Wednesday, November 20, 2013

SHEIKHA AZZAN KHALID HAMDAN AMEREJEA NCHINI ZANZIBAR AKITOKEA NCHINI INDIA ALIKOKWENDA KWA JILI YA MATIBABU

SHeikh Azzan akiwa na familia yake nyumbani kwake Mfenesini, Zanzibar
 SHEIKH  AZZAN AKIWA NA FAMILIA YAKE NYUMBANI KWAKE HAPA MFENESINI NCHINI ZANZIBAR  

Nchini Zanzibar
Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu nchini Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Azzan Khalid Hamdan amerejea nchini Zanzibar akitoke India alikokwenda kwa ajili ya matibabu na kutakiwa kurejea tena Desemba 15, mwaka huu .
Sheikh Azzan aliaachiwa kwa dhamana ya matibabu akiwa miongoni mwa washtakiwa kumi waliofunguliwa kesi atii ya uharibifu wa mali na kuhatarisha Usalama wa Taifa, kesi ambayo inaendelea Mahakama Kuu nchi ya  Zanzibar
Akihojiwa na muandishi  nyumbani kwake Mfenesini nchini Zanzibar, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Sheikh Azzan alisema baada ya kufanyiwa uchunguzi wa figo, madaktari bingwa wamemtaka kurejea tena nchini India Desemba 15, mwaka huu kwa ukaguzi wa mwisho wa afya yake.
Sheikh Azzan alirejea nchini Zanzibar Novemba 8, mwaka huu baada ya kukamilisha matibabu yake katika Hospitali ya Manipal nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu na baadaye kupumzika Muscat Oman kwa muda wa wiki kabla ya kurejea hapa nchini  Zanzibar.
Akitoa tathmini ya maendeleo ya afya yake, Sheikh Azzan alisema alipofika Hospitali jambo la kwanza alifanyiwa uchunguzi na kuonekana ana matatizo makubwa matatu moja likiwa ni kupatikana na mawe 17 katika figo zake zote mbili, alitibiwa kwa mionzi na kuvurugwa mawe.
Sheikh Azzan anasema “Walinipiga mionzi katika figo langu la kwanza na kisha wakanipiga la pili na kuyavuruga mawe yote na kutoka mwilini kwa njia ya mkojo,”
Katika uchunguzi wa daktari aliofanyiwa, Sheikh Azzan alipatikana akiwa na tatizo la maumivu ya kichwa ambapo awali alikuwa akilalamika kuwa na maumivu makali pamoja na kukosa usingizi kwa muda mrefu.
Alisema daktari alimshauri apunguze matumizi ya simu ya mkononi (mobile phone) ili kujaribu kutuliza hali hiyo pamoja na kumpa dawa za kupunguza maumivu kwa muda wa miezi miwili mfululizo.
Akitaja tatizo la tatu, Sheikh Azzan alisema madaktari waligundua ana michubuko na vidonda katika tumbo na kutakiwa katika hatua ya awali kujipangia mlo na kuacha kula baadhi ya vyakula vikiwamo vile vyenye virutubisho vya Protein kama nyama ya ng’ombe, kuku, samaki, zabibu na maboga.
Alipoulizwa kama atarejea rumande Sheikh Azzan alisema, hakuna masharti ya kutakiwa kurejea gerezani lakini alisema Jaji Mkuu wa nchi ya Zanzibar alisema ripoti na uamuzi wa daktari utaheshimiwa kulingana na tatizo la kiafya linalomkabili.
“Sijapewa muda maalumu wa kurudi gerezani, kauli ya Jaji Mkuu, madaktari ndiyo watakaoshauri kama nipumzike kwa muda gani kabla ya kurejeshwa rumande na nina imani ripoti itakapowasilishwa watajadiliana,” aliongeza kusema Sheikh Azzan. 

No comments:

Post a Comment