Friday, December 27, 2013

UPANGA WA DHAHABU NI MUHIMU ZAIDI YA MAISHA YA MWANANCHI WA ZANZIBAR


JESHI LA POLISI NCHINI ZANZIBAR LIFANYIWE MABADILIKO ZAIDI-WAWAKILISHI WA AMKA SASA.

Wajumbe wa baraza la wawakilishi wametaka jeshi la polisi nchini Zanzibar lifanyiwe mabadiliko ya uongozi kutokana na kushindwa kuwakamata wahalifu wa vitendo vya mauwaji, tindikali na kuibiwa upanga wa dhahabu ndani ya jeshi hilo.(DUUUH SASA NDIO MNAJUWA KAMA ASKARI WENYEWE NI WEZI..?)
Mwakilishi wa jimbo la Chaani Ussi Jecha amesema jeshi la polisi nchini Zanzibar limeshindwa kukabiliana na vitendo hivyo na kuitia doa nchi ya Zanzibar kwa kuibiwa upanga wa dhahabu unaotumika kwenye mikutano ya nchi wanachama wa SAPCO.
Amesema kutokana kushindwa kuwakamata wahalifu hao na kuibiwa upanga huo iko haja ya kulifanyia mabadiliko jeshi hilo badala ya kufanyiwa mabadiliko ya kamishna pekee.
Nae waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais mnafiki Aboud amesema kumetokea vitendo vingi vya uhalifu, lakini jeshi hilo limeshindwa kuwakamata wahalifu.
Amesema hali hiyo bado inaonesha jeshi hilo lina matatizo na kuunga mkono ushauri uliotolewa na mwakilishi huyo wa kutaka jeshi lifanyiwe mabadiliko ya uongozi…
Kuhusu wizi wa upanga wa dhahabu uliotokea mikononi mwa jeshi la polisi nchini Zanzibar Aboud amesema uchunguzi wake unaendelea na nchi ya Bostwana itakayokuwa mwenyekiti wa mkutano wa SAPCO imejitolea kutoa upanga mwengine bila ya kulipisha.

No comments:

Post a Comment