalo halina ushahidi wa kimahakama. “Nawauliza wahariri, pale magazeti yanapotumika kuchochea ndivyo sivyo tufanyaje..?? Je, huo ndio uhuru wa habari?” alihoji.na sisi wandishi tunawauliza nyinyi viongozi munaiba mamillioni kwa mamillioni na kunyanganya watu ardhi zao na kujitajirisha je tufanyeje...?? je huo ndio uhuru wa kuwa kuongoza..? ukiwa kama kiongozi wa watu kuiba mamillioni kwa mamillioni na kutumia na familia yako hali yakuwa rai wengine wanakufa na nje na maradhi je sisi tufanyeje..?
Nchemba kwa upande wake alisema hakuna haja ya kusubiri sheria mpya na kwamba kusubiri kunaweza kutoa mwanya kwa vyombo vya habari kuitumbukiza nchi kwenye machafuko.Nchemba nchi haitatumbukia katika machafuko kwa sababu ya wandishi wa habari laa ila itatumbukia katika machafuko kwa sababu yenu nyinyi viongozi wezi na munaojifikiria nyinyi tu na wake zenu na mahawara wenu na kuwasahau wananchi wanao kufa na nja,hawana paa kuishi,hawana kazi,hawana madawa hospitalini n.k.

Friday, November 8, 2013

VIDEO-RAISI WA NCHI YA TANGANYIKA IKIHUTUBIA KATIKA BUNGA LA NCHI YAKE YA TANGANYIKA NA KULALAMIKA KUHUSU UMOJA WA EAC

AMA KWELI M.MUNGU MKUBWA MSIKILIZE ANAVYO LALAMIKA NA KUSIKITIKA NA KUJIDAI KUWA NCHI YA TANGANYIKA HAINA UBAYA WOWOTE KATIKA USHIRIKISHO WA EAC. WEWE SEMA KWELI HAWA MARAISI WA NCHI YA KENYA,UGANDA,RWANDA NA BURUNDI WAMEKUSHTUKIZIENI SIO MAJUHA KAMA KILE KIBUSHUTI SHEIN UTAKIGAUZA UNAVYOTAKA MAANA WEWE SINDIO UMEMUWEKA LAKINI HAWA WANAKILI NA WASHAWAJUWA WATANGANYIKA WAONGO,WEZI,MAJAMBAZI,SIO WAMINIFU NA WAUWAJI. MNAFIKIRI MTAWANDANGANYA NA PRADO KAMA MNAVYO WADANGANYA VIONGOZI WA ZANZIBAR..? ATI WANASEMA WANATAKA MAMBO YAENDE HATUWA KWA HATUWA. MBONA BASI WAZANZIBARI MPAKA LEO MUNATULAZIMISHI TUBAKI KATIKA MUUNGANO FEKI..? ANAJIDAI KUWA NCHI YA TANGANYIKA HAIKO TAYARI KUNGANISHA ARDHI KATIKA EAU LAKINI MAFUTA NA GAS YA NCHI YA ZANZIBAR MPAKA LEO HAMUTAKI YAWE YA WAZANZIBARI WALAHI MNAFIKI NI MNAFIKI TU HEBU MSIKILIZENI NYINYI WAPUMBAVU WAKUBWA VIONGOZI WA ZANZIBAR NA MUAMKE SIO KAZI KULA MAPESA YA WIZI NA KUVUNJIA WATU NYUMBA ZAO NA VIBADA VYAO VYA KUTAFUTA RIZIKI MSIKILIZE HUYU KIKWETE NA NYINYI MNASINZIA TU BARAZANI BADALA YA NYINYI PIA KUMUAMBIA MBONA WEWE HUTAKI KUNGANISHA HICHI KATIKA EAC BASI NA SISI PIA HATUTAKI WAPUMBAVU KAZI KULEWA MKIZINI NA WAKE ZA WATU NA KUIBA NA KULA MALI YA UMMA NA KUNYANGANYA WATU MASHAMBA YAO HILO NDIO MUJUWALO VIONGOZI WA ZANZIBAR WAPUMBAVU WAKUBWA NYIEEE

Thursday, November 7, 2013

BEEF HILO LINAPIGA HODI PESA KWELI ZINA LANAA SIO MCHEZO

DAIMOND KAKA MTU
DOGO S KIDE MDOGO MTU

NYINYI KAMA DUGU KWELI KAENI MUZUNGUMZE KAMA WATU WAZIMA MUHESHIMIANE HATA KAMA SIO DUGU PIA KAENE MUZUNGUZE TAFAUTI ZENU MUYAMALIZE KIJITU KIZIMA.

NCHINI TANGANYIKA KWAJENGWA BANDARI MPYA BAGAMOYO, DOLA BILLIONI 1.2 KWA JILI YA UPANUZI WA MAGATI SABA BANDARI YA DAR


Ufanisi katika ukusanyaji wa mapato huenda ukaongezeka Bandari ya jiji la Dar es Salaam nchini Tanganyika baada ya Kampuni ya Uingereza kuahidi kutoa zaidi ya Dola 1 bilioni kwa ajili ya upanuzi wa magati saba.
Akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Justine Greening, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Charles Tizeba alisema upanuzi huo utaleta ufanisi katika shughuli za bandari, kukuza biashara na mapato.
Tizeba alisema Kampuni ya Trade Mark East Africa, ndiyo itashughulikia upanuzi huo na kuwa muda sahihi wa kuanza mradi bado haujawekwa wazi kwa kuwa upo katika hatua za mwanzo.
“Ushirikiano huu una manufaa makubwa na sisi tunatarajia upanuzi wa bandari utakuwa wa mafanikio makubwa kiuchumi. Taifa litanufaika kimapato na ushirikiano wetu na Uingereza utaongezeka pia,” alisema Tizeba.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari za nchi ya Tanganyika (TPA), Injinia Madeni Kipande alisema bandari hiyo kwa sasa ina uwezo mdogo wa kuingiza na kutoa mizigo kutokana na kulemewa, hivyo upanuzi huo utaleta mabadiliko makubwa kiutendaji.
Alisema Kampuni ya TMEA bado inafanya upembuzi yakinifu ili kupata gharama halisi za mradi wa upanuzi wa bandari ingawa gharama zinazotarajiwa ni kiasi cha Dola 1.2 bilioni.
Injinia Kipande alisema baada ya upanuzi huo, bandari itaweza kupokea meli kubwa kutoka nchi mbalimbali.
Pia alisema meli hazitakaa kwa muda mrefu bandarini na badala yake uingizwaji na utolewaji wa mizigo utakuwa wa kasi.
“Changamoto kubwa hapa ni wingi wa meli ambazo bandari yetu haiwezi kuzifanyia kazi. Ingekuwa tuna gati nyingi ufanisi ungekuwa mkubwa zaidi na mapato yangeongezeka,” alisema Kipande.
Kwa sasa bandari hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo msongamano wa mizigo tatizo ambalo linatajwa kuchangiwa na ukosefu wa ushirikiano baina ya watendaji wakuu.
Pia imeelezwa kuwa ucheleweshwaji wa mizigo bandarini ni kiasi cha asilimia 67 jambo ambalo linatajwa kuchangia kushuka kwa mapato na ufanisi.
Changamoto nyingine inayotajwa kushusha ufanisi katika bandari hiyo ni miundombinu chakavu ambayo inasababisha kupungua kwa idadi ya mizigo kwa kiasi cha asilimia 87 kutoka nchi jirani zinazotumia bandari hiyo kama Zambia, Uganda na Zimbabwe.
Hata hivyo, TPA inatarajia kuongeza kiwango cha uingizaji na utoaji wa mizigo hadi kufikia tani milioni tano ifikapo mwaka 2015, kuimarisha ulinzi na usalama na kuwa kitovu kikuu cha utoaji wa mizigo Afrika Mashariki na Kati.

Wednesday, November 6, 2013

ATI NCHI YA ZANZIBAR YAONGEZA MISHAHARA KWA WAWAKILISHI RAI TWAENDELEA KUFANYWA MAZOMBI

VIONGOZI WA NCHI YA ZANZIBAR SIO MAZOMBI BALI MAZOMBI NI SISI RAI WA ZANZIBAR TUNAO WACHAGUWA VIONGOZI HAO HAO KILA BAADA YA MIAKA KUMI HATA KAMA NI JIZI, JIUWAJI,LIMETUVUNJIA NYUMBA AU VIBADA VYETU VYA KUTAFUTA RIZIKI, LINATHULUMU MUDA UKIJA TU TUNALITILIA KURA LIBE VIZURI TENA NA TENA SASA UTAMWITA ZOMBI KWELI HATA MAZOMBI NI SISI RAI.
1. Wawakilishi wamepewa nyongeza ya 750,000/= na ushei
2. Walimu 25,000/= minus Ushei
Ukiachilia yote yanayofanywa na serikali yetu — kutimua timua dala dala pale Darajani, kuvunja nyumba za watu Bububu/Mwanyanya n.k — kupandisha bei ya umeme kwa asilimia zaidi ya 80% kuanzia Novemba 1/2013 — sasa SMZ SEREKALI YA MATHALIMU NA MAJIZI YASIOKUWA NA HARUMA NA RAI WAKE  imekuja na MPYA:
1. Imegeza mishahara ya ‘wafanyakazi’ wa SMZ wote. Wajumbe wa Baraza la wawakilishi watalipwa laki saba na nusu.
2. walimu wamepewa nyongeza ya 25,000/= kama una Phd kama huna; kama umesomesha miaka mitatu, kumi, 20, mmoja n.k katika mfumo kama huo. Almuradi serikali yetu imejaa ‘big thinkers’.
Nimekupeni picha halisi, sitaki kwenda sana katika details – mjue tu kuwa hiyo ndio nyongeza au SMZ wanaita ‘marekebeisho ya mishahara’.Marekebisho haya sio kwa wananchi wavuja jesho bali viongozi na wake zao na watoto wao hii nchi ya Zanzibar sio nchi ya wananchi bali ni nchi ya Viongozi na wake zao na watoto wao basi.
Kuna nyongeza ya siri kwa wakurugenzi na makatibu wakuu, sijui ngapi — maana ndio siri tena, almuradi wamevuna chao sihaba.
Wachunguzi wa mambo — hao hao waajiriwa wanasema kuwa kama hesabu ziko sawa, wao wangaliweza kuongezwa kama 100,000/ kutoka ama kiasa ya wajumbe wa BLW au hao wakurugenzi na pesa itabaki nyingi kwao.
Kuna walimu wamesomesha hao viongozi wa leo, na bado mshahara wao ni 100,000/ au laki moja unusu — wengine ni Master Degree, wengine na PHD holder, na wengine ni graduate lakini katika specialization fulani.
priority ni kujenga mnara wa kutimiza miaka 50 ya mapinduzi, upumbavu mtupu mnara wa mapinduzi tunafurahia kuuwa watu,kunajisi wake zawatu na watoto wa kike,kuowa watoto wawatu kwa lazima,kuwanyowa watu ndevu kwa vigae,kupiga watu mikwaju unguja na pemba,kunyanganya watu mashamba yao na kuyakata heka .
Haramu juu ya haramu na sasa kwajengwa mnara wa kukumbuka haramu kisha ijumaa misikitini allah akbari yagujuuuu mnara wa mapinduzi wakati  hatuna dawa, wanafunzi wanakaa chini, na ugawaji wa rasilmali [mishahara ndio huo mnauona]. Vichekesho vitupu.leo mlo moja Zanzibar watu wanaupata kwa mbinde astahafiru allah.
Ndio pale nilisema kuwa Zanzibar hatuna wawakilishi. Leo wao wameongezwa mara 100 ya kiwango cha wafanyakazi wengine,tunategemea kweli watasema nini hawa..? wameshatiwa kufuli mdomoni. Nyie wenzangu wengine mtaendelea kupigwa bao tu na hadithi za katiba mpya, kwenda kibanda maiti kucheza ngoma, na mambo kama hayo ama Kidumu Chama Mapinduzi au Haki Sawa kwa Wote. Hiyo Hakiiiiiiiii…………..na hiyo ndio Kidumuuuuuuuuuu…….!
Mimi sioni ajabu sana kuna haya maana mawaziri wetu ni akina Haruna Ali Suleiman, Haji Omar Kheri, Ramadhan Abdullah Shaban, Mohammed Aboud na kama hao — si wa kujua A wala B, wao ‘ulaji tu’ ndio wanaoujua.
 BEI YA UMEME KUANZIA NOVEMBA 1, 2013 IMEPANDA KWA ASILIMIA 80% NA ZAIDI, LAKINI WALIOIBA NA KUHUJUMU MABILIONI WAPO PALE PALE, SASA TUNALIPA SISI WAVUJA JASHO MPAKA MAVI YATUTOKE.MUZA MISHKAKI,BATATA ZA UROJO,MUZA MAZIWA,MUZA CHIPS,DALADALA,MSUKUMA RIKWAMA,MCHUKUZI,MUZA MATOFALI,MBEBA NA MCHIMBAJI MCHANGA N.K. MTALIPA UMEME MPAKA MAVI YAWATOKA SIMUNATAKA UMEME.

Friday, November 1, 2013

NCHI YA TANGANYIKA YATAFUTA WASHIRIKA WAPYA NJE YA EAC KWA NINI NA NYINYI MNAPENDA MUUNGANO..???

HII NDIO NCHI YA TANGANYIKA NA NCHI YA ZANZIBAR MUUNGANO OYEEE 

Serikali ya Tanganyika imeanza kutafuta washirika wapya wa kibiashara nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kujitokeza msuguano kati yake na baadhi ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo. Duru za habari zinaripoti kuwa, maafisa wa ngazi za juu wa nchi ya Tanganyika wameanzisha mazungumzo na serikali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Msumbiji kwa madhumuni ya kubuni ushirikiano wa kibiashara katika siku za usoni.

Pia ujumbe wa nchi ya Tanganyika umekutana na maafisa wa nchi ya Burundi kwa mazungumzo kama hayo. Hii ni katika hali ambayo, Waziri wa nchi ya Tanganyika anayehusika na masuala ya nchi za Afrika Mashariki kwa upande wa nchi ya Tanganyika, Samuel Sitta ameliambia bunge la nchi yake ya Tanganyika kuwa, Dar es Salaam haina budi ila kuangalia mipango mbadala katika masuala ya ushirikiano wa kiuchumi baada ya kuibuka dhoruba kali ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hatua ya Tanganyika ya kutafuta washirika wapya nje ya EAC inatokana na kutengwa na kuekwa ubao na nchi hizo na mataifa ya Rwanda, Uganda na Kenya kwenye mradi mkubwa wa kupanua miundombinu miongoni mwa nchi hizo za Afrika Mashariki.

Free Zanzibar People From Mkoloni Mweusi Tanganyika tumengunduwa kuwa Congo ndio ndugu zao kweli kweli na nchi ya Tanganyika wanaweza kushirikiana kwani mwenye nguvu achukue chake migodi yote ya nchi ya Congo wana control wenye bkuvaa uniform za jeshi hawana sharia wala kanunu chukua chako mapema kama kilivyo chama cha Serekali ya Tanganyika CCM Chukuwa Chako Mapema,basi ndivyo ilivyo nchi ya Congo wakuu ndio wanao kula wanyonge kufeni na njaa.

Rushwa hali ya juu hata askari wakawaida akishavaa magwanda na kalashinkov mkono basi yeye raisi anawezankukusimamisha akachukua anachotaka mila zao katika nchi ya Congo na nchi ya Tanganyika sawawa bora waunde community yao.  Leo nchi ya Rwanda inasifika kwa kua haina corruption nchi ya Tanganyika no1 kwa corruption wataweza kusikilizana...??? Watanganyika hawajijui nini wanachofanya isipokua wanachokijuwa wao ni WIZI NA KUUWA WATU.