Friday, December 27, 2013

ALIKUWA NAHODHA SASA NI MPIGA DEBEE (HANA JIPYA ANABWABWAJA TU KAMA MLEVI WA GONGO PALE ALABAMA)


Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa nchini Tanganyika ambaye atii ni Mzanzibari, Shamsi Vuai Nahodha amesema licha ya kuvuliwa uwaziri ataendelea kuwa kiongozi wa kisiasa na kukitumikia chama chake na wananchi bila ya kuvunjika moyo.(wachawee)
Nahodha, ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa ametoa kauli hiyo siku chache baada ya kutimuliwa kwenye Baraza la Mawaziri na Rais Jakaya Kikwete wa nchi ya Tanganyika kutokana na uzembe kuto kuufahamu kazi yake katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
Akihutubia wanachama wa CCM na Wahafidhina wenzake na kumsikiliza kwenye Ofisi ya chama hicho Mkoa wa Mjini Magharibi, hapa nchini Zanzibar, Nahodha alisema yaliyomtokea ni mambo ya kawaida katika medani za utumishi wa umma.(bora nichekea kwanza hahahahahaha hukujuwa wakati ule unamrisha majeshi yawauwe wapemba...?? kwamba iko siku kiti utakiwacha ulipo kikuta..?)
“Pamoja na hayo yaliyotokea, nitaendelea kulitumikia taifa,(tunakuliza taifa lipi..?? maana la Tanganyika lishakutimuwa, kama ni la Zanzibar omba mungu shein andele kuwa raisi wa kisonge au hata hapa Zanzibar pia tutakutimuwa maana huna faidi hata moja) chama changu na wananchi kwa uaminifu, juhudi na uwezo wangu wote,” alisema Nahodha, ambaye pia ni Mwakilishi wa Mwanakerekwe.
Alisema amewajibika serikalini kutokana na matakwa ya wajibu katika utendaji wa pamoja na kusema kitendo hicho ni mfano wa ajali inayoweza kumkuta mtu yeyote katika safari ya maisha.(hata bado hii dunia tu baba bado akhera sasa)
“Sina kinyongo wala muhali, yaliyotokea ni mambo ya kawaida katika medani za uongozi, wajibu na dhati yangu ni kuwa mtii kwa Serikali zote. Pia kuitumikia CCM na kushirikiana na wananchi wenzangu. Binadamu hawezi kujiepusha na mitihani, ”alisema Nahodha. Alisema alikabidhiwa dhamana na viongozi wake ili kulitumikia taifa na kutimiza wajibu ipasavyo katika nyadhifa mbalimbali na yaliyomtokea ameyapokea kwa mikono miwili na hana kinyongo.(ata ukiwa na kinyongo kitampata nani unafikiri..?)
Mauwaji ya Wazanzibari (Mapinduzi)
Akizungumzia mauwaji ya Wazanzibari (Mapinduzi) ya Zanzibar, Nahodha alisema ni ufunguo uliofungua milango ya fursa kwa wananchi wanyonge waliokandamizwa na ukoloni (haya makandamizo ya mkoloni mweusi Tanganyika huyaoni maana unakula nao sahani moja ila iko siku utayaona pale ukibaki na kijumba chako tu bila ya madaraka yoyote.) huku akisifu uongozi kwa miaka minane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, hayati Mzee Abeid Amani Karume.
Alisema kiongozi huyo licha ya kuongoza Mapinduzi ya Januari 12, 1964,(wacha kusema uwong mzee karume hakuongoza mapinduzi wala hakuwepo kabisa hapa Zanzibar na hata alikuwa hajuwi kama kuna mauwaji ya wazanzibari yanakuja kutokea alikuwa huko Tanganyika ulikotimuliwa) aliifanyia mema Zanzibar na watu wake katika kuwaletea maendeleo na kwamba atakumbukwa na vizazi vyote hadi mwisho wa dunia.(Nahodha wewe ni mema yapi uliyo wafanyia Wazanzibari au maendeleo gani uliyowaletea watu wa jimbo lako tu wachana na Zanzibar kwa ujumla jimbo lako tu ni maendeleo gani uliyowaletea...??)
“Kufanya Mapinduzi haikuwa kazi nyepesi. Waliofanya walikuwa ni majasiri na wazalendo. Juhudi zao ni matunda haya leo baada ya miaka 50 kupita nchi ikiwa katika utulivu na amani,” (ni nani aliyekudanganya Nahodha kuwa kabla ya mauwaji ya Wazanzibari(mapindizi) hapa Zanzibar palikuwa hapana utulivu na amani..?)  alisema Nahodha, ambaye alikuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar kuanzia mwaka 2000 hadi 2010. na hana moja alilolifanya la faidi kwa Wazanzibari.
“Uongozi wa Mzee Karume ni mfano wa aina yake, mwaka 1964 hadi 1972 aliiletea mabadiliko makubwa Zanzibar. Alijenga viwanda, makazi bora, elimu bila malipo, barabara na kuimarisha huduma za jamii,” alisema Nahodha.(mzee karume kafanya yote hayo kwa 1964 mpaka 1972 wewe Nahodha umefanya nini kuanzia mwaka 2000 hadi 2014..?)
“Nasikia kuna watu hawataki kulisikia neno Mapinduzi, hao ni wapuuzi na wapuuzeni. Mapinduzi na Muungano ni uti wetu wa mgongo, Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Karume waliona mbali, tusibeze mitazamo yao kwa tamaa za madaraka,” alisema.(yupi hapa mwenye tama ya madaraka wewe au sisi muwakilishi,mbunge,cheo walicho kuvuwa Watanganyika,hukutosheka ulekuwa unataka kuwa raisi wa Tanganyika ndio maana wamekutimuwa sasa ni nani mroho wa madaraka Nahodha..?)
Kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Nahodha alisema angependa ubaki katika mfumo na Serikali mbili na kusema pamoja na uzuri wake, zipo changamoto na kasoro zinazohitaji kurekebishwa na kuwa na muungano wenye nguvu za kiuchumi.(yagujuu mbona hukuyasema hayo ulipokuwa na vyeo vya Kitanganyika..?)
Alisema kazi ya kurekebisha makosa ni nyepesi lakini wazo la kuvunja Muungano lina gharama kubwa kuliko inavyofikiriwa na baadhi ya watu wanaotaka uvunjike.(wewe hamia huko Tanganyika Wazanzibari hatuti viraka sisi hatuna asili ya viraka.)
“Sina uwezo wa kuwachagulia watu kitu wanachokipenda na kukitamani. Imani yangu ni kwamba nje ya Muungano hatutabaki salama kama ilivyo sasa.(in shaa allah shari unayotutakiaya itakurudia mwenye na sisi tutajitenga na kuwa na nchi yetu ya Zanzibar kwa amani) Muungano wetu umekuwa kinga na nguzo kwa nchi zetu mbili na usalama na wake,” alisema Nahodha.
Aliitolea mfano Sudan Kusini ambayo ilitaka ipewe mamlaka yake kamili akisema hivi sasa imejikuta ikiwa katika machafuko na vita ya wenyewe kwa wenyewe pamoja na kuibuka kwa mgawanyiko wa kijamii unaotishia mustakabali wa Taifa hilo.(usitulete vitisho vya sudan wala kwengine ulimwenguni wao wanakili zao na sisi tuna akili zetu sisi sio kama wewe unategemeya akili za nyerere ambaye ashakufa ndio maana huweze hata kufikiri maana akili zako zishakufa nyerere kenda nazo.)
“Itazameni Sudan Kusini, tusipokuwa waangalifu na makini yanaweza kutukuta. Angalia vita ya Somalia inaitesa Kenya na kutukosesha amani, tusikubali kugawanywa na viongozi ambao wanawaza madaraka.”moja wapo ni wewe unayetaka kuwagawa wazanzibari waendele kuwa chini ya MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA NA SIO KUWA HURU.

No comments:

Post a Comment