Friday, December 20, 2013

DULA HUSSENI NI MZANZIBARI KWELI AU NI CHOGO LILILO TUMWA KUJA KUHARIBU MDAHALO WA KUMBUKUMBU YA UHURU WA ZANZIBAR!!!


WATU WANASEMA KUWA WAO SIO WAZANZIBARI JAPOKUWA WAMEZALIWA ZANZIBAR LAKINI SIO WAZANZIBARI SAWA TUMEFAHAMIYANA VIZURI SAANAAAA

IWEJE BASI HAWA WAWE WAZANZIBARI..??NA WENGI WAO HAWA HAWAKUZALIWA HASWA HAPA ZANZIBAR WALIKUJA MIGONGONI MWA MAMA ZAO WAKITOKEA NYASA NA TANGANYIKA AU WALILETWA TU KUJA KUTAWALA KWA NGUVU ZA MASULTANI WAKITANGANYIKA WAKOLONI WEUSI NI VIPI WAO WAWE WAZANZIBARI NA WALIO ZALIWA HAPA WASIWE WAZANZIBARI....?
DULA HUSSENI NI MZANZIBARI KWELI AU NI CHOGO LILILO TUMWA KUJA KUHARIBU MDAHALO WA KUMBUKUMBU YA UHURU WA ZANZIBAR!!!
Siku ya tarehe 14 Disemba, kule Forest Gate jijini London Uingereza, kulifanyika mdahalo wa kihistoria kuhusu kumbukumbu ya Uhuru wa Zanzibar wa Disemba 10 mwaka 1963. Mdahalo huu uliandaliwa kwa hisani kubwa ya jumuiya ya MUWAZA ikishirikiana na Wazanzibari walio wengi wanaoishi hapa Uingereza, hasa hasa Wazanzibari wanaoishi London.
Mdahalo huu ni miongoni mwa harakati chache za Wazanzibari wenye uchungu na nchi yao kutaka kudumisha na kuilinda historia ya nchi yao ambayo inaelekea kufifia katika siku za hivi karibuni. Itambulike kwamba, Zanzibar ilikuwa chini ya Utawala wa Waarabu wa Oman kuanzia miaka ya 1840 pia ikiwa himaya ya Uingereza hadi Disemba 10 mwaka 1963 nchi hiyo ilipopata Uhuru. Uhuru ambao si wengi kati ya wananchi na vizazi vipya kuutambuwa ipasavyo.
Kuna sababu lukuki zinazofanya tukio la uhuru wa Zanzibar liwe halitambulikani kama inavyotegemewa. Katika nchi zote zilizotawaliwa, siku ya uhuru ndio sikukuu pekee inayowaunganisha wananchi wa aila zote na imani zote bila kuwagawa. Kama hili ni kweli, Zanzibar haimo katika nchi za aina hii kwa sababu ni nchi pekee ambayo haisherehekei uhuru wake na badala yake, inasherehekea Mapinduzi ya mwaka 1964 siku ambayo ilitakiwa kuwa siku ya majuzi maana wazanzibari wengi waliuliwa na machogo.
Uhuru na Mauwaji ya Wazanzibari (mapinduzi) kwa Zanzibar zimekuwa ni dhana mbili kuu ambazo zinaichanganya historia, akili na hata fikira za watu mbali mbali hapa nyumbani na nje ya nchi. Kuna wanaoamini kuwa Zanzibar ilipata uhuru mwaka 1963 – hawa ndio akina MUWAZA na wengineo wenye imani na msimamo kama huu. Kuna wanaoamini kuwa Zanzibar haikuwahi kupata Uhuru na kama ilipata ulikuwa uhuru JINA au uhuru wa Bandia na sio hata wa Bendera. Kundi hili ndio lile akina Dula Husseni,Borafya,Shein,Ali Vuai N.K. – Kijana ambaye alitoa maoni makali na yenye kutafautiana na karibu wote waliohudhuria mdahalo pale Forest Gate siku ile. Hali ambayo ilimfanya aonekane mtu wa ajabu ijapokuwa maoni yake yalipasa kusikilizwa na kuthaminiwa kwa upande mwengine. Vyoyote iwavyo, dhana hizi mbili- Uhuru na Mauwaji ya Wazanzibari (Mapinduzi) ndio mpaka hapa zinaunda kambi mbili ambazo kiutafiti na kiuhalisia ndio hasa zinazowakilisha jamii ya watu wa Zanzibar walio nje na ndani ya nchi yao. Ukweli ni kwamba, ndani ya Zanzibar wako akina MUWAZA wengi na wako akina Dula Hussein idadi chekea.
Nimelazimika kumtaja Dula Husseni katika hafla ile nzima kwa sababu alikuwa mtu wa aina yake. Mtu wa kipekee yaani ‘Unique’ katika mdahalo ule pale Forest Gate siku ile. Upekee wa Dula Hussein umekuja kwa sababu ya misimamo yake iliyotafautiana na wajumbe wengine wote waliokuwepo pale. Misimamo ambayo haikuwa matarajio ya Wazanzibari wengi kumsikia Mzanzibar mwenzao halisi akiweza kuitowa mitazamo yake ile hadharani kiasi kile.
Msimamo wa MUWAZA ulikuwa ni wa kuutambuwa na kuuenzi uhuru wa Zanzibar wa Disemba 10 mwaka 1963. Msimamo huu hautowi nafasi ya Mauwaji ya Wazanzibari (Mapinduzi) ya Zamzibar ya mwaka 1964 kuwa ndio jiwe la msingi la kuianzia historia ya Zanzibar huru kwani kimsingi, MUWAZA inaamini kwamba, Mapinduzi hayafanyiki kwenye nchi isiyokuwa huru. Huu ndio mtazamo na hoja ya wale wasioamini mapinduzi kuwa ndio tukio muhimu la Uhuru wa Zanzibar. Kwa mtazamo kama huu, tunafahamu kwamba hakuna Mapinduzi bila ya Uhuru. Na hapa ndio MUWAZA iliposimamia hoja zake na Wazanzibari wengi kwa Ujumla.
Tukigeuza upande wa pili wa shilingi, tunaona sura ya Dula Husseni na kaumu yake. Yaani wafuasi wake wenye msimamo na mitazamo kama yake. Kwa maoni ya Dula Husseni, Wazanzibari waafrika kwa fikra zake – yaani watu weusi wenyeji wa Zanzibar hawapaswi kujivunia Uhuru wa mwaka 1963 kwani haukuwa uhuru kweli. Haukuwa Uhuru uliomkomboa mtu mweusi kwa thana zao.Ndio wakaja na Mkulima na mkwezi. Dula anaendelea kwa kusema kwamba utasemaje Zanzibar imepata uhuru wakati bado kuna Sultani juu ya kiti..?? Tena Sultani wenyewe wa Omani ingawa amezaliwa Zanzibar yeye na baba yake. Uzawa huo haumfanyi yeye awe Mzanzibari. Kwa maana hiyo, Uhuru wa mwaka 1963 haukuwa uhuru bali ulikuwa changa la macho tu kwa Wazanzibari kwani hatamu ya utawala bado ilikuwa kwa Muarabu. Kwa maana hiyo, Dula Husseni anadai kwamba wanaoshangiria na kuutukuza Uhuru wa Zanzibar wa mwaka 1963, ni vibaraka wa Ukoloni wa Kiarabu wasiomtakia mema Mzanzibari ambaye ni mkulima na mkwezi. Kwa mantiki hii, Dula Hussein anayatmbuwa rasmi mapinduzi ya mwaka 1964 kuwa ndiyo hasa yaliyomkombowa Mzanzibari mweusi, dhidi ya makucha ya mkoloni Mzungu na Muarabu. Kwa mantiki hii hakuna Uhuru wa Zanzibar hoja ambayo inaleta dhana nyengine ya kuyafanya mapinduzi ya Zanzibar kuwa ndio Uhuru wenyewe pia. Kwa lugha nyepesi hapa Mapinduzi ni Uhuru na dhana hizo zinaweza kutenganishwa iwapo hali isiyohusiana na hii ya Zanzibar inahusika. Kinyume na hapo, dhana hizi mbili haziwezi kutenganishika.
Naam! Baada ya kutowa hoja hizi zilizochafuwa hali ya hewa katika ukumbi ule uliojaa wafuasi wa MUWAZA wenye kuamini Uhuru wa mwaka 1963, Dula Husseni aliamsha hisia kali na maoni yenye kuagawika pale ukumbini. Kikubwa kilichojitokeza pale ni kumuona Dula kama ni mtu aliyepotoka na kupotosha ukweli lakini ukweli unabaki kuwa aliyoyasema yana Ukweli mkubwa ndani yake, na kwa upande mwengine, wanayodai MUWAZA yana ukweli pia. Tushike lipi..?? Kwa mimi nitaanza hapo paa Mzee Karume yeye hakuzaliwa Zanzibar kabisa dula unatuambiyaje hapo..? John Okello aliyeyaongoza mapinduzi ya kuwauwa Wazanzibari ni mganda dula unatuambiyaje..? ikiwa dula anasema kuwa uhuru wa 1963 ni wa bandiya na wa 1964 ni wa haki kwakuwa aliyekalia kiti alikuwa ni mfalme ok je ni kwa nini ASP ilishiriki katika mkutano wa kudai uhuru wa 1963 kule london..? je ni kwa nini wasipinduwe wakati bado Mgereza alikuwa akitawala..? je ni kwa nini baada ya mapinduzi tu ya zanzibar hao walio itwa ndio wazanzibari walio pinduwa walianza kuuwana wenywe kwa wenyewe..? dula je zanzibar sasa wewe unaona iko huru chini ya mkoloni mweusi Tanganyika..? Dula tunakuliza kusema kwamba Zanzibar imepata uhuru1964 wakati bado kuna Sultani wa kitanganyika juu ya kiti na amri zote zinatoka Dodoma..?? Je baba yake Mzee karume na Mzee karume waamezaliwa Zanzibar...?? babu yake Ali hassan Mwinyi na baba yake Ali Hassan Mwinyi wamezaliwa Zanzibar...?? Pima, fikiria na amuwa! Tumia haki yako ya kujieleza na kutowa maoni bila Kumnyooshea kidole mwengine.

Maasalaam!

No comments:

Post a Comment