Wednesday, November 13, 2013

DKT MVUNGI AFARIKI DUNIA NCHI YA TANGANYIKA HAIKALI WALA HAITEMBELEKI KWA MAJAMBAZI WALIO KITHIRI NCHINI HUMO

Dkt. Mvungi akisindikizwa kupanda ndege kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Hii ni picha ya Dkt. Mvungi akisindikizwa kupanda ndege kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
kumbe huko ndio anako kwenda kumalizika.

Wakati ikiwa ni jana tu ambapo Waziri wa mambo ya ndani wa nchi ya Tanganyika Dkt . Emmanuel Nchimbi alitangaza kushikiliwa kwa watu tisa wanaotuhumiwa kuhusika na ujambazi na kumkatakata kwa mapanga Dkt. Sengondo Mvungi aliyekua mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Mpya na kiongozi wa NCCR-Mageuzi.
Habari zilizopatikana jioni hii zinasema kwamba mjumbe huyo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dakta Sengodo Mvungi amefariki dunia majira ya saa tisa alasiri; katika hospitali ya Mill Park huko Afrika ya Kusini alipokuwa akipata matibabu ya majeraha ya mapanga.
Dkt. Mvungi alijeruhiwa kwa kukatwa katwa  mapanga kichwani usiku wa kuamkia Jumapili Oktoba 3 Mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Mill Park, Johannesburg, Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment