Friday, December 6, 2013

MUSITAKE KUMPA BICHWA KUBWA HUYO SHEIN KAMA KWELI YEYE NI RAISI NA MWENYE BUSARA NA AWACHIYE MASHEIKH WA UAMSHO BASI TUONE HIZO BUSARA ZAKE

Sheikh Azzan Khalid, mmoja wa washitakiwa kwenye kesi ya viongozi wa Uamsho.
Sheikh Azzan Khalid, mmoja katika viongozi wa Uamsho na wakombozi wa nchi ya Zanzibar.

TAASISI zinazopaswa kutoa haki katika pande zote za nchi mbili yani Tanganyika na Zanzibar zimeendelea kuigeuza kesi atii ya jinai inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI) nchini Zanzibar kuwa “uwanja wa kufanyia mazoezi”, baada ya kuiakhirisha tena kesi hiyo kwa mara nyengine.
Safari hii kesi hiyo imepigwa kalenda ikiwa imetoka kusikilizwa rufaa yake na Mahakama ya Rufaa ya nchi ya Tanganyika au wakoloni weusi huku bado jalada lake likiwa halijafika Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar kwa kuendelea na taratibu zinazostahiki.
Akizungumza na waandishi wa habari nje jengo la jengo la Mahakama Kuu Mjini magharibi nchini Zanzibar, wakili anayesimamia watuhumiwa hao, Salum Toufiq, alisema upande wa mashitaka ulikata rufaa Mahakama ya Rufaa ya Tanganyika kwa madai ya kupinga maamuzi yaliyotolewa na  Jaji Abrahamu Mwampashi wa Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar kwamba Mrajis hakupaswa kusikiliza kesi hiyo kisheria.
Mapema Jaji Mwampashi alikuwa ametoa hukumu kuwa mrajis aliyewanyima dhamana wateja wake hakuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kisheria. Hiyo ni baada ya upande wa utetezi kupeleka maombi ya dhamana kwa hoja kuwa Mrajis wa Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar, ambaye ndiye aliyewanyima dhamana wateja wake, hakuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi, na hivyo ya kuzuia dhamana.
Hata hivyo, Wakili Toufiq amesema Jaji Mwampashi aliona vifungu vilivyotumika ni sahihi na hata kama kulitokea makosa hapo awali, mahakama ilipaswa kutafuta njia ya kurekebisha. Kwa uamuzi wa Jaji Mwampashi, vifungu vilivyotumiwa na upande wa utetezi ni sahihi na Mrajis hakuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Upande wa mashtaka haukuridhika na maumuzi ya Jaji Mwampashi wa Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar na waliamua kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya nchi ya Tanganyika.
“Lakini Mahakama ya Rufaa wamehukumu kesi hii kwa kifungu kimoja tu cha mamlaka na ikatoa maamuzi kwamba Jaji wa Mahakama Kuu, Abraham Mwampashi, hakuwa na uwezo wa kuyafanyia mapitio maumuzi ya Mrajis wa Mahakama Kuu ya nchi ya Zanzibar,” alisema Wakili Toufiq huku akiongeza kwamba Mahakama ya Rufaa iliamuru mapitio lazima yafanywe na hakimu au jaji yule yule ambaye ametoa mamuzi ya awali.
Viongozi wa Uamsho ambao wameendelea kusota rumande kwa zaidi ya mwaka sasa ni Farid Hadi Ahmed (41) mkaazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Mselem (52) mkaazi wa Kwamtipura, Mussa Juma Mussa (47) mkaazi wa Makadara na Azzan Khalid (48) mkaazi wa Mfenesini.
Wengine ni Suleiman Juma Suleiman (66), mkaazi wa Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakar Suleiman (39) mkaazi wa Tomondo, Ghalib Ahmada Juma (39) mkaazi wa Mwanakwerekwe, Abdallah Said (48) mkaazi wa Misufini na Majaliwa Fikirini Majaliwa. Wote atii wanashitakiwa kwa makosa matatu yanayojumuisha kuharibu mali, uchochezi, ushawishi na kuhamasisha fujo na kula njama ya kufanya kosa
Kosa la nne linamkabili mshitakiwa namba nne,Sheikh  Azzan Khalid, ambaye anadaiwa kutoa maneno ya matusi kwa kamishna wa polisi wa mtumwa wa wakoloni weusi Tanganyika atii yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Vitendo hivyo vinadaiwa   kufanyika kati ya Oktoba 17, 18 na 19 katika maeneo tofauti katika manispaa ya mji mkuu wa nchi ya Zanziba ambapo washitakiwa hao wote wanayakana makosa yote hayo.
Kwa mara nyengine tena, kesi hiyo imeakhirishwa na watuhumiwa wamerudishwa tena rumande hadi Desemba 16 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment